Julai 2017: Nyongeza za mishahara na kupandishwa vyeo - Kilio cha Watumishi wa Umma

Sikubaliani na hili mkuu. Udhaifu wa watu wengine hawawezi kubebeshwa watoto wasio na hatia na pengine ndio wakombozi wa kesho.

Fikiria walimu wako wangefanya hivi leo hii ungekuwa wapi?
Kuna "voluntary action na unvoluntary action" ivi mkuu unajua ukali wa naisha wanaokumbana nao watumishi hasa walimu? Mkuu tunajua watoto wana dream zao kama sisi ila mwalimu nae anadream za kuishi kwenye nyumba yake, kudrive n.k so kumdiscourage kiasi hiki sio ubinadamu.... tujiandae kupokea mabateshi wa kuzidi kuanzia mwakani

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Yaani mtu umekaa kabisa unasubiri salary slip kwa matumaini makubwa kwamba yule bwana ataongeza mshahara mwezi huu. Hata kama angeongeza, ingekuwa kiduchu sana, not worth all that anticipation. Kazi sana huko kwa Mnyampara.
 
Salaam wanajamvi

Naomba nichukue fursa hii kusikitishwa sana kwa awamu hii ya tano!! NI MWAKA WA PILI SASA INCREMENT HAIPO!!

Hili swala halijatokea kwa bahati mbaya ni watu tuliowapa dhamana wameamua kufanya hivyo!! Kwa mara ya mwisho annual increament ilikua july 2015, hadi leo watumishi hawajaongezwa na ongezeko hilo lipo kimkataba, yaani kila ifikapo July 01 ya kila mwaka mkataba unamtaka mwajiri aweke hilo ongezeko lakini toka 2015 hawajawahi ongeza!!!

Vyama vya wafanyakazi vipo lakini ni kama vipofu hata kubweka tu hakuna. Tunakatwa kila mwezi 2% ya mshahara kwenye hivi vyama ili vitetee maslahi ya watumishi lakini nichelee kusema wanatuibia pesa tu kwani hakuna walifanyalo!!!

Uonevu ukizidi huzaa chuki na hasira na unaweza pelekea visasi. Msituone wajinga hatuna la kuwafanya lakini ghadhabu na machungu ya dhuluma hizi zipo ndani ya mioyo ya watumishi!!!

Naomba niishie hapa!!!!!!!
 
Back
Top Bottom