Jukwaa la katiba live!

Jukwaa la katiba live!

Matangazo hayo kupitia decoder ya TING yanakatikakatika sana sijui ni hujuma au uzembe wa Mafundi mitambo.Ninahitaji madaraka ya Rais yapunguzwe,Muungano wa Tanzania na Zanzibar uwe wa SHIRIKISHO usiwe wa kupunguza uwezo wa Serikali ya Zanzibar,Mahakama ya Kadhi itajwe kwenye Katiba,Mafao ya Watumishi kwenye mifuko yote ya jamii ilingane ,Wakuu wa Wilaya wasiwepo,Majaji wateuliwe na Rais na WATHIBITISHWE NA BUNGE.
 
Kuna jamaa (mlemavu) kasema watu wengine wanachukulia kuwasaidia walemavu shs 50 na mia mia ndo njia yao ya kwenda mbinguni, teh teh teh ... asante jogi kwa kutuhabarisha.
 
Watu wengine bwana. Eti Profesa profesa profesa profesa profesa profesa. Mtu badala ataje jina.
 
Povu inamtoka anayejiita mwanasheria wa ccm baada ya kueleza sera zilezile za katiba iliyopo azomewa na kupigiwa makofi aache kuendelea
 
daah mwanasheria wa sisiem amekuwa nawakati mgum sana kuwasilisha aliyotumwa na mkuu wa kaya,ukweli hawajamaa hawakubaliki hadi kuzomewa.
 
mjadara nimeupenda sana yaani sema asilimia kubwa ya watanzania hawaangalii tv lakini wangeweza kuangalia ni somo tosha kabisa kwenye katiba maana wameeleza kila nyanja ya wanajamii na makundi mbalimbali
 
prof. Msumari wa mwisho kwa jeneza, ilitokea kesi ikasajiliwa znz mahakama ya rufaa, ikaletwa mahakama ya rufaa tanganyika, ikakaliwa, kwa mwendelezo wake hukumu ilikuja toka kuwa zanzibar si nchi, kwa hiyo hapawezi kutokea uhaini huko zanzibar

e bwana acha kutuzingua,huyo proff hana jina?????????????????????????????
 
Kuna jamaa (mlemavu) kasema watu wengine wanachukulia kuwasaidia walemavu shs 50 na mia mia ndo njia yao ya kwenda mbinguni, teh teh teh ... asante jogi kwa kutuhabarisha.

mkuu, nilikimbia kuendelea kutoa update, nilitafuta nafasi nami nichangie, ingawa hivyo nilikosa. Huyo mlemavu alinitia simanzi kiukweli.
 
e bwana acha kutuzingua,huyo proff hana jina?????????????????????????????

ukishikwa shikamana, sio unajilegeza kama mtarimbo uliolala doro.
 
Last edited by a moderator:
hata mimi nimeoiona hiyo...

alidhani kujisifia u-ccm ingemlipa, jasho limemtoka. Hakushangaa mwenye kitengocha propaganda (nape) hakwenda, kasakiziwa yeye!!!
 
Prof. Lengo la muungano ilikuwa ni chanzo cha kuunda umoja wa afrika,
kwa maana nchi nyingine zingejiunga baadaye, zambia ilionyesha nia lakini baada ya kuyaona masharti "ambayo ni zanzibar pekee iliyakubali" haikuwa tayari kujiunga, na haikutokea nchi nyingine ya afrika kujiunga.

Hili neno, "kuunda umoja wa Afrika" linatumika vibaya sana. Muungano wa miaka 48 wenye lengo la kuunda umoja wa Afrika haujapata wanachama wengine wa kujiunga.
Ni kwa sababu ni muungano wa kipuuzi? Kama nitaazima maneno ya Jenerali Ulimwengu au ni muungano wa hovyo?

Nini kimezuia nchi nyengine kujiunga na muungano huu. Kama Zambia ilikuwa na hamu/ kiu ya kujiunga ni nini kilirudisha nyuma Zambia kutimiza azma hiyo?
Kuna member Buchanan pia aliwahi kudokeza kuwa Comoro inataka kujiunga na Muungano wa Tanganyika na Zanzibar. Nini kilitokea pia ambacho kimefanya Comoro irudishe majeshi nyuma?

Huu muungano ni wa aina ipi? Je nia ya kuunda umoja wa Afrika bado ingalipo?

Zambia ilipewa masharti yepi? Je huyo Prof. ameyataja? Kama ndio, tuhabarishe mkuu.
 
Back
Top Bottom