dubu
JF-Expert Member
- Oct 18, 2011
- 3,500
- 3,481
Heshima kwenu wakuu,
Kuna sehemu nimesikia audio ya Baba wa Taifa Mwalimu Julius K Nyerere akikemea Tabia ya watu kujifanya Mungu watu na kuanza kufukuza kazi wafanyakazi kisa tu wapo juu ya hao wafanyakazi. Baba wa Taifa alikemea tabia ya Mtu kujifanya anafukuza wafanyakazi kisa tu yupo juu yao.
Anaanza kwa kusema;
"Na huyu ni mtu sawasawa, ana akili sawasawa na mwenzie lakini anamwambia Mtu mwingine "Tangu leo huna kazi". Aah! bwana mkubwa, kazi ni uhai kazi ni kufa na kupona nina watoto nyumbani, unaniambia tangu leo sina kazi nifanye nini?
Lakini anao uwezo, Mtu mmoja anapewa uwezo wa namna hii wa kushiba au kutoshiba, wa kula au kutokula, wa kujua wapi pa kulala au ulale polini, anapewa mtu mmoja juu ya mtu mwingine.
Tukakataa siku za mwanzo kabisa za kupata uhuru wetu, tukageuza sheria tukatunga sheria kwa kufanya kazi iwe ni kazi ngumu sana kwa msimamizi wa kazi kumfukuza mfanyakazi, tumefanya makusudi kabisa kuweka sheria ile, lakini inalalamikiwa "Lakini wewe Mwalimu wewe rudisha unyampala bwana, mambo hayawezi kwenda vizuri. Rudisha unyampala bana, wewe ndiye umeharibu nchi unaona sasa wafanyakazi hawakubari kila mtu anajidai sana". Ulipata kuona kuna mahala watu wote wapo sawa?
sasa hili tunalikataa kabisa...KABISA...!!
Hayo yalikuwa ni maneno ya Hayati Baba wa Taifa Nyerere.