Jumba la Wachawi

Jumba la Wachawi

JUMBA LA WACHAWI
Mwandishi/mtunzi; Zulfa Huseni
SEHEMU YA 13

“Nimekuja kwenye dunia gani hii sasa mimi” niliongea peke yangu, kila mtu aliyekuwa pale stendi aliniona kama mwehu, kwani wakati mimi naishangaa hii dunia mpya na watu wao ambao walionekana ni watu walio endelea mno kuanzia mavazi yao hata mwonekano wao,lakini pia na wao pia walikuwa wakinishangaa mimi na kuona ni binadamu niliye tokea sayari ya mbali mno na kuangukia katika dunia yao.
Wakati huo ilikuwa ni saa moja, watu walizidi kuwa wengi katika hili jiji jipya la Dar es salam asubuhi hio.
Niliangalia katika lile jacketi langu na kuiona ile kadi yangu ya TTCL sasa nikaona njia nzuri ni kuwasiliana na ndugu zangu kwanza akiwa ni pamoja na mchumba wangu Thabit nikiamini angalau kutoka kwao nitaweza kupata suluhu ya matatizo yaliyokuwa yananikabili.
Sasa kazi ikawa ni kutafuta kibada cha TTCL, kwakweli nilizunguka sana pale mnazi mmoja kutafuta kibanda cha TTCL lakini niliambulia patupu.. ilikuwa ni jambo jingine lilio nistajabisha awali kabla sijakumbwa na mazingaombwe yale vibanda vya Kampuni ya simu ya TTCL pale mnazi mmoja vilikuwa vimetapakaa tele kama uyoga ajabu ni kuwa mwaka huu nilio ambiwa ni elfu mbili na kumi na sita hapakuwa na kibanda hata kimoja.
Japo sikuwa nataka kuuliza jambo lolote kwa mtu yeyote kutokana na kuonekana tahira, lakini ilinibidi niulize.
“Vibanda vya kupiga simu vimehamishiwa wapi” Nilimuuliza fundi viatu aliyekuwa akifungua ofisi yake majira yale.
“Vibanda gani?”
“Vya TTCL”
“Mmh!. sijahi kuviona hivyo vibanda maeneo haya” alijibu yule jamaa.
Sasa nikaona nisizidi kuwapa watu faida ya kuonekana hamnazo kutokana na maswali yangu.
Nilirejea stendi na kupanda basi lililokuwa likieleka buguruni., nikaona ni vizuri nifike nyumbani kwangu kwanza nioge, kisha nile chakula kwani toka chakula nilichokula kule Dodoma na wenzangu akina Lovenes na mr Magembe matiku sikuwa nimekula chochote hadi asubuhi hii, niliona hilo ni jambo zuri kulitekeleza kabla ya kuendelea kutafuta ufumbuzi wa masaibu niliyo kuwa nayo.
Kwani hadi wakati huo ilibidi niamini kuwa huenda mimi pengine ndio nimekumbwa na jinamizi kichwani mwangu linalo nifanya nijione nipo katika karne ya 21 mwaka elfu mbili na kumi na sita.
Hata basi lile la mjini lilikuwa ni basi la kisasa sana katika Dar es salamu hii mpya ukilinginisha na yele yetu.
Nikiwa nimezama katika bahari ya mawazo nilistushwa na sauti ya konda aliyekuwa akidai nauli yake, niliingiza mkono katika lile jacketi langu na kutoa shilingi tano na kumpa konda.
“Hii nini unanipa?” Konda aliniuliza kwa ghadhabu.
“Si nauli ama unadai nini?”
Hiyo ndio nauli? Kitu gani hicho unanipa wewe sister?” alijibu yule konda kwa ukali huku akiwa amenitolea macho yake mekundu.
Hata abiria aliyekuwa pembeni yangu pia alinishangaa, “hizo pesa za zamani sana ant hakuna anetumia tena pesa hizo we uko dunia gani” abiria wa pembeni alisema.
“Oyaa lipa nauli we sister kama huna shuka chini,.. asubuhi hii.. tusianze kutiliana nuksi time hizi” alisema tena yule konda kwa ukali. Niliendelea kustajabu mazingaombwe yale yaliyokuwa yananitokea katika maisha yangu.
Niseme tu, pengine hiki ninacho kieleza hapa wengi wenu mtafikiri ni hadithi za kubuni, lakini napenda nikwambie ndugu yangu unae soma maandishi haya, kwanza napenda uelewe kuwa uchawi upo kwani hata vitabu vyote vitakatifu vimeeleza juu ya uwepo wa uchawi, hivyo katika haya nikuelezayo hakuna neno hata moja nililoongezea chumvi katika hayo ambayo nimekwisha yaelezea, na nitakayo yaeleza yote yaliyo nitokea mimi Zahara katika maisha yangu.
Kila kitu ni ukweli mtupu, na nimeona sina namna ya kuelezea haya katika jamii na jamii ikanielewa tofauti na kutumia njia hii ya maandishi.
“Lipa pesa wewe sister” alinistua yule konda.
“Sasa kama ndio hivyo mie sina pesa” nilisema kwa upole.
“Suka eeh, zuia hapo mtu ashukie maana nisha ona naletewa za kuleta hapa” alisema yule konda akimtaka dereva asimamishe gari kisha nishushwe.
Lakini yule abiria aliyekuwa kiti cha pembeni alitoa noti mpya mchoni mwangu, noti ya shilingi elfu moja na kulipia nauli za watu wawili, zogo la mimi na konda likaisha.
Niliendelea kushangaa namna pesa ilivyokuwa haina thamani, kwenye hii dunia mpya . noti ya shilingi mia tano ni nauli ya mjini!. Pesa hiyo ilikuwa ndio posho yangu ya katikakati ya mwezi katika dunia yangu niliyotoka.
Lakini sikujali sana kwani kadri nilivyo endelea kuwa na jamii ndivyo nilivyozidi kuonekana mtu wa zamani, hali ambayo nilianza kuchukia.
Ilinichukua dakika ishirini na ushee kufika Buguruni malapa, napo huko kwa kiasi kikubwa mandhali yalikuwa yamebadilika mno, nyumba zilikuwa zimelundikana kila mahali mithili ya siafu.
Taratibu nilianza kutembea kuelekea nyumbani kwangu, nilikuwa nikitembe lakini nikiamini muda wowote lolote linaweza kutokea mbele yangu na kuibua taharuki nyingine moyoni mwangu.
*********************
 
JUMBA LA WACHAWI
Mwandishi/mtunzi; Zulfa Huseni
SEHEMU YA 14

Ilinichukua dakika ishirini na ushee kufika Buguruni malapa, napo huko kwa kiasi kikubwa mandhali yalikuwa yamebadilika mno, nyumba zilikuwa zimelundikana kila mahali mithili ya siafu.
Taratibu nilianza kutembea kuelekea nyumbani kwangu, nilikuwa nikitembe lakini nikiamini muda wowote lolote linaweza kutokea mbele yangu na kuibua taharuki nyingine moyoni mwangu.
*********************

Mbele ya macho yangu, nilishuhudia jumba bovu lililokuwa limegemea upande mmoja, uchakavu wa jumba hilo ukiwa wa kiwango kikubwa, kulikuwa na nyumba nyingi mtaa ule ambazo zilijengwa bila mpangilio mzuri wa kiramani.
Mtaa ule ulikuwa na nyumba nyingi ambazo sio nyumba bora, takataka zikiwa zimetapakaa eneo lote, kulikuwa na pitapita za watu wengi, kelele nyingi kila mahala.
Ni uswahilini.
Maeneo yaliyo kaliwa na watu wa kipato duni.
Macho yangu yaliendelea kuganda katika lile jumba bovu ambalo pengine ndio lilikuwa jumba baya na bovu katika nyumba zote zilizo kuwa mtaa ule.
Nyumba hii ndio ile nyumba iliyokuwa nyumba nzuri mtaa wote siku moja kabla ya siku hii,lakini leo ndio ilikuwa nyumba mbovu kuliko zote.
Nilipiga hatua kusogea katika nyumba ile. Kulikuwa na watoto waliokuwa wakicheza pembeni ya nyumba ile hatua chache palikuwa na bibi aliyekuwa amejilaza katika mkeka, niliendelea kusogea pale kwa yule bibi.
Moyo wangu ulikuwa ukipiga mkumbo nikiwa nimekata tamaa kwa kiwango cha mwisho,
“Shikamoo bibi..mama” nilimwamkia yule mwanamke mzee, baada ya kumfikia, hakuwa mzee sana kama nilivyo mwona kwa mbali, alikuwa katikati ya umama wa makamo na uzee.
“Marahaba mjukuu wangu hujambo” aliitikia, nilimwangalia vizuri yule bibi mama na kugundua jambo lililozidi kuustua moyo wangu, yule alikuwa ni mama mwenye nyumba wangu {mama Leila} ambaye jana kabla ya siku hii ndiye aliye nipatia namba ya mtu aliyekuwa ameokota vifaa vya ofisini kwangu vilivyokuwa katika jacket langu, mtu aliyeniingiza katika maisha ya mazingaombwe.
Jana kabla ya leo alikuwa ni mwanamke wa miaka kati ya thelathini na thelathini na tano hivi, lakini siku hii ambayo kwangu ilikuwa ni siku ya pili tangu niachane nae, tayari alikuwa ni bibi wa miaka kama sitini ama sitini na tano.
“Mama Leila kitu gani kinatokea katika maisha mbona sielewi, jana tu tumeachana ukiwa kijana, leo nakuona umekuwa mzee, nini kinatokea mama, eeh..kwanini mambo haya yanakuwa hivi,” niliuliza huku machozi yakinitoka, nguvu nazo nikihisi zinakwisha mwilini mwangu.
Yule bibi alitayahari kwa yale maneno yangu, akakaa vizuri pale mkekani kisha akanitizama usoni vizuri.
“Wewe ni nani..Za…Za..Zahara” alisema huku akinitizama kwa mshangao mkubwa. “ndio ni mimi mama Leila nimekumbwa na mambo makubwa mama..kila kitu katika maisha yangu kimeharibika..”
“Ni wewe Zahara ama mwanawe na Zahara!!..”
Yule bibi au mama Leila alizidi kuniuliza kwa mshangao…kisha akaendea kunisaili kwa maswali.
“Wewe ni Zahara huyu aliye kuwaga’ mpangaji wangu?”
“Ndio mama Leila ni mimi haswaa niliye ondoka jana baada ya kunipa namba ya yule baba aliye chukua Jacket langu lililokuwa na vitu muhimu vya ofisini.
“Hata sio wewe,..japo ulicho kisema kuna ukweli kidogo lakini sio wewe..labda useme wewe ni mtoto wa Zahara nitakukubalia..ila sio Zahara huyu niliye kuwa namjua mimi..halafu hilo unalo lisema halikuwa jana” alisema yule bibi, akionyesha wasiwasi na mimi.
Sauti moja mawazoni mwangu ikanambia, kama nisipo kuwa jasiri na imara katika kueleza ukweli juu ya mambo yaliyo nikuta kuna uwezekano wa kuonekana ni mtu majinuni.
“Mama najua kuna vitu visivyo vya kawaida vimetokea katika maisha yangu, lakini nahitaji uwe makini kunisikiliza kile nitakacho kueleza kisha nione nitapata vipi msaada dhidi ya masaibu yangu, kwanza uwe na utayari wa kunisikiliza”
Nilisema nikimkazia macho yaliyo onyesha kuwa sikuwa na mzaha na kile kilichokuwa kinatoka mdomoni mwangu.
“Hebu ngoja… kwanza twende taratibu wewe mwana,.”Alisema yule bibi akionekana kutoafikiana na mimi moja kwa moja “unasema wewe ni Zahara mpangaji wangu?”
“Ndio”
“Ulikuwa wapi miaka yote hiyo?.. Na kwanini umri wako unaonekana upo vilevile? Kama kweli wewe ni Zahara huyu nimjue mie..maaana ni miaka mingi mno imepita kama angalikuwa ni Zahara basi pengine sasa hivi ungekuwa mama wa miaka hamsini lakini.. Zahara wewe unaonekana bado mmbichi kabisa binti wa miaka ishirini na nne tu”
Alisema yule bibi maneno yaliyo niingia kabisa ndani ya mtima wangu, na kwakweli niseme tu sasa nafsi yangu iliukubali ukweli kuwa katika maisha yangu uchawi wa ajabu uliusika kusimamisha umri wangu kwa kujiona nimeishi ndani ya nyumba kwa siku moja tu, kumbe nimeishi zadi ya miaka takribani thelathini.
Nilifikiri kwa muda kidogo, kisha nikasema , “kama utakuwa tayari kunipa muda wako nieleze jambo, labda maswali yako na mashaka yako yote dhidi yangu yatajibiwa katika maelezo nitakayo yatoa kwako.”
Mama Leila aitikisa kichwa kuonyesha ishara ya kukubaliana na ombi nililo omba, nilianza kumsimulia kila kitu kilicho tokea, nilimweleza toka mwanzo tukiwa safarini tukitokea kule katika mji wa geita, nilivyo mwona yule baba ambaye hadi wakati huo sikuwa nalijiua jina lake, kusahaulika kwa jacket langu, kurejea tena dodoma na kulikosa kisha kurudi Dar na yeye kunipa taarifa za uwepo wa mtu huyo aliyekuwa akinitafuta na kisha kuingia katika masaibu mkubwa.
Hadi namaliza kueleza mama Leila alionekana kustajabishwa na mkasa huo wa ajabu kabisa, pamoja na kwamba alionekana kunielewa vema lakini bado alionekana kuwa na maswali lukuki ambayo hakujua ni kwa namna gani ayapangilie katika kuuliza.
“Kwahiyo wewe unavyo ona mwaka ule ulivyondoka hapa kumfuata huyo mtu ilikuwa ni jana usiku?” aliniuliza mama Leila akiwa amechanganyikiwa kama tu ambavyo mimi nilivyokuwa katika mkalanganyiko wa kifikra siku ile nilivyo toka nje ya jengo lile kwa mara ya kwanza na kuona mabadiliko makubwa ya mandhali yaliyotokea mbele yangu kwa masaa machache niliyokuwa mule ndani.
 
JUMBA LA WACHAWI
Mwandishi/mtunzi; Zulfa Huseni
SEHEMU YA 15

“Kwahiyo wewe unavyo ona mwaka ule ulivyondoka hapa kumfuata huyo mtu ilikuwa ni jana usiku?” aliniuliza mama Leila akiwa amechanganyikiwa kama tu ambavyo mimi nilivyokuwa katika mkalanganyiko wa kifikra siku ile nilivyo toka nje ya jengo lile kwa mara ya kwanza na kuona mabadiliko makubwa ya mandhali yaliyotokea mbele yangu kwa masaa machache niliyokuwa mule ndani.
“Ndio mama ilikuwa ilikuwa ni jana usiku.. tena usiku wa saa sita ama saba kama sikosei.. yanii kwa namna nyingine naweza nikasema ilikuwa ni usiku wa kuamkia leo ama ni leo”
Nilisema, na hapo mama Leila akazidi ‘kupalanganyika’ kwa mambo yale akatikisa kichwa kutokubaliana kabisa na jambo lile.
“Mwanangu kwanza nikupe pole sana.” Alisema Mama leila, akisita kidogo kisha akaendelea.
“kwakweli umenieleza tukio la ajabu ambalo sijawahi kulisikia katika maisha yangu yote hapa ulimwenguni, nalazimika kukubaliana na wewe kwa namna moja ama nyingine, lakini pia naweza nisikubaliane na wewe kwa upande mwingine vilevile..”
Alisema mama Leila, sikuona tena haja ya kuendelea kumfanya yule mama anielewe maneno yangu kwani kwa vyovyote vile ingemchukua muda mwingi kunisadiki.
“Sasa mama,kuna vitu nataka kujua, kitu gani kiliendelea kipindi chote ambacho ninyi mliona ni mimi sipo nyumbani kwa kipindi kirefu.” Nilisema.
“Aagh..sasa huko unako elekea ni mapema sana, kwanza nataka nijilidhishe na maelezo yako Zahara” alinidakiza, akiwa ni mwenye kutaka kuelewa mambo mengi dhidi ya yaliyo nisibu.
“Sawa mama uliza tu” nilimjibu.
“Kwanini unafikiri huyo mtu alikupeleka wewe katika hilo jumba la kichwawi na si mtu mwingine.?”
“Kwakweli hadi sasa hivi Mama Leila hilo swali bado kwangu ni kitendawili”
“Na umesema ulibakwa?” nilijibu kwa kutikisa kichwa huku taswira ya tukio lile kuingiliwa kimwili na yule baba ikijidhihilisha tena mbele yangu.
“Pole sana”
“Asante”
“Iliwezekanaje uingiliwe kimwili, muda huo huo upate mimba tena mimba kubwa na muda mchache ujifungue?”
“Hilo pia sijui, nisime tu hata mie pia sijui mambo haya yaliwezekanaje kutokea, na labda tu nikwambie siku ile hata mimi nilishangaa kama wewe unavyo shangaa sasa” nilijibu, mama Leila alifikiri kwa muda kisha akaniuliza tena.
“Kwani mwanangu uliwahi kuwa na ubaya na mtu katika maisha yako mama?”
“Kivipi mama Leila?”
“Agh..unajua Zahara katika hii dunia kuna watu wanavisasi vya ajabu usije kuwa uliwahi kukwaruzana na mtu akamua kukufanyia ushenzi huo”
Nilifikiria kidogo maneno yale lakini hata hivyo sikuwahi kuwa na ugomvi na mtu yeyote katika siku za ukubwa wangu.
“Hata sijawahi kuwa na ugomvi na mtu”
Tuliendelea kuongea mengi na mama Leila hadi kiasi fulani akawa anaamini hadithi ile ya ajabu niliyo mpa.
Ilikuwa ni zamu yake kujibu maswali yangu yote niliyo muhoji, kusema ukweli kila neno lililotoka kinywani mwake lilininyong’onyesha mno,
Alisema; “mwaka 1989 baada ya wewe kuwa umepotea katika mazingira ya kutatanisha taarifa zako zilizagaa kila kona wakati huo, kulikuwa na uvumi mwingi juu ya kupotea kwako ghafla kiasi kile,”
Aliendelea kusema; ndugu zako hususani wazazi wako walitumia muda mwingi katika maisha yako kukutafuta japo wapate hata mwili wako tu, lakini kadili siku zilivyo yoyoma ndivyo jambo hilo la wewe kupotea lilivyozidi kupotea katika vichwa vya watu wengi na kuhesabika kama ni miongoni mwa watu walio poteza maisha na mwili wako kutooneka, kila mtu anajua kuwa wewe ‘ulishakufaga’ siku nyingi tu.
Mwazoni mwa mwaka 1999 nilipata taaarifa zisizo njema kwakweli” Alisema na kunikazia macho, moyo ulikuwa ukinienda kasi, nikaelewa kuna bomu linakuja masikioni mwangu na kwenda kuupasua moyo wangu, akaendelea kusema.
“Taarifa zisizo njema, nilisikia wazee wako walifariki kwa kuangukiwa na nyumba, kutokana na mvua kubwa za alumino zilizo kuwa zikinyesha miaka hiyo..kibaya kuliko vyote..Alisema mama Leila. Akajiweka sawa pale alipo kuwa ameketi, halafu akanisogelea na kunishika bega kama ishara ya kunifariji kwa taarifa ile aliyokuwa akinipa. koo langu lilikuwa na donge zito, sikujua machozi yalinitoka muda gani kwani nilistuka tu pale matone ya machozi yalipo nichuruzika na kupenya hadi katika kinywa kilichokuwa wazi kwa mshangao wa taarifa ile, ni ile chumvi chumvi ya machozi ndio iliyonijulisha kuwa nilikuwa nikitiririkwa na machozi kwa kasi.
“Kibaya kuliko vyote..” aliendela kusema mama Leila. “yule mdogo wako uliyekuwa ukimsomesha alikuwa akiitwaje vile?”
“Nasri”
“Naaam.. Nasri.. nilipokea taarifa za kijana huyo kwakweli hazikuwa taarifa njema..yupo Gerezani anatumikia kifungo cha miaka sitini jela.,inasemekana aliua kwa bunduki..alifanya uhalifu wa kuvunja na kuua..alikuwa jambazi..mwizi..mtumia madawa ya kulevya,.bange, na petrol”
Alisema mama Leila. Kwakweli nililia sana siku ile, dunia niliiona ni kubwa mno huku mimi nikijona mdogo kama nukta..
“Inawezekanaje mtoto wa shule afanye hayo yote?” nililalamika mno, zaidi ya yote nilimlaumu yule baba mchawi kwani ndiye mtu aliye badilisha kabisa dira ya maisha yangu.
Siku ile tuliongea mengi na mama Leila na niseme tu ilifikia hatua yule mama alinielewa vema juu ya masaibu yaliyokuwa yamenikuta, na niseme pia kwa kiwango kikubwa nashukuru yule mama alionekana kunielewa kadri nilivyokuwa nikiendelea kuzungumza nae..
“Vipi kuhusu Thabit?” atimae nilimuuliza mama Leila juu ya mchumba wangu Thabit..
“unamwongeleaThabit Talib mjukuu wa marehemu mzee mwaikimba?”
“Ndio”
“Kwakweli yule kijana ni miaka mingi imepita sijamwona ila niliwahi kusikia kuwa hivi sasa yupo huko Mwanza japo sina uhakika,”
“Wakati nimepotea yeye hakuwahi kujishughulisha kunitafuta?” niliuliza, japo sikujua kwanini niliuliza swali lile.
“Hilo kwakweli sijui..sikuwahi kumwona toka ulivyo potea” alisema mama Leila.
Tangu wakati huo Sikuwa na uelekeo maalumu, sikuwa na mbele wala nyuma katika hii dunia mpya, si mashariki wala magharibi, sikuona kama ninalolote muhimu katika maisha.
******
 
JUMBA LA WACHAWI
Mwandishi/mtunzi; Zulfa Huseni
SEHEMU YA 16

“Kwakweli yule kijana ni miaka mingi imepita sijamwona ila niliwahi kusikia kuwa hivi sasa yupo huko Mwanza japo sina uhakika,”
“Wakati nimepotea yeye hakuwahi kujishughulisha kunitafuta?” niliuliza, japo sikujua kwanini niliuliza swali lile.
“Hilo kwakweli sijui..sikuwahi kumwona toka ulivyo potea” alisema mama Leila.
Tangu wakati huo Sikuwa na uelekeo maalumu, sikuwa na mbele wala nyuma katika hii dunia mpya, si mashariki wala magharibi, sikuona kama ninalolote muhimu katika maisha.
**********************

Nilikuwa nikiishi nyumbani kwa mama Leila yapata wiki, pale katika ile nyumba yenye kuegama’ upande mmoja.
Nilikuwa ni msichana mgeni kabisa katika jamii ile mpya, hata wale watu wachache waliokuwa wakinifahamu wengi wao hawakuwa tayari, kuamini kama mimi ndiye yule Zahara waliye mfahamu toka miaka ile, wengi wao kama sio wote waliamini kwa vyovyote vile mimi ni mtoto wa Zahara.
“Mtoto wa marehemu Zahara anafanana na mama yake vilevile” mtu mmoja wa zamani alikuwa akiongea na mwenzake mtaani nilikokuwa nikikatiza.
“Huyo binti mwenyewe anaitwa Zahara na nasikia anadai yeye ndiye Zahara”
“Binti huyo anajitia umajinuni Zahara hawezi kuwa yeye, Zahara alikwisha fariki miaka mingi mno toka mwanzoni mwa mwaka themanini na tisa”
Yalikuwa ni maneno niliyowahi kubahatika kuyasikia, kila mtu alikuwa akisema lake juu yangu kadri alivyo weza kunijua.
Nilikuwa ni msichana wa miaka ishirini na nne tu, nilikuwa ni mtu mshamba katika mambo mengi mno, kila kitu katika maisha yangu kilikuwa kipya.
Sikuwa mimi tena yule mwandishi wa magazeti maalufu hapa nchini, gazeti nililokuwa nikiandikia halikuwepo kabisa katika ulimwengu wa magazeti.
Nilikuwa ni binadamu mpweke, marafiki ndugu na jamaa wengi wao niliwapoteza miaka mingi.
Nilikuwa nikimsaidia kazi za kuuza chakula mama Leila. Kila mara nyakati za usiku tulikuwa tukibeba meza majiko na vyombo kisha tunauza chakula gengeni.
Siku moja tulikawia kidogo kumaliza kuuza biashara, ilikuwa yapata kama saa tano kasoro za usiku, siku hii biashara haikuwa nzuri sana.hivyo kutokana na muda kuwa umekwenda ilitubidi tufunge na kurejea nyumbani.
Kwakuwa usiku ulikuwa umekwisha kuwa mkubwa moja kwa moja tulifikia kitandani na kulala.
Wakati nimekwisha pitiwa na usingizi, kwa mbali nilikuwa nikisikia sauti ya mtoto mchanga ikilia, ilinijia kama ndoto, lakini nikagundua haikuwa ndoto muda wote ilikuwa ikitengeneza karaha kichwani mwangu, nikafumbua macho kivivu nikihisi huenda alikuwa ni mtoto nyumba ya jirani aliyekumbwa na masaibu ya kuto kulala usiku ule.
Lakini nilistuka nilipo gundua sauti ile haikuwa inatokea nyumba ya pili kwa jilani, isipokuwa sauti ile ilikuwa inatokea chumba cha pili mule mule ndani.
Sasa vipi sauti hii ya mtoto itokee ndani ya nyumba ile wakati,ndani ya jumba lile tulikuwa tukiishi wawili tu!. Niliwaza.
Sauti ile ilizidi kulia kwa kasi, nilipatwa na mashaka na woga mkubwa, nilianza kumwamsha mama Leila aliyekuwa akikoroma.
“Mama Leila, we mama Leila” nilimwita huku nikimtikisa, ajabu ni kuwa mama Leila alikuwa akiendelea kukoroma na kutoonesha dalili za kuamka.
Na nilivyokuwa nikizidi kumwamsha mama Leila kwa nguvu ndivyo sauti ya mtoto ilivyozidisha kasi ya kulia.
Sasa nikawa natetemeka na jasho likinitoka kwani niliona dhahili mazingaombwe mengine yanakaribia maisha yangu. Niliona hilo ni tukio jingine ambalo linakuja katika maisha yangu na pengine ni tukio litakalo badilisha tena maisha yangu japo sikujua safari hii maisha yangu yatakuwa katika hali gani.
Mara sauti ya kichanga ilinyamaza ghafla, halafu muda huo huo vikafuatia vicheko vingi.Yanii ilikuwa ni kana kwamba wale watu walikuwa wakinicheka mimi kutokana na namna nilivyokuwa na woga na wasiwasi uliotokana na kusikia sauti ya yule mtoto akilia.
“Ninyi ni akina nani?” nilisema kwa sauti kali ya kushurutisha.
Vicheko vikanyamaza na kukawa kimya, yanii kimya cha ghafla kama vile hakukuwa na vicheko. “Ninyi ni akina nani..eeh?” nilirudia tena kuuliza kwa ukali baada ya kuwa kimya.
Kimya kingine..
Sikusikia chochote wala chakara chakara yoyote, nilitega sikio kwa makini nikitegemea kusikia labda minong’ono ya wale watu lakini kulikuwa na ukimya wa ajabu, ukimya ambao hata sisimizi angetambaa chini ungeweza kumsikia, hali ya ukimya usiku ule ulikuwa ni eneo lote la mtaa ule wa buguruni malapa.
Niliogopa sana, kwa muda wa dakika sita hadi kumi, nilibaki nimekaa pale kitandani nikitegemea kusikia chochote wakati wowote, lakini muda ulizidi kwenda bila kusikia chochote.
“Inamaana hawa walozi wananiogopa ama?” niliwaza.
Wakati huo mama Leila alikuwa akiendelea kukoroma. “Hii hali si ya kawaida vimbweka vyote hivi mtu anakoroma kama amekufa!”
Baada ya kukaa kitako kitandani kwa muda mrefu pasina kusikia kituko chochote, niliamua kulala, wakati huo ilikuwa yapata saa saba na madakika za usiku.
Nilijilaza huku nikifikiria suluhu ya matatizo haya yaliyokuwa yananiandama katika maisha.
Nikiwa pale kitandani usingizi ukiwa umegoma wasiwasi ukiwa mwingi mara nikasikia kitu kingine, nilisikia sauti kama ya moto, tena moto mkubwa unao waka kwa kasi, moto ule ulikuwa ukiwaka nyumba ya pili.
Nilikurupuka pale kitandani na kuwasha mshumaa, kisha nikasogea katika dilisha na kufungua kisha nikatupa macho nje.
Sikuamini nilicho kiona moto mkubwa ulikuwa ukiwaka katika nyumba ya jirani, nyumba ile ilikuwa ikiungua kwa kasi kubwa.
 
JUMBA LA WACHAWI
Mwandishi/mtunzi; Zulfa Huseni
SEHEMU YA 17

Nilikurupuka pale kitandani na kuwasha mshumaa, kisha nikasogea katika dilisha na kufungua kisha nikatupa macho nje.
Sikuamini nilicho kiona moto mkubwa ulikuwa ukiwaka katika nyumba ya jirani, nyumba ile ilikuwa ikiungua kwa kasi kubwa.
Na mara nikasikia sauti nyingi kutokea nje “moto, moto, moto,moto” sauti za watu wengi zilikuwa zikipiga kelele.
Ule moto ulikuwa ukiwaka kuelekea katika nyumba yetu, niliogopa mno, na hapo nikarejea kitandani na kumwamsha mama Leila kwa nguvu zaidi, lakini mama Leila hakuamka, alikuwa ni kama mtu aliye kunywa pombe nyingi mno na kuwa hajiwezi. Nilichukua maji ya baridi na kumwagia ili amke na tutoke nje ya nyumba ile ili kuokoa maisha yetu kwa kuungua na moto uliokuwa unawaka kwa kasi kuja nyumbani kwetu.
Lakini wapi, mama Leila hakuamka.
Akili yangu ilifanya kazi upesi upesi, niliona ni vema nitoke nje nikaombe msaada kwa watu waje kumtoa nje mama Leila hata kwa kumbeba ili kuokoa maisha yake kutokana na moto uliokuwa ukiwaka kuja katika nyumba ile.
Nilifungua mlango na kutoka nje.
Lakini ile natoka tu nje, sikuamini macho yangu, ajabu ni kuwa hapakuwa na kitu kile nilichokuwa nakiona wakati nimo mule ndani.
Hapakuwa na moto uliokuwa ukiwaka na kuchoma nyumba, na hata zile sauti zilizo kuwa zikisema “moto, moto moto” HAZIKUWEPO TENA.
Pale nje palikuwa hakuna mtu hata mmoja kulikuwa kimya na eneo lile lilikuwa shwari kabisa.
Nilihisi mwili ukinisisimka kwa kituko kile, nilijikuta nikiwa nimeduwaa huko hofu kuu ikiwa kifuani mwangu, mate mepesi yalinijaa mdomoni na hapo nikajikuta napiga kelele nyingi na kupiga hatua kubwa kurejea ndani.
Nilipo ufikia mlango wa kuingia ndani nilipo usukuma, haukufunguka, nikasukuma tena kwa nguvu lakini ulikuwa mgumu, ulifungwa kwa ndani, haukufunguka.
Na wakati huo huo nikasikia vile vicheko vya awali vikitokea mule ndani.
Niliendelea kutishaka pasina kifani.
Sasa nikawa sielewi, aidha niingie ndani ambamo kuna viumbe visivyo onekana ama nibaki pale nje.
Jibu rahisi likaja, ni kheri kubaki pale nje kuliko kuingia mule ndani ambamo kuna viumbe wa ajabu tena wasio onekana, wenye kutia wasiwasi na mashaka, lakini bado hofu yangu ilikuwa juu ya mama Leila aliyekuwa akikoroma mule ndani, sikujua nini hatma ya uhai wake mule chumbani ndani ya lile jumba.
Nilisogea hatua kadhaa kutoka pale mlangoni vile vicheko kutokea mule ndani nikawa navisikia kwa mbali na badae kidogo vikayeyuka.
Nikiwa pale nje nikawa nasogea katika ukuta wa jumba lile la mama Leila,nikawa ukingoni kabisa mwa ukuta ule, nikajikunyata, umeme wa tanesko uliokuwa ukiwaka wasaa ule mara ukakatika, na kufanya kuwa na giza zito, giza jeusi, nilizidi kuogopa lile giza kwakweli sikujua nikimbile wapi, moyo wangu haukuwa tayari kurejea mule ndani usiku ule.
Nikaendelea kujikunya nyuma ya jumba lile katika ukuta, joto siku hii lilikuwa ni kubwa usiku ule. Kwa wakazi wa Dar wanaelewa hili.
Nikiwa pale ukutani, mbu walikuwa wakinishambulia vibaya mno.
Bado mashaka yangu yalikuwa makubwa dhidi ya mama Leila mule ndani japo zile sauti sikuzikia tena kutokea ndani.
Kukawa na kiupepo kidogo, joto likapungua kiasi, kiupepo kile kikaongeza kasi ya kuvuma, na joto nalo likawa linapungua, hata mbu pia wakapunguza kasi ya kuniuma.
Ule upepo ulio anza kuvuma kama mzaha ukawa upepo mkubwa ukawa unapeperusha takataka nyingi mtaani na kuzisukuma hovyo, mapaa ya nyumba za uswahilini yalikuwa yakilalama kutokana na kuzongwa na upepo ule.
mimi niliendelea kujikunyata katika ukuta wa lile jumba.
Machozi yalikuwa yakinitoka na kulia, nilia sana kwa uchungu, sikujua nilimkosea nini Mungu katika maisha hata kukumbwa na mambo yale.
Kila kilichokuwa kinatokea katika maisha yangu kilibakia kuwa kitendawili ambacho sikujua nani wa kunitegulia.
Nilijiona ni mtu mwenye mkosi mkubwa katika maisha, siku zote niliamini Mungu ndiye mtatuzi wa mitihani yote migumu kwa waja wake. Bahati mbaya kuliko zote nilizowahi kuwa nazo katika maisha, sikuwa ni mtu mwenye kumcha Mungu.
Sikumbuki mara ya mwisho kumsujudia Muumba wangu ilikuwa mwaka gani, hili halina maana kuwa sikuwa na dini ama kuamini katika uwezo wa Mungu lahasha.
Isipokuwa ni kule kujiweka mbali na Mwenyezi wangu, kwani pamoja na mambo yote hayo bado sikuwa na misingi ama njia na taratibu sahihi ya kumuomba Mungu wangu kama ambavyo alivyo amrisha katika vitabu vyake vitakatifu.
Mara ule upepo uliokuwa unavuma ulibadilika na kuwa kimbunga..kimbunga kilichokuwa kinavuma kwa kuzunguka, kilikuwa kikizunguka kuja katika uelekeo nilikuwapo mimi.
Niliendelea kujikunyata, nikiwa naogopa mno hali ile, usiku ule ulikuwa ni usiku mwingine wa kutisha na kuogopesha.
Kile kimbunga kilifika eneo lile nililokuwa nimejikunyata na kuvuma kwa kasi mbele yangu.
Hata vile vitu vilivyokuwa vikizungushwa na kimbunga kile vilikuwa vikizunguka kwa kasi kama pangaboi .
Hakikuwa kimbunga cha kawaida, hilo nililielewa, nikiwa nimejikunyata niliangalia vizuri mbele ya kile kimbunga japo kulikuwa na giza lakini niliweza kuona kiumbe kilichokuwa katikati ya kimbunga kile.
“Uwiiii, mamaaa ,ooooiii” nilipiga kelele nyingi nikiwa nimetoa macho najiburuza kwa makalio kurudi nyuma, mkono wangu nikiwa nimeiweka mbele kuzuia kile kiumbe nilicho nilicho kiona, huku mkono wangu mwingine nikiwa nimeziba mdomo, macho yenye mshangao na hofu kubwa yamenitoka pomoni.
Kilikuwa ni kiumbe cha kutisha mno, alikuwa ni kama kichwa cha nyati, huku umbo lake likiwa kama la ndege popo, alikuwa na rangi nyekundu umbo lake lote, Macho yake yalikuwa makubwa kama bundi huku zile mboni za macho yake zikiwa zinamg’ao wa rangi ya dhahabu.
Na kadri nilivyokuwa nikijiburula pale chini ndivyo kiumbe yule alivyokuwa akipiga hatua ndogo kunisogolea akiwa katikati kimbunga kile, kwa hiyo hapo unaweza kuwa umeelewa, yanii kadiri nilivyokuwa nikijongea nyuma ndivyo kile kimbunga kilivyokuwa kikinisogelea taratibu.
 
JUMBA LA WACHAWI
Mwandishi/mtunzi; Zulfa Huseni
SEHEMU YA 18

Na kadri nilivyokuwa nikijiburula pale chini ndivyo kiumbe yule alivyokuwa akipiga hatua ndogo kunisogolea akiwa katikati kimbunga kile, kwa hiyo hapo unaweza kuwa umeelewa, yanii kadiri nilivyokuwa nikijongea nyuma ndivyo kile kimbunga kilivyokuwa kikinisogelea taratibu.
Nikafika mwisho wa kona ya ukuta ule sasa nikawa sina eneo la kusogea, yule kiumbe akazidi kunikaribia nilikuwa nikilia kama mtoto, nilijikojolea.
Niligundua kitu kingine kwa yule kiumbe, alikuwa na miguu kama ya binadamu lakini katika kiganja cha mguu alikuwa na kwato kama za ng’ombe.
Mikono yake ilikuwa ya binadamu lakini yenye manyoya mengi na kiganja kikubwa. “uwiiiii” nilipiga ukelele kubwa, akili yangu ilinambia kuwa jini alikuwa mbele yangu.
Yule kiumbe aliniangalia kwa macho yake ya kuogopesha, mimi pia nikabaki nikiwa nimekodoa macho mbele ya kiumbe yule na kuwa kama mtu aliyenata katika lundo la ulimbo.
Mara nikasikia sauti fulani niliyo wahi kuisikia mahala fulani, ulikuwa ni wimbo usio kuwa na maana ninayo weza kuielewa, na hata wakati ile sauti inaendelea kupenya masikioni mwangu nikawa nahisi nazongwa na hali fulani ya kupoteza fahamu.
Ni hapo nilipo kumbuka kuwa sauti ile nilipata kisikia katika lile jumba la ajabu kule mjini, Agrey Kariakoo.
Nikazidi kuelekea kuzama katika kina kirefu cha bahari ya usingizi.
Sikuwa tayari kwa hilo, nikakumbuka mbinu niliyo itumia kuepukana na ile sauti ya ajabu,
Hapo nikasokomeza vidole masikioni mwangu, nikiziba masikio sauti ile isipenye ndani ya kichwa changu.
Wakati napambana na tendo lile yule kiumbe alikuwa akinitizama huku sura lake baya likiniangalia kwa hasira kubwa.
Sasa kukawa hakuna ninacho kisikia zaidi ya kuona yale yalikuwa mbele yangu.
Upepo wa kimbunga uliendelea kuvuma kwa kasi na kadiri nilivyokuwa nikiziba masikio yangu ndivyo upepo ulivyokuwa ukiongeza kasi ya kuvuma, na yule kiumbe akitizima kwa jicho kali la hasira.
Lakini wakati vile vituko vinaendelea kutokea mara nilistuka nilipo mwona mama leila akitokea nyuma ya nyumba ile.
“Wee Zahara” aliniita huku akinitizama kwa mshangao. Nilipo mwona nilijiburuza pale huku nikijiweka mbali na yule kiumbe kusogea mahala alipo kuwa amesimama mama Leila.
Wakati nafanya matukio hayo mama Leila alishikwa na mshangao mkubwa juu yangu, alionekana ni mtu mwenye kutahayari huku maswali yakiwa mengi kichwani mwake.
Hapo nikagundua jambo moja, ama mawaili, kwanza mama Leila hakuwa anamwona yule kiumbe aliyekuwa mbele yangu, pamoja na kwamba kulikuwa na kimbunga kilicho kuwa kikizunguka kwa kasi hatua chache mbele yangu.
Lakini jambo la pili nilielewa kuwa mama Leila alikuwa na maswali mengi juu yangu, vipi usiku ule mkubwa, usiku wa giza niwe nje kama mwanga, lakini vipi niwe ni mtu mwenye mashaka woga na wasiwasi kama mtu aliye ona jini mbele yake.
“We Zahara una nini? Mbona hivyo? na mbona huku sasa usiku huu?”.
Sikujibu lolote, isipokuwa nilijikuta nikipiga ukelele wa hofu na kusimama kiwazimu kisha nikatoka mbio kuelekea pale alipo kuwa mama Leila.
Kitendo kile, kilimwogopesha mama Leila yeye pia aligeuka na kukimbilia ndani, alisukuma mlango wa ndani na kujichoma ndani hatua chache nyuma mimi pia linijitoma ndani kwa kasi kisha tukashindilia komeo kwa ndani.
Tukawa tunahema kwa zamu huku mashaka makubwa yakiwa ndani yetu.
“Nini kimetokea?” mama Leila alihoji.
“Hata sijui..ila ni majini..humu ndani kuna majini na wachawi?”nilisema kimajinuni.
Mama Leila hakunitizama ila alisikiliza kauli yangu kisha akatikisa kichwa kunikatalia. “Hayo majini humu ndani yameingia lini..miaka nenda rudi sijawahi kuona japo unyoya sasa mimi sikuelewi kwakweli Zahara”
“Mama Leila nimekuamsha mno ila hukuweza kabisa kuamka, vituko vilivyo tokea humu ndani leo si vya kawaida” nilisema, japo uso wa mama Leila alionekana kuanza kujutia uamuzi wa kuishi na mimi ndani ya nyumba yake, uso wake ulizungumza zaidi ya kinywa chake.aliona kama mimi nimemletea mabalaa nyumbani kwakwe.
Tulibaki kimya kila mtu akiwaza lake, huku ule mvumo wa upepo huko nje ukiwa umepotea.
“Nimeona kimbunga kikivuma kwa kasi mbele yako nini maana yake? Na kwanini muda huu ukawa nje?” mama Leila aliniuliza.
Nilimweleza kila kitu kilivyo kuwa usiku ule, tangu vile vituko ndani ya nyumba kutokea chumba cha pili,moto kuwaka nyumba ya jirani na kisha kile kimbunga cha ajabu.
Ilikuwa ni habari ya kutisha kwa mama Leila lakini bado ilikuwa ni kama hadithi ya kufikirika kwa upande mwingine.
“Labda naweza kukuelewa kwa huo upepo kwakuwa nimeuona lakini nashndwa kuelewa maelezo yako kuhusu hiki chumba cha pili ulicho sema kuna sauti ya mtoto mchanga na vicheko, hii ni stoo na humo hakuna vitu vingi zaidi ya makorokoro yasiyo na kazi..”
Nilinyamaza kwakuwa sikujua namna ya kuendela kueleza.
“Haya mambo ya kiswahili tuwapelekee waswahili mwanangu au unaonaje?” alisema mama Leila baaada ya kifiri kwa muda wa nukta kadhaa.
“Sijaelewa mama”
“Ninamaana kuwa kesho kukicha twende kwa mtaalamu huko bagamoyo.”
Niliifikiri rai hiyo, nikaona siyo wazo baya wala siyo wazo zuri.
Baya lisilokuwa na madhala ni jema lisilo na faida, niliamini hivyo, nikalala kuisubiri kesho.
*************

Siku iliyofuatia alikuwa mama Leila aliyeanza kuamka.
“Zahara” aliniamsha.
“Abee ma..ma” niliitika usingizi ukiwa bado machoni mwangu.
“Sasa mie itabidi nizungukie madeni yangu, ili tupate senti kidogo tutakayo iacha huko kwa mtalamu tuendako, maa na humu ndani sent iliyopo haitoshi.”
Alisema mama Leila kisha akaondoka. mie nilibaki pale nyumbani nikifanya usafi wa nyumba na mwili wangu mwenyewe. Si unajua mwanamke mazingira, Saa saba juu ya arama mama Leila alirejea.
“Pesa imepatikana mwanangu lakini safari ya bagamoyo itabidi iwe kesho maana sasa hivi muda umekwenda mno na hili foleni la Dar tunaweza kufika huko saa tatu usiku.” Alisema huku akiangalia saa ya kwenye simu yake na muda ulionyesha ilikuwa ni saa saba mchana.
“Mie sina neno mama Leila, chochote usemacho ni sawa tu”. Nilisema, na atimae tukakubaliana kesho ndio iwe siku ya safari.
Siku hiyo hatukwenda kuuza chakula usiku gengeni kwani hatukuwa tumetayarisha chochote.
 
JUMBA LA WACHAWI
Mwandishi/mtunzi; Zulfa Huseni
SEHEMU YA 19

Alisema huku akiangalia saa ya kwenye simu yake na muda ulionyesha ilikuwa ni saa saba mchana.
“Mie sina neno mama Leila, chochote usemacho ni sawa tu”. Nilisema, na atimae tukakubaliana kesho ndio iwe siku ya safari.
Siku hiyo hatukwenda kuuza chakula usiku gengeni kwani hatukuwa tumetayarisha chochote.
Nilitumia muda mwingi kuwaza maisha yangu, mambo mengi yaliyo pita katika kichwa changu yaliniumiza mno.
Uhai wangu ulikuwa nusu duniani nusu kuzimu,.niliishi maisha ya dhiki japo kitaaluma nilikuwa mwandishi wa habari.
Usiku ulipo ingia muda wote nilikuwa nikifikiria safari ya kwa mganga huko bagamoyo, bado sikuwa na uhakika kama kuna binadamu anaeweza kuwa na uwezo wa kuzuia viumbe vilivyokuwa vimezingira maisha yangu.
Ulikuwa ni usiku mwingine nikiutafuta usiingizi, huku tumaini langu likiishia mikononi mwa mganga tutakae kwenda kumwona kesho huko wilayani bagamoyo mkoa wa pwani.

*************

Asubuhi ya siku iliyofuatia, tuliamka mapema na kupata staftahi ya chai na maandazi kisha tukajiweka vema na safari ya kuelekea bagamoyo ikaanza.
Tulipanda basi hadi makumbusho kituo kipya cha mabasi ya mjini awali ikiwa pale mwenge, hapo tukachukua gari jingine na sasa tukaanza safari ya kuelekea bagamoyo kwa mganga wa kienyeji.
Siku hii ya juma pili hakukuwa na foleni kubwa kwa muda wa nusu saa tulikuwa tumekwisha pita tegeta na sasa tulikuwa tukiitafuta bunju.
Mita kama hamsini mtu mmoja aliyekuwa na gari lake dogo, akionekana kama ni mtu aliye haribikiwa na usafiri wake, alilipiga mkono basi letu dogo aina ya costa.
Mvulana yule aliingia ndani ya basi kisha safari ya kuelekea bagamoyo ikaendelea.
Tulipo fika Kituo kimoja mbele abiria aliyekuwa ameketi siti moja na mimi aliteremka, na yule kaka aliye panda basi akiwa ameharibikiwa na usafiri wake njiani aliketi katika siti.
“Habari yako ant?” alinisalimia. Hata sauti yake ilipo toka kinywani mwake tumbo langu lilipuka na moyo wangu ukapata mstuko, nikajaribu kuikumbuka ile sauti niliwahi kuisikia mahala gani.
“Mambo vipi ant?” yule mtu alinisalimia tena
Nilikuwa kama mtu aliyepigwa nusu kaputi,nikabaki nimemkaodolea macho yule mtu.
“Wewe ni Thabit Talib?”
“Nani…mimi?”
“Ndio”
“Hapana..ila mzee Thabit Talib ni baba yangu mzazi.
Umemjua vipi baba yangu”
Yule kijana alisema, Tumbo lilipata joto nikawa nahema kwa kasi, lakini wakati nafikiria maneno ya yule kijana tulikuwa tumefika katika kituo cha kijiji cha msata bagamoyo, na hapo ndio ilikuwa kituo anacho shukia yule kijana.
“Any way, tumejuana juu juu..lakini labda siku moja tutafahamiana zaidi,..shika hii”alisema huku akitoa kadi yake ya biashara iliyokuwa na mawasiliano yake na kunipatia, kisha yeye akateremka katika gari.
Nilibaki katika gari nikitafakari lile tukio na kuona ni kama mkanda wa sinema unaopita katika maisha yangu.
Tuliendelea na safri na mwendo wa kilometa kadhaa tukawa katika mji wa bagamoyo.
Tulivyo shuka katika gari nilimweleza mama Leila juu ya kukutana na mtoto wa Thabiti mvulana aliyekuwa mchumba wangu wa zamani.
Mama leila pia alishangaa sana, lakini hatukuwa na namna ya zaidi ya kuacha maisha yaende kama yalivyo.
Tulitembea mwendo kiasi sikumbuki ni eneo gani mama Leila alinipeleka pale Bagamoyo lakini ninacho kumbuka safari yetu ilishia katika kijumba kidogo cha makuti kilicho zingirwa na wigo mkubwa wa fensi ya mifenesi.
“Karibuni jamani karibuni..”
Tulikaribishwa na kijana wa miaka kati ya ishirini na nne ama tano, alikuwa mchangamfu mdada mzuri na mrembo wa kuvutia lakini uzuri wake ulipotezwa na matunzo duni aliyoyapata katika maisha yake.
“Asante ..asante sana” mama Leila aliitikia huku tukiketi katika mkeka mkubwa uliokuwa chini ya mti wa mpogopogo.
“Haya mtalaamu tumemkuta?”
“mmh..hapana kaenda musikitini ila ndio mida yake hii”
Alisema yule mdada chaurembo asiyekuwa na matunzo.
Tulikaa kumngoja mtalaamu na baaada ya kama ya nusu saa alirejea babu akiwa katika kanzu nyeupee.
“Mwenyewe huyoo anakuja” alisema yule dada chaurembo, na wote tuligeuza kichwa kumtizama.
Alikuwa ni mzee wa miaka kati ya sitini ama sabini, alijikongoja taratibu kuja usawa wa pale mkekani tulipo kuwa tumeketi.
Alipo karibia mita kama kumi na mbili kutoka pale mkekani, mara alisimama ghafla na akabaki ameduwaa huku macho ya uwaoga amenitumbulia, akawa anatetemeka huku ngurumo fulani ya vitu kama maruhani ikawa inamtoka.
“Weweeee!” alisema kwa mshangao akinisonta na kidole.
Kila mtu aliyekuwepo pale alibaki na taharuki kuu, hata yule dada niliye mpachika jina la chaurembo aliogopa.
“Umebeba viumbe wabaya na hatari mnoo sogea mbali na eneo hili upesi..tokaaa..nasema tokenii hapa!.”
Yule mganga alifoka akinitizama kwa hofu na mshangao akawa ananifukuza.
Niliendelea kushangaa kile kituko huku yule mganga akiendelea kunitaka nipotee upesi eneo lile.
Hatukuwa na namna zaidi ya kuondoka haraka pale kwa mganga, lakini si mimi wala mama Leila kila mtu alikuwa na hofu kubwa moyoni mwake.
Na hata nilivyokuwa nikimwangalia mama Leila nilimwona kabisa kuwa alikuwa akiniogopa mno.
“Sasa nikwambie kitu Zahara” alisema Mama Leila akitoa noti mbili za shilingi elfu kumi na kunikabidhi
“Niambie tu mama Leila”
“Naomba uniwie radhi sana kwa hili ninano kwenda kuliamua kwa sasa”
“Lipi hilo?”
“Kwakweli siwezi kuishi na wewe zaidi, niwe tu mkweli ndugu yangu, kwa sasa nakuogopa, kama mtaalamu ninaye mwamini ile kukuona tu kashindwa hata kusikiliza tatizo letu kwa vitu ulivyo navyo mwilini mwako
 
JUMBA LA WACHAWI
Mwandishi/mtunzi; Zulfa Huseni
SEHEMU YA 20

“Niambie tu mama Leila”
“Naomba uniwie radhi sana kwa hili ninano kwenda kuliamua kwa sasa”
“Lipi hilo?”
“Kwakweli siwezi kuishi na wewe zaidi, niwe tu mkweli ndugu yangu, kwa sasa nakuogopa, kama mtaalamu ninaye mwamini ile kukuona tu kashindwa hata kusikiliza tatizo letu kwa vitu ulivyo navyo mwilini mwako.
Vipi mimi niweze kubeba matatizo haya kiasi hicho, kwakweli ndugu yangu siwezi?”
“Sasa mama Leila kama wewe ukiamua pia kuniacha wapi pawe kimbilio langu, kumbuka matatizo haya niliyo nayo sijapenda mie kuyapata.
Lakini pia kumbuka kwa sasa sina sehemu yoyote ni nayo weza kusema nitakwenda kuishi zaidi ya kwako mama Leila…tafadhali” nilisema kinyonge huku kamasi na machozi vikinitoka kwa pamoja.
“Pole lakini sina wazo tofauti zaidi ya hilo nililokwisha amua, nafsi ya uhai wangu ni muhimu kuliko kitu chochote Zahara.. nasikitika sana lakini sina jinsi”
Alisema mama Leila, kisha akasimamisha bodaboda na kumtaka dereva ampeleke stendi ya mabasi ya Makumbusho.
Kwa Muda wa dakika tano nilibaki nimebunga’aa pale barabarani nikiona maisha yangu hayana thamani hata kidogo.
Mfululizo wa matukio ya ajabu yaliyokuwa yakinitokea katika maisha yangu yakawa yanapita katika fikra zangu mithili ya mkanda wa filamu.
Nilifikiria kwa muda kisha nikaona sina namna zaidi ya kurejea Dar ili kuona kama nitaweza kumshawishi mama Leila ili aendelee kunipa hifadhi nyumbani kwakwe nikiwa natafuta ufumbuzi wa masaibu yangu.
Nilifika jioni Buguruni, na nilipo fika nyumbani kwa mama Leila sikumkuta, zaidi ni kuwa nilikuta begi dogo lililokuwa na nguo zangu chache likiwa limewekwa pale mlangoni huku mlango ukiwa umefungwa kwa kufuri kubwa.
Hali hiyo ilimaanisha mama Leila hakuhitaji kabisa kuendelea kushi na mimi pale nyumbani kwakwe.
Nilishusha pumzi ndefu huku nikijaribu kufikiria wapi pa kwenda jioni ile.
Nilibeba lile begi la nguo na kuondoka pale kwa mama Leila.
Kwa mujibu wa saa yangu ya mkononi ilikuwa yapata saaa moja za jioni, giza lilikuwa limekwisha funika nuru ya jiji la dar es salam, nikawa nazipiga hatua kuelekea mjini, japo sikujua uelekeo ule hatma yake itakuwa ni wapi ila niliendelea kujisukuma kwa mbele vitendawili vingi katika maisha yangu vikiwa vimezingira ufahamu wa akili zangu.
Kufumba na kufumbua nikajikuta nimefika mitaa ya jangwani, hapo nikastuka na akili yangu ikarudi kufikiria cha kufanya zaidi juu ya hatma ya maisha yangu kwa usiku ule wa siku hiyo.
Nikawa mbele ya viwanja vya jangwani, katika nyasi kavu nikaketi kitako huku macho yangu yakielekea angani na kutizama nyota na mwezi huku nikiwa na wivu dhidi ya nyota zile, nikaona bora ningekuwa nyota pengine ningekuwa na furaha na maisha kuliko kuwa binadamu nisiye na mbele wala nyuma huku mitiahani mizito ikiwa imechukua nafasi kubwa katika maisha yangu.
Wakti nikiwa katika mawazo yale mara nikajikuta nazungukwa na wavulana kama sita watatu kati yao wakiwa na panga na visu.
“Leta begi hilo” mmoja alisema akinisogelea na kukwapua lile begi langu la nguo.
Mara moja nikaelewa wale walikuwa ni wezi.wakati sijajua nifanye nini mwingine alinifikia na kunipokonya ile pesa niliyokuwa nimepewa na mama Leila.
Lakini nilipo taka kupiga kelele nilijikuta napigwa vibao vikali na kutakiwa kutulia kama maji ya mtungini.
Walipo ona wamemaliza kuninyang’anya kila kitu hawakuniacha hivi hivi.
Wakanipiga na kunitaka nivue nguo zangu zoote huku kila mmoja akionekana kutaka kunibaka.
“Hapana kaka zangu msinifanyie hivyo ni dhambi kwa Mungu kunifanyia hivyoo”
“Unazijua dhambi wewe., hebu toa hicho kichupi chako upesi kabla sijakucharanga na panga sasa hivi”
Jamaa alisema kwa ukali macho yake mekundu yaliyo athiriwa na bange yaliniogopesha sana.
Nilivua lakini siku tayari kuona nafanya mapenzi na vijana wale wahuni.
“Sasa mnaonaje kama mkifanya kwa hiyari yangu kuliko kuniingilia kwa nguvu?”
“Ni wewe tu utakavyo amua, ukipenda ukubali kwa hiyari yako na utukatie mauno na ukipenda ukomae kama gogo ni wewe na roho yako sisi tunacho taka ni uroda tu”
“Sasa naombeni msinikabe kwa nguvu mtafanya mapenzi na mimi kwa zamu hadi hamu yenu iishe” nilisema kwa kwa sauti ya kubembeleza na huruma kidogo.
Hata nilipo pata kusema hayo jamaa watatu katika wale sita wakaonekana kugutuka kidogo kutokana na rai ile.
“Oyaa masela kama vipi tujikatae huyu demu inawezekana ana moto, vipi akubali kirahisi hivi tena bila hofu kufanya mapenzi na sisi sote kwa zamu?”
Jamaa mmoja alisema akimaanisha inawezekana kuwa nikawa na ukimwi hata nikakubali kufanya nao mapenzi kwa zamu ili pengine na mimi niwaambukize huo ukimwi.
“Eti wee una ukimwi?”
“Kusema ule ukweli sitaki kuwaongepea kaka zangu,. Mimi kweli nina ukimwi, naishi na ukimwi huu mwaka wa pili sasa”
Nilisema kwa kujiamini nikiona ile fikra ya yule jamaa hakika ndio njia pekee ya kujinusuru na tatizo lile la kutaka kubakwa na wale wahuni.
Lakini baada ya kusema hilo nikidhani wale jamaaa wataniacha na kuondoka zao lakini kilicho tokea huwezi kuamini mpenzi msomaji.
Nilikutana na kipigo cha haja kutoka kwa wale vijana wa kiume nilipigika hadi nikahisi safari ya kuelekea kuzimu inaninyemelea.
“Fala wewe unataka kutuaa kwa ngoma kirahisi hivyo.” Nilisukumiziwa teke la tumboni na kutoa mguno mkali hapo hapo jamaa mwingine alinilapua konde la usoni na kunipasua mdomo huku damu zikawa zinanitoka puani na mdomoni.
 
JUMBA LA WACHAWI
Mwandishi/mtunzi; Zulfa Huseni
SEHEMU YA 21

Nilikutana na kipigo cha haja kutoka kwa wale vijana wa kiume nilipigika hadi nikahisi safari ya kuelekea kuzimu inaninyemelea.
“Fala wewe unataka kutuaa kwa ngoma kirahisi hivyo.” Nilisukumiziwa teke la tumboni na kutoa mguno mkali hapo hapo jamaa mwingine alinilapua konde la usoni na kunipasua mdomo huku damu zikawa zinanitoka puani na mdomoni.
****************

Ta, ta, ta, mshale wa saa ya ukutani ulikuwa ukitoa sauti ndogo katika chumba kidogo lakini chenye mlundo wa fenicha za kisasa.
Kulikuwa na ukimya hakuna kilicho sikika zaidi ya sauti ya mshale wa saa ya ukutani iliyokuwa ikilia ta, ta, ta.
Nilijinyanyua kivivu kutoka katika chumba kile kidogo kichwa kikiwa kinaniuma vibaya mno. “niko wapi hapa” nilijuliza mwenyewe.
Lakini kabla kumbukumbu zangu hazija kaa sawa bin sawia mlango ulifunguliwa kisha akaingia mwanamke aliyekuwa ameva shati la kijivu lililochomekwa vizuri ndani ya suruali ya rangi ya buluu iliyowiva aina ya ‘jeans’ iliyo mkaa vema na kulidhihirisha umbo lake la kuvutia ambalo mara moja lilimletea mtu yeyote aliyekuwa akimtizama yule mwanamke wakati ule hisia ya tarakimu ‘nane’ ukijichora kichwani mwake.
Sura yake mzuri ya kuvutia ulikuwa umejaa wahaka mkubwa baada ya kuniona nimeketi kitandani.
“Vipi mrembo wajionaje”
“Safi tu”
“Pole sana ilikuwa wakuue wale mafedhuli.
Kama sio kuwahi kuwatiamua Wallah sasa hivi ungekuwa mochwari” Alisema yule mrembo sasa sura yake ikawa na mengi maswali dhidi yangu.
“Waitwaje?”
“Zahara”
“Kwanini usiku ule ulikuwa pale”
“Ni habari ndefu”
“Nieleze kwa kifupi?”
Ilinibidi niongope kuwa nilikuwa mgeni kutokea mkoani ambaye nilikuwa nikifanya kazi za ndani lakini nikafukuzwa na mwajiri wangu baada ya kutokea kutoelewana baina yetu
Yule dada alikaa kimya kwa muda wa dakika tano kisha akanigeukia na kusema; “kwa hiyo ungependa nikusaidieje”
“Nisaidie hifadhi, mahala pa kuishi dada yangu nikiwa natafuta kazi nyingine ya kufanya”
“Kwanini usirudi kwenu?.. halafu kwenu ni wapi?”
“Kwetu ni iringa ila hata hivyo sina nauli ya kurudi kwetu”
“Sawa nitakupatia hiyo pesa siku mbili hizi” alisema yule dada ambaye badae nilikuja kumfahamu kuwa alikuwa akiitwa ant Latifa.
Nikiwa naishi pale kwa ant Latifa siku mbili badae alinipatia pesa kiasi cha shilingi elfu hamsini kama nauli ya kunirejesha mkoni kwetu kama alivyo elewa yeye.
Alfaji hiyo baada ya kuagana nae akidhani naelekea ubungo, nilipanda basi la kigamboni na kuelekea feli , huko niliamini nikifika feli nitapata kazi yeyote hata ya kuchuuza samaki kazi itakayo niwezesha kusukuma maisha yangu yaliyokuwa hayana thamani kwa wakati huo.
Wakati nipo katika gari konda alivyo niomba nauli wakati natoa noti katika mfuko wa gauni mara nikapata kuona kadi ya yule kijana mwenye kufanana na Abdallah Talib.
Baada ya kumlipa konda pesa yake nikawa naipitia ile kadi ya yule kijana.
Jina katika ile kadi ilisomeka mr Uwesu Talib Abdallah. Kulikuwa na jina la kampuni yake na mawasiliano yake.
Baada ya kushuka katika lile basi la mjini nilielekea kibanda cha kuchaji simu na kununua vocha kisha nikamwomba yule mtu kibandani simu yake kwa muda.
Nilipiga namba moja katika zile zilizo kuwapo katika ile kadi kisha kwa muda mfupi simu ilipokelewa.
“Haloo habari yako?” sauti ilitokea upande wa pili baada ya simu tu kupokelewa. Alikuwa ni yule kijana niliye kutana nae katika basi la bagamoyo.Uwesu Abdallah.
“Ni njema ndugu”
“Nazungumza na nani na unashida gani?”
Kimya.
“Nazungumza na nani na unashida gani?”
Alirudia teena kuuliza yule mtu. Nilijikuta napata kigugumizi, sio kwamba nililokuwa nataka kusema lilikuwa zito.. lahaasha.
Isipokuwa sikuwa na lakusema.. “hivi nimempigia ili nimwambie nini sasa”
Nilijiuliza huku nikijiona bwege,
“Nazungumza na nani na unashida gani?”
Alinisutua tena.
Niliamua kukata simu. Halafu nikabaki najishangaa. Swali kuu likiwa ni kwanini nimempigia simu, na nashida nae ipi.
Nilituliza akili yangu kwa muda kidogo badae nikapata kulewa kitu, kwanini nilimpigia.
Nilibonyeza kitufe cha upande wa kulia chenye rangi ya kijani kisha nikaipiga tena ile namba.
“Hivi wewe ni nani unae nipigia simu halafu huongei?” alizungumza kwa ukali baada ya kupokea.
“Mimi Zahara”
“Zahara..! Zahara gani?” nilimkumbusha kuwa tulikutana katika basi la bagamoyo. Alifurahi baada ya kunikumbuka na kuomba niende nikamtembelee huko Tabata kimanga alipokuwa akiiishi.
Kwakuwa niliona Uwesu anaweza kunisiaida kitu fulani katika maisha nilimkubalia kwenda kumwona siku hiyo hiyo.
“Karibu sana bibie,” alinikaribisha ndani mwake, ndani ya sebule kubwa lililosheheni thamani ghari.
“Asante habari za siku mbili tatu”
“Safi tu”
Alinikaribisha kinywaji cha baridi kisha tukaendelea na mazungumzo.
“Ulisema unafahamiana na mzee wangu mzee Talib Abdallah?”aliuliza.
Nilifikiria kwa muda nikaona jibu sahihi la kumpaa kijana yule ni hili; “ndio namfahamu kwakuwa alikuwa mchumba wangu miaka ishirini iliyopita”
Uwesu alikunja uso baada ya kumpa jibu lile kisha akawa ananitizama kwa mtazamo wa kiudadisi, jicho lake lilitaka kujua kama nakunywa pombe ama natumia madawa ya kulevya.
Nilielewa sentesi yangu ilimchanganya Uwesu ila nikaiacha iendelee kuingia kichwani mwake.
“Nini unajaribu kuzungumza wewe?” Uwesu alisema tena akinikazia jicho kali.
“Baba yako alikuwa mchumba wangu wa zamani”
“Kwahiyo hilo ndio lililokuleta.. kuja kunieleleza kuwa ulisha tembea na baba yangu mzazi!”
Alisema tena kwa ukali lakini kwa sauti ya chini
 
JUMBA LA WACHAWI
Mwandishi/mtunzi; Zulfa Huseni
SEHEMU YA 22

Nilielewa sentesi yangu ilimchanganya Uwesu ila nikaiacha iendelee kuingia kichwani mwake.
“Nini unajaribu kuzungumza wewe?” Uwesu alisema tena akinikazia jicho kali.
“Baba yako alikuwa mchumba wangu wa zamani”
“Kwahiyo hilo ndio lililokuleta.. kuja kunieleleza kuwa ulisha tembea na baba yangu mzazi!”
Alisema tena kwa ukali lakini kwa sauti ya chini.
“Hapana lililonileta hapa si kuja kuanika yale niliyo wahi kuyafanya na baba yako ila nimekuja kushare matatizo yangu na wewe ili nione vipi nitapata msaada”
“Msaada juu ya nini?” aliuliza tena jicho lake likiendelea kuwa kali usoni mwangu.
Nilianza kumweleza ‘A’ mpaka ‘Z’ juu ya mkasa wa maisha yangu.
Kama ilivyokuwa kawaida Uwesu alionekana kushangazwa na mkasa ule wa ajabu kabisa.
“Aisee!. pole sana simulizi ya maisha yako inasisimua sana”
“Nimekwisha poa”
“Kwahiyo siku ile tumekutana katika basi ndo ulikuwa unakwenda kwa mganga kutafuta ufumbuzi wa hayo maswahibu?”
“Ndio”
“Inaonesha tatizo lako ni kubwa sana”
“Ndivyo mtaalamu alivyo sema japo sijui ni kitu gani kinacho nisibu haswaa”
Uwesu alinyamaza kusema, akatoa pakiti ya sigara na kuipachika mdomoni kisha akawasha kiberiti cha gesi katika sigara na kuvuta mkupuo mmoja mkubwa kisha akapuliza moshi mwingi angani halafu akasema.
“Kwahiyo hadi kunieleza yote hayo ulipenda mimi nikupe msaada gani?”
“Waswahili wanamsemo usemao zimwi likujualo..”
“Achana na semi za kiswahili go to the point tafadhali” alinikatisha.
Nilishusha pumzi ndefuu kisha nikasema, “nahitaji kuonana na baba yako”
Uwesu alinitizama kwa kina akashusha pumzi ndefu kifua chake kikapanda juu na kushuka pindi alipovuta pumzi na kuzitoa nje.
“Pole sana ma mdogo..” alisema akavuta sigara yake kisha akatoa moshi mwembamba katika tundu za pua yake kisha akaendelea kusema.
“Baba yangu nimekwisha mzika miaka mingi sasa”
“Nini!!” nilipatwa na mshangao moyoni huku uchungu ukinishika nikashindwa kuzuia matone ya machozi katika macho yangu.
Uwesu alizunguka kutokea pale alipokuwa ameketi katika kiti chake cha kuzunguka na kunifuata.
“Pole sana, kwani ulitaka baba akusaidie jambo gani?” aliniuliza.
“ Baba yako ndio kimbilio langu na tegemeo nililokuwa nimebakiza katika maisha, sasa nimebaki mimi tu, mimi peke yangu, nani atakae kuwa tayari kushare matatizo yangu teena” niliongea kwa uchungu machozi yakinitoka.
“Pole sana Zahara, usijali nitakusaidia katika kila hali.”
“Huwezi Uwesu.. huwezi, matatizo yangu ni makubwa mno inahitaji mtu anaye ijua thamni yangu haswaa na si vinginevyo.”
Uwesu alinipiga piga begani kama ishara ya kunifariji, kisha akanitaka niongozane nae katika lile jumba lake.
Aliniongoza hadi katika chumba kimoja kikubwa.
“Karibu na jisikie upo nyumbani kesho nitafanya jambo kwa ajili yako.” Alisema Uwesu. Tangu hapo
nilikuwa nikiishi pale kwa Uwesu kwa muda wa wiki, ndani ya lile jumba tulikuwa tukiishi watu wanne yanii Uwesu, mimi, ndugu yake na uwesu aliyeitwa Cholo ambaye alikuwa akisoma kidato cha pili pamoja na mlinzi wa getini.
*****
Siku moja Uwesu aliniita na kunitaka tutoke na kusema kuwa alikuwa na maongezi na mimi.
“Tunakwenda wapi?”
“We nifaute tu”
Tuliingia katika gari na kuanza safari nisiyo jua wapi tunako elekea.
Tulishika njia ya kuelekea mjini lakini tukiwa manzese tiptop mita kadhaa tuliingia magomeni mwembe chai na safari yetu ikaishia mbele ya geti jeusi huku ndani yake kukiwa na jengo kubwa la kifahari.
Alipiga honi mara mbili kisha geti likafunguliwa tukajitoma ndani.
Tuliishia katika sebule kubwa lilitandikwa zuria kubwa la manyoya, katika sebeule lile hapakuwa na kitu kingine zaidi ya Tv aina ya flat sreen lililogandishwa ukutani.
“Keti hapo” alisema Uwesu. Yeye aliingia katika moja ya vyumba vilivyokuwa mule ndani alionekana ni mwenyeji mule ndani.
Sekunde chache baadae alirejea akiwa ameongozana na mkaka mfupi mweusi.
“Karibu sana bibie” yule mkaka mweusi alinikaribisha kwa uchangamfu .
“Asante,” niliitikia pasina kuelewa kwanini nakaribishwa eneo lile nisilo lijiua.
“Zahara”
“Abee”
“Siku moja ulinieleza unamatatizo..” alisema huku akinitizama usoni. “matatizo ya viumbe wa ajabu, viumbe wanaochezea maisha yako.” Alisema tena.
Nilitikisa kichwa kumkubalia.
“Sasa leo nimekuleta huku kuangazia ufumbuzi wa maswahibu hayo.” Alisema huku akiachia tabasamu akinitizama kwa macho yaliouliza je umefurahia suprise hii.
Nilichia tabasamu huku macho yangu yakimjibu kuwa hakika hii ilikuwa ni siku niliyokuwa nikiisubiri kwa hamu.
“Safi sana kutana na shekh Hussein Maalim huyu ni mtaalamu aliyejikita katika mambo ya nyota na tiba”
Alisema Uwesu, Shekh Hussein alinipa mkono huku akisema karibu sana Zahara.
“Wakati tumegusana viganja vya mikono yetu mara ghafla nilihisi kama nimeguswa na waya wa umeme uliokuwa umechubuliwa, kwani nilihisi nikitetemeshwa mwili wote tendo lile lilitokea si zaidi ya sekunde tatu.
Nilipiga ukelele wa kuogofya huku nikiondoa mkono wangu kwa nguvu na upesi.
Uwesu alishanga nikaoana akinitizama kwa macho ya udadisi.
 
JUMBA LA WACHAWI
Mwandishi/mtunzi; Zulfa Huseni
SEHEMU YA 23

“Wakati tumegusana viganja vya mikono yetu mara ghafla nilihisi kama nimeguswa na waya wa umeme uliokuwa umechubuliwa, kwani nilihisi nikitetemeshwa mwili wote tendo lile lilitokea si zaidi ya sekunde tatu.
Nilipiga ukelele wa kuogofya huku nikiondoa mkono wangu kwa nguvu na upesi.
Uwesu alishanga nikaoana akinitizama kwa macho ya udadisi.
“Uwesu mgonjwa wetu ana viumbe wengi na hatari mno”.
Alizungumza kwa utulivu akiachia tabasamu jepesi lakini meno yake hayakuonekana, kisha akasema tena.
“ Uwesu nenda kule chumbani na bibie umsitiri mwili wake.”, sikujua nataka kustiliwa kitu gani lakini kwakuwa nilikuwa tayari kupata msaada niliamua kutii kama nilivyo takiwa.
Tuliingia katika chumba,Uwesu alinitolea juba lililokuwa katika begi la nguo na kunitaka nivae kiheshima kama mwanamke wa kislamu awavyo.
“Unaonekana mwenyeji katika nyumba hii Uwesu?” nilimuuliza wakati nikimaliza kulivaa lile juba.
“Nitakueleza tukitoka hapa.”
Baada ya kumaliza zoezi la kuustili mwili wangu.
Tulirejea kule sebuleni alikokuwa shekh Hussein.
“Sasa tutakwenda kusoma sulat-fatiha mara kumi kisha sulat-nass halafu tutamalizia sulat-Jinni.
Nafikiri baada ya hapo Allah atatia wepesi inshallah.”
Alisema huku akifunua msahafu na kujiweka vizuri kama kwamba anangejea pilau la nyama.
Upesi alianza kusoma zile aya takatifu yeye peke yake huku akiwa amefumba macho akionekana amezama zaidi kiroho.
Hata kabla ile Aya ya kwanza kufika katikati,.. ghafla nilihisi kizungu zungu kikubwa huku nikiona maluweluwe na michoro ya ajabu isiyo ashiria chochote mbele yangu.
Nikaoana kama dunia inayumba kutoka upande mmoja kwenda mwingine huku mimi nikiwa juu yake naelea.
“Uwiiii” nilipiga ukelele wa kuogofya baada ya kuona naelekea kuanguka lakini ajabu nikajiona kama dunia ilivyokuwa ikizunguka na kuyumba yumba huku mimi nikiwa juu yake chini yake kulikuwa na shimo kubwa ambalo mwisho wake haukuonekana zaidi ya giza zito..
Sasa dunia ikawa inayumba huku ikinisukuma mimi kuangukia katika lile shimo la giza “uwiii! Nakufaa” nilipiga ukelele mwingine wa nguvu huku nikijaribu kushika kwa nguvu pale chini ili nisiteleze zaidi na kuangukia katika lile shimo la ajabu.
Lakini kadili yule shekh alivyokuwa akisoma zile aya katika kile kitabu ndipo nilipokuwa nikijiona nina pata nguvu halafu nikiwa na tumaini kubwa la kujikomboa kwa kutoanguka katika lile shimo.
Hali hiyo ikawa inajirudia kila mara. Yule shekh akawa anakazana kusoma ile Aya kuu kabisa katika kitabu kile kitakatifu. Niseme tu na kadili alivyokuwa akizungumza yale maneno ambayo sikujua tafsiri yake zaidi ya kujua ni maneno matakatifu ya Mungu yaliyo andikwa katika kitabu chenye kuitwa Qurani, nilikuwa nikipata nguvu japo kuna wakati nilikuwa nabanwa mwili mzima na kitu kama praizi.
Ikafikia hatua nikaoana ni kheri yule shekh asitishe zoezi lake la kutamka yale maneno kwani alivyokuwa akisoma yale maneno katika kile kitabu ndivyo nilivyokuwa nikizidi kufinywa katika mwili wangu na vitu nisivyo viona. Mara zoote Macho yangu yalikuwa yanaona ukungu mbele yangu..nikawa nalia kwa uchungu lakini sidhani kama sauti yangu ya kilio ilisikika kwa shekh pamoja na Uwesu.
Hali ile iliendelea hadi nikajikuta giza linazunguka mboni za macho yangu na sikujua kilicho endelea teena

********

Nilizinduka baada ya risaa limoja na kujikuta bado nipo pale sebuleni Uwesu na shekh Hussein akiwa pembeni yangu.
“Pole sana bibie”
“Asante” nilijibu huku kumbukumbu zangu zikirejea upesi mno.
“Imekuwaje kwani”
“Mshukuru Allah kwakuwa ndiye daktari wa madaktari, hakika ulikuwa na viumbe wabaya mno katika mwili wako, viumbe waliokufanya kuwa kifungoni kwa miongo mingi mno.” Alisema Shekh Hussein alivuta bilauri ya maji na kuyanywa kidogo kisha akaendelea kusema.
“Siwezi kusema mengi uzuri ni kuwa kila kitu Uwesu amerekodi katika kamera hii..” alisema huku akitoa kamera ndogo ya sony na kuifungua.
“Tizama mwenyewe”
Alinipa ile kamera ikiwa ‘On’ tayari kuonyesha tukio zima lilivyokuwa wakati ule Shekh Hussein akiwa anasoma zile Dua takatifu na mimi nikiwa katika mkanganyiko mkubwa wa maluweluwe.
Nilijiona natutumuka mwili mzima huku ukelele wa kutisha ukitoka kinywani mwangu, macho nilikuwa nimekodoa huku uso wangu ukibadilika na kuonekana katika namna kama ya mzuka.
“Aghaghaagh,” nilikoroma kama mtu anae kata roho mwili umenikakamaa hadi mishapa ikiwa inaonekana. “Mnataka nini ninyi binadamu” sauti ya ukali ilinitoka kinywani mwangu, ajabu ni kuwa pamoja na kwamba nilionekana mimi ndiye ninae ongea lakini sauti iliyo sikika ilikuwa ya kiume.
Hapo nilipatwa na mshangao mkubwa nikasogeza karibu ile kamera kisha nikaendelea kujitizama.
“Nasema ninyi binadamu mnataka nini kwetuu?”
Shekh Hussein aliendelea kusoma zile dua, akawa kama kwamba hakusikia wala kuona chochote kilicho kuwa kikinisibu.
“Basi basi basi.. tunatoka.!! Usiendelee kutusomea kisomo hicho kinatutesa, twatokaa” sauti kutoka kinywani mwangu ilisema.
Sasa hapo nikiwa naangalia ile kamera nikaelewa kuwa kumbe nilikuwa na majini katika mwili wangu.
“Ninyi ni akina nani na kwanini mpo kwa huyu binti mkiyachezea maisha yake huku mkimfanyia mazingaombwe yenye kutisha kiasi hiki?” atimae Shekh Hussein aliuliza kwa upole huku akinitizama kwa upole ilihali mimi nilikuwa nikimtizama kwa jicho kali na la hasira.
 
JUMBA LA WACHAWI
Mwandishi/mtunzi; Zulfa Huseni
SEHEMU YA 24

Sasa hapo nikiwa naangalia ile kamera nikaelewa kuwa kumbe nilikuwa na majini katika mwili wangu.
“Ninyi ni akina nani na kwanini mpo kwa huyu binti mkiyachezea maisha yake huku mkimfanyia mazingaombwe yenye kutisha kiasi hiki?” atimae Shekh Hussein aliuliza kwa upole huku akinitizama kwa upole ilihali mimi nilikuwa nikimtizama kwa jicho kali na la hasira.
“Kwa niaba ya wezangu naitwa Jini Sipra kutoka katika bahari ya mbali niko mwilini mwake kwa bahati mbaya tu, sio kwa makusudi”
“Kivipi?” Shekh Hussein aliuliza tena.
Nikiwa nimeendelea kushika ile kamera Shekh Hussein pamoja na Uwesu walinitizama kwa jicho lililosema tizima kwa makini hiyo record kuna maelezo yanayo toa fumbo la maswahibu yako yoote.
Nilirudisha macho katika ile tape iliyokuwa ikiendelea kucheza.
Na hapo nikajiona mimi kupitia majini yaliyo kuwa kichwani mwangu yakisimulia mkasa woote ulio tokea miaka mingi hadi mimi kujikuta naingia katika mkondo wa kuwa ndani ya viumbe wa ajabu walio badilisha dira na mwangaza wa maisha yangu.
Yale majini yaliyokuwa kichwani mwangu yalieeleza hivi…
*
;IRINGA, MIAKA MINGI
ILIYOPITA
Kundi kubwa la ng’ombe lilikuwa katika malisho katikakati ya misitu ya kitonga,kengele ndogo zilizo fungwa katika shingo za mifugo hiyo zililindima pande zote ndani ya msitu huo wenye nyasi nyingi za kijani kibichi na miti mirefu,
Jioni hii ya saa kumi na mbili, Kalindimya kijana mchungaji wa mifugo hiyo alikuwa akijitahidi kuwaswaga wale ng’ombe wenye kukaribia mia mbili, aliwasukuma kwa mijeredi ng’ombe wa nyuma, muda ulikuwa umeakwisha wa yeye kuendelea kuwa katika malisho, mbwa wake wawili, waliendelea kuwa kando yake muda wote wakingojea amri yoyote kutoka kwa bwana wao, jua lilizama na giza kuchukua nafsi yake, kalindimya alikwisha fika katika zizi kubwa la ng’ombe lililokuwa ndani ya msitu ule, pembeni ya zizi kulikuwa na kijumba kidogo cha nyasi ambacho kilitumika kama hifadhi kwa mchungaji yule mwenye kuitwa Kalindimya.
Baada ya kuhakikisha mifugo yote imeingia katika zizi alielekea katika kijumba chake kwa ajili ya kupumzika.
Ni dhahili mtu yule alikuwa ni mfugaji mwenye kuendesha ufuguaji wake katika mtindo wa kuhamahama{shifting cutvation}.
Mara tu alipo fungua mlango alikutana na harufu nzuri ya manukato ambayo kamwe hakuwahi kusikia mahala popote, “pengine ni mauwa ya mwituni” alijifajili kwa kuondoa mashaka yaliyo kuwa moyoni mwake,hata alipo geuka na kukipa mgongo chumba chake kwa kutengeneza kiegesheo cha mlango wa makuti, ndipo alipo hisi kuwapo na ugeni mule ndani.
Aligeuka upesi na macho yake yakakutana na mwanamke mrembo ambaye hakuwahi kumwona katika hii dunia,
Alibabaika kidogo huku akijiuliza apige kelele, akimbie,au akabiliane nae. Hakuwa na jibu.
Alibakia ameduwaa kwa uzuri wa kiumbe yule, binti yule alimsogelea na kumzunguka pande zote, huku akichezea nywere zake ndefu na nyeusi tii, macho yake yakizunguka kama goroli mwendo wake ukiwa wa madaha na pozi za kujinyonga nyonga, lakini hata hivyo midomo yake iliachia tabasamu jepesi la dharau, kisha kwa suti nzuri ya kisichana akasema “naitwa Shakira, ndiye malkia wa msitu huu wa kitonga, nitakuona siku nyingine”
Hata kabla Kalindimya hajatia neno mtu yule alitoweka kama moshi, jaamaa alibaki katika mashaka makubwa, huku akiamini ametokewa na mzimu wa msitu ule,
Hiyo ilikuwa ni siku ya kwanza Kalindimya kutokewa na kiumbe yule katika msitu ule mnene… ikaja siku ya pili akiwa katika machungo… ikatokea siku ya tatu akiwa amelala usiku…ikatokea siku nyingene tena akiwa kajipumzisha, mwisho ikawa ni mazoea tu, kila mara Shakira akawa anamtokea yule mfugaji wa ngo’mbe.mwisho Kalindimya akazoea hali ile, shakira akawa rafikiye na kalindimya, wakazoeana mno, mazoea yakazaa upendo..
Uliibuka upendo wa ajabu mno kwa hawa watu wawili, Kalindimya alishii na huyu kiumbe kama mke na mume kwa miaka mingi katikatiu kabisa ya msitu kitonga.
Hatimae Shakira alishika mimba na miezi tisa badae alizaliwa mtoto wa kiume, mtoto ambaye alikuwa nusu jini nusu binadamu aliye fahamika kama Karogoyo,
Watu hawa walitengeneza kijiji chao ndani ya msitu ule,na walishi kwa mapendo ya hali ya juu, siku moja mtoto huyu alipatwa na ugonjwa wa ajabu, na ghafla alifariki dunia.
Jini mwenye kuitwa Shakira aliumia mno kwa kifo cha mtoto wake aliyempata kutoka kwa binadamu yule mchungaji.
Miaka mingine badae alizaliwa mtoto mwingine aliye itwa Zahara, alikuwa ni mtoto mzuri kuliko hata uzuri wenyewe.
Siku moja yule mwanamke jini mwenye kuitwa shakira aliuwawa na waganga wa kibinadamu waliokuwa wanakuja katika msitu wa kitonga kuchimba dawa za miti shamba ambazo walikuwa hawazitumii kwa matumizi mazuri katika jamii.
Lakini pamoja na hilo tangu afariki yule jini Shakira malkia wa msitu kitonga ndani ya msitu huo kumekuwa hakuna amani hata kidogo, kila binadamu anayeingia ndani ya msitu huo uliobalikiwa kuwa na dawa za miti shamba, lazima apotelee humo daima.
Na yule mfugaji na mwanae Zahara hadi leo hawajulikani walipo..
***
Tape is full..ndio neno lililotokea katika tape ile ndani ya kamera na hapo ukatokea ubuluu kuonesha kuwa ile tape ilikuwa imejaa.
“Ayaaa imekwishaaa!!” nililopoka kwa fadhaa huku nikimtizama shekh Hussen kisha nikarejesha macho upesi katika kamera.
Sikuweza kuona tena kwakuwa pale ndio ilikuwa mwisho wa ule uzi wa mkanda wa filamu.
Bado sikuweza kuelewa chochote katika yale yaliyosimuliwa na majini waliokuwa katika kichwa changu zaidi ya kuona kuna uhusiano wa majina tu kati ya jina langu na la yule kiumbe aliye elezewa katika simulizi ile.
Bado niliona sijapata jibu kamili la kitendawili hiki, zaidi nilijikuta nasombwa na wimbi la maswali katika kichwa changu.
Nilibaki nimeduwaa nikiukodolea macho ule ubuluu katika camera kwa nukta kadhaa.
 
JUMBA LA WACHAWI
Mwandishi/mtunzi; Zulfa Huseni

SEHEMU YA MWISO

Bado sikuweza kuelewa chochote katika yale yaliyosimuliwa na majini waliokuwa katika kichwa changu zaidi ya kuona kuna uhusiano wa majina tu kati ya jina langu na la yule kiumbe aliye elezewa katika simulizi ile.
Bado niliona sijapata jibu kamili la kitendawili hiki, zaidi nilijikuta nasombwa na wimbi la maswali katika kichwa changu.
Nilibaki nimeduwaa nikiukodolea macho ule ubuluu katika camera kwa nukta kadhaa.
“Umeelewa kitu” sauti ya shekh Hussein ilinistua.
Nilitikisa kichwa kumkatalia kuwa sijaelewa lolote, nikahamisha macho yangu katika kile kikamera nikawa namtizama yule shekh.
“Huyo zahara ndio nani aliyekuwa anazungumziwa?” niliuliza wahaka ukiwa umenijaa.
Yule shekh aliachia tabasamu jepesi huku akihesabu tasbihi iliyokuwa mkononi mwake, kisha akasema.
“Kama sio mkanda wa hiyo divu ya kamera kujaa basi ungepata jibu la kitendawili chako chote.”
“lakini kwakuwa sisi tulikuwa mashuhuda wa kile kilichokuwa kikielezwa na viumbe vilivyokuwa ndani ya mwili wako hatuna budi kukueleza mambo yoote tuliyo yasikia, ama sivyo bwana Uwesu?”.
“Kabisa kabisa” Uwesu aliitikia huku akitikisa na kichwa chake kuafikiana na maneno ya shekh Hussein.
Nilijiweka sawa tayari kwa kusikia sababu ya mimi kuingia katika majanga yale ya ajabu kabisa.
“Historia inaonyesha baada ya kila binadamu anayeingia kwenye ule msitu na kutokomea kusiko julikana waganga na waganguzi kutoka maeneo mbalimmbali walikaa na kuweka shauri la pamoja.
Lazima suluhu la vifo vinavyo tokea katika msitu kitonga ipatikane ufumbuzi,na ufumbuzi pekee ilikuwa ni kuondoa mzuka na majini waliokuwa wanaangamiza waganga waliokuwa wakienda kuchimba dawa katika msitu ule ambao unasadikika ndio eneo lenye utajiri wa mitishamba mingi pengine kuliko eneo lolote katika bara la afrika.
Lakini hadi sasa ninavyo ongea na wewe bado halijapatikana suluhu ya tatizo hilo,bado kuna vita kubwa kati ya majini na waganga wa jadi dhidi ya msitu huo Zahara.”
Alisema shekh Hussein na kukaa kimya kidogo.
Nilifikiri kwa muda maneno yake lakini bado katika yote aliyoyasema bado sikuona jibu la kitendawili changu.
“Bado sijaelewa kitu Shekh” nilisema huku nikimkodolea ndita katika paji langu la uso zimejichora.
“Ni kwamba wewe ndio Shakira, yule jini aliyesadikiwa kuwa ameuawa na waganga wa jadi.”
“Nini!” mshutuko mkubwa ulinivaa baada ya kauli ile, nikabaki mdomo wazi kwa nukta sisizo hesabika, kope za macho yangu zikikapua, uso wa mshangao usoni huku tumbo langu likipata joto.
“Mimi ni nani?!..jini..kivipi niwe jini?..kiaje?” nilisema.
Shekh yahaya alitabasamu kisha akasema, “mimi nilitegema ungehoji vipi uwe jinni halafu usumbuliwe mwilini mwako na majini mengine ilihali wewe ni Jini”
“No no shekhe..hata hili la kutaka tu kujua mimi nakuwaje jini ilihali tangu utoto hadi ukubwa naijua vema familia yangu haikuwa na mambo yoyote yenye unasaba na mambo haya ya secret society ni muhimu kuliko hilo ambalo ungependa nianze kuhoji, na nafikiri hilo litakuwa ni swali la pili baada ya hili la kwanza kujibiwa maana unaposema kwamba mimi ni jini maana yake ni kwamba hata wazazi walio nizaa nao ni majini ama sivyo basi sio wazazi wangu.” Nilisema kwa kulalama huku sura yangu bado ikiwa ni yenye kutawaliwa na taharuki isiyo kifani.
“Utafundishwa elimu za majini na utaelewa hili, kwa ufupi ni kuwa binadamu hawezi kuua jini, lakini jini anaweza kuua binadamu.
Wale waganga walicho kifanya ni kupiga nusu kaputi jini shakira, kwa miaka mingi mno.
Na wewe ukiwa katika usingizi ndipo unapopata njozi kuwa kuna siku uliwahi kuwa binadamu, lakini kiasili wewe sio binadamu.”
Alisema Shekh Hussein huku akiwa amenikazia macho makavu pasina kusema neno, nilimtizama yule shekh kwa sekunde chache nikamwangali Uwesu, yeye pia alikuwa akinitizama kwa mashaka kidogo huku akimung’unya midomo kama mwenye kumungu’nya tambuu, macho nikayarejesha kwa Shekh Hussein kisha nikahoji.
“Kwahiyo unataka kujaribu kusema kila kitu kilicho tokea tangu nikiwa mtoto hadi nakuwa yote ni ndoto niliyokuwa naota nikiwa nimelala?”
“Haswaaa, ni ndoto lakini si ndoto”
“Kivipi ni ndoto lakini si ndoto” niliuliza kwa wahka.
“kilicho tokea katika maisha yako na kujiona ni mtu mwenye familia, ndugu jamaa,marafiki na hata mchumba wa dhati ni sahihi kabisa jambo hilo ni la kweli, lakini si ndoto kwakuwa kuna siku itakayokuja na kuona, na kugundua kama kuna mahala uliwahi kutokea na kuishi huko kwa miaka mingi, na siku hiyo utakapo patwa na hali hiyo ndipo utakapo jielewa rasmi wewe ni nani?”
Yule shekh aliendelea kunieleza vitu ambavyo sio tu kwamba sikumwelewa lakini pia mambo yale yalikuwa hayaningii akilini hata kidogo.
“Hahahahaha..!! unajua unanieleza mambo ambayo kila nikijaribu kulazimisha utashi wangu uelewe hilo lakini ubongo wangu unagoma kabisa kuelewa aisee”
Nilisema huku cheko dogo lenye mchanganyiko wa fadhaa likinikitoka.
“Zahara” aliniita shekh Hussein huku akinitizama kwa makini zaidi.
“Abee”
“Unaonaje na na sisi akili zetu zishindwe kuelewa kuwa ulitekwa nyara na mzee aliyeokota jacketi lako wakati unatoka Geita, kisha akakuingiza katika chumba ambacho alikubaka, siku hiyo hiyo ukapata mamba na siku hiyo hiyo ukajifungua mtoto, na siku ya pili ulivyo toroka katika jumba ukakuta sio mwaka 1989 bali ni mwaka 20016, unaonaje na sisi tukubeze kwa maelezo hayo?”
“Lakini mimi huo uliousema hapo ni ukweli uliotokea mbele kabisa ya macho yangu”
Nilijibu upesi upesi huku nikiwa nimetoa macho.
Yule shekhe alinicheka kwa pozi, cheko ambalo ndani yake lilisema ‘acha ubwege hebu fungua akili yako sasa’
“Sasa huu si muda wa kukulazimisha ukubali haya nikuelezayo jukumu lako ni kusubiri, muda utaongea zaidi” alisema Shekh Hussein.
“Kwamba badae nitakuwa jini?” nilimdakiza.
“Sio badae still wewe ni jini kama majini mengine, kinacho tokea na kujiona wewe ni binadamu hata mimi sijui.”
“Kha!!”..nilichoka.
“Unaonaje ukineleza sababu ya mimi kubakwa, kuzaa mtoto ndani ya lile jumba na kuingiliwa na viumbe wa ajabu mwilini mwangu na kunitesa kwa miaka yote hiyo” Hatimae niliona niulize swali ambalo pengine jibu lake lingenipa maana ya matatizo yote yale katika maisha yangu.
“Niseme mara ngapi kwamba wewe ni jini, yale yote yaliyotokea katika lile jumba ni mwendelezo wa juhudi za waganga kujaribu kukuzuia usizidi kuwaangamiza wataalamu wanakwenda kusaka dawa kwenye msitu kitonga kwa kazi zao mbalimbali.
Kuingiliwa kimwili, kuzaa mtoto na kupigwa nusu kaputi kwa miaka zaidi ya 25 yote hayo ni kinga za kukuzuia Zahara, unajua wewe ni kiumbe hatari mno Zahara.
Kwakweli kadili nilivyo zidi kuambiwa mambo yale na yule baba nilijikuta hadi mimi najiogopa.
********
Baada ya mambo yote hayo hakuna binadamu yoyote aliyekubali kuishi ama kuwa karibu na mimi kwa kuamini mimi ni Jini.
Si uwesu wala mtu mwingine yeyote aliyekuwa tayari kuwa karibu na mimi, ajabu ni kuwa, taarifa za kwamba mimi ni kiumbe wa ajabu zilitapakaa mno katika baadhi ya maeneo hapa jijini.
Siku moja niliwahi kuona gazeti la udaku lisilo maarufu likitoa habari juu ya sakata la maisha yangu japo, mwanidhsi aliandika ile habari kwa kuipika mengi yakiwa ya uongo na machache ya ukweli, bado mtu yoyote angesoma habari ile lazima asinge acha kutishika mno kwa mambo yale yaliyokuwa kama hadithi za kufikirika.
Kwa siku zile za awali nilikuwa nikiishi kwa yule shekhe, naweza nikasema ni shkhe Hussein yeye peke yake ambaye hakuwahi kuniogopa katika uhai wangu wa mwishoni. Lakini hata hivyo bado sikuona furaha wala tumaini la maisha kama binadamu yoyote.
Sikuwa na kitu muhimu chochote katika dunia, sikuwa na chochote cha kupoteza katika ulimwengu huu. Nilijiona ni kikatuni tu mbele ya mamcho ya kila aliye mbele yangu.
Sikuona thamani ya utu wa wangu hata siku moja.
Hivyo basi kutokana na hayo yoote yaliyonisibu na yanayo endela kunisibu siioni haja ya kuendelea kuishi katika huu ulimwengu mpya kwangu.
Asihusishwe mtu yeyote na kifo changu.
Naomba maaamuzi yangu yaheshimiwe..

By marehemu
Zahara..
Mwisho
***********
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom