Juhudi za Gwajima katika siasa, kipi anatafuta?

Robethn

JF-Expert Member
Aug 18, 2015
2,103
352
Mchungaji Gwajima wa kanisa la Ufufuo anaonekana kuwa na juhudi kubwa za kisiasa ktk kipindi hichi kiasi cha kuachana na shughuli za mafundisho ya Mungu. Hayo ameyathibisha wakati akiongea na waandishi wa habari.

Katika maelezo yake amesema ni muda mrefu sana amekuwa akijihusisha na shughuli hizo za siasa kwa siri pasipo waumini wake kutambua, amekuwa akihudhuria ktka vikao mbalimbali vya maamuzi vya CHADEMA kwa siri kubwa. Amenukuliwa leo akisema;

"Usiku ule mheshimiwa Lowassa, sasa akaingia kwenye kamati kuu na mimi nilikuwemo ndani ya kamati kuu kuhakikisha amefika salama na alipokelewa pale nje na Dr Slaa na Prof Baregu na mwenyekiti wa chama chetu na watu wengine. Mzee Lowassa akaongea, wote tukasimama kwa pamoja na kapiga makofi, tulimkubali na tukampokea".

Kitendo hicho kinatia shaka juu ya huo wema wake kwa Lowassa kiasi cha kumfanya kuacha shughuli za kufundisha na kuabudu badala yake kujikita kukesha kwenye vikao vya kisiasa kwa siri.

Aidha amejitapa na kudai kuwa alifanya ushawishi kwa Josephine na maaskofu wengine kumuunga mkono mzee Lowassa!

WATANZANIA TUJIULIZE, NI KIPI KILICHOPO NYUMA YA PAZIA KATI YAO?
 
wewe ulifurai slaa alivyomlipua naomba utuliee maumivu yakuingia gwajima ametumia njia ile ile aliyotumia slaa kujibu mashambulizi
 
Acha afanye siasa watakimbia nchi wenyewe kuanzia mwezi october
 
Gwajima mbona kaeleweka wenye akili tumemuelewa..nani alikuambia kuwa ukiwa kiongozi wa kiroho ufai kuwa mwanasiasa..mchungaji kiongozi mama lwakatare.ni mbunge viti maalum ccm...unamshangaa ngwajima mshangae jk aliemteua uyu mama kuwa mbunge wake...Dr.Slaaa anamizigo kapewa na ccm na gwajima anaijua iliko na waliompatia pia.mkibisa mwambieni dr.mihogo akatae adharani kama amjaaumbuka...Tunamchagua Lowasa cc watz tumekwishaamua...
 
Dr Magufuli atashughulika na watu wa namna hii waongo na wachochezi
 
makitoro

Nimemsikiliza Gwajima.
Inabidi nimpe pole Silaa na heko Gwajima. Gwajima ni master.

1. Gwajima ni rafiki mpambe mkubwa Lowassa katika safari ya Matumaini.

2. Gwajima ndo alikuwa mshenga wa kumpeleka Lowassa Chadema. Na kahakikisha kamfikisha.

3. Haihitaji kufikiri sana kuwa kikwazo kikubwa cha Lowassa kuingia Chadema ilikuwa ni Dr. Silaa juu ya tofauti za kiitikadi na vita ya Silaa dhidi ya Lowassa na Ufisadi.

4. Je nani aliyepewa kumshughulikia Silaa? ....

5. Gwajima akiwa mshenga alijua kuwa ujio wa Lowassa Chadema ni wa kuendeleza Safari ya Matumaini hivyo lazima Silaa apigwe chini ama sivyo hakuna cha safari wala nini.

6. Gwajima alijikita pote pote. Walinzi wake, na watiifu kwake ndio waliokuwa wakimlinda Dr. Silaa. Hawa sio walinzi wa Chadema wala watiifu kwa Chadema. Mlinzi kila akiona nyendo anaripoti kwa Gwajima. Mlinzi aliyekuwepo Landmark karipoti vizuri sana.

7. Gwajima alijua kila linalotokea kwa Silaa na alimdhibiti. Hata msg iliyodhaniwa imeandikwa na Silaa.. ilikuwa imetoka kwa Mlinzi wa Gwajima anayemlinda Silaa.

8. Hii habari ya kufungiwa ndani, kudhibitiwa na Josephine..kutupiwa mizigo ni story inayoelezwa na Gwajima, walinzi wake na viongozi wa Chadema (walioambiwa na Gwajima na watu wake).
Gwajima ambaye ni mpambe mkuu wa safari ya matumaini (tangu alivyogawa malimao pale Arusha) na alivyokuja kufanya ushenga kumleta Chadema.

9. Unganisha dots mwenyewe...ukishindwa usilie nye nye nyenye nyenye..sijui utakua umekula maharage ya wapi wewe.

Ha ha ha ha.
 
Last edited by a moderator:
.....Rais Kikwete ni mpole sana yaani mtu mdogo kama Gwajima anafanya 'battle' na vyombo vya Dola kabisa.Huyu mtu anapaswa kuoneshwa kuwa serikali ipo,ina meno na inauma....
 
Kwaiyo tatizo nn,,, sio vbaya kwa kiongoz wa din kushughulikia siasa,,kwan huyo slaa sio kiongoz wa din?
 
.....Rais Kikwete ni mpole sana yaani mtu mdogo kama Gwajima anafanya 'battle' na vyombo vya Dola kabisa.Huyu mtu anapaswa kuoneshwa kuwa serikali ipo,ina meno na inauma....
Kama umemsikiliza na ukaelewa gwajima ka rifaa gazeti la mtanzania...mengine siri yake
 
Kwajima anataka raisi ajaye ampe viwanja tanganyika Packers vya kawe bure ili kanisa lake sihamishwe pale kawe Gwajima ni mfa maji anatapatapa tu.
 
Back
Top Bottom