Julai 2017: Nyongeza za mishahara na kupandishwa vyeo - Kilio cha Watumishi wa Umma

bcb661ed211ffd7569fb215ac117991d.jpg
Weita leta Balimi ingine

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ifike hatua tupunguze masihara kwenye mambo ya msingi. Pia ifikie hatua uvumilivu ufike kikomo tuseme basi yatosha. Ifike hatua tujitambue na wajue thamani ya kila mtanzania na mtumishi pia. Bila watumishi hii nchi haiwezi endelea.

Watumishi waserikali hii wamekuwa wavumilivu sana na ni wavumilivu ambao wanatakiwa kupewa pongezi. Ni mwaka watatu sasa lakini bado wamekuwa na matumaini kwa viongozi wao kuwa ipo siku wataelewa umuhimu wao. Lakini viongozi wabinafsi na wenye chuki wameshindwa kulielewa hilo.

Haiwezekani na ni ngumu kuamini kiongozi uliopewa dhamana ukashindwa kutambua thamani ya wanaokusaidia kazi kwa kujali maisha yako halafu uendelee kuwahubiria hapa kazi tu. Ni kazi gani hiyo ambayo wasema bila kujali kuwa hao watumishi wanategemewa na familia zao.

Hivi yahitaji darubini ya aina gani kutambua mchango wa watumishi kwenye jamii waliyopo bila kujali familia zao. Watumishi wengi ndio wanaowasadia ndugu na majirani kuenda shule kwa kuwalipia karo. Wengi wetu tumesoma kwa kusaidiwa na ndugu na jamaa bila kujali hata kile kidogo wanachopata. Leo hii mtanzania aliyezaliwa Tanzania anashindwa kulielewa hili. Yawezekana sio mtanzania maana kama angekuwa mtanzania basi natumai angejua vyema jinsi maisha ya watanzania yalivyo.

Waziri mwenye dhamana akiwa ndani ya bunge alijibu hoja ya nyongeza kwa madaha sana. Na akathibitisha kuwa wameongezea bajeti ili kutoa ongezeko la mishahara kwa watumishi. Hivi hilo ongezeko amelitoa kwa familia yake au amejiongezea yeye mwenyewe. Kwa sababu imejidhihirshwa wazi kwa watumishi hawajaongezewa chochote mpaka sasa, hivyo ulaghai kwa viongozi tuliowachagua umeendelea kujidhihirisha. Kama hili dogo tu wameshindwa kulitekeleza kwa watumishi wao ambao ni wanyonge vip hayo mengine wanayohangaika na watu wanao kula nao sehemu moja.

Sasa ni wakati wenu watumishi kudai haki zenu ni wakati wa kupigania haki yenu. Kwa kuanza kuna haja ya kuwabana viongozi waliokaribu yenu na kingine ni kuungana kwa pamoja bila kujali utofauti wa kada zenu wala dini mpaka kielewekee.

Sauti ya mnyonge hutolewa na mnyonge hakuna asiye mnyonge atakuja kupigania haki yenu. Hao viongozi wenu wa kisiasa ni wanafiki na wapo kuangalia maslahi yao tu.

Sent using Jamii Forums mobile app
Ni watanzania wachache sana wenye kulielewa hili watanzania tumekwisha yani sijui tulimkosea nin mungu, maisha yanavyozidi kua magumu kwa mfanyakazi basi hata Kwa mkulima yakua magumu Mara Mbili.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom