Waku habarini. Habari zilizopatikana toka kwa makada watiifu toka ccm ni kwamba baadhi ya makada wa ccm hawana imani na ujio wa masalia waliotimuliwa na chadema ikiwemo juliana shonza na mtela mwampamba ndani ya chama chao kipya cha ccm. Baadhi ya makada yasemekana hawana imani wala amani mioyoni ya kufanya nao kazi pamoja na kwa uwazi za chama hicho. Baadhi ya makada wamemtahadharisha Nape nnauye juu ya kuwapa kila jambo na mambo ya chama chao hao vijana. Mjumbe mmoja wa kamati kuu amenukuliwa akisema kuwa ' inabidi ccm iwe na tahadhari na vijana hawa isije ikawa wamekuja kupeleleza mambo ya chama chetu halafu baadae wakatukimbia' mwisho wa kunukuu. Wakuu inasemekana baadhi ya makada wanawasi wasi na wanahoji kwa nini waje ccm na wasiende vyama vingine vya upinzani? Wengine wanasema ukiwaangalia kwa makini mioyo yao iko upinzani halafu miili iko ccm! Wakuu nimenyetishiwa na kigogo mmoja toka makao makuu ya chama. Nawasilisha.