Juma Duni: UKAWA imebaini kuna kura hewa milioni 9

Juma Duni: UKAWA imebaini kuna kura hewa milioni 9

Aisehi!!

Hata hesabu ya kujumlisha, ukatoa, ukazidisha na kugawanya haujui???!!!

Kumbe kweli kipaumbele cha kwanza elimu, cha pili elimu na cha tatu elimu

Kauli za uzushi kama anaushahidi autoe vinginevyo ni kukata tamaa.
 
Hembu Ukawa Msiwe Wapuuzi..Hivo Ni Vituo Tu,na Haimaanishi Vituo Vyote Vitakuwa Na Exactly Number Of People Yan 450.Vituo Vingine Vinapungufu Ya Hapo.Mf.Jimbo Lana Watu 1200 Hapo Tunategemea Kuwa Na Vituo 3.cha 1 Chenye Watu 450,cha 2 The Same Cha 3 Kitakuwa Na Watu 300 Kufikisha Idad Ya Wapiga Kura 1200.Sasa Nyie Ndugu Zetu Mnachukuwa Jumla Ya Vituo 72000 Zidisha Idadi Ya Watu Kila Kituo 450, Mkidhani Kila Kituo Kitakuwa Na Exactly Number.Jaribuni Kutuliza Akili Zenu,msishikiwe Akili Angalia Had Duni Naye Kashkiwa Akili Sijui Na Nani?
 
Hayo ni kwa mujibu wa mgombea mwenza wa Chadema Babu Duni.Amesema NEC wamendaa vituo vya kupiga kura 22,000 ambapo kwa idadi ya wapiga kura 450 kwa kituo ni jumla ya wapiga kura takriban milioni 33 tofauti na takwimu za tume za wapiga kura milioni 24

Source: Channel ten habari

Kiongozi umepotoka kidogo.

NEC imesema imeandaa na kuvitambua vituo 72,000 vya kupigia kura.
Ambapo (kwa mujibu wa NEC) kila kituo kitakuwa na si zaidi ya wapiga kura 450.

Kwa hesabu za kawaida tu:
450×72,000=32,400,000.
Idadi hiyo inazidi idadi ya waliojiandikisha ambao ni around 23M.

Kwa idadi ya waliojiandikisha kulitakiwa kuwe na vituo vya kupigia kura around 52000.

Hivyo basi inaonekana wazi kuna vituo hewa zaidi ya 19,000 vitakavyo kuwa na wapiga kura zaidi ya 8.55M

Kufuatia sintofahamu hiyo UKAWA imeitaka NEC kulitolea ufafanuzi suala hili.
 
dah hapo jamani mmezidi, hapo ni makadirio ya juu, huwezi kuweka vituo vibalance na wapiga kura uliokadiria kwa kila kituo.
unaweza kukadiria wapiga kura 450 kila kituo but ikaja kuwa vituo havina uwezo wa kufikisha wapiga kura 450.
 
Mxaada tafadhali Duni bado yupo jamani
 
Na bado mtataga mwaka huu.mnajuta kumfahamu Dr.John Joseph pombe Magufuli.
 
Hizi kauli inabidi NEC watoe ufafanuzi.
Na wawaruhusu viongozi wa vyama mbalimbali kukagua daftari la wapiga kura.
 
Watu wanataka kuingia ikulu sio longolongo kama mlivyozoea
 
Hizi kauli inabidi NEC watoe ufafanuzi.
Na wawaruhusu viongozi wa vyama mbalimbali kukagua daftari la wapiga kura.

Tatizo Nyie Wenzetu Kila Kituo Mshakitukana Na Kukiona Hakifai.Haya Maswali Na Hoja Zenu Za Kipumbavu,kila Siku Kailima Anazijibu Kupitia Vyombo Mbalimbali Esp Cloudsfm,sasa Kwakuwa Nyie Ni Wajuaji Na Kuona Kila Kitu Kwenu Ni Kuonewa Ndo Mana Hamuishi Kulalama Kila Siku,kila Siku Nyie Kwenu Ni Kulalamika Tu....
 
Ukawa wamekurupuka sana, hesabu haiko hivyo.
Mf. Kituo cha kuandikisha kilichokuwa na watu 1000 kitakuwa na vituo 3 vya kura kwa idadi ya A:333, B: 333 na C:334.
Ukawa, wazee wa kukurupuka, mtaendelea kuaibika mkishapata majibu ya NEC.
Mnatakiwa kuchunguza badala ya kuingia vyombo vya habari bila uchunguzi
 
Mzee kapanikishwa na matukio ya Arusha huyu.

Kwa mtu mwenye akili timamu kama Mzee Duni hawezi kuamini matokeo ya watu kujazwa kwa mabasi na Malori. Kazungumzia vituo na idadi ya wapiga kura.
 
Hembu Ukawa Msiwe Wapuuzi..Hivo Ni Vituo Tu,na Haimaanishi Vituo Vyote Vitakuwa Na Exactly Number Of People Yan 450.Vituo Vingine Vinapungufu Ya Hapo.Mf.Jimbo Lana Watu 1200 Hapo Tunategemea Kuwa Na Vituo 3.cha 1 Chenye Watu 450,cha 2 The Same Cha 3 Kitakuwa Na Watu 300 Kufikisha Idad Ya Wapiga Kura 1200.Sasa Nyie Ndugu Zetu Mnachukuwa Jumla Ya Vituo 72000 Zidisha Idadi Ya Watu Kila Kituo 450, Mkidhani Kila Kituo Kitakuwa Na Exactly Number.Jaribuni Kutuliza Akili Zenu,msishikiwe Akili Angalia Had Duni Naye Kashkiwa Akili Sijui Na Nani?

Wewe ndiyo Mpuuzi wa mwisho duniani, Iyo taarfa niya nec kwenda kwa nan? Na kwann hawakutoa ufafanuzi huo? ambao hata ww ulikuwa hauhufaham, umehufahamu baada ya bob Duni kuongea na kufungua akili yako kama ya lusinde, mafii yako kaa kimya wakat wanaume wanafanya yao, Hakuna goli la mkono na rais ni Lowasa!
 
Hayo ni kwa mujibu wa mgombea mwenza wa Chadema Babu Duni. Amesema NEC wamendaa vituo vya kupiga kura 22,000 ambapo kwa idadi ya wapiga kura 450 kwa kituo ni jumla ya wapiga kura takribani milioni 33 tofauti na takwimu za Tume za wapiga kura milioni 24.

Chanzo: Channel ten habari
Ukawa wanatapa tapa.halafu inasaidia kuwachanganya nyumbu
 
Wewe ndiyo Mpuuzi wa mwisho duniani, Iyo taarfa niya nec kwenda kwa nan? Na kwann hawakutoa ufafanuzi huo? ambao hata ww ulikuwa hauhufaham, umehufahamu baada ya bob Duni kuongea na kufungua akili yako kama ya lusinde, mafii yako kaa kimya wakat wanaume wanafanya yao, Hakuna goli la mkono na rais ni Lowasa!

Nyie Ndo Wapuuzi Kila Siku Kailima Anajibu Maswali Kwenye Vyombo Mbalimbali Vya Habari,sikilizeni Radio Acheni Kuropoka,huyo Duni Haji Akili Yake Alikuja Nayo Ni Kuzidisha Wakati Vingine Havizidishiki.Sikilizeni Vyombo Vya Habari,tatizo Lenu Nyie Kila Kituo Mshakitukana Na Kukisusia Mwisho Wa Siku Ndo Haya Sasa Kulalamika Tu.Hili Swala La Duni Haji Alishalitolea Majibu Kailima Hata Leo Kalijibu Tena Cloudsfm
 
shule moja morogoro ina mwalimu mmoja wanafunzi mia saba -CCM hoyeee hapa kazi tu
 
Sasa hiyo ni speculation
Babu aache kupiga kelele anajiaibisha.
Inawezekana kabisa kuna kura hewa lakini hii ni speculation!
Wafanye uchunguzi wa maana si mahesabu ya estimates
UMOJA wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) unaoundwa na vyama vinne vya upinzani vimedai kubaini mchezo mchafu ambao unataka kufanywa na serikali ya CCM kwa kushirikiana na Tume ya Uchaguzi ya Taifa (NEC). Anaandika Dany Tibason, Dodoma … (endelea).
Hali hiyo imejitokeza kutokana na kile kinachodaiwa kuwa NEC imetoa takwimu za upotoshaji ambazo zinalenga kuwapa ushindi CCM na kutimiza adhima yao ya ushindi wa goli la mkono.
​
Kauli hiyo ilitolewa jana na Mgombea Mwenza wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kwa mwanvuli wa Ukawa, Juma Duni Haji alipokuwa akizungumza na waandishi mjini hapa.
Mgombea huyo alisema kuwa takwimu zilizotolewa na NEC hazina ukweli wowote na kuna kila sababu ya kutolewa ufafanuzi takwimu hizo wamezipataje.
Amesema kwa mujibu wa tume ya uchaguzi inaonesha watu ambao wanastahili kupiga kura ni milioni 23.7 na vituo vyote vya kupigia kura vitakuwa ni 72,000 na kila kituo kitakuwa na watu 450.
Amesema katika kufanya ujanja ujanja NEC inaonekana kuwa na wapiga kura hewa milioni tisa ambapo kuna vituo hewa 20,000 kwa ni vituo halisi vinatakiwa kuwa 53,000 na siyo 72,000.
Mbali na hilo Haji alifafanua kuwa kwa hesabu ya kuwa na vituo 72,000 kama hesabu ya Tume inavyoelekeza ni wazi wapiga kura wanatakiwa kuwa milioni 32 na siyo milioni 23 tena.
Kutokana na hali hiyo Duni amemtaka mwenyekiti wa tume ya uchaguzi Jaji Damian Lubuva kuhakikisha anatoa mchanganuo mzuri wa mahesabu ya wapiga kura vituo utoa.
“Kamwe hatuwezi kukubali tume kwa kushirikiana na serikali kutafuta ushindi wa goli la mkoni kama ilivyozoeleka kwa chama hicho.
“Hata hivyo natahadharisha serikali ikilazimisha kutaka inachokitaka wao, bila kusikiliza watu wanataka nini, ni wazi kuwa kunaweza kutokea machafuko kwani watanzania kwa sasa wamechoka na wanataka mabadiliko,” alisisitiza Duni.
Akizungumzia kuhusu safari zake, amesema mpaka sasa kafanya mikutano katika majimbo 130 ambayo mengi yao yapo vijiji na watanzania wanamalalamiko yanayofanana.
Amesema wananchi wamechoshwa na manyanyaso kwani wamekuwa wakimbizi katika nchi yao na mbaya zaidi wananyanyaswa na wazawa wenzao na wala siyo wageni.
Amesema watanzania wamechoshwa na mipango isiyokwisha ambayo uchangishwa kwa lazima bila kuona mabadiliko yoyote ya ambayo wanatakiwa kuyapata.
Almesema watanzania wengi wanakumbwa na huduma mbovu ya afya, elimu, miundombinu, ukosefu wa walimu mashuleni pamoja na shule nyingi kukosa madawati.
Mbali na hilo alieleza kuwa amebaini kwamba wanachi wengi hawana uhuru kwa kufanya kile wanachokitaka kutokana na watawala wengi kuwatisha wananchi.
“Inasikitisha jinsi askari wanyama pori wanavyowashambulia wananchi hususani wale wanaoishi karibu na hifadhi jambo ambalo linaanyima haki wananchi kufanya maamuzi,” amesema Duni.
 
Back
Top Bottom