Julius Nyerere: Tunakataa na tunapinga kabisa hii tabia ya Mtu kufukuza Mfanyakazi

Mtatafuta reference zote ku-justify wanaotumbuliwa ila JPM yuko sahihi, JKN anasmaili sasa hivi huko juu kwa kusema That's my boy (JPM), keep goin!!
Kwasababu kampa baba,mama au ndugu zako vyeo siku wakifukuzwa ndoutajua kwanini MWL nyerere aliyasema hayo.uongozi nikipaji unaweza kuwa mkali na watu wasifanye Kazi wakakukomoa kwa kufanya Kazi za hovyo lakini unaweza kuwa mwenye busara watu wakajituma kufanya Kazi kwa weledi na ufanisi mkubwa,muda ndio msema kweli siku hazigandi tutayaona hayo mafanikio ya utumbuaji 2020 kama yatajenga viwanda na kuinua uchumi wa nchi,anaowaongoza sio mbuzi wala ng'ombe ni binadamu wanaakili tusubiri muda
 
mkuu, huo ndio msimamo wangu hata mimi. watanzania tulikuwa tumefikia pabaya sana, kina mnyika walikuwa wanamtukana tuu JK bila hofu, wafanyakazi wa UMMA walikuwa wanaboronga tuu majukumu yao bila hofu, watu walikuwa wanajichukulia tuu mikopo benki bila kurudisha, watu walikuwa wanawaza dili mwanzo mwisho bila hofu.

leo JPM anawanyoosha watu wawe na nidhamu potelea mbali hata kama ni ya uoga, kuna watu tena wenye maono yao kabisa kama kina jenerali ulimwengu eti wanabeza. WATANZANIA TUKUBALI TUKATAE, HAKUNA NIDHAMU BILA WOGA/ HOFU.

JPM awapige kwanza mkwara wa kufa mtu, watanzania wawe na hofu kuwa wakiharibu, watawajibika. ikiwakaa akilini vizuri hii, ndio utaona nidhamu inashamiri. narudia tena, HAKUNA NIDHAMU BILA HOFU, kanyaga twende JPM, hapo hapo usiachie, ikibidi kanyaga zaidi kwa nguvu zaidi mpaka watanzania tutie adabu. tumedeka mno ndio maana maendeleo yetu duni.

Mfumo kaka, ajenge mfumo, hivi akiondoks yeye akaja mwingine easy going nchi si inakuwa hivyohivyo?
 
Najua lengo lako ni nini,mtu pekee katika dunia hii anayestahili kuitwa GREATEST ni Mungu,unaweza tu ku edit ukaweka neno lingine la kumsifia Raisi wetu mpendwa hayati Julius K.Nyerere ili ilete maana inayokusudiwa.
Hayo umeyasema wewe,Mungu ni Mungu tu ataendelea Kua Mungu.Wenye akili timamu wamenielewa,once again Nyerere was the GREATEST.
 
Nyerere mwenyewe wakati wa utawala wake kafanya madudu mengi tu achilia mbali kufukuza watu kazi alikuwa anawaweka watu vizuizini kisa walimpinga tu na kutofautuana mitazamo, na wengine walimkimbia kuhofia usalama wao.
 
Heshima kwenu wakuu,

Kuna sehemu nimesikia audio ya Baba wa Taifa Mwalimu Julius K Nyerere akikemea Tabia ya watu kujifanya Mungu watu na kuanza kufukuza kazi wafanyakazi kisa tu wapo juu ya hao wafanyakazi. Baba wa Taifa alikemea tabia ya Mtu kujifanya anafukuza wafanyakazi kisa tu yupo juu yao.

Anaanza kwa kusema;

"Na huyu ni mtu sawasawa, ana akili sawasawa na mwenzie lakini anamwambia Mtu mwingine "Tangu leo huna kazi". Aah! bwana mkubwa, kazi ni uhai kazi ni kufa na kupona nina watoto nyumbani, unaniambia tangu leo sina kazi nifanye nini?

Lakini anao uwezo, Mtu mmoja anapewa uwezo wa namna hii wa kushiba au kutoshiba, wa kula au kutokula, wa kujua wapi pa kulala au ulale polini, anapewa mtu mmoja juu ya mtu mwingine.

Tukakataa siku za mwanzo kabisa za kupata uhuru wetu, tukageuza sheria tukatunga sheria kwa kufanya kazi iwe ni kazi ngumu sana kwa msimamizi wa kazi kumfukuza mfanyakazi, tumefanya makusudi kabisa kuweka sheria ile, lakini inalalamikiwa "Lakini wewe Mwalimu wewe rudisha unyampala bwana, mambo hayawezi kwenda vizuri. Rudisha unyampala bana, wewe ndiye umeharibu nchi unaona sasa wafanyakazi hawakubari kila mtu anajidai sana". Ulipata kuona kuna mahala watu wote wapo sawa?

sasa hili tunalikataa kabisa...KABISA...!!

Hayo yalikuwa ni maneno ya Hayati Baba wa Taifa Nyerere.

Umechanganya mambo, Mkubwa!
Wapo watu waliotungiwa sheria kama hiyo na wapo watu ambao waliachiwa madaraka ya kufukuza. Rais miaka yote anafukuza. Usidanganyike.
Uliza Edwin Mtei aliondokaje kazini tena na huyo huyo baba wa taifa.
 
Back
Top Bottom