Juma Tomas Zangira | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Juma Tomas Zangira

Discussion in 'Jukwaa la Historia' started by Kibukuasili, Nov 2, 2011.

 1. Kibukuasili

  Kibukuasili JF-Expert Member

  #1
  Nov 2, 2011
  Joined: May 15, 2010
  Messages: 858
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Huyu bwana miaka mingi ya nyuma alipata kesi iliyovuma sana hapa nchini. Wakati huo akiitwa "jasusi wa kwanza Tanzania" nakumbuka alifungwa lakini sikumbuki ni miaka mingapi.
  nilikua mdogo sikuweza kufuatilia sana kesi hiyo. Kama kuna mtu anakumbuka atuwekee habari.
   
 2. Yegomasika

  Yegomasika JF-Expert Member

  #2
  Nov 2, 2011
  Joined: Mar 21, 2009
  Messages: 7,126
  Likes Received: 23,736
  Trophy Points: 280
  Hata mimi naikumbuka hii habari, jamaa ni kama alikuwa mfanyakazi wa Kilimanjaro Hotel enzi hizo...ila sikumbuki hii kesi iliishia wapi!.
   
 3. Manumbu

  Manumbu JF-Expert Member

  #3
  Nov 3, 2011
  Joined: Oct 28, 2009
  Messages: 1,751
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 135
  soma Tanzania Law Report ya mwaka 1980 sikumbuki ukurasa. hii kesi imeripotiwa humo ndani. bahati mbaya kitabu changu kimepotea ningekujuza nini kilimtokea. ila kwa sasa sijui atakuwa wapi.
   
 4. Kibukuasili

  Kibukuasili JF-Expert Member

  #4
  Nov 3, 2011
  Joined: May 15, 2010
  Messages: 858
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  asante mkuu, nitaipata wapi ripoti hiyo. Ipo mtandaoni?
   
 5. N

  Ndinani JF-Expert Member

  #5
  Nov 3, 2011
  Joined: Aug 29, 2010
  Messages: 5,413
  Likes Received: 734
  Trophy Points: 280
  Huyu Juma Thomas Zangira alikuwa mtu wa intelligence miaka ya mwanzo ya Uhuru wetu wa Bendera, na alikuwa karibu sana na Oscar Kambona. Alikuja kufungwa baadae na alipotoka ndio akawa na kibarua pale Kilimanjaro Hotel enzi hizo.
   
 6. FaizaFoxy

  FaizaFoxy JF-Expert Member

  #6
  Nov 3, 2011
  Joined: Apr 13, 2011
  Messages: 58,107
  Likes Received: 22,155
  Trophy Points: 280
  Victims wa Udikteta hao.
   
 7. Leonard Robert

  Leonard Robert JF-Expert Member

  #7
  Nov 3, 2011
  Joined: Apr 22, 2011
  Messages: 9,150
  Likes Received: 2,471
  Trophy Points: 280
  tanganyika hutajawai kuwa na dicteta..ndo maana unatukanwa na vijana.
   
 8. FaizaFoxy

  FaizaFoxy JF-Expert Member

  #8
  Nov 3, 2011
  Joined: Apr 13, 2011
  Messages: 58,107
  Likes Received: 22,155
  Trophy Points: 280
  The death of Julius Nyerere, African independence leader and longtime dictator
  of Tanzania
  , evoked a flood of encomiums worldwide. The praise is misplaced.
  Nyerere's approach devastated much of postcolonial Africa (Forbes,
  1999).


  Source: http://www.google.com/url?sa=t&rct=j&q=&esrc=s&source=web&cd=5&ved=0CD8QFjAE&url=http%3A%2F%2Farchive.lib.msu.edu%2FDMC%2FAfrican Journals%2Fpdfs%2Fpolitical science%2Fvolume8n1%2Fajps008001004.pdf&ei=KP-yTtf8FtLQ4QTGxKTwAw&usg=AFQjCNGy424aTDnoJY69_pO-4AKRnTNNBg&sig2=ryyQwqahDMBSeTOZJOGPAQ
   
 9. Mphamvu

  Mphamvu JF-Expert Member

  #9
  Nov 4, 2011
  Joined: Jan 28, 2011
  Messages: 10,708
  Likes Received: 934
  Trophy Points: 280
  faiza mbweha hata sikuelewagi? sasa hayo si mtu mmoja kama wewe ameamua kujiandikia mtandaoni? sawasawa na mtu achukue huu utumbo wako humu jf aseme ni reference! ati kwa hisani ya faiza mbweha wa kariakoo! mwe?
   
 10. Safety last

  Safety last JF-Expert Member

  #10
  Nov 4, 2011
  Joined: Mar 24, 2011
  Messages: 4,224
  Likes Received: 164
  Trophy Points: 160
  Alihukumiwa kwa kesi ya kama si espionage ni uhaini ,alikuwa anawasiliana , kukusanya taarifa za siri kati ya mwaka 1971-1977 na mzungu john wilson kuhusu msimamo wa Tanzania ktk nchi za Rhodesia na mtizamo wa nyerere ktk maswala ya uchumi wa nchi.

  Huyo mzungu John Wilson alikuwa(alijifanya) mfanyabiasha ila hukumu yake ya miaka 20 jela ilitenguliwa na majaji Nyalali,kisanga ,lugakingira mahakama kuu hadi miaka 13,sababu walishindwa kuproove kimaandishi maelezo aliyokuwa akimtumia huyo john wilson (zilipatikana barua za huyo mzungu tu wala si JTZ),na yeye alisema aliyokuwa akimwambia ni mambo ambayo hata vyombo vya habari magazeti,radio vilikuwa vikiripoti ukaonekana ni ushahidi then kifungo kikapungua ila alionekana ni tishio kwa usalama wa taifa, Tanzania law report 1980.
   
 11. Humphnicky

  Humphnicky JF-Expert Member

  #11
  Nov 4, 2011
  Joined: Dec 1, 2010
  Messages: 1,808
  Likes Received: 526
  Trophy Points: 280
  hakuhasiwa?
   
 12. Humphnicky

  Humphnicky JF-Expert Member

  #12
  Nov 4, 2011
  Joined: Dec 1, 2010
  Messages: 1,808
  Likes Received: 526
  Trophy Points: 280
  ZANGIRA, L Mahakama ya Rufaa ya Tanzania, mnamo Machi 20, 1978, inampunguzia kifungo jela kutoka kutumikia miaka 20 hadi 13 Bw. Juma Thomas Zangira, Mtanzania wa kwanza kupatikana na hatia ya kufanya ujasusi (spying) dhidi ya nchi hii. Wakitoa hukumu ya kuunguza adhabu hiyo, Majaji Francis Nyalali (Jaji Mkuu), Robert Kissanga, na Kahwa Lugakingira, wanaeleza kuwa sababu kuu tatu zimepelekea kupunguzwa kwa adhabu ya Zangira ni pmaoja na ushirikiano wa dhati alioutoa kwa waliomkamata na kumshtakji wakati wa shauri lake, ukweli kuwa hilo lilikuwa ni kosa lake la kwanza; muda aliokuwa ameshakaa kifungoni, na pia kuwepo kwa utata wa hapa na pale katika kuthibitisha kosa lake, ingawa sababu hii ya tatu haikuungwa mkono na Majaji Lugakingira na Kissanga ambao walisema waendesha mashtaka walithibitisha kosa pasipo shaka yoyote. Kiini cha mashtaka hayo kilielezwa na serikali ya Tanzania kuwa Zangira alikuwa akikusanya taarifa za siri za Tanzania kati ya 1971 na Julai 1977 na kuzipeleka kwa mtu mmoja aitwaye John Wilson ambaye hakufafanuliwa alikuwa wa nchi gani na akiwa na mamlaka gani.
   
 13. Kibukuasili

  Kibukuasili JF-Expert Member

  #13
  Nov 20, 2011
  Joined: May 15, 2010
  Messages: 858
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  kwa hiyo miaka ya mwanzo ya 90 alitoka. Yuko wapi huyu jamani atueleze ukweli au ndio kapotea?
   
 14. Kifimbo Cheza

  Kifimbo Cheza JF-Expert Member

  #14
  Oct 26, 2012
  Joined: Nov 13, 2011
  Messages: 221
  Likes Received: 53
  Trophy Points: 45
  Ninaomba mwenye full story ya kesi ya ujasusi dhidi serikali ya TZ aliyoshtakiwa mtu aliyeitwa JUMA THOMAS ZANGIRA miaka ya 1980s, atujuze. Na huyo mtu aliishia wapi?
   
 15. Kimbunga

  Kimbunga Platinum Member

  #15
  Oct 26, 2012
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 13,012
  Likes Received: 1,817
  Trophy Points: 280
 16. M

  Magesi JF-Expert Member

  #16
  Oct 26, 2012
  Joined: Jul 10, 2012
  Messages: 2,590
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Yuko wapi sasa na anafanya nn?
   
 17. LINCOLINMTZA

  LINCOLINMTZA JF-Expert Member

  #17
  Oct 26, 2012
  Joined: Mar 15, 2011
  Messages: 1,640
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Usipopevuka kiakili JF basi sahau sehemu zingine.
   
 18. p

  promi demana JF-Expert Member

  #18
  Oct 26, 2012
  Joined: Oct 9, 2012
  Messages: 309
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Hivi wakuu maana halisi ya ujasusi huwa ni nini? Ujambazi au uajngiri au ukibaka? Pia tofauti ya jasusi na gaidi.
   
 19. NgumiJiwe

  NgumiJiwe JF-Expert Member

  #19
  Oct 26, 2012
  Joined: Mar 15, 2011
  Messages: 867
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 35
  kama sikosei huyu mzee alishafariki baada ya kuugua kwa muda mrefu
   
 20. 124 Ali

  124 Ali JF-Expert Member

  #20
  Oct 26, 2012
  Joined: Apr 25, 2010
  Messages: 5,706
  Likes Received: 2,389
  Trophy Points: 280
  Ujasusi ni umbea uliokomaa ,kuingilia habari za watu ,kuzitoa nchi moja kupeleka kwengine !
   
Loading...