Juma Raibu Meya aliyevuliwa Madaraka Moshi adaiwa kung'oa miundombinu aliyoiweka alipokuwa madarakani

Erythrocyte

JF-Expert Member
Nov 6, 2012
117,789
218,420
Hii ndio taarifa mpya iliyotufikia kwenye Jumatatu hii ya Pasaka , Kwamba Mheshimiwa Juma Raibu aliyekuwa Meya wa Manispaa ya Moshi Mkoani Kilimanjaro , kabla ya kung'olewa hivi karibuni , ameanza kampeni kabambe ya kuondoa miundo mbinu yote aliyojitolea akiwa madarakani .

Wakati wa madaraka yake alisaidia kutengeneza miundo mbinu ya maji kwenye uwanja wa Mandela uliopo Kata ya Pasua , ili kusaidia vijana wanaotumia uwanja huo , Sasa baada ya kung'olewa kwenye Umeya naye akaamua Kama Mmbwai basi iwe Mmbwai tu , kang'oa miundo mbinu yote ya maji aliyosaidia .

Zipo Taarifa kwamba anapanga kung'oa mabati yote aliyosaidia kwenye mashule mbalimbali pamoja na Zahanati .

Aliyekuwa_Meya_wa_Manispaa_ya_Moshi%2C_Juma_Raibu_ameng%E2%80%99oa_miundombinu_ya_maji_aliyoku...jpg


===
Aliyekuwa Meya wa Manispaa ya Moshi, Juma Raibu ameng’oa miundombinu ya maji aliyokuwa ameiwezesha kufungwa wakati akitumikia wadhifa huo, hatua aliyochukua siku chache baada ya kung’olewa kutokana na tuhuma mbalimbali.

Taarifa ya gazeti la Raia Mwema inaeleza kwamba juzi alikwenda katika Uwanja wa Mandela ulioko Pasua na kung’oa miundombinu ya maji aliyoitoa siku za nyuma kwa vijana wanaotumia uwanja huo.

Mkazi wa Pasua, Waziri Shemanguzo amesema kwamba kitendo alichokifanya si cha kiuungwana kwani hata kama ametolewa, kwenda kuondoa misaada aliyoipatia jamii sio jambo la kiuungwana.

UPDATES
- Juma Raibu: Sijaondoa msaada wowote niliotoa Moshi, gazeti limetumika kunichafua
 
Hii ndio taarifa mpya iliyotufikia kwenye Jumatatu hii ya Pasaka , Kwamba Mheshimiwa Juma Raibu aliyekuwa Meya wa Manispaa ya Moshi Mkoani Kilimanjaro...
Ukishatoa misaada ukapokelewa sehemu husika na wewe ukaridhia kutoa kwa moyo. Toka muda huo hiyo misaada siyo ya kwako Tena ni mali ya mlengwa aliyepewa misaada. Hivyo kuja kuchukuwa Tena bila taarifa ya mlengwa huo ni wizi na uhujumu uchumi. Hivyo huyo jamaa anaweza shitakiwa na kufungwa.
 
Back
Top Bottom