Jumba la Wachawi

Madame S

JF-Expert Member
Mar 4, 2015
17,172
34,278
JUMBA LA WACHAWI

Mwandishi/mtunzi; Zulfa Huseni
SEHEMU YA 1
UTANGULIZI;

Gari lilikuwa likiendeshwa kwa kasi mno, ni kwenye barabara ya Alhasan mwinyi, ni gari dogo aina ya Hyundai ya rangi ya kijivu, speed kali ya lile gari ilifanya kila mtu aliye bahatika kuliona ageuze shingo yake na kubaki akishangaa mwendo mkali wa lile gari dogo.
Mtu aliyekalia siti ya mbele ambaye alikuwa akiliendesha lile gari alionekana kujawa na mashaka na wasiwasi usio na mfano.
Mguu wake wa kulia uliokuwa umevalishwa viatu vya kuchomeka [open shoes}uliendelea kukanyaga kikanyagio kilichokuwa kikilifanya lile gari liende kwa speed ya ajabu mno.
Mikono ya mtu huyu ambaye aliyekuwa amevaa kanzu nyeupe na balaghashia ya kijivu ilikuwa imekamata kwa nguvu zote uskani wa lile gari.
Macho ya mtu huyu mwenye mwenekano wa mumiini mzuri wa dini ya kislamu, macho yake yalikuwa makini mbele.
Lakini hata hivyo sio kwamba umakini wa macho ya mtu huyu pale mbele yalikuwa kama ambavyo alivyokuwa akiitizama barabara, lahasha.
Fikra zake zilikuwa mail nyingi kutokea mule ndani ya gari,ni sahihi kabisa kama nikisema ni kiwiliwili tu cha mtu yule ndio kilikuwa ndani ya gari, lakini akili yake ilikuwa umbali mrefu mno.
Dakika kumi na ushee kiwiliwili kile zilimtosha kabisa kufikisha gari lile mahala alipokusudia.
Mahala alipokuwa akili yake, akili iliyokuwa imetelekeza kiwiliwili chake kwenye kigari kidogo.
Sasa baada ya kufika eneo lile la jumba ambalo sio sahihi kuliita la kifahari wala sio sahihi pia kuliita jumba chakavu, ilikuwa ni nyumba ya kawaida tu ambayo kwa mikoa fulani fulani katika hii nchi pengine thamani yake isingezidi milioni 70.
“Zahara..weweee” yule mtu alipaa sauti, “Zahara….Zahara” aliita kwa vituo huku akitembea upesi upesi kuelekea ndani ya jumba lile, zaa..hara..we..weee, zaha..ra sauti kubwa lakini yenye mitetemo ya hofu na mashaka ilimtoka tena.
Mtu yule alikuwa akiita hukua akitembea upesi upesi akipita katika kikorido kilicho tenganisha kuta mbili zilizokuwa zikitizamana huku ukingoni kukiwa na vyumba vya watoto, cha baba na mama jiko, bafu na maliwato.
“Zahara weee uko wapi wewe”
Mtu yule aliyevaa kanzu na baraghashia alizidi kuita.
Kimya.
Nyumba yoote ilikuwa kimya ziaidi ya ukimya wenyewe. Hata mtu yule alivyokuwa akiendelea kuita sauti ya mwangwi ikawa inajibu sauti ile, japo mule ndani hapakuwa eneo tupu.
Aliishia katika chumba ambacho mbele yake kulikuwa na mlango ambao ulikuwa haujafungwa vizuri.
“Zaharaa…”
Mtu yule aliipaza sauti na kuita tena.
Lakini mwangwi wa sauti yake ndio ulio mwitikia.
Atimae alisukuma mlango ule.
“UwiiiII!, subhanallah, Allah akibar!!”
Mtu yule aliachia ukulele wa fadhaa huku maneno kadhaa ya tauhidi yakimtoka.
Alikuwa ameduwaa huku macho yake yakishuhudia tukio ambalo kamwe hakuwa tayari kuona uhalisia wa jambo lile..
Alikuwa na hofu na mashaka, lakini pia alikuwa na huzuni, picha ya mwili wa mwanamke aliyekuwa mbele yake huku akiwa hauna uhai ulimtisha!.
Lakini haukuwa kumtisha tu bali ulimtia simanzi, tangu afahamiane na mwanamke yule zililikuwa ni siku tatu tu zimepita kabla ya mauti kumkuta Zahara.
Hakuogoapa eti kwakuwa kulikuwa na maiti ndani ya jumba lake no, aliogopa kwakuwa mwanamke aliyekuwa amekufa mbele yake hakuwa binadamu wa kawaida.
Alikuwa ni JINI.

Hilo la binti yule kuwa Jini alilijua yeye na mtu mwenye kuitwa Uwesu, japo binti yule alipojaribu kuelezwa hilo alipinga kwa nguvu na hoja za kila namna, kiumbe yule aligoma kabisa kuelewa na kukubali jambo lile.
Kuwa yeye ni Jini.
Mtu yule akiwa bado ni mwenye taharuki, alipata utulivu wa ghafla baada ya macho yake kutua katika notebook kubwa iliyokuwa kando, hatua chache kutoka mwili wa yule binti ulipokuwa ukining’inia kwenye kamba.
Haikuhitaji mwalimu kuelewa kuwa kwa vyovyote vile marehemu kabla ya kufa aliandika ujumbe ndani ya notebook.
Mtu yule alisogea upesi na kufunua ile note book na kuanza kusoma kile kilicho andikwa ndani ya notebook ile.
Mambo yaliyo andikwa mule yanataisha, yanahuzunisha, lakini pia HAKUKUWA NA JIBU LA KITENDAWILI HIKI.
Marehemu aliandika hivi.


28/3/1989
Ulikuwa ni msafara wa watu watano, wawili kati yao, pamoja na mimi mwenyewe, tukiwa ni waandishi wa habari waajiriwa wa kampuni ya film Tanzania ambayo ilikuwa ni kampuni ya habari na matangazo iliyo jihusisha pia uchapaji wa magazeti ya Tabasamu na Sunday, wakati wale wengine wawili walikuwa ni wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam ambao walikuwa wanafanya tafiti kwa ajili ya shahada yao ya pili pale mlimani.
Tulikuwa ni watu wenye furaha kubwa kutokana na namna ambavyo kazi yetu ilivyo kwenda sawa bin sawia, ilituchukua zaidi ya wiki mbili tukiwa mkoani Geita tulikokwenda kikazi, ambapo kampuni ilituteuwa kwenda huko kuangazia matukio yaliyokuwa yakiendelea kutokea katika mkoa wa geita ambayo kwa kiasi kukubwa yalikuwa yakigusa hisia za watu wengi nchini na hata duniani kwa ujumla…migogoro ya wakulima na wafugaji.
Siku hii ya Juma tano ya tarehe 28/3/1989 ni tarehe ambayo haiwezi kufutika katika akili yangu pengine hadi siku ya kiama.
Safari ilikuwa ndefu mno kiasi fulani ilinichosha, lakini hata hivyo kila nilivyo fikiria matunda ya kazi iliyotupeleka huko kwakweli nilipata nguvu kubwa.
Mwendo mkali wa Landcruser iliyokuwa ikiendeshwa na bwana Magembe Matiku tulitazamia kati ya saa mbili ama saa tatu tutakuwa tumekwisha wasili jijini Dar.
Tulindoka mkoani Geita mapema alfajiri. Awali wakati tunaanza safari ndani ya ile Landcreuser kulirindima maongezi vicheko na utani mwingi miongoni mwetu, lakini kadiri muda ulivyozidi kuyoyoma ndivyo zile bashabasha zilivyo zidi kuyeyuka,hii ni kutokana na umbali mrefu wa safari yetu uliosababisha kukinaiwa na safari ile ndefu.
Saa tisa juu ya alama tuliingia mkoa wa Dodoma, hapo bwana Magembe Matiku dereva wa ile landcruser alitutaka tupate chakula cha mchana kabla ya kuendelea na safari ile, tuliingia katika hotel iliyokuwa ndani ya kituo cha mafuta cha Gapico na kujipatia chochote.
Jua lilikuwa ni kali mkoani Dodoma tofauti na mikoa tuliyopita huko nyuma, jacket nilililokuwa nimevaa halikuwa na nafasi tena katika maungo yangu.
Nililivua.
Wakati naliondoa lile jacket maungoni mwangu nililiweka katika mgongo wa kiti nilicho kuwa nimekalia kisha nikaendelea kushambulia chakula kilichokuwa mezani kwangu kwani njaa ilikuwa ikiniuma kisawasawa.
Katika meza niliyo kuwa nimeketi, sikuwa peke yangu tuliketi wawili mimi na Lovenes huyu alikuwa ni mfanya kazi mwenzangu tuliyekuwa pamoja katika ule msafara wa geita.
Hatua chache kidogo kulikuwa na meza iliyokaliwa na watu watatu yanii bwana Magembe Matiku ambaye ni dereva wa kampuni yetu,pamoja na john, na mwenzake Fidelix hawa ni wale wanafunzi wa chuo kikuu cha Dar es salama waliokuwa katika utafiti wa masomo yao.
Sambamba na hilo, katika viti vingine vilivyokuwa mule katika hotel ile kulikuwa na watu wengine wengi tu ambao walikuwa wakijipatia chakula mchana ule,upande wa mbele wa meza niliyokuwa nimekaa kulikuwa na meza nyingine iliyokaliwa na mkaka aliyekuwa akinitumbulia macho pindi tu nilivyo saula jacket katika maungo yangu.
Macho yetu yaligongana mara mbili, awali nihisi imetokea bahati mbaya na nikaendelea kushughulika na kula, macho yakiwa katika sahani.
Angalau sasa tumbo langu lilishiba, nikanyanyua uso wangu kuangaza eneo la kunawia mikono,lakini wakati nafanya hilo, bahati mbaya tena nikagonganisha macho na yule mwanaume kwa mara nyingine tena, hapo nikagundua kuwa yule kaka alikuwa akinitizama muda wote, pia alikuwa akiniangalia katika namna ambayo ilinielewesha kitu gani kilikuwa kinapita katika akili ya yule mtu.
Ajabu ni kuwa, pindi nilivyo pata kugonga nisha macho na yule mtu kwa mara hii ya tatu nilipatwa na kitu fulani cha ajabu katika mwili wangu hali iliyo nifanya nistajabu.
Nilipapatwa na ganzi chini ya mapaja yangu lakini wakati huohuo nikajikuta naingia katika siku zangu japo nilikuwa na wiki moja tangu nitoke katika hedhi na siku zangu za hedhi huwa hazina kawaida ya kubadilika kiasi kile.
Upesi akili yangu ikaanza kufikiri kuhusu mkoba wangu ulio kuwa ndani ya ile landcrueser ambao ndani yake kulikuwa na pedi ambazo huwa natembea nazo wakati wote.
Nazipiga hatua kwenda kunawa mikono, kabla ya kuendea mkoba kwa ajili ya kujihifadhi na damu iliyokuwa inachafua nguo yangu ya ndani.
Wakati niko nanawa mikono, niligeuza shingo kumwangalia yule mtu, nikaona bado ananitizama katika namna ile ile. Nafikiri macho yake yalikuwa yakivutiwa na uzuri wa sura nilio jaliwa na Muumba, na pengine labda macho yake yalivutiwa na umbo langu lililokuwa kama namba nane, ninge kuwa nimevaa blauzi ya kubana ningesema labda yale macho yalikuwa hayajiwezi kwa sababu ya maziwa yangu saizi ya embe dodo bichi, lakini kwa bahati mbaya au nzuri nilikuwa nimevaa shati lilionikaa vizuri ikiwa kwa ndani ya kifua changu nikiwa nimeyabana maziwa yangu kwa sidiria ndogo.
Sasa vipi huyu mtu anitumbulie mimacho kaisi kile..!
Anajua yeye mwenyewe.
“Zahara vipi tena mbona hivyo?” Lovenes alinistua wakati nikitoka ndani ya hotel ile kuelekea mahala lilipokuwa gari.
“Aagh!. we acha tu shost niko period mwenzio nafuata mkoba garini nichukue pedi nijistiri”
Nilimjibu haraka haraka kwa sauti ya chini, kisha nikazipiga hatua upesi kwenda lilipokuwa gari. Lakini wakati huo huo bwana magembe matiku na Fedelix pamoja na John nao walikuwa wanatoka mule hotelini
“Jamani hatuna muda wa kupoteza wapenzi inabidi tufike Dar kabla ya saa tatu usiku” alisema bwana Magembe akichezesha chezesha lundo la funguo mkononi mwake.
Niliongeza mwendo hadi katika ile landcruser nikachukua mkoba wangu uliokuwa na pedi kisha kikaelekea maliwato na kujihifadhi.
Wakati huo, yule mtu aliye patwa na ugonjwa wa kuniangalia angalia hovyo nilikuwa nimekwisha msahau katika akili yangu.
Dakika kumi zilizo fuata tulikuwa ndani ya gari tukiuacha mji wa Dodoma na joto lake, gari lililokuwa likiendeshwa na bwana Magembe likiwa katika mwendo mkali hatari.
Kulikuwa na maongezi ya hapa na pale ndani ya gari..lakini wasaa ule niliishia kuelekeza macho yangu huko nje nikiangalia vijumba vifupi na vidogo vya makuti vilivyo kandikwa kwa udongo, yakiwa ni makazi ya wanakijiji wafugaji jamii ya wagogo.
Dakika arobaini baadae watu wote walikuwa wanasinzia isipokuwa mimi na bwana Magembe. Kulirindima ukimya garini zaidi ikiwa ni mlio wa gari uliokuwa ukilalama kutokana na vile bwana magembe alivyokuwa akilivuta kisawasawa.
Ni hapo nilipo kumbuka walkman yangu ya CD kifaa nilicho kitumia kusikiliza muziki mbalimbali niliyo ihifadhi katika CD…..na wakati nakumbuka kifaa kile ndipo hapo moyo wangu ulipopiga “paaaaaaa” kila kitu kilipita katika akili yangu kama tamthilia.
Nikajikuta napiga ukulele wa fadhaa.
 
JUMBA LA WACHAWI
Mwandishi/mtunzi; Zulfa Huseni
SEHEMU YA 2

Ni hapo nilipo kumbuka walkman yangu ya CD kifaa nilicho kitumia kusikiliza muziki mbalimbali niliyo ihifadhi katika CD…..na wakati nakumbuka kifaa kile ndipo hapo moyo wangu ulipopiga “paaaaaaa” kila kitu kilipita katika akili yangu kama tamthilia.
Nikajikuta napiga ukulele wa fadhaa. “Jacket languuuuuuu!!..” Nikamstua kila mtu aliyekuwa amelala.
Na sasa nikakumbana na maswali lukuki kutoka kwa wenzangu..vipi nibwate kwa sauti kubwa kiasi kile kwa ajili ya jacket..thamani yake ni kubwa kwa kiwango gani hata nibweke namna ile na kuondoa kabisa utulivu wa watu mule garini.
Nilibaki nimeganda nimekodoa macho, mdomo wangu ukiwa wazi,lakini mkono wangu wa kushoto ukiwa umefunika domo lile, sura yangu ikiwa imejaa mshangao mkubwa.
“Zahara kwani hilo Jacket la kazi gani tena ilihali Dar lingeenda kukaa katika begi, tena pengine lingeishia kuwa chakula cha mende na panya”.
Alisema John akimaanisha hapakuwa na sababu ya kujutia kulisahau Jacketi ilihali mahala ninako kwenda ni sehemu ya joto kali ambapo uhitaji wa masweta na majacket haupo.

“Naenda kufanya nini Dar bila lile jacket jamani? ndani ya hiyo nguo kulikuwa na kila kitu ambacho kilitupeleka Geita.kitabu chenye data zote kipo katika mfuko wa jacket, camera ndogo yenye picha za video na still ipo katika mfuko wa jacket, kinasa sauti kilichokuwa na sauti za mahojiano tulizo fanya na wale jamaa waliokuwa wanagombana kuhusu mipaka, kifaa kile kimo katika mfuko wa jacket,na hata zile karatasi za maswali na majibu ya mkuu wa mkoa zoote zimo katika mfuko wa jacket.. lakini pia, hata vitambulisho vyangu vyote vimo katika lile jacket”
“Nooooo!!.” Nini tunafanya jamani!!. nini hiki aagh” bwana Magembe alipiga kelele baada ya kutoa malezo yale. Na mwisho alikanyaga breki ghafla na gari likasimama katikati ya barabara huku tairi za gari zikijiburuza katika lami na kutoa mlio mkali wa mburuzo.
Kwakweli maelezo yangu yalimchanganya kila mtu hasa wale wafanyakazi wenzangu,vifaa vilivyokuwa katika jacket vilikuwa ni vitu muhimu kwa mustakabali mzuri wa ajira zetu.
Kamwe mkurugenzi isingeweza kutuelewa kama tungerudi bila taarifa yoyote ya geita ilihali ofisi iligharamia gharama zote za utafiti wa makala ile na hata kutulipa pesa nzuri tu kwa kipindi chote ambacho tulikuwa mkoani Geita.
“Sasa tunafanya nini jamani” aliuliza Lovenes.
“Unajua kama huu ni uzembe wa kipuuzi ulio ufanya wee Zahara” badala ya kujibu bwana Magembe Matiku aliyekuwa amefura kwa hasira alinitupia lawama.
Nilijisikia vibaya mno kwa maneno yale ya bwana Magembe lakini sikuwa na lakufanya kwani kweli kosa lilikuwa langu japo sikukusudia kulitenda.Sikujibu chochote zaidi ya kuwa kimya nikingoja maamuzi ya wenzangu juu ya ni kitu gani watafanya.
“Hatuna chaguo jingine zaidi ya kurudi Dodoma” Fidelix aliyekuwa kimya muda mwingi alishauri,ushauri ulioungwa mkono na John na hata Lovenes, Bwana Magembe alikuwa amevimba kwa hasira alitizama saa yake ya mkononi na kuona ilikuwa ni saa kumi na mbili na robo za jioni.
Aliachia breki na kuingiza gia kisha akaliondoa gari kwa kasi na kukata kona kwa kasi na kulielekezea kule tulikotoka.
Safari ya kurudi Dodoma ikaanza.
Ilituchukua dakika arobaini na tano nyingine kufika Dodoma mjini na hapo tukanyooka na barabara kama tunaelekea singida na kilometa moja nyingine tukawa tumefika katika kile kituo cha mafuta ambacho kilikuwa na huduma ya mgahawa.
Hapo ilikuwa yapata saa mbili kasorobo usiku.
Nilikuwa wa kwanza kushuka katika gari na kukimbia ndani ya ule mgahawa,nilipo ingia ndani macho yangu moja kwa moja katika kiti nilichokuwa nimekalia ambapo ndipo nilipo weka lile jacket.
Moyo wangu ulinidunda kwa nguvu kutokana na kile nilicho kiona, kiti kile kilikuwa kitupu.lile jacketi halikuwepo mahala pale.
Sasa nilianza kuona dalili ya kupoteza kibarua chuangu kinacho niweka mjini mimi na familia yangu.
Kwa muda wa nusu dakika niliweza kuona maisha ambayo nitakwenda kuishi muda mfupi ujao baada ya kufukuzwa kazi katika kampuni.
Nilimwona mama mwenye nyumba wangu {mama Leila} namna atakavyo kuwa akinisumbua juu ya kodi yake ambayo ilikuwa ikielekea ukingoni, niliona namna wazazi wangu watakavyo kuwa wakinipigia simu mara kwa mara na kuhitaji msaada wa kifedha kutoka kwangu hali ya kuwa wakati huo mifuko yangu itakuwa imetoboka kwa kutokuwa na ajira yenye kuniingizia pesa.
Lakini pia, niliona namna mdogo wangu Nasri namna anavyo sitisha masomo yake kwa kushindwa kuendelea kumsomesha kwa kukosa ajira yenye kuniingizia fedha.
“Vipi dada yangu kulikoni?” nilistushwa na sauti ya muhudumu wa mgahawa ule aliyekuwa amesimama nyuma yangu na kunishangaa namna nilivyokuwa nimeganda mithili ya sanamu.
Lakini kabla sijamjibu, muda huohuo akina Lovenes nao wakaingia.
“Vipi umeliona” wote waliniuliza kwa pamoja kana kwamba waliambizana.
“Hapana, kiti ni kitupu, jacket halipo”
“Shuuuuph” mr Magembe alishusha pumzi huku mikono yake ikiwa kiunoni.
“Kwani kuna nini jamani”Muhudumu wa ule mgahawa aliuliza.
“Kuna jacket nililisahau katika kiti hiki wakati tulipo kuja kula chakula hapa kama lisaa limoja hivi limepita”
“Jacket la rangi ya kaki..?”
“Ndiooo” niliitikia upesi upesi nikihisi kuna uwezekano wa kulipata ile nguo kwa kuona muhudumu yule anaifaahamu.
“Hiyo nguo niliichukua na kuipeleka ofisini lakini alikuja mkaka mmoja jina lake nimelisahau alisema lile jacketi ni la mwenzenu ambaye mpo nae katika safari moja mkitokea geita na ulikuwa umelisahau na mmemtuma yeye aje kulichukua hapa”
“ Whaaat!.”
Wote tuliuliza kwa mshangao, kwa pamoja.
“Kwani ninyi huyo mtu hamjamtuma na hamjui?!” Muhudumu aliuliza tena kwa mshangao.
“Hicho kitu unacho sema kigeni kabisa.hatumjui huyo mtu” John alisema.
“Na kwani huyo mtu yukoje” niliongezea kwa kuuliza.
“Mkaka mweusi mrefu ana kitambi kidogo, wakati ninyi mnakula chakula yeye alikuwa amekaa katika kiti hicho hapo” Hapo taswira ya yule mtu aliyekuwa akinikodolea mimacho yake mibaya hadi nikaingia katika siku zangu sura yake ikanijia mbele yangu
“Blood fool mijitu mingine sijui ikoje kudada’deki ni lile likaka lililokuwa limekaa hapo likiniangalia hovyo” nilisema kwa ukali huku nikihisi huzuni isiyo na kifani
“Basi huyo mvulana atakuwa ni mwizi” lovenes alisema pia kinyonge.
“Sasa tunafaanya nini?” mtu mwingine aliuliza, mie nguvu zilikwisha, niliona nilichokuwa nimebakiza ni kufukuzwa kazi na kuingia uraiani na kupambana na ukali wa maisha kwa namna nyingine.
“Kuna kituo cha polisi hapo mbele kama hamto jali tuongozane tukafungue kesi” alisema yule mfanya kazi wa ule mgahawa.
Tulikubaliana na ushauri wa yule muhudumu tulikwenda kituo cha polisi na kufungua kesi kisha tukapewa Rb.
Baada ya hapo safari ya Dar ikaanza tena.

********

Saa sita na nusu za usiku tuliingia jijini kila mtu alikuwa amechoka vibaya..baadhi ya watu walishukia Ubungo ila kwakuwa mr Magembe alikuwa akiishi Gongo la mboto na mimi nilikuwa nikiishi Buguruni malapa alinisogeza hadi buguruni sheli na kuniacha pale.
 
JUMBA LA WACHAWI
Mwandishi/mtunzi; Zulfa Huseni
SEHEMU YA 3

Saa sita na nusu za usiku tuliingia jijini kila mtu alikuwa amechoka vibaya..baadhi ya watu walishukia Ubungo ila kwakuwa mr Magembe alikuwa akiishi Gongo la mboto na mimi nilikuwa nikiishi Buguruni malapa alinisogeza hadi buguruni sheli na kuniacha pale.
Pale nilichukua bajaji usiku ule na kumtaka dereva anipeleke malapa.
Njaa ilikuwa inauma lakini sikuwa na hamu ya kula chakula chochote, nilikuwa mnyonge mno.
Usiku ule nilikuta geti la nyumbni kwangu limefungwa nilizunguka katika dirisha la mama mwenye nyumba na kumgongea anifungulie mlango.
“Eeh Zahara huyoo!”
“Ndiye mimi mama”
“Karibu mwanangu za huko”
“Salama tu mama za hapa”
“Hapa kwema mwanangu sijui mnatunyima nini huko”
“Mvua, matope na baridi”
Nilisema kwa utani, na hapo mama akacheka huku mimi nikifungua komeo la mlangoni kwangu na kuingia ndani.
“Halafu….we zahara ”
“Abee mama”
“Kuna baba mmoja amekuja hapa leo kukuulizia mara kumi kumi” alisema mama mwenye nyumba.
“Baba yupi huyo?”
“hajaniambia jina lake ila anasema mlikuwa wote huko usukumani huko uliko kuwa na mlikuwa katika safari moja leo”
“Unasema!!” moyo wangu ulipiga mkumbo kama mdundo wa nyimbo za Marijani Rajabu, taswira ya yule mtu kule katika mgahawa ikanirejea tena usoni mwangu.
“Unasema kweli mama?”
“Ndio..kwanini nikuongopee mama”
“Hakuacha chochote hapa”
“Ameacha”
“Kaacha nini?”
“Namba ya simu”
Kidogo nilipata nguvu nikaona tumaini jipya la maisha yangu.,kwani niliamini nitavipata vifaa vyangu,na kwa mara ya kwanza nilijikuta naomba toba kwa Mungu wangu kwa kumuhisi vibaya yule mtu.,kwakweli hakuwa ni mtu mbaya angekuwa mwizi kama ambavyo tulimuona kamwe asinge fika pale nyumbani kunitafuta ilihali akiwa ameiba vitu vyangu
“Mungu wangu nisamehe kwa kumuhisi vibaya huyu kaka” nilisema kimoyo moyo huku nafsi yangu ikiwa na furaha.
Jambo moja ambalo sikuwahi kujiuliza muda ule ni vipi mtu yule alinifahamu mimi kuwa nilikuwa geita na pia kujisema kuwa alikuwa na mimi pamoja huko geita, lakini kubwa kuliko yote ni vipi alipajua nyumbani kwangu ninapo ishi.
Nikiwa bado ni mwenye faraja moyoni, mama mwenye nyumba alinipa kipande cha karatasi kilicho kuwa kimeandikwa namba ya simu.
Kwa mara nyingine nilishukuru mno,niliingia ndani mwangu na kuwasha taa kisha nikaketi kitandani, kabla ya kufanya lolote nilitoa kadi yangu ya posta na kutoka nje kutafuta vibanda vya simu.
Sikupata tabu kupata kibanda cha simu,.niliandika zile namba kisha nikazipiga
Simu ilita upande wa pili kwa muda kidogo kisha ikapokelewa na sauti nzito yenye mkwaruzo.
“Hellow”
“Habari yako kaka” nilisalimia
“Sijambo..ooh Zahara, hujambo bibie” alijibu yule mtu, nilistuka kidogo, vipi huyu mtu anijue namna hii,amejua vipi jina langu.
“Safi tu, nafikiri ni wewe uliyekuja kunitafuta nyumbani kwangu?”
“Bila shaka”
“Na bila shaka ni wewe uliye ondoka na jacket langu kule Dodoma?”
“Haswaaa” alijibu tena yule mtu, nilishusha pumzi ndefu nikahisi furaha ikiongezeka moyoni kwa kulipata jacket langu lililokuwa na vitu muhimu.sikujali wala sikuwa na habari tena na namna yule mtu alivyotumia utaratibu wa kulichukua lile jacket kule katika mgahawa, kilicho kuwa katika akili yangu wakati huo ni kuhakikisha naipata ile nguo yangu hususani vitu vilivyokuwa ndani ya lile jacket
“Sasa nalipata vipi hilo jacket?” niliuliza.
“Njoo agrey kariakoo”
“Sasa hivi?” niliuliza kwa mshangao huku nikitizama saa na kuona ilikuwa yapata saa saba na nusu usiku.
“Ndio lazima iwe sasa hivi vinginevyo unaweza kulikosa, mie kesho asubuhi naondoka na basi la chakito kuelekea mlalo huko lushoto.
Nilisimama wima nikapatwa na taharuki ya kulikosa jacket, japo sikuwa tayari kabisa kulikosa tena lile jacket.
Niliagana na yule mtu na kumuhakikishia kuwa nitakuwa mtaa ule wa Agrey muda mchache ujao.
Nilikurupuka na kutoka mule ndani bila hata kumwaga mama mwenye nyumba usiku ule na kutokomea mtaani.
Nilipanda basi la mjini kwa miaka hiyo yalikuwa ni yale mabasi ya kizamani kabisa yenye kuitwa chai maharagwe lililo nipeleka hadi mtaa wa agrey kariakoo.
Hapo nilisimama mbele ya stendi ya mabasi ya tabata na buguruni kisha nikaingia katika kibanda cha kupiga simu na nikampigia simu tena yule mtu.
“Shuka mbele kidogo huku, kama unakuja mnazi mmoja, tizama upande wa kushoto utaona ATM ya NMB kisha ingia katika ghorofa inayofuatia, panda juu hadi orofa ya nne, utanikuta katika korido ya milango ya lifti nakungoja..”
Baada ya kupewa maelekezo hayo nilizipiga hatua kuelekea eneo lile nililoelekezwa, bahati ni kuwa hapakuwa mbali.
Dakika chache nyingine nilikuwa katika lift ya jengo lile ambalo sikujua ni jengo linalo jishughulisha na nini, kilicho nistajabisha ni kuwa hapakuwa na mlinzi katika jengo lile.
Lakini hata hivyo sikujali sana kwani kilicho nipeleka pale ni vitu vyangu vya ofisini na si vinginevyo.
Sekunde kumi nyingine milango ya lifti ilifunguka,tayari nilikuwa orofa ya nne,
Nilitoka ndani ya ile lift.
Hapo nikakutana na yule mtu mwenye kupenda kunitizama. Alipo niona aliachia tabasamu ambalo nililiona kule Dodoma,lile tabasamu liliongea kitu, nafikiri lilisema “nimekutana na mwanamke mrembo”.
“Karibu Zahara” alinikalimu huku akinipa mkono tabasamu lake likizidi kustawi usoni mwake.
“Nakushukuru sana”. Nilijibu huku na mimi nikimpa zawadi ya tabasamu, akanionyesha ishara nimfuate, wakati naongozana nae, macho yangu yalikuwa yakisaili ile nyumba ilikuwa ni kama hotel ya kisasa kwani kila tulipo pita katika korido, niliona vyumba vilivyo andikwa namba mithili ya vyumba vya hoteli ya kisasa, sikuwa na uhakika sana na hisia zangu kuwa huenda ile nyumba ikawa hoteli kwani nilivyo ingia katika ile nyumba sikuona mapokezi wala sikukutana na mtu yeyote mbali na yule mbaba mwenyeji wangu
 
UMBA LA WACHAWI
Mwandishi/mtunzi; Zulfa Huseni
SEHEMU YA 4

“Nakushukuru sana”. Nilijibu huku na mimi nikimpa zawadi ya tabasamu, akanionyesha ishara nimfuate, wakati naongozana nae, macho yangu yalikuwa yakisaili ile nyumba ilikuwa ni kama hotel ya kisasa kwani kila tulipo pita katika korido, niliona vyumba vilivyo andikwa namba mithili ya vyumba vya hoteli ya kisasa, sikuwa na uhakika sana na hisia zangu kuwa huenda ile nyumba ikawa hoteli kwani nilivyo ingia katika ile nyumba sikuona mapokezi wala sikukutana na mtu yeyote mbali na yule mbaba mwenyeji wangu.
Safari yetu ilishia mbele ya mlango mmoja ulio andikwa Room No 104. alisukuma mlango wa chumba kile na kujitoma ndani, “karibu Zahara..pita ndani”
“Asante”, niliingia ndani ya chumba kile, kilikuwa ni chumba nadhifu ndani kukiwa na kila kitu cha thamani kinacho takiwa kuwapo chumbani.
Niliketi katika kochi huku macho yangu yakizidi kusaili mule ndani,.sikuwa na wasiwasi na lolote.
Kitu kimoja ambacho sikuwahi kukijua wasaa ule ni kuwa uwepo wangu eneo lile ungeweza kunisababishia madhila makubwa mno ambayo nisingeweza kuyasahau kwa milongo mingi juu ya mgongo wa ardhi.
Yule mtu alisogea katika kabati la nguo na kufungua, kisha alitoa jacket langu na kunikabidhi, nilifurahi, muda huo huo nilianza kulipekua ili kuona kama vifaa vyangu vipo salama.
Naama vitu vyangu vyote vilikuwa salama, nilishusha pumzi ndefu na kuhisi furaha nyingi moyoni. “Asante sana kaka yangu, sina cha kukulipa kwakweli, ila nashukuru mno kwa wema wako vitu hivi ni muhimu mno”
Yule mtu alitabasamu, lakini hakufumbua mdomo, alitizama pembeni bila kujibu shukrani zangu kwa sekunde sita au saba kisha akasema, “usijali Zahara ilikuwa ni lazima hili litokee ili upate kunifahamu”
“Yeah.. ni kweli, hakika Mungu ndio mapangaji wa kila kitu ulimwenguni”
“No, no,no hili halihusiani na mipango ya Mungu Zahara, huu ni mpango wa sisi wanadamu”
“What!!”
Niliuliza kwa mshangao, maneno ya yule mtu yalinichanganya.
Yule mtu alinisogelea pale sofani na kuketi mkabala na mimi.
“Huu ni mpango wangu mahsusi” alisema tena kwa utulivu huku akinitumbulia macho yake makali pasina kupepesa kando.
Nilifikiri kwa muda, nikaona kwa dakika nyingine tena nashindwa kabisa kumuelewa yule mtu yale maneno yake.
“Any way, acha niseme tu nashukuru na sasa wacha mie niondoke maana usiku usha kuwa mkubwa” hatimae niliona ni kheri niage na kuondoka maana sikuwa na sababu nyingine ya kuumiza kichwa kwa maneno ya yule mtu ambayo nilihisi alitamka pasina kufikiri, aidha hisia zingine zikaniambia pengine alikuwa amekunywa pombe kidogo na kuvuruga kidogo ubongo wake.
Nilisimama na kuzipiga hatua kuelekea mlangoni, “sawa kila kheri mrembo” yule mtu alisema, sikumjibu zaidi ya kuachia tabasamu lililosema “tuko pamoja”
Nilipita katika ile korido na kukata kulia kuelekea katika lifti. Pale katika korido ya lifti nilikuta lifti zote tatu zikiwa zinatumika, hivyo nilisisima na kusubiri kwa muda kidogo.
Dakika moja badae mlango wa lifti moja katika zile tatu ukafunguka, bila kuchelewa nikajitoma ndani.
Nilibonyeza kitufe kilicho andikwa G1, lifti ilishuka chini na sekunde tano tayari taa ya kijani ikaonyesha nimekwisha fika G1, nilitoka ndani ya lifti ile nikiamini sasa naweza kutoka nje ya jengo lile na atimae kurejea nyumbani usiku ule.
Ajabu ni kuwa, pale lifti ilipo simama na mimi kutoka nje, nilikutana na mzingira mageni machoni mwangu. Halikuwa eneo la nje ila nilipo chunguza vizuri niligundua nilikuwa orofa ya kwanza, hapo nikagundua nilifanya makosa wakati nilipo kuwa mule ndani ya lifti ile, sikutakiwa kubonyeza ‘G1’ badala yake nilitakiwa kubonyeza ‘G’ pekee, hiyo ingenipeleka hadi chini kabisa ya ghorofa lile.
Lakini hata hivyo sikuona tabu kwani chini hapakuwa mbali ni kiasi cha kushuka ngazi kama nne na kuweza kuwa nje ya jengo lile.
Nilizifuata ngazi na kuanza kushuka chini. Eneo lile lilikuwa kimya, kulikuwa na taa za bulb kubwa zilizo toa mwanga hafifu wa rangi ya njano, nilishuka ngazi ya kwanza na sasa nikashika ngazi ya pili. Chini ya ile ngazi ya pili, nilipata kuona kitu..
Eneo lilikuwa kimya kama nilivyo pata kusema. Mwendo wangu wa kasi wa kushuka ngazi ukabadilika na sasa nilishuka taratibu nikitupia macho kitu nilicho weza kuona, na hapo nika jua alikuwa ni mtu.
Alikuwa amejikunyata pembezoni mwa zile ngazi, alikuwa amejifunika shuka nzito la rangi nyekundu mwili wote kasoro kichwani.
Jambo moja lilipita kichwani mwangu, kwa vyovyote vile yule mtu atakuwa ni mlinzi, wazo hilo lilizidi kustawi katika akili yangu baada ya kutizama saa na kuona ilikuwa yapata saa nane kasoro dakika kumi za usiku, “ hawezi kuwa mtu wa kawaida eneo hili,tena muda huu pasina kuwa ni mlinzi”
Hatua zangu zikiwa za kawaida kabisa nilifika eneo lile ambapo mtu yule alikuwa amejikunyata, nilimpita pasina kumsemesha lolote na kukuta kushoto kwa ajili ya kuanza kushuka ngazi zinazo fuatia.
Ila ghafla.
Sauti ilitoka kwa yule mtu ilinifanya nitishike vibaya mno,yule mtu alisema, “Usiku mwema Zahara” niligeuza shingo na kutupa macho yangu na kumwangalia yule mtu, hapo nikakutana na kitu ambacho kilinifanya hali ya mshangao, niliduwaa, macho yamenitoka,midomo imefumbuka kama lango la daradara aina ya UDA la mbagara, nikaanza kutokwa na jasho, kitu kisicho cha kawaida nikaona kinanyemelea maisha yangu.alikuwa ni yule mtu aliyekuwa na jacketi langu lililokuwa na vitu muhimu vya ofisi.
Nilijikuta nataka kutimua mbio ila miguu ilikuwa mizito nikabaki nimeganda namtizama yule baba.
“Hivi Zahara pamoja na kusaidia kibarua chako hujataka kunifahamu hata jina langu bibie?”. Yule mtu aliuliza huku akisimama kwa tabu eneo lile.
“We umefikaje fikaje hapa?” badala ya kujibu nilijikuta namtupia swali huku nikiendelea kumshangaa na sasa haukuwa mshangao tu bali ulikuwa ni hofu kubwa iliyochanganyikana na mshangao.
Yule mtu alisimama wima akiwa bado amejifunika lile shuka jekundu, miguuni akiwa peku.
“Katika maisha yangu ya Kichawi sijawahi kuona mwanamke msomi lakini wakati huo huo ni zumbukuku wa mwisho kama wewe!.” Yule mtu alisema, kauli ile ilinifanya mwili wote uingiwe na baridi na kuwa kama mithili ya mtu aliye mwagiwa maji ya baridi. Pumzi zilinitoka kwa kasi sasa nikaona kumbe nimekutana na kiumbe kisicho cha kawaida, sikutaka zaidi kuyatafakari maneno mengine ya yule mtu, neno ‘Mchawi’ lilitosha kabisa akili yangu kuiamrisha miguu yangu ikimbie kwa kasi eneo lile.
Nilitoka mbio nikiwa nimekumbatia jacket langu kifuani nikitoa yowe dogo la msaada, nilizishuka ngazi upesi upesi upesi huku nikiyumba hovyo.
Nikamaliza zile ngazi sasa nikashika ngazi za mwisho na kuwa chini ya jengo lile, wakati nashuka ngazi ya kwanza, ngazi ya pili ile nashuka ngazi ya tatu tu.. nilijikuta nikifunga breki ghafla na kubaki nimesimama huku nikiweweseka.
Yule mtu alijitokeza kutokea kona ya mwisho ya ile ngazi, alitembea kikakamavu kunisogelea huku mwendo wake ukifanana kabisa na viumbe aina ya saibogi, alikuwa akinijia kwa mwendo wa kunyata lakini akijiamini, macho yake yakiwa makali, huku sura yake kwa ujumla akiifinya na kufanya awe na mwenekano wa kutisha, alichanua vidole vya mikono yake na kutanua mikono yake huku akitoa ngurumo ndogo mithili ya mtu aliye pandisha majini na akawa ananisogelea. Kwakweli niliogopa mno.
Kwa muda wa sekunde zisizo zidi tatu, nilibaki nimebung’aa nikishangaa yale mambo yaliyo kuwa yanajiri mbele yangu katika jumba lile kabla ya kujikuta nikipiga kelele kwa nguvu.
“Mamaaaa, mamamaaa nakufaaaa uwiiiiii nisaidieniii” nilipiga kelele nyingi huku nikitoka mbio kupandisha ngazi kurudi juu.
Nilikuwa nahema kwa kasi, nikizidi kupiga kelele huku nikijitahidi kuzipanda ngazi za jengo lile kujitenga na yule mtu wa ajabu, mashaka makubwa yalikuwa kifuani kwangu.
Sikumbuki vizuri nilipanda ngazi hadi orofa ya ngapi, ila ninacho kumbuka ni kuwa ilifikia hatua mapafu yangu yalichoka, nilichoka kupiga mayowe kwa nguvu huku nikizipanda ngazi tena nikiwa nakimbia.
 
JUMBA LA WACHAWI
Mwandishi/mtunzi; Zulfa Huseni
SEHEMU YA 5

Nilikuwa nahema kwa kasi, nikizidi kupiga kelele huku nikijitahidi kuzipanda ngazi za jengo lile kujitenga na yule mtu wa ajabu, mashaka makubwa yalikuwa kifuani kwangu.
Sikumbuki vizuri nilipanda ngazi hadi orofa ya ngapi, ila ninacho kumbuka ni kuwa ilifikia hatua mapafu yangu yalichoka, nilichoka kupiga mayowe kwa nguvu huku nikizipanda ngazi tena nikiwa nakimbia.
Niliangaza nyuma yangu na kuona niko peke yangu, hapakuwa na mtu yeyote aliye kuwa akinifuata lakini pia hakujitokeza mtu kunisaidia, pamoja na kwamba nilikuwa nikipiga makelele ya hali ya juu, lakini hata hivyo sikumwona tena yule mtu wa ajabu.
Sasa nikiwa najisukuma kwa mbele kwa mwendo wa kutembea nikiendelea kuzipanda zile ngazi, nilikuwa nahema kwa kasi, machozi na kamasi vilikuwa vikinitoka kwa pamoja, woga wa kuingia katika mikono ya mchawi ulikuwa mkubwa.
“Mungu wangu wa mbinguni uko wapi sasa muda huu!.huoni ninavyo ingia katika madhila haya? Sasa unangoja nini kunisaidia Yarabii..” nilijikuta nikitamka yale maneno huku nikiwa nimepagawa katika kiwango cha mwisho.
Nilizidi kuzipanda ngazi bila kuona dalili yoyote ya kufatwa ama uwepo wa mtu katika jengo lile, eneo lote lilikuwa kimya, ilikuwa ni sauti ya vishindo vya hatua zangu kupanda zile ngazi ndio zilizo sikika.yanii ilikuwa ni kama kwamba kile kilicho tokea muda mchache kilikuwa hakija tokea.
Ni hapo nilipo ingiwa na fikra hizi, kuwa huenda ndani ya ghorofa hili kulikuwa na mtu mmoja tu yanii yule mtu mchawi.
Wakati nalitafakari hilo akilini mwangu wazo jingine likanijia, “kwanini nazidi kuelekea juu ama ndani zaidi ya jengo hilo?” nilijiuliza mwenyewe swali hili lakani jibu lake lilikuwa ni jepesi tu, nikajipatia jibu mwenyewe kuwa “naelekea juu ama ndani zaidi ya jengo lile kwakuwa namkimbia yule mtu asiye wa kawaidi” lakini nikajiuliza tena, “kama namkimbia yule mtu asiye wa kawaida kwa kuingia ndani zaidi ya jengo lile eneo ambalo inavyo onyesha ndio himaya yake na anajua kona zote za jengo lile, je zile hazitakuwa ni sawa na mbio za siafu.? Na hiyo si ni sawa na kujiingiza ndani ya kichaka cha adui?.”
Nilijiuliza..
Lakini ubongo wangu haukupata jibu. Ni hapo nilipo hisi sauti fulani ikinitahadhalisha kuendelea kuzipanda ngazi za jengo lile.
Nilisimama ghafla na kubaki nimeganda. “Sasa nifanye nini Mungu wangu” nilisema kwa sauti ya ya kunong’ona. Mwisho niliazimia Lazima nitoke nje ya jengo hili liwalo na liwe lakini lazima niwe nje.
Kwa mara nyingine nikajikaza kama mwanamke nikageuka nyuma na kuanza kuzishuka ngazi tena, wakati nikiwa nashuka chini kwa bahati upande wangu wa kulia mwa ukuta niliona kuna mtungi wa gesi lakini pembeni ya mtungi huo kulikuwa na shoka ndogo ya chuma yenye rangi sawa na ile ya ule mtungi wa gesi.
Bila kujiuliza mara mbili niliifyatua ile shoka iliyokuwa umepachikwa katika kishikizio chake pale ukutani, sasa nikawa tayari kupambana na yule baba machawi pale itakapo bidi.
Nikaendelea kuteremka taratibu nikiwa na tahadhali kubwa, wakati huo ilikuwa yapata saa saba na dakika hamsini.
Kitu kingine ambacho ningependa ndugu msomaji ufahamu, ni kuwa, tangu niingie katika jengo lile nilipata kutizama saa yangu ya mkononi mara mbili, ajabu ni kuwa muda ulikuwa ikienda taratibu zaidi ya kawaida.
Kwa kipindi ambacho nimetumia kuwasili katika lile jengo hadi kutokea kwa sinto fahamu, kwa makadirio ilikuwa yapata kiasi cha dakika thelathini lakini saa yangu ilinionyesha ni kiasi cha tofauti ya dakika tatu tu toka niingie hadi sasa.
Sikufikiria zaidi hilo kwani akili yangu ilifikiria zaidi ni kwa namna gani nitatoka Mule ndani.
Nikiwa bado nashuka zile ngazi kwa mbali nikahisi kuna chakala chakala za mtu kutokea huko chini niliko kuwa naelekea, nilipunguza mwendo nikauvaa ujasiri na sikuwa tayari kurudi nyuma, sasa nikaelewa kuwa kutokea kule chini kulikuwa kuna mtu aliye kuwa akipanda ngazi kwa kasi, zaidi ni kuwa mtu huyo alikuwa akitweta huku akitoa sauti kama ya mtu aliyepagawa kutokana na taharuki Fulani.
Sauti iliendelea kunikaribia na ilikuwa ni sauti ya mwanamke, nilisogea pembeni na kutupa macho kule chini, nilimwona mwanamke mnene kiasi, akizipanda ngazi kwa kasi lakini akiwa ni mtu aliye changanyikiwa vibaya mno.
Nilipata hofu moyoni, nikalewa kwa vyovyote vile mwanamke yule lazima atakuwa amekutana na yule baba mwenye kujisema kuwa yeye ni mchawi.
Nilisimama pale katika ngazi kumngoja yule mwanamke nikiamini kwa vyovyote vile masaibu yaliyomkuta yanafanana na yangu hivyo sina budi kuunguna nae na kuangalia njia ya kutatua sintofahamu ile.
Yule mwanamke sasa alianza kupanda ngazi moja kabla ya kuanza ngazi ya pili niliyokuwa nimesimama mimi.
Na wakati anamaliza zile ngazi ile anaanza tu kupanda, alisimama ghafla na kupiga ukulele mwingi wa hofu baada ya kuniona mimi.
“Nyamaza,..nyamaza..tulia tafadhali, mie sio mtu mbaya”, nilisema kwa sauti ya juu, yule mwanamke alitulia kidogo akawa ananiangalia kwa mashaka makubwa.
“Tulia tafadhalia mimi pia nina matatizo kama yako” niliendelea kumsihi yule mwanamke.alibaki akihema huku akiliangalia lile shoka nililokuwa nimelikamata, kwakweli ilimchukua sekunde kadhaa kabla ya kuniamini.
“Wanakuja” yule mwanamke alisema huku akihema kwa kasi.
“Akina nani!”
“wanakuja kuniua tukimbie..wako wengi..wanakuja” alisema yule mwanamke wa makamo pasina kunipa taarifa vizuri.
“Wako wapi akina nani?” nilimuuliza.
Lakini hakujibu zaidi ya kusonta kwa kidole kuonyesha kuwa wako huko aliko toka na kabla sijasema kitu kingine yule mwanamke alitoka mbio na kuzidi kupanda juu.
Moyo wangu ulipiga paaaa, nilihisi tumbo linapata joto huku mate mepesi yakijaaa mdomoni lakini pia jasho jembamba lilinitoka maungoni mwangu.
Nikabaki nimesimama pale moyo wangu ukishindwa kabisa kwenda mbele lakini pia akili yangu haikuwa tayari kabisa kurudi nyuma nilibaki nimegenda kama sanamu la askari pale posta.
Yule mama alizidi kuziparamia ngazi na kutokomea kabisa kule juu. Sasa nikaelewa kuwa kumbe kuna watu zaidi ya mmoja katika hili jengo, si kama nilivyokuwa nikifikiria hapo awali.
Nikiwa bado pale, shoka langu likiwa mkononi, nilitupa macho yangu kule chini nilikokuwa naelekea, nilicho kiona kilinitisha sana.
Watu wanne wanaume walikuwa uchi wa mnyama, walikuwa wamebeba mwili wa mtu aliyekuwa kama mtu aliye ungua na moto,mwili wa yule mtu aliye kuwa amebebwa katika machela ulikuwa na nyama nyekundu iliyoonyesha kama mtu yule amebabuliwa na mafuta ya moto, wale watu walikuwa wamejipaka masizi meusi usoni mwao na kufanya waonekane kama vinyago vya kimakonde. Walikuwa wakizipanda ngazi kuja juu nilikokuwa mimi huku wakiimba nyimbo Fulani kwa lugha ambayo sijawahi kuisikia hapa duniani.
Kwakweli nilijikuta nikipiga kelele nyingi na kutoka mbio huku nikitupa kile kishoka na kupanda juu mradi nijiweke mbali na jambo lile la kutisha.
 
JUMBA LA WACHAWI
Mwandishi/mtunzi; Zulfa Huseni
SEHEMU YA 6

Nikiwa bado pale, shoka langu likiwa mkononi, nilitupa macho yangu kule chini nilikokuwa naelekea, nilicho kiona kilinitisha sana.
Watu wanne wanaume walikuwa uchi wa mnyama, walikuwa wamebeba mwili wa mtu aliyekuwa kama mtu aliye ungua na moto,mwili wa yule mtu aliye kuwa amebebwa katika machela ulikuwa na nyama nyekundu iliyoonyesha kama mtu yule amebabuliwa na mafuta ya moto, wale watu walikuwa wamejipaka masizi meusi usoni mwao na kufanya waonekane kama vinyago vya kimakonde. Walikuwa wakizipanda ngazi kuja juu nilikokuwa mimi huku wakiimba nyimbo Fulani kwa lugha ambayo sijawahi kuisikia hapa duniani.
Kwakweli nilijikuta nikipiga kelele nyingi na kutoka mbio huku nikitupa kile kishoka na kupanda juu mradi nijiweke mbali na jambo lile la kutisha.
Niliendelea kwenda kasi, atimae nikafika mwisho kabisa wa ghorofa lile, nilikuwa niko juu kabisa ya lile jengo pale juu kukiwa na eneo kubwa la wazi, kulikuwa na mitambo mbali mbali ya vitu kama setelite pamoja na antena.
Nilisogea mwisho wa ukuta na hapo niliweza kuona mandhali ya jiji la Dar es salam, jiji lilikuwa kimya, mataa ya umeme yakifanya mji kunga’aa na kuvutia. Kwakweli machozi yalinitoka.
Nilijikuta nalia kama mtoto mdogo, sasa niliona kama ndio naiona nchi kwa mara ya mwisho na badae kushikwa na wale watu na kufanywa mbuzi wa kafara.
Niliangalia chini nikaona niko umbali mrefu kutoka ardhini kiasi kwamba kama ikitokea umeanguka kutoka kule juu basi ukifika chini mifupa yote huna.
Nililia mno, sikujua kwanini yote haya yananitokea mimi, nilijiona ni mwanamke mwenye bahati mbaya katika siku za ukubwa wangu.
Niliikumbuka familia yangu, nikawakumbuka wafanyakazi wenzangu hususani timu nzima niliyokuwa nayo kule safarini geita. Kwakweli nilihuzunika mno, nilitamani nipaze sauti yangu na iwafikie watu ambao wangeweza kuja kunipa msaada lakini sikuweza.
Na mwisho mawazo yangu yakakita kwa Thabiti Talib Mwaikimba ni mpenzi tuliye kuwa na ndoto kubwa ya pamoja, ndoto ya kufunga ndoa ndogo tu ya mkeka, tuwe na biashara yetu ndogo itakayo leta matokea makubwa,
kisha tuzae mtoto mmoja mzuri ambaye tutamsomesha hadi chuo kikuu.
Lakini kila kitu hadi wakati huo, niliona kinaeleka kubaki kuwa hadithi tu kama zile za mwandishi Adam Shafi.
Nikiwa bado nafikiria mambo yale mara nikasikia vishindo, nilikurupuka upesi nikajisogeza karibu na lilipo kuwa sinki kubwa la maji aina ya sim tank kwa lengo la kujificha.
Nilipo sogea tu pale katika lile sinki mara moyo wangu ukapiga mkumbo na kujikuta naruka hatua moja kwa pembeni kisha nikabaki nimebung’a.
Yule mwanamke niliyekutana nae kule ndani alikuwa amejificha pale, alikuwa amejikunyata miguu yake ameikumbatia karibu kabisa na kifua chake huku kichwa chake akiwa amekiegemeza katika magoti yake.
Ajabu ni kuwa yule mama alikuwa ameganda hatikisiki wala hasemi lolote, wakati huo huo wale watu waliokuwa uchi huku wamebeba machela iliyokuwa na mwili wa mtu aliyekuwa amebabuka mwili wote waliwasili eneo lile.
Hapo hapo nilikurupuka na kusogea upesi pale alipokuwa amejikunyata yule mwanamke. “wa..wa.me..fika” nilisema kwa kunong’ona kumwambia yule mwanamke.
Nilikuwa natetemeka vibaya mno, nilichungulia kidogo, nikaona wanashusha mwili wa yule jamaa aliyekuwa katika machela ambaye bila shaka alikuwa amekwisha fariki na kuuweka chini.
“uu..wiii leo..mama..ya..ngu weeee!!” nililia, mwili wote ukiingiwa ubaridi,ila yule mwanamke alibaki akiwa vile vile ameganda hasemi wala hajibu lolote hata ile hofu yake haikuwepo.
Nikahisi kitu kisicho cha kawaida kwa yule mwenzangu, nilimtizama nikamwona uso wake ukiwa ni wenye hofu kubwa ila macho yake yamekodoa sehemu moja bila kope za macho yake kupepesa.
Hakuna kiungo katika mwili wake kilichokuwa kinatikisika. “Hey..hey” niliiita.
Kimya.
“Hey wee ma..ma” niliita tena kwa kunongo’na.
Kimya tena, hakukuwa na jibu.
“Wewe..mbo..na hu,.semi ki..tu?” nilimsemesha kwa kunongo’ona.
Kimya kwa mara nyingine.
Nilimsogelea nikamgusa, hapo hapo yule mama akaanguka chini kama mzigo.niliruka hatua moja nyuma kwa woga.
Hapo nilipata kujua kuwa yule mama alikuwa amekufa. Nilichanganyikiwa sana. Nililia nikifinya sauti yangu kwa chini ili wale watu wasinisikie.
“Wewe mama sasa unafanya nini hivyo!” nilisema kibweege huku nikitetemeka kama mtu mwenye degedege, yule mtu alikuwa amekufa huku akiwa amekodoa macho kama kwamba kabla ya kifo chake aliona tukio baya la kuogopesha.
“Hellow Zahara”, ghafla..sauti ilitokea nyuma yangu…nilistuka, “uwiii”,niliruka kwa hofu huku nikiachia ukulele kisha niligeuka, macho kwa macho nikakutana na yule baba,. “uwiiiiiiiiiiiii” nilipiga kelele nyingi za hofu.
Na bila ya kutarajia nikajikuta nazungukwa na wale watu wanne waliokuwa na masizi usoni mwao mithili ya vinyago vya kimakonde.
“Toka..to..ka..to..ka” nilisema kwa fadhaa kama kwamba nafukuza nyani shambani. Wale watu wakawa wananisogelea taratibu huku wakiwa wamekodoa macho yao na vidole vya mikono yao wamevichanua kama majini, lakini yule baba mchawi mwenye shuka jekundu yeye alikuwa amesimama vilevile.
Kadri walivyokuwa wakinisogelea ndivyo nilivyo ona kifo changu kinazidi kuwa karibu yangu.
“Mamaaaaaaa” nilipiga ukulele mkubwa wakati wale watu wanne walipo nifikia, na sauti yangu ikasambaa katikati ya jiji usiku ule, huku mwangi ukiniitikia kwa mara ya pili masikioni mwangu.
Sasa mikono ya wale viumbe ikanikamata, ikaushika mwili wangu kwa pamoja, nilihisi mwili wote unakufa ganzi punde baada ya kuguswa na wale viumbe. Lakini wakati huo huo nikabebwa kwa nguvu ya ajabu na wale watu wakawa wameni-ning’iniza juu juu kunipeleka mahala nisipo pajua.
Nilipiga ukulele mwingi kujaribu kufurukuta na kujinasua kutoka katika mikono ya wale watu lakini mikono yao ilikuwa na nguvu za ajabu kadri nilivyo zidi kufurukuta ndivyo mikono ile ilivyozidi kunibana kwa nguvu hadi nikawa napata maumivu.
Walinipeleka ndani ya lile jengo kisha wakaniingiza ndani ya chumba kimoja miongoni mwa vyumba vingi vilivyokuwapo katika nyumba ile ya ghorofa
Bila kutarajia nikajikuta narushwa hewani, niliachia ukulele wa kuogofya baada ya tukio hilo lakini nikajikuta naangukia sehemu laini yenye kunesa nesa. Ilikuwa ni kitandani.
“Waiiii..uwiiiii” nilipiga kelele nyingi huku nikikurupuka pale nilipo angukia na kujiweka sawa.akili yangu niliona kama inazunguka kwani nilikuwa ni mtu mwenye mashaka makubwa vibaya mno.wale watu wanne walisimama kukizunguka kile kitanda kisha sura zao wakazielekeza juu huku macho wameyatoa vibaya.
“Ninyi ni akina nani na mnataka nini kwangu?” nilijikaza na kuuliza jasho likinitoka katika maungo yangu.
Hapakuwa na majibu niliyoyapata, wote waliniipuza kama kwamba hawakusikia swali langu. “nini hii? Kitu gani kinatokea katika maisha yangu mimi? Kwanini yote haya yananisibu mimi?” nilijiuliza mwenyewe lakini sikuwa na majibu na sikuona mtu wa kunipa majibu yale.
Wale watu wakiwa wanatizama juu na kuwa kama wanazungumza maneno Fulani kwa kunong’ona mara mule ndani ulianza kutoka moshi mweupe, niliona moshi mzito mweupe lakini sikujua ni wapi moshi ule unatokea,ule moshi ukasamba mule ndani na kuacha halafu Fulani nzito nisiyoweza kuielezea.
Aisee haya mambo endelea kuyasikia tu yanahadithiwa katika riwaya kwakweli ni mambo yenye kutisha si kawaida.
Kwa Dakika nilikuwa nimejikunyata katika kona ya kitanda kile kilichokuwa kimetandikwa mashuka mekundu huku rangi ya kuta za chumba kile ikiwa ni rangi ya maziwa.
 
JUMBA LA WACHAWI
Mwandishi/mtunzi; Zulfa Huseni
SEHEMU YA 7

Wale watu wakiwa wanatizama juu na kuwa kama wanazungumza maneno Fulani kwa kunong’ona mara mule ndani ulianza kutoka moshi mweupe, niliona moshi mzito mweupe lakini sikujua ni wapi moshi ule unatokea,ule moshi ukasamba mule ndani na kuacha halafu Fulani nzito nisiyoweza kuielezea.
Aisee haya mambo endelea kuyasikia tu yanahadithiwa katika riwaya kwakweli ni mambo yenye kutisha si kawaida.
Kwa Dakika nilikuwa nimejikunyata katika kona ya kitanda kile kilichokuwa kimetandikwa mashuka mekundu huku rangi ya kuta za chumba kile ikiwa ni rangi ya maziwa.
Nilijaribu kukisaili kile chumba haraka haraka nikaona kile kilikuwa ni chumba kikubwa tu kilichokuwa na vitu vichache tu, kabati la nguo, televisheni ndogo ya Hitachi, saa ya ukutani aina ya Ajanta, meza ndogo ya kioo iliyo beba simu ya mezani, na panga boi lililokuwa limefungwa ukutani ambalo lilikuwa likizunguka kwa kasi na kutoa upepo mkali mule ndani.
Kwakweli nilikuwa ni mtu mwenye hofu kuu, niliendelea kujikunyata pale katika kona ya kitanda huku nikilia na kumuomba Mungu wa mbinguni kimya kimya.
Mara macho yangu yakashuhudia tukio jingine lililonifanya nipige kelele nyingi,
Alingia yule baba akiwa na vazi lake lile lile,sura lake amelichafua kwa mikunjo mikunjo iliyo jipinda kama mkeka wa kisukuma huku akionekana ni mtu mwenye hasira kubwa, lakini kubwa kuliko vyote alikuwa ameshikilia kichwa cha yule mwanamke niliyekutana nae katika ngazi kabla ya kumkuta akiwa amekufa pale mafichoni.
“Mme..mchi..nja mtu.. na kumnyofoa kichwa?” nilisema kwa kitetemeshi, uzito wa kile nilicho kiona kilinielemea na kuniwia vigumu kuamini, nilikuwa nimeduwaa macho nimeyatumbua kwa yule baba huku mdomo wangu ukijikuta unaachama mshangao uliochanganyikana na hofu vikishika hatamu, kwakweli tukio lile lilikuwa kubwa mno kwangu.
Toka nizaliwe sikuwahi kushuhudia tukio baya na la kuogopesha kama lile, akili yangu haikuwa tayari kuamini tena kama wale walikuwa ni binadamu walio zaliwa na mwanamke, “bila shaka ni majini haya, mashetani, mizuka”, sikuona sifa stahiki za wale viumbe.
Mwisho niliishia kulia kwa uchungu na kusubiri zamu yangu ya kuchinjwa na ile mizuka.
Yule baba alisogea na kile kichwa kilichokuwa kinatiririsha damu kisha ile damu akawa anainyunyuzia katika kile kitanda nilichokuwa nimekalia.
Nilijikuta najitapikia hovyo huku nikihisi kichefu chefu cha hali ya juu.
Baada ya kufanya tukio lile yule baba aliwapa wale watu kile kichwa na mara wale watu wakaanza kukigombania kile kichwa kwa kukitafuna na kunyonya damu iliyokuwa inatoka katika shingo.
Kwa mara nyingine nikajikuta natapaika hadi nikahisi nguvu zikiniishia.wale watu wenye masizi na miilini mwao wakiwa uchi walitoka mule ndani huku wakiendelea kukishambulia kile kichwa cha binadamu.
Nikaelewa kitu,.
Kwa tukio lile nikapata kunga’amua kwa wale viumbe wenye masizi ndio vile viumbe vyenye kuitwa misukule, ama wengine wanaita ndondocha, lakini pia nikapata kuelewa kuwa yule baba mchawi wale misukule walikuwa ni viumbe vyake anao wafuga.
Kwa faida ya wale wasio elewa, Misukule ama mandondocha ni wale binadamu walioaminika kuwa wamefariki dunia lakini badala yake wanakuwa wamechukuliwa kichawi na wachawi kwa dhumuni maalumu.,
Nililifahamu hili upesi kutokana na habari za viumbe wa namna hii niliwahi kusoma katika vitabu hasa vile vya Ally Mbetu na pia hata kupata bahati ya kusikia hadithi zao kutoka kwa watu tofauti tofauti.
Sasa mule ndani tulibakia wawili tu, mimi na yule baba.
“Sijawahi kufanya jambo lolote baya” nilisema huku nikimtizama yule mtu kwa huruma,mtu ambaye muda mfupi ulio pita tulikuwa marafiki tena rafiki aliyenisaidia kuvipata vitu vyangu, lakini sasa kawa mtu mbaya na hatari kwa maisha yangu.
Yule mtu hakujibu kitu, alinyanyua mikono yake juu na kuanza kuzungumza vitu Fulani kwa lugha nisiyo ijua wala kuwahi kuisikia katika ulimwengu. Na kadili alivyokuwa akizungumza maneno Fulani hali yangu ilikuwa ikibadilika.
Nilikuwa nikijisikia kitu kama usingizi mzito ukizikumba mboni za macho yangu. “Mungu wangu ndio nakufa hivyo..” usigizi mzito ulikuwa ukinijia kwa kasi, wakati yule mtu akikazana kutamka maneno yale kwa nguvu tena kwa kuyarudia rudia. “kumbe ndivyo hivi mtu akitaka kufa inavyo kuwa” niliwaza wakati giza la ajabu likinipitia katika ufahamu wangu.
******************
Siku moja katika maisha nilidhani kubadilisha ndoto zangu na kuvurugikiwa ilihitaji miaka mingi jambo hilo kutokea. Nilidhani kuisha kwa uzuri wangu na kila nilichokianzisha toka nilipokuwa mdogo ilihitajika miaka mingi kama ile niliyokuwa nayo sasa. Nilikuwa msichana wa miaka 24 tu mwenye ndoto kubwa ambazo tayari sasa zilikuwa zinaeleka kutimia asubuhi ya siku inayo fuatia. Nilitarajia Kendesha gari zuri la kifahari na familia yenye furaha mchumba mzuri nitakea funga nae ndoa ndogo tu ya mkeka itakayo jumuisha watu wachache sana, ndicho kitu nilichokiwaza katika muda wote wa maisha yangu. Kwakweli Hatima ya maisha yetu anayeijua ni Mungu na kamwe huwezi kumuona na kumuomba muda zaidi maisha yafikapo tamati, kila kitu huvurugika pale jioni ya maisha yako ifikapo. Milango ya ndoto zako hufungwa na giza nene hutanda mbele, hata fimbo ya kukuongoza njia hupotea. Mwanga hufifia na woga hukusonga. Hiyo ndiyo hali iliyonipata katika usiku wa giza ni baada tu ya kupoteza jacket langu lililokuwa na vitu muhimu vya ofisini ambalo liliokotwa na mtu wa ajabu.
Kichwa changu kilikuwa kizito, nilipo fumbua macho, hata macho nayo yaalikuwa mazito, kwa mbali niliona ukungu mbele yangu huku nikiona kufifia kwa vitu vilivyoonekana mbele yangu.
Nikiwa nimelala, chali macho yangu yakiwa yanitizama katika dari ya chumba nilicho kuwepo huku fahamu zangu zikiwa hazija kaa sawa nilihisi chakara chakara ubavu wangu wa kulia. Nikageuza shingo yangu.
Mtu mwanaume alikuwa uchi huku akichezea sehemu zake zilizokuwa wima kama ukuni mkavu, alikuwa akiniangalia huku akilamba lamba lips za midomo yake.
Sasa mtiririko wa matukio yote yaliyo tokea kabla ya kupitiwa na usingizi mzito yakarejea tena upya, nikajikuta nataka kupiga kelele, lakini ajabu sikuwa na nguvu hata ya kufumbua mdomo.
Ni wakati huo huo pia nilipogundua kuwa hata mimi pia nilikuwa uchi wa mnyama pale nilipokuwa nimelala chali.
“Nataka kubwakwa ‘Yaillah’, uko wapi wewe Mungu? Basi mungu fanya miujiza yako,.sitaki kubakwa na mashetani mimi” niliomba kimoyo moyo huku nikijaribu kujitikisa pale kitandani, lakini nilikuwa kama mtu aliyepigwa nusu kaputi.
Machozi yalinitoka baada ya kugundua sina namna ya kuzuia kile kinacho onekana kutaka kutokea muda mfupi ujao.
Kama nilivyo tegemea yule baba alipanda kitandani akawa mbele ya mapajaa yangu huku sehemu zake zikinitizama kwa uchu!.
Yule mtu alichukua chupa ndogo nyeusi, kisha akafungua mfuniko na kutoa dawa fulani iliyokuwa na mafuta kama ya griselin ila yale yalikuwa ya njano. Kisha akayanuia kwa sauti ndogo yale mafuta, kisha akajipaka katika lile jogoo lake kubwa.
Baada ya hapo akanisogelea na kunitanua mapaja yangu,.kwakweli ndugu msomaji huwa kila nikifkiria tukio hili, akili yangu inashindwa kabisa kulifuta na kusahau jambo hili la kinyama.
Niseme tu kuwa huwa najihisi haya{aibu}kuelezea eneo hili, lakini kwakuwa nahitaji ulimwengu wote utambue juu ya maisha yangu na ukweli kuhusu mimi sina budi kuficha jambo hata moja katika yale mengi yaliyo nisibu.
Mara zote nimekuwa ni mtu ninae hitaji uhuru wangu, labda kuna watu wanaweza kuona ninajidhalilisha katika hili na niseme tu nimekuwa mwanamke ninae amini katika zile falsafa za mr Sankara nilizo wahi kusoma katika vitabu nilipokuwa chuo kikuu pale mlimani alisema “ili kuleta mabadiliko na mitazamo chanya ni lazima kuwa na hali fulani ya uendawazimu. Ila tusiufikirie uendawazimu huu wa kuokota makopo bali ule ukichaa mzuri wa kuamini katika mambo au misingi fulani na kuisimamia kwa dhati pamoja na changamoto nyingi. Kwa kuamini kwa dhati katika mabadiliko haya na kutaka kuboresha maisha,” hivyo sina budi kueleza ukweli mtupu bila kujali nani ataniona mwendawazimu.
Wazungu wana msemo usemao, to be healthy you have to share your problems with others!”
 
JUMBA LA WACHAWI
Mwandishi/mtunzi; Zulfa Huseni
SEHEMU YA 8

Kwa kuamini kwa dhati katika mabadiliko haya na kutaka kuboresha maisha,” hivyo sina budi kueleza ukweli mtupu bila kujali nani ataniona mwendawazimu.
Wazungu wana msemo usemao, to be healthy you have to share your problems with others!”
Yule baba alipokuwa akiniingilia kwakweli nilihisi maumivu makali mno kiasi kwamba niliona kama utumbo unataka kutoka.maumbile ya yule mwanaume yalikuwa ni makubwa mno.aliniumiza.
Alikuwa akiingiza na kutoa upesi upesi, huku pumzi zake zikimtoka kwa kasi, alikuwa katika mahaba mazito juu ya mwili wangu.
Na mara zote wakati ananizini nilikuwa nikiona dunia inazunguka kwa kasi huku mimi nikiwa ndani yake, yalikuwa ni mateso yasiyo mithilika.
Yule mtu alinibaka hadi hamu yake ilipokwisha, nilikuwa nasikia sehemu zangu zote zinawaka moto.
Sikujua kama yule mtu aliningiza katika maswahibu yale yote kwa sababu ya tendo lile, lakini pia sikuwa na uhakika wa asilimia zote kama mtu yule anaweza kuishia kunifanya vile kisha akaniachia uhai wangu.
Nilikuwa nikitweta huku maumivu makali yakinisulubu, hasira zilikuwa zimenipanda vibaya mno, lakini sikuweza kuongea kila nilivyo hitaji kufanya hivyo.
Yule mtu alikuwa ameniroga na kunifanyia ukatili ambao sikustahili kabisa, sikuona kama nilikuwa na kosa la kutendewa unyama ule.
Kwakweli sikuona hata faida ya kuishi.
Yule mtu alipotoka mwilini mwangu, alifungua kabati lililokuwa mule ndani na kutoa shuka jekundu kisha akajifunika, halafu akasogea mbele ya kitanda changu kisha akaanza kufanya vitendo vile alivyokuwa anafanya kisha nikapitiwa na usingizi wa ajabu.
Namna nilivyokuwanimelala chali machozi yalikuwa yakinichuruzika pembeni ya macho yangu na kutiririka hadi masikioni.
Yule mtu alikazana kuzungumza maneno yale ya ajabu, na hata yale maneno yake yalipoingia ndani ya ngoma za masikio yangu nilianza kukumbwa na hali ile kama ya awali.
Usingizi mzito ulikuwa ukininyemelea kwa kasi, hazikufika sekunde kumi na tano tayari nilikuwa nimekwisha zama katika bahari ya usingizi.

******************

Sikujua fahamu zilinirudia baada ya muda gani au baada ya siku ngapi kwani kichwani mwangu nilikuwa nikipitiwa na taswira nyingi za ajabu ambapo zilifuataiwa na vipindi virefu vya kiza na utupu mrefu akilini,miongoni mwa yale yaliyo pita ni tukio la kuingiliwa kimwili na yule baba, nilikuwa nikimwona namna alivyokuwa akikazana kuniingilia huku akitokwa na pumzi nzito za huba huku mimi nikipatwa na maumivu yasiyoweza kuelezeka.
Nakumbuka, kuna wakati nilijihisi kuchoka mno kutokana na kulala muda mrefu nilifumbua macho na kuona mwanga hafifu,. Mule ndani kulikuwa kimya hakuna kilichosikika zaidi ya mishale ya saa ya ukutani iliyokuwa ikizunguka taratibu huku ikilia “ta,ta, ta, ta” nilijaribu kuamka nikaona nina nguvu za kutosha.
Niliamka pale kitandani na kukaa kitako, nilikuwa myonge mithili ya teja wa madawa ya kulevya mwenye kuhudhurua clinic.
Macho yangu yalitizama ile saa ya ukutani kwakweli sikuamini kile nilicho kiona.
Ile saaa ilionyesha ilikuwa yapata saa kumi usiku. “Inamaana kulala kote kule bado hakuja kucha asubuhi” nilijiuliza huku nikijikagua mwili wangu uliokuwa umevalishwa tena nguo zangu zote ikiwa ni pamoja na lile jacketi lililokuwa na vitu vya ofisini vyote.
“Au nimelala siku mbili humu ndani huyu baba akiwa amenigeuza mkewe” niliendelea kujiuliza, lakini sikuwa na jibu kamili japo nilihisi kuwa kunauwezekano niliishi mule ndani kwa muda wa siku mbili nikiwa usingizini.
Nilipokuwa najikagua mwili wangu ndipo nilipo ona jambo jingine lililonifanye nitishike vibaya mno.
Tumbo langu lilikuwa kubwa kama kwamba nilikuwa na ujauzito wa mizezi tisa na muda wowote naweza kujifungua. “Mungu wangu nini hii tumboni mwangu.,nina mimba! Nimebakwa na nimepata mimba.. Lakini..hii mimba inakuwaje iwe kubwa kwa siku mbili tu.!”
Nilinong’ona peke yangu machozi yakinitoka, “ni ukatili wa kiwango gani natendewa mimi Zahara..nabakwa hadi napewa mimba..kwanini msiniue tu..kwanini sijafa ..kwanini mniacha hai hadi sasa.. https://jamii.app/JFUserGuide you” nililia mno, jambo lile lilikuwa ni kubwa mno. Nilijiona ni kiumbe nisiye na faida ya kuishi duniani tena.
Mwili wangu ulikuwa mnyonge mno, nilihisi kabisa ndani ya tumbo langu kuna kiumbe. Lakini jambo lililokuwa la kustajabisha ni kuwa ile mimba iliwezaje kukuwa kiasi kile kwa siku mbili tu ambazo niliamini nilikaa mule ndani.
Nilinyanyua mkono wangu na kutizama saa yangu ndogo niliyowahi kupewa zawadi na mpenzi wangu Thabit Talib Mwaikimba, kwa mujibu wa saa yangu ya mkononi ilinionyesha ilikuwa ni saa kumi kama ambavyo ile ya ukutani ulivyosema, lakini katika kutaka kupata uhakika zaidi nilibofya ile saa ili nione ilikuwa ni siku gani na tarehe ngapi maana siku ya mwisho kuingia mule katika lile jengo ilikuwa ni usiku wa saa saba siku ya alhamisi ya tarehe 29/3/1989.
Saa yangu ilinionyesha kitu kilicho nifanya kuanza kupata hisia kuwa huenda nipo katika ndoto mbaya usingizini.
Ile saa ilinionyesha kuwa ilikuwa ni siku ya alhamisi ya tarehe ya tarehe hiyo hiyo 29/3/1989. yanii ilikuwa ni usiku ule ule.
“Sasa hii miujiza gani tena jamani yanii kulala kote kule kumbe hata masaa matatu hayajaikwisha!.” Lakini hilo lilikuwa ni dogo katika kubwa lililoumiza mtima wangu.
Vipi niwe na mimba kubwa kama ya miezi tisa ilihali niliingiliwa kimwili lisaa limoja tu lililopita.
Niliona ninalo bomu kubwa ambalo linalokuja kulipuka katika maisha yangu muda mchache ujao.
“Sasa nifanye nini” nilijiuliza, wazo la kutoroka mule ndani lilinijia, nilisimama wima nikasogea pale mlangoni, bado ukimya wa ajabu uliendelea kushika hatamu.
Nikashika kitasa na kukinyonga kushoto, kitasa kiliachia “kwachaa” nikatoka kwa kunyata nikiwa na tahadhari kubwa.
Niliangalia kulia na kushoto nikaona nipo katika kikorido kirefu kilichokuwa na vyumba vingi vilivyo fungwa pembeni yake.
Nikatizama mazingira yale kisha nikashika uelekeo ambao nilihisi ni uelekeo sahihi wa kunitoa nje ya jumba lile.
Tumbo langu lililokuwa na kiumbe ndani yake lilikuwa zito na lilikuwa likiuma, nilikuwa nikisikia kitu kilicho kuwa tumboni ambacho bila shaka alikuwa ni mtoto akicheza cheza tumboni.
Niliendelea kujisukuma kwa mbele huku nikiwa na tahadahli kubwa, sikuwa na woga tena, sikuogopa kifo kwani hata hivyo sikuona faida ya kuishi katika dunia ilihali nikiwa ni binadamu niliye na kovu baya moyoni mwangu ambalo siwezi kulisahu hadi siku naingia kaburini.
Nikiwa nazipiga hatua mara ghafla nilianza kusikia sauti kwa mbali.
Ile sauti ilipenya masikioni mwangu na kunifanya nipate kizunguzungu, sauti ya yule baba akizungumza maneno ambayo huwa yananifanya nizingirwe na usingizi mzito.
Yale maneno yalizidi kupenya katika masikio yangu pasina kuelewa mzungumzaji yupo sehemu gani, lakini kwa namna nilivyokuwa nikisikia ilikuwa ni kama mzungumzaji yupo maili nyingi kidogo kutoka pale nilipokuwepo mimi, kwani ile sauti ilingia katika masikio yangu kama mwangwi.
Nilianza kupepesuka nguvu zikiniishia huku Giza la ajabu likivaa mboni za macho yangu.
Na wakati huo yule mtoto tumboni mwangu alikuwa akicheza,giza liliendelea kutanda mbele yangu na kujikuta nguvu zinaninishia na kuanguka chini kama mzigo.
Baada ya muda mrefu kupita nikiwa katika dimbwi la usingizi, mara nilistuka nilipohisi sauti kali ikililia masikioni mwangu, ilikuwa ni sauti ya mtoto mchanga.
Nilifumbua macho yangu na kujikuta nipo katika kile kile chumba mtoto mdogo wa mwaka mmoja akiwa pembeni yangu katika kitanda.
Na nilipo rejewa tu na fahamu zangu, tukio baya la kubakwa na yule baba ndio ilikuwa kitu cha kwanza kupita katika ubongo wangu.
Nilijinyanyua kitako na kuketi pale kitandani. Mtoto mzuri wa kike alikuwa pembeni yangu.
Yule mtoto hakuwa analia tena baada ya mimi kuamka.nilijiangalia tumbo langu na kuona mabadiliko, sikuwa na mimba tena, nilijiona niko tofauti katika maungo yangu.
Matiti yangu yalikuwa makubwa na yaliyo lala ilihali awali matiti yangu yalikuwa wima.
 
JUMBA LA WACHAWI
Mwandishi/mtunzi; Zulfa Huseni
SEHEMU YA 10

Nilisimama kwa ungalifu nikavaaa raba zangu, kisha nikauendea mlango, wakati huo ilikuwa yapata saa kumi na nusu ya tarehe 29/3/1989, na majira hayo muadhini alikuwa akiadhini kule katika jumba la ibada.
Nilitoka nje ya chumba kile na kunyata taratibu, nilitembea upesi upesi katika ile korido eneo lote bado lilikuwa kimya kabisa, niliongeza mwendo nikawa natembea kwa kasi kubwa,atimae nikawa nakimbia.
Nilipopiga hatua kadhaa nikiwa mbali kidogo kutokea katika kile chumba, nikaona korido ndogo ambapo pembeni yake kulikuwa na lifti, nikaona hiyo inaweza kuwa njia nzuri ya kunitoa upesi katika lile jengo.
Mara ghafla nikasikia ile sauti ya ajabu, lakini safari hii sikukubali kabisa kuendelea kubaki mule katika lile jengo, niliziba masikio nikatimua mbio.
Nilikimbia kuelekea eneo lile, upesi nikajotoma ndani ya lifti moja katika tatu zilizo kuwa pale, kisha nikairuhusu inishushe chini, sekunde kumi tayari mlango wa ile lift ulifunguka na nilikuwa chini kabisa ya ghorofa lile..ile sauti ilikuwa ikipotea kwa mbali kabisa.
Bila kuzubaa nikakimbia kuufuta mlango wa kunitoa nje, kama masikhara nikajikuta nipo nje ya jengo lile.
Kwakweli ilikuwa ni furaha kwangu, nilijiona ni kama mfungwa niliyekuwa na kufungo kikubwa gerezani na sasa nimekuwa huru.
Pamoja na kwamba nilikuwa ni mtu mwenye furaha ya kuwa nje ya jengo lile lakini nilijikuta nikisimama na kuduwaa hatua chache mbele ya jengo lile katika mtaa wa agrey kariakakoo kutokana na kile nilicho kiona mbele yangu.
Nilikutana na mji mgeni mpya tena mpya kabisa mbele ya macho yangu, mji uliokuwa umejengwa ukajengeka maghorofa mengi, mazuri tena marefu kwenda juu.
“Nipo wapi hapa” sauti moja iliniuliza mawazoni mwangu, japo mtaa ulikuwa ni ule ule nilio ufahamu miaka yote tena palikuwa ni Dar es salamu ninayo ijua kabisa.
Lakini Asubuhi hii jiji hili lilikuwa tofauti kabisa, nilizipiga hatua kuelekea mnazi mmoja nikizidi kushangaa mandhali mazuri ya jiji la Dar es salam.
“Kitu gani kinatokea katika maisha yangu huku nipo katika dunia gani tena?” nilijiuliza mwenyewe bila kuwa na majibu.
Wakati naelekea mnazi mmoja tayari ilikuwa ni majira ya saa kumi na moja alfajiri katika Dar es salam hii mpya majira yale kulikuwa na watu wengi mno mida hiyo tofuati na Dar niliyokuwa ninaijua mimi. Watu hawa walionekana wako ‘bize’ kila mtu alikuwa ni mwenye kujali mambo yake.
Nilifika mnazi mmoja na kuelekea katika kituo cha basi, bado niliendelea kupagawa na namna mandhali yalivyo badilika ghafla kiasi kile.
Lakini pamoja na kuwa mji huu mpya machoni mwangu kuwa na majengo mapya yenye kuvutia bado kuna baadhi ya majengo niliona yako vilevile mathalani jengo la ushirika pale mnazi mmoja, jengo la chama cha mapinduzi, pamoja na nyumba za taifa{ nation housing} ambazo nyingi zilikuwa zikikaliwa wahindi.
Hali ilinisukuma kuuliza tofauti ile ninayo iona mbele ya macho yangu kama na wezangu pia wanaona kama nionavyo mimi, ama ni maono yangu tu, kwani kusema ukweli toka hapo sikuwa najiamini hata kidogo, niliamini kwa vyovyote vile wale wachawi niliokutana nao katika lile jengo kuna namna watakuwa wamenifanya katika ufahamu wangu wa akili.
“Kaka samahani”
“Bila samahani dada yangu”
“Hivi mbona naona leo mji umebadilika mno tofauti na siku nyingine za nyuma nini kimefanyika usiku wa leo?” niliuliza mkaka aliyekuwa anangojea usafiri kituoni.
“labda sijalielewa swali lako dada yangu, mji umebadilika kivipi yanii uonavyo wewe?”
“Kwani wewe huoni huu utitiri wa haya maghorofa?, huoni namna barabara zilivyo za kuvutia? Huoni kama leo watu ni wengi tofauti na siku zingine?..Huoni?” nilisema kwa kulalama kidogo, nikionyesha sura ya kumaanisha kile nilicho kuwa nakizungumza.
Yule mtu alinitizama kwa kina kidogo kichwani mwake akahisi anazungumza na mlevi wa pombe aina ya mataputapu.
“Ndivyo kulivyo kila siku” alinipa jibu moja kisha hakushughulika tena na mimi, nilimwona katika uso wake akinisoma mimi kama mlevi wa mataputapu.
Upesi sauti moja ikanambia inawezekana ulikaa mule ndani kwa masiku mengi mno ndio maana kumekuwa na mabadiliko makubwa katika mji huu, lakini bado sauti nyingine ikaniambia hata kama nitakuwa nimekaa mule ndani kwa masiku kadhaa mji huu hauwezi kuwa umebadilika kwa kiwango hiki., mabadiliko yale hayakuwa ya miezi sita ukiachilia mbali hata kwa mwaka mmoja tu ingehitaji miaka zaidi ya ishirini ndio kuwe vile..
Lakini sauti moja ikanijia ambayo niliona kidogo imenipa wazo la kujua utata ule, sauti ilinambia, angalia saa na tarehe ya leo, upesi niliangalia tarehe katika saa yangu ya mkononi.
Sikuamini kile ambacho macho yangu yaliona,. “MWAKAA elfu mbili na kumi na sita..!.” Nilijikuta nibwata kwa nguvu huku nikibaki nimeduwaa.
Hapakuwa na mtu aliye nijali pale kituo cha basi cha mnazi mmoja, nilihisi huenda saa yangu ilikuwa mbovu, kwani kabla ya kuitizama muda ule nilikwosha itizama wakati nipo ndani ya jengo lile na ikanionyesha ilikuwa ni tarehe 29/3/1989.,sasa vipi huku nje inionyeshe ni mwaka mwingine wa mbele kabisa, ambao sikuwahi kufikiria kama uhai wangu unaweza kufika huko.
Mambo mawili yakawa katika ubongo wangu, jambo la kwanza inawezekana ile saa yangu niliyo kuwa nimeivaa mkononi ds ikawa ni mbovu, na jambo la pili inawezekana saa ile isiwe mbovu ila tu nikawa nipo katika ulimwengu mwingine kabisa wa kichwawi.
Lakini bado wazo hilo nililipinga kabisa kwani pale nilikuwa katika mji ninao ufahamu sana, mji wa Dar es salam, japo ulikuwa umebadilika mno.
“Samahani kaka yangu eti leo ni siku gani?tarehe ngapi? na mwaka upi?” niliuliza mshangao mkubwa ukiwa usoni mwangu,.nilisha anza kuhisi kuna bomu linaninyemelea katika maisha yangu.
Yule mtu ambaye hakuwa anavutiwa na maswali yangu, alionekana kukereka kwa masawali yangu ambayo yalionekana ni ya kipuuzi kwakwe.
 
JUMBA LA WACHAWI
Mwandishi/mtunzi; Zulfa Huseni
SEHEMU YA 11

Yule mtoto hakuwa analia tena baada ya mimi kuamka.nilijiangalia tumbo langu na kuona mabadiliko, sikuwa na mimba tena, nilijiona niko tofauti katika maungo yangu.
Matiti yangu yalikuwa makubwa na yaliyo lala ilihali awali matiti yangu yalikuwa wima.
Lakini hata sehemu zangu za siri, kwakweli vile nilivyokuwa najiskia awali si sawa na muda ule. Hapo nikaelewa kuwa ile mimba iliyoingia kimaajabu nilikuwa nimejifungua tena kimaajabu, na inavyo elekea nilijifungua wakati ule nimepoteza fahamu.
Lakini ajabu nyingine mbele yangu ni yule mtoto pembeni yangu. Alikuwa ni mtoto mkubwa wa mwaka mmoja ambaye swali kuu likawa yule mtoto amewezaje kukua upesi kaisi kile. Wakati nalifikiria hilo saa yangu ya mkononi bado ilinionyesha ilikuwa ni tarehe 29/3/1989. siku ya alhamisi.
“Inamaana haya mambo yanenda halaka hivi kwa dakika ama ni kwa kutegema siku miezi na miaka”
“No lazma niondoke eneo hili, leo lazma niondoke siwezi kuishi humu! Nini hatma ya maisha yangu?.kama kufa na acha nife tu, lakini siwezi kuendela kuishi kifungoni kiasi hiki” nilendelea kuwaza nikiwa nimeketi kitako mule ndani tukiwa wawili tu, mimi na yule mtoto mchanga.
Sasa nikawa nafikiria namna ya kukabiliana na mazingaombwe yale ambayo yamekuwa yakindelea kutokea.
Kitu kingine ambacho nimesahau kukueleza mpenzi msomaji, ni kuwa toka siku ile nibakwe na yule mbaba sikuwahi kumwona yeye wala mtu mwingine yeyote mule ndani hadi siku nilipo amka na kujikuta nipo na yule mtoto mchanga wa miaka miwili.
Nikaendela kuwaza namna ya kutoroka katika lile eneo nililo amini ni kifungo kwangu. Swali dogo likaja kichwani mwangu. Je nitoroke na yule mtoto ambaye niliamini ni wangu?
Nikapata kidogo kigugumizi katika hilo lakini sauti fulani ikanambia na kunitahadhalisha kuwa sitakiwi kuondoka na yule mtoto kwani kufanya vile ni kutengeneza mazingira ya kuandamwa na wale viumbe kwani kwa namna yoyote ile kupewa kwangu ujauzito ilikuwa ni mipango yao.
Lakini sauti nyingine ikanambia kamwe nisimwache mtoto wangu, kwani pamoja na kwamba upatikanaji wake haukuwa mwema lakini bado yule malaika atabakia kuwa damu yangu, na ni mimi mwenye jukumu la kuhakikisha usalama wa yule mtoto unakuwepo kwani mimi ndiye mama yake mzazi.
Sasa nikawa nakinzana na nguvu mbili, kuondoka na yule mtoto ama kumwacha.
Nilifikiria kwa muda mwisho nikazimia kumwacha yule mtoto mchanga.
“Sikuja na mtoto hapa, vipi niondoke na mtoto, kwanza si mtoto huyu, mtoto gani anaingia tumboni siku hiyo hiyo na kuzaliwa siku hiyohiyo kisha anakuwa siku hiyo hiyo..no siwezi kubeba matatizo haya.” Nilinong’ona peke yangu nikiteremka kitandani.
Msomaji pengine haya nikuelezayo unaweza kuhisi kabisa ni hadithi za kubuni, lakini amini nakwambia hakuna hata moja la kubuni katika hayo niliyokwisha kueleza.
Kuna wakati hata mimi sikuwa naamini wakati yananitokea lakini amini nakwambia katika huu ulimwengu kuna mengi ya ajabu ambayo yanatokea katika jamii ya siri
[secret society] ambayo ukisimuliwa unaweza usiamini asilani.
Sasa nikiwa pale, nilipo angaza chini nikaona raba zangu zikiwa chini ya kitanda, upesi nikavaa na kuwa tayari kuondoka.
Lakini ghafla.
Nilisikia ile sauti, sauti ya yule baba, alikuwa akizungumza yale maneno yenye kunifanya nipatwe na usingizi wa ajabu.
Sauti ile kama ilivyo kuwa awali, ilitokea maili nyingi, ilifika pale kama mwangwi
Na mara ilipopenya katika masikio yangu nikahisi kizungu zungu, nikaelewa kitu gani kinaenda kutokea, safari hii sikuwa tayari kabisa kuendela kulala lala pale huku wale wachawi wakinichezea kama shangazi yao, nilidhamiria kabisa kuondoka mahala pale, ile sauti ikakazana kuyatamka yale maneno, hali yangu nayo ikaendela kubadilika, kizunguzungu kikazidi kunielemea huku giza la ajabu likinizingizira.
“No no siwezi kuendelea kubaki hapa..” nilijikuta kinibwata kwa hasira wakati ile sauti ikizidi kugonga ngoma za masikio yangu.
Sasa akili yangu ikafanya kazi upesi upesi, kwakuwa ile sauti ikisikika masikioni mwangu ndio huleta madhala ya kupoteza fahamu nikaona njia pekee ya kuzuia hali ile ni kuziba masikio ile sauti nisiisikie.
Niliingiza vidole vya shahada ndani kabisa ya masikio yangu na kukandamiza kwa nguvu kuzuia ile sauti kupenya katika masikio yangu.
Sikusikia chochote zaidi ya mvumo fulani katika masikio ambao huwa unasikika pale unapoziba masikio. {Wanazuoni wa tauhidi husema ule ni mvumo wa moto wa jehanamu}.
Kwa muda wa dakika mbili niliendelea kuziba masikio pasina kusikia yale maneno, niliondoa taratibu vidole katika masikio, sikusikia kitu chochote zaidi ya sauti ya yule mtoto aliyekuwa akilia kwa nguvu.
Nilibaki nimesimama nisijue kitu gani nifanye, mara nikiwa bado nimesimama nilihisi nyayo za mtu akija kutokea nje akielekea mule ndani.
Akili yangu ikaendela kufanya kazi upesi upesi, niliruka kitandani na kulala gubigubi na kujifanya nipo katika usingizi mzito.
Zile nyayo ziliendelea kusogea mule ndani na hatimae nikahisi kitasa cha mlango kikiguswa na kisha akaingia mtu, kupitia pembe ya jicho niliweza kumwona mwanaume mzee mno akiwa amevalia kanzu nyekundu.
Nilipo mtizama vizuri mtu yule nikagundua mtu yule alikuwa ni mzee kati ya miaka themanini, lakini nipo mtizama kwa uzuri zaidi nikagundua yule mzee alikuwa akifanana mno na yule baba aliye nibaka,nikahisi pengine huenda wale watu walikuwa ni watu wa familia moja, famili gani hii washenzi wa tabia kiasi hiki, niliwaza.
Alikuwa amekamatilia vibuyu viwili vilivyo fungwa hirizi nyeusi na nyekundu.
Yule mtu alisogea hadi pale kitandani kisha akazungumza maneno fulani nafikiri ya kichawi kisha akafungua vile vibyu vyake, mara moshi mweusi ulitokea katika vile vibuyu na kusamba mule ndani, baada ya hapo alimsogelea mtoto kisha akambeba na kutoka nae nje.
Nilitaka kufanya kitu baada ya tukio lile lakini nafsi nyingine ikanionya juu ya hilo.
Niliendelea kutulia kwa namna ile ile kwa muda wa dakika tano nikitegemea yule babu anaweza kurejea. Lakini dakika tano nyingine zilipita yule babu hakutokea, nikajiongeza dakika tano nyingine za ziada ili kujilidhisha kuwa yule mtu hawezi kurejea, zilipita tano nyingine lakini hakurejea.

Nilisimama kwa ungalifu nikavaaa raba zangu, kisha nikauendea mlango, wakati huo ilikuwa yapata saa kumi na nusu ya tarehe 29/3/1989, na majira hayo muadhini alikuwa akiadhini kule katika jumba la ibada.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom