Julius malema apewa adhabu anc | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Julius malema apewa adhabu anc

Discussion in 'International Forum' started by Boflo, May 16, 2010.

 1. Boflo

  Boflo JF-Expert Member

  #1
  May 16, 2010
  Joined: Jan 20, 2010
  Messages: 4,394
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Send to a friend
  0diggsdigg

  PRETORIA, Afrika Kusini
  KIONGOZI wa kundi la vijana wa chama tawala cha African National Congress (ANC) nchini Afrika Kusini, Julius Malema, ameamrishwa kuhudhuria vipindi maalum vitakavyoweza kumsaidia kujifunza kukabiliana na hasira.

  Katika kikao cha nidhamu, Malema aliomba msamaha hadharani pamoja na kutozwa faini ya dola1,300 kwa kukichafulia sifa chama cha ANC.

  Maafisa wa chama hicho walimtia hatiani Malema, kwa kumkosea heshima Rais Jacob Zuma kwa kumkosoa hadharani kama kiongozi wa ANC.

  Malema alitoa taarifa akiomba msamaha kwa kusababisha mgawanyiko ndani ya ANC.

  Rais Jacob Zuma alimkaripia Malema hadharani baada ya kumfukuza mwandishi mmoja wa habari wa BBC katika kikao cha wanahabari, na juu ya tabia yake ya kubagua watu kwa misingi ya rangi pamoja na kumuunga mkono Rais wa Zimbabwe, Robert Mugabe.

  Chama tawala kimekuwa kikitaka kutatua tatizo la Malema kabla ya baraza kuu la Chama hicho kukutana mwishoni mwa wiki hii.

  source: Mwananchi
   
Loading...