Julio: Nimevutiwa sana na Mayele, ni straika wa ukweli

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Feb 7, 2022
2,308
5,462
Kocha Jamhuri Kihwelo Julio amesema kwa msimu huu mshambuliaji huyo wa Yanga, amefanya kazi nzuri n ani straika halisi kwa kuwa anajua kufunga.

Amesema “Licha ya kuwa mpira wa sasa hivi combination imesababisha wachezaji wengi kufunga magoli lakini Mayele anaweza kufunga popote.

“Tabu anayopata kwa sasa ni kuwa anakabwa sana, kwanza mastraika wengi siyo mafundi wa kumiliki mpira lakini Mayele ni fundi, anaweza kuukontroo mpira na kuuchezea, anaweza kupiga cheka na kutoa pasi.

“Angalia kama goli alilofunga juzi, straika mwingine ni ngumu kufunga, anatumia miguu yote miwili.

Chanzo: Wasafi FM
 
Ki ukweli Mayele ni mshambulizi mzuri na hatari kwa ligi yetu ya ndani hata lile goli alilowafunga Real Bamako siyo kila mshambuliaji angefunga.
Onyo nilishasema sibishani mpira tena na shabiki ambaye timu yake haishiriki Super League.
hapo nimeongea ukweli na ukweli usemwe...
 
MAYELE anahitaji washauri wa Saklojia.

💡 Atambue wazi ushindi wa timu ni Bora zaidi ya kutetema na yule aliyetoa assist ana heshima zaidi ya yule aliyemalizia kumfunga.

💡 Najua anataka Afrika imjue ili kuongeza thamani yake ila, pamoja na kumfunga nafasi za wazi anazopoteza kwa kulazimisha kumfunga ni nyingi Sana.

💡 Mechi ya TP mazembe nilichukua muda mwingi kumtafakari nikagundua alikuwa analizimisha kumfunga ili apeleke ujumbe kwao Kongo jinsi ALIVYO bora au anavyopendwa Tanzania. Alipoteza nafasi nyingi Sana siku hiyo.

💡 Ninachomsifu siku za katibuni kapngeza kitu kipya ambacho ni speed ya kuvutika hadi mwisho kama akina moloko na kisinda ijapokuwa kisinda ni sometimes man anaweza kukimbia mpaka akashindwa kupiga Kona na kulipita goli. MAYELE akitumia wepesi wake , akili, mbio na uwezo wa kutumia miguu yake miwili kutoa assist Yanga itakuwa inafunga mabao zaidi ya 5 Kila mechi
 
kama kunamtu atabisha huyo ajui mpira.
maombi yangu usiku na mchana ni jinsi gani timu yangu ya Simba anamchukua huyu Haaland wa Congo.

sifa nyingine ya Mayele hana majeraha ya mara kwa mara ukizingatia ni stricker anaekamiwa lakini anamaliza msimu akiwa hana majeraha ya muda mrefu au ya mara kwa mara.
Halafu haanguki hovyo. Huwa ananishangaza sana akiamua kupress na mpira kwenda golini, hata beki akimchallenge kimabavu, atakaza aende kufunga. Wachezaji wengi wa kitanzania kwenye mazingira hayo kuwa wanaanguka kwa kuzidiwa nguvu au kutafuta foul au penati.
 
Ndio.
huyu ndo namba tisa wa asili sasa,namba tisa wa asili huwa awajiangushi kijanja janja kutafuta penati bali huwa anapambana ascore,kwasababu kwenye tuta kunakukosa au kupata.
 
Mechi ya juzi yanga na kmc msize alikuwa anawatoka mabeki vizuri akifika eneo la mwisho anageuka kinyambe tk.
Wachezaji wengine hawafundishiki hata nabi amesema ilo.
 
Ndio.
huyu ndo namba tisa wa asili sasa,namba tisa wa asili huwa awajiangushi kijanja janja kutafuta penati bali huwa anapambana ascore,kwasababu kwenye tuta kunakukosa au kupata.
Ila huyu pale Simba angechezeshwa kama winga. Okrah akicheza kama winga angeweza kuipa Simba baadhi ya vitu hivi alivyonavyo Mayele ila ndiyo hivyo mzaha mwingi.

Huyu kumtoa pale Yanga ni ngumu sasa hivi, juzi juzi wametoka kumuongezea malipo yake maana walishaanza kunusa wahuni wanaweza kumnyakua.
 
Kumchezesha kama winger unamuharibu na awezi kukupa kilicho bora mkuu.

Yanga sahivi wanaona mbali hivi mashine kama Mayele unaachaje kumlinda kwa nguvu zote kwenye stahiki zake?.Kumbuka huyu jamaa keshaanza kuingia kwenye nchi za kaskazini huko kwenye timu zenye financial muscles.ukizubaa Pyramids wanaweka mzigo mezani.puh!
 
Back
Top Bottom