kwa hiyo chadema mnaunga mkono kupanda kwa umeme?
HahahaaaaaHuu ushauri kwa sizonje ni sawa na kumjaribu na yeye hajaribiwi
Heshima kwenu wakuu,
Kuna sehemu nimesikia audio ya Baba wa Taifa Mwalimu Julius K Nyerere akikemea Tabia ya watu kujifanya Mungu watu na kuanza kufukuza kazi wafanyakazi kisa tu wapo juu ya hao wafanyakazi. Baba wa Taifa alikemea tabia ya Mtu kujifanya anafukuza wafanyakazi kisa tu yupo juu yao.
Anaanza kwa kusema;
"Na huyu ni mtu sawasawa, ana akili sawasawa na mwenzie lakini anamwambia Mtu mwingine "Tangu leo huna kazi". Aah! bwana mkubwa, kazi ni uhai kazi ni kufa na kupona nina watoto nyumbani, unaniambia tangu leo sina kazi nifanye nini?
Lakini anao uwezo, Mtu mmoja anapewa uwezo wa namna hii wa kushiba au kutoshiba, wa kula au kutokula, wa kujua wapi pa kulala au ulale polini, anapewa mtu mmoja juu ya mtu mwingine.
Tukakataa siku za mwanzo kabisa za kupata uhuru wetu, tukageuza sheria tukatunga sheria kwa kufanya kazi iwe ni kazi ngumu sana kwa msimamizi wa kazi kumfukuza mfanyakazi, tumefanya makusudi kabisa kuweka sheria ile, lakini inalalamikiwa "Lakini wewe Mwalimu wewe rudisha unyampala bwana, mambo hayawezi kwenda vizuri. Rudisha unyampala bana, wewe ndiye umeharibu nchi unaona sasa wafanyakazi hawakubari kila mtu anajidai sana". Ulipata kuona kuna mahala watu wote wapo sawa?
sasa hili tunalikataa kabisa...KABISA...!!
Hayo yalikuwa ni maneno ya Hayati Baba wa Taifa Nyerere.
Maneno haya ya mwalimu ndio yalifanya utendaji kazi nchi hii udorore. Sheria alizotunga za kumlinda mfanyakazi ndio zilifanya tija ikapungua sana nchi hiikwa sababu ya vikao vya kujadili mfanyakazi aliyefanya kosa.
Mahali popote sheria za kumlinda mfanyakazi zikiwa nyingi basi tija hupungua.
Hofu ya kufukuzwa na kukosa kazi ndio inajenga nidhamu ya ufanyaji kazi. Hata mkisema inakuwa nidhamu ya woga lakini bila woga hakuna linalifanyika.
Hata kwenye familia watoro wanaogopa kuchelewa kurudi nyumba kwa hifu ya kuadhibiwa.
Tujirekebishe
Hivi kuna watu wana mental constipation au, ni kwanini Cdm hutajwa tajwa hata kwenye mambo yakipuuzi yasiyoihusu bila hata chembe? Shame on u! Au hujalipwa hebu isome namba hata kwa vibration
EWURA, TANESCO ni taasisi za wapinzani? Hata shetani anawashangaa kwa unafiki huu.Yan Wapinzani WAMEUMIA SANA UMEME KUTOpanda. polen sana maana ile kiki imepotea
Nakubaliana na wewe kabisa. Hata nyumbani bila mkwara mambo hayaendi sembuse nchi. Ndio maana kuna sheria tena sheria kali ili kuwe na nidhamu.mkuu, huo ndio msimamo wangu hata mimi. watanzania tulikuwa tumefikia pabaya sana, kina mnyika walikuwa wanamtukana tuu JK bila hofu, wafanyakazi wa UMMA walikuwa wanaboronga tuu majukumu yao bila hofu, watu walikuwa wanajichukulia tuu mikopo benki bila kurudisha, watu walikuwa wanawaza dili mwanzo mwisho bila hofu.
leo JPM anawanyoosha watu wawe na nidhamu potelea mbali hata kama ni ya uoga, kuna watu tena wenye maono yao kabisa kama kina jenerali ulimwengu eti wanabeza. WATANZANIA TUKUBALI TUKATAE, HAKUNA NIDHAMU BILA WOGA/ HOFU.
JPM awapige kwanza mkwara wa kufa mtu, watanzania wawe na hofu kuwa wakiharibu, watawajibika. ikiwakaa akilini vizuri hii, ndio utaona nidhamu inashamiri. narudia tena, HAKUNA NIDHAMU BILA HOFU, kanyaga twende JPM, hapo hapo usiachie, ikibidi kanyaga zaidi kwa nguvu zaidi mpaka watanzania tutie adabu. tumedeka mno ndio maana maendeleo yetu duni.
Busara,uvumilivu, unyenyekevu na hofu ya mungu unamuachia nani?JP anatamani amfikie JKN lakini kigezo cha hekima kinampwaya
Enzi za JK tulisema ni dhaifu, anahamisha na kuwalinda watumishi wabovu sasa hv tumebalisha gia angani yunawatetea tuliokua tunasema watimuliwe.................kweli siasa zimeathiri bongo zetu
Ulitegemea bavicha watapata agenda gani ya kuzungumzia utawala huu na kuikosoa serikali Mkuu?Enzi za JK tulisema ni dhaifu, anahamisha na kuwalinda watumishi wabovu sasa hv tumebalisha gia angani yunawatetea tuliokua tunasema watimuliwe.................kweli siasa zimeathiri bongo zetu
Enzi za JK tulisema ni dhaifu, anahamisha na kuwalinda watumishi wabovu sasa hv tumebalisha gia angani yunawatetea tuliokua tunasema watimuliwe.................kweli siasa zimeathiri bongo zetu
Kuishi kwa mazoea kwa bahati mbaya bado kunaendelea. Rasimu ya Katiba ya Jaji Warioba ilikua ni mwarobaini. Ilipendekezwa kuundwa chombo cha kushughulikia jinsi ya kuwapta viongo waandamiz, lakini kwa sasa tuko pale pale kwenye mazoea. Unateuliwa badala ya chombo kimoja tena chenye mchanganyiko wa watu. Ni hadi pale Katiba itakapowekwa sawa. Kwa sasa mazoea yataendelea kuwepo. Inawezekana kutoa mazoea kwa usoni yakaja mgongoni, sasa hapo ni sawa na kaz bure.Haya mambo ya kuishi kimazoea na kuleana ndiyo yaliyotufiksha hapa! Hakuna haja ya kurudi huko tena! Tunasonga mbele! Mh. rais wapo wanaoguswa sana na jitahada zako! Ongeza bidii watakuelewa tu! Kila mahali kuna wanaochelewa kuelewa na hawa ni mmoja wa hao! Ila watakuelewa tu!
Najua lengo lako ni nini,mtu pekee katika dunia hii anayestahili kuitwa GREATEST ni Mungu,unaweza tu ku edit ukaweka neno lingine la kumsifia Raisi wetu mpendwa hayati Julius K.Nyerere ili ilete maana inayokusudiwa.Nyerere was the GREATEST.
Hivi hujui hizo ni mamlaka tu za uteuzi,haiwezekani mkuu wa idara akateuliwa na rais,lakini yule anayemteua anafanya kwa niaba ya rais..hiyo ni sheria ya utumishi wa umma 2007 inavyosemaNi kuvuliwa madaraka tena ya kuteuliwa na rais hata nyerere aliwatumbua wengi na wengine kuwaweka kizuizini.