Hashim Dogo wanamjua watu waliokua wanaenda kwenye matamasha na mashindano ya ku rap enzi hizoooo hapa Dar
Hana hit yoyote iliowahi kubamba redioni hadi mtu wa mtwara au madongo kuinama akaipenda bila kumuona
Umaarufu wa Dogo Hashim ni wa kimtaani taani tu, kujua kuchana
Na ndio maana ukiomba track yake hata moja hapa utaishia kupigwa sound tu, sasa unajiuliza huyu nguli wanavyomtete ni bora hizo track zake wanasikilizaga wapi?
Most of them walimsikia anachana stajini au waliambiwa kuna kichwa kinaitwa hashimu
Jay more ni mtamu kwenye tungo lakini flow yake inachosha, hana ubunifu sana na ameshindwa kwenda na mahitaji ya walaji wake,
Pengine angejaribu kufanya kazi na maproduza wengine wakambadilisha kidogo kuliko kukomaa na majani ambaye wameshindwa kurudi kama awali