Jukwaa la Wahariri Tanzania TEF lapinga hatua ya Serikali kulifungia gazeti la MWANAHALISI

Ghazwat

JF-Expert Member
Oct 4, 2015
23,718
66,262
Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF) limesikitishwa na taarifa ya kufungiwa kwa miezi 24 kwa Gazeti la Mwanahalisi.

Kufungiwa kwa Mwanahalisi kunathibitisha kwamba Serikali bado imekuwa na 'shauku' ya kufungia vyombo vya habari licha ya kupitishwa kwa Sheria ya Huduma za Habari ya 2016 ambayo inatoa mwanya wa masuala yanayohusu vyombo vya habari kupelekwa Mahakamani na kutolewa uamuzi baada ya pande zote husika kusikilizwa.

Kwa maana hiyo, tunapinga kwa Gazeti la Mwanahalisi kama ambavyo tumewahi kupinga matukio mengine ya kufungiwa kwa magazeti siku zilizopita. Uongozi wa Jukwaa la Wahariri utakutana na kutafakari hatua zaidi ya kuchukua kuhusu suala hili.

Imetolewa na;

Theophil Makunga
Mwenyekiti - Tanzania Editors Forum


b408ed41cd5d817323abee9b82d0495d.jpg
 
Huyo Theophil Makunga wakati hiyo sheria ya vyombo vya habari inapitishwa hakuwepo dodoma leo hii anaitumia kama reference.
 
Hiyo ndiyo tabia ya "udikteta" anaanza moja baada ya nyingine............

Alianza na Bunge kuzima Live...........
Watu tukawa kimya!

Akaja na kuzuia mikutano ya kisiasa kwa vyama vya upinzani.........
Watu tukawa kimya!

Amekuja kuanza kufungia magazeti yanayomsema vibaya.......
Watu tumendelea kukaa kimya!

Tutakapokuja kuambiwa wote kulala saa 12 jioni
Ndiyo wananchi "tutastuka" kuwa huko tuendako siko!
Itakuwa TOO LATE!
 
Huyo Theophil Makunga wakati hiyo sheria ya vyombo vya habari inapitishwa hakuwepo dodoma leo hii anaitumia kama reference.

Sijaona kosa hapo. Tunatumia katiba kama rejea wakati hatukuwepo wakati inapitishwa, vilevile vitabu shuleni na vyuoni vinatumiwa kama rejea japo viliandikwa kitambo.
 
Mpigeni ban mtoa maagizo kutoka juu sijui ndio malaika wa mipaka ya Tanzania, ila nae anawashwa washwa Sana duuh miaka 2 mwendo wa kuwasha washa siasa tu...

Na hawa TEF wameona watanzania ni vichwa vya mwendawazimu.
 
Mwanahalisi tangu liwe la kutetea ufisadi na wakoloni wa kizungu ni sawa magazeti ya udaku ya tandale kwa mtogole.
Hivyo, bora wamelifungia
 
Hili Jukwaa la Wahariri siku hizi ni kipaza sauti cha Mwenye Mkoa wake mpaka wakaisaliti Clouds!
 
Back
Top Bottom