Julius Nyerere: Tunakataa na tunapinga kabisa hii tabia ya Mtu kufukuza Mfanyakazi

dubu

JF-Expert Member
Oct 18, 2011
3,496
3,461
Heshima kwenu wakuu,

Kuna sehemu nimesikia audio ya Baba wa Taifa Mwalimu Julius K Nyerere akikemea Tabia ya watu kujifanya Mungu watu na kuanza kufukuza kazi wafanyakazi kisa tu wapo juu ya hao wafanyakazi. Baba wa Taifa alikemea tabia ya Mtu kujifanya anafukuza wafanyakazi kisa tu yupo juu yao.

Anaanza kwa kusema;

"Na huyu ni mtu sawasawa, ana akili sawasawa na mwenzie lakini anamwambia Mtu mwingine "Tangu leo huna kazi". Aah! bwana mkubwa, kazi ni uhai kazi ni kufa na kupona nina watoto nyumbani, unaniambia tangu leo sina kazi nifanye nini?

Lakini anao uwezo, Mtu mmoja anapewa uwezo wa namna hii wa kushiba au kutoshiba, wa kula au kutokula, wa kujua wapi pa kulala au ulale polini, anapewa mtu mmoja juu ya mtu mwingine.

Tukakataa siku za mwanzo kabisa za kupata uhuru wetu, tukageuza sheria tukatunga sheria kwa kufanya kazi iwe ni kazi ngumu sana kwa msimamizi wa kazi kumfukuza mfanyakazi, tumefanya makusudi kabisa kuweka sheria ile, lakini inalalamikiwa "Lakini wewe Mwalimu wewe rudisha unyampala bwana, mambo hayawezi kwenda vizuri. Rudisha unyampala bana, wewe ndiye umeharibu nchi unaona sasa wafanyakazi hawakubari kila mtu anajidai sana". Ulipata kuona kuna mahala watu wote wapo sawa?

sasa hili tunalikataa kabisa...KABISA...!!

Hayo yalikuwa ni maneno ya Hayati Baba wa Taifa Nyerere.
 
Lakini katiba hii hii inayompa raisi uwezo wa kutumbua yeyote katika utumishi wa umma si iliwekwa na Nyerere?

What I see aliweka ugumu wengine kutimua wenzao kazi lakini yeye kama raisi akajibakizia power hizo, Je siyo double standard hiyo?
akikujibu nishtue
 
Mtatafuta reference zote ku-justify wanaotumbuliwa ila JPM yuko sahihi, JKN anasmaili sasa hivi huko juu kwa kusema That's my boy (JPM), keep goin!!
 
Heshima kwenu wakuu,

Kuna sehemu nimesikia audio ya Baba wa Taifa Mwalimu Julius K Nyerere akikemea Tabia ya watu kujifanya Mungu watu na kuanza kufukuza kazi wafanyakazi kisa tu wapo juu ya hao wafanyakazi. Baba wa Taifa alikemea tabia ya Mtu kujifanya anafukuza wafanyakazi kisa tu yupo juu yao.

Anaanza kwa kusema;

"Na huyu ni mtu sawasawa, ana akili sawasawa na mwenzie lakini anamwambia Mtu mwingine "Tangu leo huna kazi". Aah! bwana mkubwa, kazi ni uhai kazi ni kufa na kupona nina watoto nyumbani, unaniambia tangu leo sina kazi nifanye nini?

Lakini anao uwezo, Mtu mmoja anapewa uwezo wa namna hii wa kushiba au kutoshiba, wa kula au kutokula, wa kujua wapi pa kulala au ulale polini, anapewa mtu mmoja juu ya mtu mwingine.

Tukakataa siku za mwanzo kabisa za kupata uhuru wetu, tukageuza sheria tukatunga sheria kwa kufanya kazi iwe ni kazi ngumu sana kwa msimamizi wa kazi kumfukuza mfanyakazi, tumefanya makusudi kabisa kuweka sheria ile, lakini inalalamikiwa "Lakini wewe Mwalimu wewe rudisha unyampala bwana, mambo hayawezi kwenda vizuri. Rudisha unyampala bana, wewe ndiye umeharibu nchi unaona sasa wafanyakazi hawakubari kila mtu anajidai sana". Ulipata kuona kuna mahala watu wote wapo sawa?

sasa hili tunalikataa kabisa...KABISA...!!

Hayo yalikuwa ni maneno ya Hayati Baba wa Taifa Nyerere.

afu eti mchana kweupe kabisaaa kuna watu wanataka kuwalinganisha makanjanja wa kisiasa tulionao leo na huyu mzee (rip) mwenye hekma na mpenda haki.

ulinganifu huu ni matusi ya rejareja kwa babu yetu....atakuja kuwafufukia nyie! haya!
 
Ndio mzuri huyooo. Tulipofikia tulikuwa tu nahitaji kiongozi wa namna yake tu
 
Back
Top Bottom