Jukwaa la katiba live! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Jukwaa la katiba live!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by jogi, Sep 1, 2012.

 1. jogi

  jogi JF-Expert Member

  #1
  Sep 1, 2012
  Joined: Sep 25, 2010
  Messages: 19,335
  Likes Received: 12,799
  Trophy Points: 280
  Nipo ukumbini, sizuii yeyete anayefuatilia kupitia itv kuongeza alichoona na kusikia.
  Deus kibamba ameshafungua kongamano.
   
 2. jogi

  jogi JF-Expert Member

  #2
  Sep 1, 2012
  Joined: Sep 25, 2010
  Messages: 19,335
  Likes Received: 12,799
  Trophy Points: 280
  Prof. Haoni kama ni sawa mchakato wa kuandika katiba unvyoendeshwa kwa maana ya kuminywa haki ya ushiriki huru wa wananchi.
   
 3. jogi

  jogi JF-Expert Member

  #3
  Sep 1, 2012
  Joined: Sep 25, 2010
  Messages: 19,335
  Likes Received: 12,799
  Trophy Points: 280
  naelewa una kiu ya kuhabarishwa.
   
 4. jogi

  jogi JF-Expert Member

  #4
  Sep 1, 2012
  Joined: Sep 25, 2010
  Messages: 19,335
  Likes Received: 12,799
  Trophy Points: 280
  Prof. Anachambua tofauti ya shirikisho na muungano, anatolea mfano wa shirikisho la afrika mashariki na muungano wetu wa tanganyika na zanzibar.
   
 5. jogi

  jogi JF-Expert Member

  #5
  Sep 1, 2012
  Joined: Sep 25, 2010
  Messages: 19,335
  Likes Received: 12,799
  Trophy Points: 280
  Prof. Lengo la muungano ilikuwa ni chanzo cha kuunda umoja wa afrika,
  kwa maana nchi nyingine zingejiunga baadaye, zambia ilionyesha nia lakini baada ya kuyaona masharti "ambayo ni zanzibar pekee iliyakubali" haikuwa tayari kujiunga, na haikutokea nchi nyingine ya afrika kujiunga.
   
 6. jogi

  jogi JF-Expert Member

  #6
  Sep 1, 2012
  Joined: Sep 25, 2010
  Messages: 19,335
  Likes Received: 12,799
  Trophy Points: 280
  Prof. Mkataba wa muungano ulikuwa na makubaliano 11,
  lakini kwa sasa yameongezeka na kufikia 37.
   
 7. jogi

  jogi JF-Expert Member

  #7
  Sep 1, 2012
  Joined: Sep 25, 2010
  Messages: 19,335
  Likes Received: 12,799
  Trophy Points: 280
  nawe mbona huonyeshi kama unasoma hizi post.
   
 8. jogi

  jogi JF-Expert Member

  #8
  Sep 1, 2012
  Joined: Sep 25, 2010
  Messages: 19,335
  Likes Received: 12,799
  Trophy Points: 280
  Prof. Mabadiliko ya katiba ya zanzibar automaticaly imebadilisha hati ya muungano.
   
 9. M

  Mpambanaji K Member

  #9
  Sep 1, 2012
  Joined: Dec 29, 2008
  Messages: 84
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Prof nani huyo ?
   
 10. bibikuku

  bibikuku JF-Expert Member

  #10
  Sep 1, 2012
  Joined: Feb 16, 2011
  Messages: 828
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 35
  Prof ndio nani? Majimarefu au Mwondosya??? Andika jina kamili, mie sina TV wala radio hapa nategemea unipe kitu kamili
   
 11. jogi

  jogi JF-Expert Member

  #11
  Sep 1, 2012
  Joined: Sep 25, 2010
  Messages: 19,335
  Likes Received: 12,799
  Trophy Points: 280
  Prof. Rais wa zanzibar amekuwa mjumbe wa baraza la mawaziri, hakuwa na uchaguzi ispokuwa kukubali akiisoma picha iliyompata aboud jumbe (watu wamecheka kidogo)
   
 12. bibikuku

  bibikuku JF-Expert Member

  #12
  Sep 1, 2012
  Joined: Feb 16, 2011
  Messages: 828
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 35
  nipo sana tatizo unaniletea habari nusu nusu unataka kuniboa
   
 13. jogi

  jogi JF-Expert Member

  #13
  Sep 1, 2012
  Joined: Sep 25, 2010
  Messages: 19,335
  Likes Received: 12,799
  Trophy Points: 280
  Prof. Bunge la muungano halina mamlaka juu ya serikali ya zanziba ispokuwa yale tu kwenye mkataba.
   
 14. jogi

  jogi JF-Expert Member

  #14
  Sep 1, 2012
  Joined: Sep 25, 2010
  Messages: 19,335
  Likes Received: 12,799
  Trophy Points: 280
  Prof. Katiba ibara ya 4 inajichanganya juu ya mamlaka ya bunge kwa pande hizi mbili.
   
 15. jogi

  jogi JF-Expert Member

  #15
  Sep 1, 2012
  Joined: Sep 25, 2010
  Messages: 19,335
  Likes Received: 12,799
  Trophy Points: 280
  Prof. Ibara inatoa mamlaka kwa bunge kutunga sheria ambayo inapaswa kuelekeza kuwa hiyo sheria inapaswa kutumika zanzibar tu. Prof. Anashangaa, Kama jambo husika ni la muungano vipi sheria ielekeze jambo kipekee wakati jambo lenyewe lipo kwenye hati ya makubaliano!!!
   
 16. jogi

  jogi JF-Expert Member

  #16
  Sep 1, 2012
  Joined: Sep 25, 2010
  Messages: 19,335
  Likes Received: 12,799
  Trophy Points: 280
  Ubadilishaji ama utibitishaji wa mambo inahitaji theluthi mbili kupitisha jambo husika.
   
 17. jogi

  jogi JF-Expert Member

  #17
  Sep 1, 2012
  Joined: Sep 25, 2010
  Messages: 19,335
  Likes Received: 12,799
  Trophy Points: 280
  Prof. Mahakama kuu ya tz si mahakama ya muungano, na mahakama ya znz ni kitu tofauti kabisa. Sasa ni aje
   
 18. bibikuku

  bibikuku JF-Expert Member

  #18
  Sep 1, 2012
  Joined: Feb 16, 2011
  Messages: 828
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 35
  we bwana wewe, Prof ndio nani?????????????????
   
 19. jogi

  jogi JF-Expert Member

  #19
  Sep 1, 2012
  Joined: Sep 25, 2010
  Messages: 19,335
  Likes Received: 12,799
  Trophy Points: 280
  Prof. Msumari wa mwisho kwa jeneza, ilitokea kesi ikasajiliwa znz mahakama ya rufaa, ikaletwa mahakama ya rufaa tanganyika, ikakaliwa, kwa mwendelezo wake hukumu ilikuja toka kuwa zanzibar si nchi, kwa hiyo hapawezi kutokea uhaini huko zanzibar
   
 20. jogi

  jogi JF-Expert Member

  #20
  Sep 1, 2012
  Joined: Sep 25, 2010
  Messages: 19,335
  Likes Received: 12,799
  Trophy Points: 280
  Prof. Ali hassan Mwinyi alipata kusema bungeni kuwa tuna serikali mbili kuelekea moja.
  Anamaliza kwa kusema hakuna ugumvi kati ya wananchi wa zanzibar na tanganyika.
   
Loading...