JUMA AWESO, wakazi wa goba hatuna maji wiki ya tatu sasa

JUMA AWESO, wakazi wa goba hatuna maji wiki ya tatu sasa

CHRC

Senior Member
Joined
Aug 2, 2011
Posts
166
Reaction score
226
Habari za jioni bw Aweso

Mm ni mkazi wa goba osterbay hapa jirani na bar ya Triple B,tuna muda wa wiki tatu hatujapata maji na wala dawasco hawajatoa taarifa yoyote ya nini tatizo.

Kikawaida tunapata maji kwa wiki mara moja kila siku ya jumatano, lakini imepita wiki tatu sasa hatujapata maji kabisa na hatujui tatizo nini!matokeo yake tumeishia kununua yale maji yanayouzwa katika magari ambapo inagharimu shilingi 15,000 kwa liter 1000!naomba sana ufuatilie na watu wako wa dawasa watueleeze shida ni nini??

Moderators naomba pia muupost huu uzi ktk mitandao yenu ya x, Whatsapp channel, Instagram ili dawasa na Juma aweso wauone wasaidie kutatua tatizo.
 
Waziri chawa atasaidia nini yeye na wake zake wanakula mema ya nchi kwa kuteuliwa teuliwa tu atakuja kuwakumbukeni nyie walalahoi wa goba sijui manerumango huko? pambaneni na hali zenu wenyewe wanakwambia kazi na utu na wanasonga mbele hizo sio shida zao na bado hadi 2035.
 
Back
Top Bottom