Nakumbuka wakati niko darasa la sita nikiwa nimekaa sebuleni natizama tamthilia baba akaja akasema, " unajifunza nini hapo? weka TVT" basi nikaweka.
Kulikuwa kipindi kimoja wanajadili watu fulani wengi walikuwa wazee mmoja akasema " unavyomwona rais wa nchi alivyo. Basi ujue yeye ni wastani wa wananchi wa kawaida katika ufikiri hata pia utekelezaji."
Sasa najiandaa kulala hapa nikakumbuka hii siku ghafla na haya maneno yanajirudia akilini sijui alimaanisha nini yule mzee.