Jukwaa linaloogopwa

Alwaz

JF-Expert Member
Apr 29, 2010
7,115
10,822
Nimetembelea blogu nyingi kuona ipi ni bora na iliyotengenezwa kitaalamu kutoa fursa bora kwa watumiaji wake.Jamii forums nimegundua ndipo penyewe.
Jf ina uvumilivu wa mambo mengi lakini inaogopa sana jukwaa la Dini na Imani.Mara leo lipo mara limefutwa!.Hofu ni nini?.
 
JF haina dini - Wewe ni M-dini?
 
Wanaolifuta ndio wanaliogopa au wachangiaji ndio wana hofu nalo??:sad:

Hebu tupatie mtazamo wako juu ya hilo jukwaa
 
Lakini hujakatazwa kujadili dini au kutoa hoja ya dini.Si uiweke kwenye hoja mbalimbali uone kama thread yako itafutwa?
 
i think ni vizuri kukawa na thread za mambo ya dini kwani kuna admin wa ku control, kama itaonekana kuna thread ina wa offend wengine ni inafutwa tu!
 
JF haina dini - Wewe ni M-dini?
Haiwezekani kwamba JF haina dini.Kama ni hivyo mbona inaogopa dini?,kama kweli hilo jukwaa hufutwa na kurudishwa kila baada ya muda.
 
Kwa hiyo dini ya JF ni ipi na kwa nini kuna dini hiyo?
 
Wanaolifuta ndio wanaliogopa au wachangiaji ndio wana hofu nalo??:sad:

Hebu tupatie mtazamo wako juu ya hilo jukwaa
Askofu huoni kwamba wanaolifuta ndio wanaoligopa!.Kwa sababu wao ndio wameshikilia mpini.Wachangiaji hawana hofu nalo,wataalamu kama wewe askofu mupo wengi.Na hueanda kuna moderator mmoja tu ndio mdini au tuseme anaogopa dini.
 
Kwa hiyo dini ya JF ni ipi na kwa nini kuna dini hiyo?

Kwa jinsi huu msamiati wa udini unavyotumika kwengine hii dini ina uwezekano kwamba ni kama ya huko.Mfano tunasikia serikali haina dini lakini huwa inaumwa sana ukristo ukishambuliwa na hauna habari uislamu ukiumizwa. Kwa mfano kupitia sheria ya ugaidi.
 
Hapo chacha!!
Kama wewe unapenda kuanzisha topic inayohusiana na mambo ya imani si uanzishe? kwa nini unalalamika.

kwanza kwa nn unasema mambo ya dini badala ya mambo ya imani?
 
Imani na dini huenda pamoja ndio maana hata jukwaa tunaloongelea limeitwa dini na Imani.
 
Kwa mfano kupitia sheria ya ugaidi.

Usitetee magaidi, kule Iraq na kwingineko wanapiga mabomu hata misikiti, hawaangalii kama umefuga ndevu na kuvaa gauni (aka kanzu) watakulipua tu ndugu! Kama hujui kufa chungulia kaburi! Ukali wa Sheria unatokana na ukali wa kosa na utendaji wake na pia kusambaa kwake!
 
Kwa jinsi huu msamiati wa udini unavyotumika kwengine hii dini ina uwezekano kwamba ni kama ya huko.Mfano tunasikia serikali haina dini lakini huwa inaumwa sana ukristo ukishambuliwa na hauna habari uislamu ukiumizwa. Kwa mfano kupitia sheria ya ugaidi.
basi ushaeleweka, kumbe mambo yetu yaleee!!!! anzisha angalao blog basi uwe unaweka kero zako zinazohusu dini yako dhidi ya nyingine kama unavyotaka.
 
haya tena mengine ..halijawahi kufutwa labda kama kuna marekebisho ..

Dada First Lady labda humu jukwaani unaingia ukiwa unasinzia au unafikiri mbali pengine kuzimu ndio maana huwa huangalii vizuri.Hili jukwaa tangu mimi nije hapa huwa linapotea potea sana.Lenyewe si jukwaa kubwa kama majukwaa mengine.Haiwezekani kuwa linaharibika kila mara kiasi hicho.Lazima itakuwa ni jukwaa linaloogopwa na aliyepewa dhamana ya kuliangalia.
 
Imani na dini huenda pamoja ndio maana hata jukwaa tunaloongelea limeitwa dini na Imani.
kumbe jukwaa lenyewe unalijua? kwanza jukwaa lile ni la premium member!! fanya utaratibu kwa invisible kwanza!
 
basi ushaeleweka, kumbe mambo yetu yaleee!!!! anzisha angalao blog basi uwe unaweka kero zako zinazohusu dini yako dhidi ya nyingine kama unavyotaka.

Naamini maelezo yako si msimamo wa admin wa Jamii forums.Kwa sababu kama wahusika wangekuwa na msimamo huo basi wasingeingia kwenye Internet,badala yake mijadala yote wangefanya kwenye kompyuta zao majumbani mwao.
 
kumbe jukwaa lenyewe unalijua? kwanza jukwaa lile ni la premium member!! fanya utaratibu kwa invisible kwanza!

Bahati mbaya ilikuwa sijuwi kwamba Invisible ndiye anayeliendesha.Wewe unayefahamiana naye mwambie afanye mipango ili mtambo wake usizimike kila mara.Kwa sababu mimi hili jukwaa ndilo ninaloona litawapeleka wana jamii pema kwa anyetaka na pabaya kwa anayetaka.
 
Back
Top Bottom