Jua limezama

Rungu

JF-Expert Member
Feb 23, 2007
3,932
1,726
Hivi ni sawa kusema jua limezama? Kama linazama huwa linazama wapi, manaake ukweli ni kwamba dunia ndio inayozunguka. Jua liko pale pale. Mbaya zaidi wabongo tunatabia ya kuita Ulaya eti ni majuu, kama vile sisi tupo sehemu flani iliyoko chini. Kijeografia hii si kweli. Hakuna nji iliyeko juu bana. Huko juu kuna mawingu n.k!

Tafadhali changia tueleweshane.
 
Hii ni lugha tu. Na katika lugha zote kunakuwepo na misemo au phrases ambazo scientifically hazileti maana. Hebu fikiria hii kitu "She broke my heart" unafikiri kweli Moyo umevunjwa?
Au angalia hii, "nimezama kwenye dimbwi la mapenzi" dimbwi lenyewe halionekani kwa macho.
Na kuhusu neno MAJUU, ilianzia kwa kufikiria kuwa mtu anakatiza mawingu yaliko juu, kama njia ya kwenda huko ulaya, na kwingineko.
 
Nimekusoma! Lakini:
Na kuhusu neno MAJUU, ilianzia kwa kufikiria kuwa mtu anakatiza mawingu yaliko juu, kama njia ya kwenda huko ulaya, na kwingineko.
naona sio sahihi kwa sababu Afrika ya kusini tunakuita bondeni ingawa nako tunakatiza mawingu kufika. Nadhani hii ya majuu inatokana na ramani ya ulimwengu ilivyowekwa na kuonekana kama vile bara la Ulaya liko juu na bara la Afrika liko chini kwa hiyo kututia imani kwamba tuko chini ya Ulaya.
 
Nimekusoma! Lakini: naona sio sahihi kwa sababu Afrika ya kusini tunakuita bondeni ingawa nako tunakatiza mawingu kufika. Nadhani hii ya majuu inatokana na ramani ya ulimwengu ilivyowekwa na kuonekana kama vile bara la Ulaya liko juu na bara la Afrika liko chini kwa hiyo kututia imani kwamba tuko chini ya Ulaya.

Neno majuu lilianza kutumika muda mrefu sana, kwa maana niliyoeleza hapo juu, hata ilikuwa ukienda Argentina au Australia, ilikuwa na majuu tu. La bondeni lilianza kupata umaarufu miaka ya 90 vijana wallipoanza kuzamia kwenda kule baada ya apartheid regime kuondoka madarakani na kuwaachia akina Nelson. Ni maneno tu mtaani ambayo watu hujianzishia, halafu yanaendelea kutumika hata kama si sahihi. Nafikiri, pia utakuwa ume-note sasa hivi kuwa watu wanatumia neno kuchakachua kumaanisha tendo la ngono, maana hii inaweza ikadumu muda mrefu, lakini actually, si maana yake halisi.
 
Pia usisahau nafasi ya pande za dunia (Kask. Kus. Mash. na Magh.)

Ni mara nyingi watu kutumia CHINI kumaanisha 'Kusini' na JUU kumaanisha 'Kaskazini'. Kama tunakubaliana hapa then Ulaya ni majuu kwa kuwa ipo Kaskazini (Juu) ya Afrika na Afrika Kusini ni bondeni sababu ipo Kusini (Chini).
 
Haya Nanren nimekupatapata. Nakumbuka neno chakachua lilikua ni mtindo wa dansi wa bendi ya Urafiki Jazz ya Friendship Textile Mills (Ubungo) wakati wa 70's. Naona limeibuliwa tena na hawa hawa wanasiasa wa sasa ambao wakati ule ndio walikuwa mayanki waliokuwa wanavaa raizoni!
 
Hivi ni sawa kusema jua limezama? Kama linazama huwa linazama wapi, manaake ukweli ni kwamba dunia ndio inayozunguka. Jua liko pale pale.
Ukitaka kutumia kiswahili fasaha, kuzama kwa jua ni Machweo na kinyume chake ni Mawio...! Hali hii ni muonekano wa chini ya upeo wa macho kama matokeo ya mzunguko wa dunia.

Mbaya zaidi wabongo tunatabia ya kuita Ulaya eti ni majuu, kama vile sisi tupo sehemu flani iliyoko chini. Kijeografia hii si kweli. Hakuna nji iliyeko juu bana. Huko juu kuna mawingu n.k!

Tafadhali changia tueleweshane.
Unalo lizungumza ni sahihi, lakini kwa mtazamo wa kijiografia na haswa ukitazama ramani ya dunia, utaona kuwa nchi nyingi za ulaya zipo Kaskazini ya Afrika, hii ndio imepelekea kwa nchi za Ulaya tuzione kama zipo juu ya bara la Afrika (Kiramani).

Na kuhusu juu kuna mawingi, pia hii ina mushkeri, kwa sababu dunia yetu ina umbo kama la yai (Tufe), kwa kiswahili rahisi umbo la dunia ni Duara...! Sasa unaposema juu, unamaanisha wapi... Labda muelekeo wa juu ya kichwa... Lakini hapo hapo mtu wa upande wa pili dunia juu yake ni miguuni kwako...! Kwa sababu anapoonyesha muelekeo wa juu, ni upande tofauti ambao wewe wa upande wa pili utaonyesha.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom