'Juice' kwa Kiswahili inaitwaje

MAJI YA MATUNDA (tunda lililokamuliwa maji yake yanaitwa maji ya matunda)

TOGWA (Jamii ya uji unaotengenezwa kiutaalam sana. kwa kutumia mtama uliooteshwa kama wa kutengeza pombe za kienyeji kusagwa kwa kutumia mawe ya asili au kutwanga kwa kinu, pia kwa mijini wanatumia hata ugali uliobaki kutengeza hiyo togwa ila ni kwa utaalam sana, togwa za mjini sio za kuziparamia jamani unaweza kunyweshwa kiporo cha ugali)
 
"Utupa" ni aina ya sumu. Tujihadhari - "Maji ya matunda" si sumu. Hata "utomvu" haifai kutumika kwenye muktadha ya maji ya matunda.
 
kila lugha inatabia ya kukopa maneno ili kukuza msamiati wake neno juisi limekopwa kutoka katika kiingereza neno juice
 
Kiswahili bado ni lugha masikini sana wa msamiati. Ukweli ni kwamba mpaka sasa neno 'juice' halina mwenza wake wa Kiingereza. Kwa hiyo waliosema 'maji ya matunda' wako sahihi, lakini 'juisi' pia ni sahihi kwa kuwa ni moja tu ya maneno lukuki ya Kiswahili yaliyoazimwa kutoka Kiingereza. Mengine ni kama peni, penseli, shati, sketi, basi, rula, feni, mota, spika, redio, bucha, nk.
 
Mmenikumbusha TOGWA lililokuwa linauzwa hapo Fire brigade Dar (faya), enzi hizo paliitwa "mwembe togwa".

Bora hiyo "juice" ingeitwa togwa... Badala ya kutohoa na kuitwa juisi.

Duh, unapajua Mwembetogwa?

We unaijua Dar.

Nyerere safari moja alienda Sweden, akaambiwa tuna wakimbizi wa kisiasa kutoka Tanzania. Akasema nataka kuwaona. Akapelekwa sehemu akakutana nao. Kakutana na vijana wamejilipua CUF. Akamuuliza mmoja, wewe mkimbizi? Unatoka wapi? Akasema Dar. Nyerere akamuuliza, Dar sehemu gani? Akajibu Faya. Nyerere akamwambia Faya hii hapa Mwembetogwa? Hakuna mkimbizi wa kutoka pale tangu panaitwa Mwembetogwa.

Akawaambia wa Swede hawa jamaa ni wakimbizi wa kiuchumi tu, hakuna mkimbizi wa siasa hapa.

Waswede wakafanya uchunguzi, wakajiridhisha, Jamaa wakapigwa palanja. Wakarudi Dar.

Ulivyotaja Mwembetogwa umenikumbusha hiyo story ya Nyerere alivyowazibia maisha wakimbizi feki kutoka "Mwembetogwa".
 
Kiswahili bado ni lugha masikini sana wa msamiati. Ukweli ni kwamba mpaka sasa neno 'juice' halina mwenza wake wa Kiingereza. Kwa hiyo waliosema 'maji ya matunda' wako sahihi, lakini 'juisi' pia ni sahihi kwa kuwa ni moja tu ya maneno lukuki ya Kiswahili yaliyoazimwa kutoka Kiingereza. Mengine ni kama peni, penseli, shati, sketi, basi, rula, feni, mota, spika, redio, bucha, nk.

aaah mkubwaaa! kiswa ni Tajir wa msamiat bhaana!, kukopa co kipmo cha kupma uteshelez wa lg. kwani lg. yyt ina sifa ya kukopa au kuathir lg. nyngn Xo maneno meng yaliokopwa ktk lg nyngn yapo il kukidh mahtaj ya wanajamii lg. hzo znakdh haja za ma2miz kwa wanajamii wk! #KiSw AhILI Sio Maskin Wa Msamiat Bali Watumiaj Wa Kisw. ndio Maskin Wa Msamiat"
 
bado nasuburi jibu halisi kwa mwana lugha atakaye toa neno sahihi la JUICE kwa kiswahili,nimepata maneno kadhaa kama togwa lakini hii ni kilugha(kihehe ni pombe ya kusindikwa) shurubat ni kiarabu maana ya maji ya matunda oman wanatumia sana neno hili kwa juice kama kiswahili hatuna neno lake niambiwe ili niendeleee kuwa mtohoahaji pia
 
Back
Top Bottom