masanzakona
JF-Expert Member
- Jan 2, 2014
- 228
- 121
Wakuu, nahitaji kwenda kijiji kuona mashamba yangu, je jumatatu ni sikukuu ya maulid au?
Nijuzeni tafadhali
Nijuzeni tafadhali
Maulid (kuzaliwa kwa mtume )
huwa inaadhimishwa kila January 14?naomba kujuzwa wakuu!
Siyo tarehe 14 mkuu, haitumiki Gregorian calender, inatumika Islamic, ambayo nadhani ni mwezi huu MFUNGO SITA.Haiwezi kuwa constant tarehe14 au Constant January, kwa kuwa Kiislam mwezi muandamo una siku 29 na 30 pekee! Hauna siku 28 au 31. Ndo maana katika mzunguko wa mwaka wa kawaida, kuna UPUNGUFU WA SIKU11 kati ya mwaka wa Kiislam na mwaka wa Gregorian Calender. Na hii inatokana na uwepo wa siku29 na 30, wakati kule kuna siku28, 29, 30 na 31. Hivyo kwa tofauti hiyo ya siku11, baada ya miaka33, yaani33*11=363, ambapo tunasema baada ya miaka33 kunakuawa na angalau mwaka mmoja nyuma!
Maulid (kuzaliwa kwa mtume )
huwa inaadhimishwa kila January 14?naomba kujuzwa wakuu!
ni kwasababu umezoea kudanganywa.ukweli hutoufurahia.
Sikukuu ya maulid itakuwa usiku wa jumatatu kuamkia jumanne mkuu. Kwa hiyo jumanne ndo siku ya mapumziko
na mapinduzi lini?
mkuu CHAZA nashukuru sna kwa kunielimisha,ila nimeona hiyo press release toka Bakwata wametumia Gregorian Calender.i.e tar,mwezi na mwaka!
Mkuu MZAWATA huwa ni kwann husheherekewa usiku na sio mchana kama sikukuu nyingine za Kiislam?(mfano Idd)