Leo nataka kuzungumza na Jumuiya ya Wanausalama (Intelligence Community), Hivyo mada ya leo ni ngumu ina matumuzi makubwa ya akili kuliko mambo ya siasa za vyama ambako huko matumizi ya akili huwa yako likizo badala yake hisia na mihemko huwa inatuongoza. Kwahiyo kama ulikosa chanjo ya surua, pepoounda na majano, unaonywa upite uende kwenye kusara za watu mnaofanana nao huko.
Mwaka jana mwanzoni niliandika makala hapahapa inayotoa angalizo juu ya vombo vya ulinzi na usalama kuyamulika kwa jicho la tai mashirika ya kimataifa yasiyo ya kiserikali yanayofanya kazi zao nchini,
Nilitoa angalizo lile nikitumia rejea ya taaluma yangu kama mtaalamu wa masuala mtambuka ya uchunguzi na upelelezi wa kimataifa nikiwa na Leseni ya NCFE Level 3 inayotambuliwa na Jumuiya ya Madola nikituama kwenye Ujasusi wa kisaikolojia (Forensic Pychology). Miezi 7 tu baadae likatokea tukio la 29 oktoba 2025, Na ripoti ya Tume/Hotuba inasema tukio hilo “lilifadhiliwa”.
Hii inafuatia madai ya nchi nyingi duniani kwamba mashirika haya yanatumika kijasusi na nchi za kimagharibi, Madai hayo yaliwahi kutolewa na Rais wa Kenya Willium Ruto, aliyekuwa Rais wa Ufilipino Rodrigo Roa Duterte, Aliyewahi kuwa Rais wa Zimbabwe Robert Mugabe, Aliyekuwa Rais wa Venezuela Maduro nk
Kwamba nani alifadhili tukio lile? Jibu tunalipata kwa badhi ya waandaaji wa tukio ambao wengi baada ya kuiwasha moto nchi na kusababisha mauaji makubwa walifanikiwa kutoroka nchi nakukimbilia nje kama vile Nairobi, Ulaya na Marekani, na wanahifadhiwa huko kwa msaada wa mashirika ya kimataifa kama vile FORD FOUNDATION, HRW, AMNEST INTERNATION, nk. Na hivyo ndivyo kusema hawa ndio Wafadhili wenyewe. Binafsi Mashirika ya kimataifa dunuani nayatambua kama vitendea kazi vya Nchi za Magharibi kwaajili ya kueneza sera zake za nje, na kudumisha ushawishi wao.
Lakini muhimu zaidi vyombo vya ulinzi na usalama moja ya jukumu kubwa juu ya mashirika haya yanayokuja kufanya kazi nchini ni kuwajua kwa undani viongozi wa mashirika hayo hasa Mkuu wa shirika hilo au Mwenyekiti wa bodi wa shirika husika, Mfano mdogo nimeona Balozi mteule wa Marekani nchini Tanzania ameanza kutoa maoni kinzani na yasiyo ya kidiplomasia akiwa hata bado hajaripoti nchini, Kimsingi kwamjibu wa Roma Protocol kwa maoni yangu, Huyu Balozi mteule, Tanzania inatakiwa kumkataa asiwakishe Marekani katika ubalozi wa hapa nchini, Roma protocol inaelekeza namna nje ya mawasiliano ya kibalozi na hauwezi kuwa na maoni binafsi baada ya kupewa kituo cha kuwakilisha, Maoni yako yoyote wewe balozi yanahesabika kama kauli ya nchi yako. Na kwa maoni yangu kauli ile si ya kibalozi wala sio ya kidiplomasia.
Mfano wa pili, Ford Foundation inaongozwa na Bi Heather Gerken ambae rais wa 11 wa Ford Foundation tangu kamate madaraka mwezi Novemba 2025, akimrithi Darren Walker. Bi Gerken kabla ya kushika nafasiyo alikuwa mkufunzi wa Chuo cha Sheria cha Yale nchini Marekani na ni mtaalamu anayetambulika kimataifa katika sheria ya katiba na demokrasia.
Shirika lingine ni Human Right Watch likiongozwa na Philippe Bolopion, huyu ni mkongwe kwa miaka 13 akihudumu ndani ya Human Rights Watch na ni mtaalamu wa habari katika maeneo yenye migogoro, kwa lugha rahisi ni kuwa huyo huingia mstari wa mbele wa vita kuripoti maendeleo ya vita nk. Kama hujui basi huko huwa hawaendi waandishi wa habari za akina Carrymastori. Lazima upite cadet kwanza ujue na kutumia silaha nk.
Nasema haya nikiwa naelewa visa vingi vinavyohusu haya mashirika NGOs, namna yanavyotumiwa na CIA, MI6, FSB na mashirika mengine ya Kijasusi duniani, Ngoja nikupe kisa kimoja pengine kitazubua akili yako na kutoka usingizini, Tusafiri kwa pamoja hadi katika jiji la Otawa Canada, Huko tunamkuta Jasusi Joe Bassey kutoka Perrot Island nchini Canad ambae mwaka juzi aliachia nyaraka za siri zinazofichua kwamba Bi Claire Dubois, mwanamke Mfaransa katika miaka 30 iliyopita aliwasili Burkina Faso akijifanya kama mkurugenzi wa NGO ya Magharibi iitwayo Hope Forward, ambayo shughuli zake kuu ilikuwa ni kusaidia elimu ya wasichana na afya ya wanawake.
Bi Claire alijionyesha kama mwanamisaada ya kiutu aliyelenga kusaidia wanawake wa Kiafrika, akitembelea vijiji, shule, na masoko, na kutumia muda mwingi kusifu uongozi wa Burkina Faso kwenye televisheni ya serikali.
Walakini, nyuma ya shuguuli hii ya kibinadamu, Bi Dubois alikuwa akijishughulisha na ujasusi. Alikuwa akikusanya taarifa za kijasusi kwenye tovuti za kijeshi, ikiwa ni pamoja na vituo vya mafunzo ya kijeshi, vituo vya mafuta, na vituo vya uongozaji wa ndege zisizo na rubani, akitumia kivuli cha kazi ya kibinadamu.
Katika kazi zake zilizoonekana ni za kiraia lakini alibeba simu mbili-moja ya kiraia na ya pili ni simu maalumu kwa mawasiliano kijasusu na aliitumia kutuma barua pepe zilizowekwa katika mfumo wa ulinzi imara ambazo ni ramani zilizochakatwa vizuri na picha za setilaiti za maeneo nyeti ya kijeshi, kwenda kwa watu wa NATO na majasusi wemgine wa kigeni.
Shirika la ujasusi la Burkina Faso kwa msaada wa Shirika la Ujasusi la Urusi FSB tayari lilikuwa limetilia shaka shughuli Mama huyu na kufuatilia mawasiliano yake kwa ukaribu sana hasa kuingilia mawasiliano ya simu yake ambayo ilikuwa ikitumia Setelaiti. Baads ya kujiridhisha kwamba Bi Claire anafanya shughuli za kijasusi kweli, Walifanikiwa kuzuia nyaraka hizo zisiwe zinawafikia Nato na washirika kwakuwa tayari mawasiliano hayo ya Bi Claire walikuwa wameyaingilia kila akituma email zilikuwa zinaingia Moscow sio Brusels tena.
Rais Ibrahim Traoré aliwaamuru majasusi wake wamwache aendelee kukusanya nyaraka za misheni yake ili wamkamate akiwa na ushahidi halisi. Na baada ya miezi kadhaa, Hatimaye, alikamatwa na kuwekwa hadharani katika Kongamano la Kitaifa la Mamlaka ya Afrika, ambapo rais aliwasilisha nyaraka zake za siri na barua pepe zote moja kwa moja jukwaani, akifichua shughuli zake za kijasusi kwa ulimwengu. Na baadaye akazuiliwa kimya kimya na serikali licha ya shinikizo la nchi za magharibi kwakutumia mgongo wa azimio la kidiplomasia, Rais Traoré alisisitiza juu ya uwazi na haki, akisisitiza usaliti wa kuaminika ni adui wa Bukinafaso.
Japo taarifa hii majasusi wa Ufaransa walifanikiwa kuizima na ikaonekana ni uzushi tu, lakini katika korido za kijasusi duniani inatoa somo muhimu la nini kama nchi zina wajibu wa kucheza disko la mashirika ya kimataifa hasa haya yanayojiita ya watetezi wa haki za binadamu au haki za kidemokrasia nk.
Swali la kujiuliza, ni mashirika mangapi ya kigeni yako nchini na yanafanya shughuli walizosema watafanya bila kuwa na agenda nyingine? Wanafuatliwa kwa kiwango gani? Jibu lipo Lumumba!
Na Yericko Nyerere
View attachment 3586885