Juni 10 IMF & World Bank kuamua iwapo Tanzania tunakidhi kupewa mkopo tulioomba kupambana na corona au hatustahili

The Evil Genius

JF-Expert Member
Mar 21, 2014
5,458
17,253
June 10 bodi ya wakurugenzi wa shirka la fedha Duniani na Bank ya Dunia kuamua iwapo tunastahili kupewa msamaha na mkopo kupambana na corona au laa.

Mwezi April IMF na WB walitengeneza kitu kinaitwa Catastrophe Containment and Relief Trust ili kusaidia nchi masikini kupambana na madhara ya corona.

Kwenye hiyo relief programme nchi masikini zitasamehewa kulipa madeni yake hadi miaka 2.

Tanzania tumeomba tusamehewe chini ya hiyo relief programme ili tupate pesa ya kutusaidia kupata vifaa tiba vya kupambana na corona.

Kwenye barua yake ya kuomba serikali imesema imeshindwa kufanya vipimo na kufuatilia muenendo wa corona kwa sababu ya ukosefu wa pesa.

IMF imesema June 10, 2020 bodi itaamua kama tunakidhi vigezo kusamehewa au lah.

Soma barua ya IMF kwa serikali.
FB_IMG_1591384040960.jpg
 
Hapo kwenye kutoa ripoti hadharani,kuna watu inabidi tu wakubali kishingo upande.

Hata kama itakuwa ni kusamehewa kulipa madeni kwa muda huo kutokana na athari za corona kiuchumi, nafuu hiyo inaweza kutumika zaidi katika kujenga miundombinu na si kugusa moja kwa moja maisha ya watu maana awamu hii inathamini zaidi maendeleo ya vitu kuliko watu unless unafuu wa kulipa madeni uendane na mashariti maalumu kuhakikisha wananchi wananufaika nao moja kwa moja.

Kwa mfano,kwa hapa nchini,serikali inatakiwa kutumia unafuu huo wa kulipa madeni(kama utatolewa) ama kwa kuongeza mishahara ya watumishi au kulipa madeni yao,kufidia sekta zilizoathirika na covid kama utalii,n.k.
 
Ina maana wanaenda kupigia magoti mabeberu?? Hahahaa njaa hainaga baunsa...eti tusitishane, fyuuuu
 
Kigogo kesharusha hii document mitandaoni!!

Hapo kwenye kutoa ripoti hadharani,kuna watu inabidi tu wakubali kishingo upande.

Hata kama itakuwa ni kusamehewa kulipa madeni kwa muda huo kutokana na athari za corona kiuchumi, nafuu hiyo itatumika kujenga miundombinu na si kugusa moja kwa moja maisha ya watu maana awamu hii inathamini zaidi maendeleo ya vitu kuliko watu unless unafuu wa kulipa madeni uendane na mashariti maalumu kuhakikisha wananchi wananufaika nao moja kwa moja.

MATAGA wanamtamani GOGOKi Kinoma sema ndio hivyo kawazidi sana yaani GAP la distance ya Dunia na jua.
 
FB_IMG_1591384048668.jpg
FB_IMG_1591384055059.jpg

Barua ya serikali kuomba IMF na World Bank pamoja na wafadhili kuisajdia ili ipate pesa kupambana na corona.

Serikali inasema ina hali mbaya.

Serikali inakiri kua kuanzia July 2020 hali itakua mbaya kiuchumi.

Serikali inakiri kua vifo vingi vimetokea majumbani mbali na hospitali.

Serikali inaomba wafadhili kuipiga jeki.
 
Sasa, nchi yako inapopitia magumu. Wewe unapata faida gani.,?
Ni vyema nchi inapopitia magumu tukawa wawazi watu wote waelewe.

Haiwezekani unatangazia watu kwa majigambo kua huna gumu lolote, wewe kwako mambo byeee halafu unaenda kwa mangi kupiga magoti na kumlamba miguu unaomba akukopeshe sukari au unga watoto watakufa njaa.

Hii lazima watu watakushangaa. Kwani kuna ubaya mtu kua na changamoto? Kwa nini usiwe muwazi.

Kweli masikini hana kiapo. Pamoja na majigambo yote kumbe ndani umetepeta .
 
So unataka kusema ukijitangaza kuwa wewe ni maskini utapewa msaada.
Au hao watoa msaada wanataka udhalilike ndio wakusaidie.
Inasaund poa hivyo?
 
So unataka kusema ukijitangaza kuwa wewe ni maskini utapewa msaada.
Au hao watoa msaada wanataka udhalilike ndio wakusaidie.
Inasaund poa hivyo?
Si wananchi tunakuelewaje kiongozi unaetuambia kila kitu kiko sawa na wala huhitaji misaada yao tuko vizuri halafu kumbe unaenda kuwalamba na kuwapigia magoti watu unaowananga kila siku kua ni mabeberu
 
Ukilia njaa kwa wananchi walkout huo ni udhaifu kwa kiongozi. Inabidi upambane kwa kila mbinu kuhakikisha chakula kinapatikana.
Huwezi lalamika kwa wanao chakula hakipo wakati uko na jinsi ya kupata chakula huo ni uzembe. Hata kwa kuiba unawezafanya ili kuokoa familia na kufedheheka.
 
Back
Top Bottom