JPM punguza mihemko baba, ccm itakudodea

JPM punguza mihemko baba, ccm itakudodea

Ccm wameacha misingi iliyowekwa zamani huwezi kuwa kiongozi kama ujapitia vyuo vya chama pale unafundwa tazama viongozi waliopita,uongozi ni jambo linalogusa maisha ya watu,sasa kama MTU kasukumiziwa tu ili kuukabili upepo inakuwa ni hatari kwa ustawi wa chama.
 
Napata wasiwasi na mwenendo wa chama cha mapinduzi ktk awamu hii ya tano. Hali ndani ya chama hiki bila shakai ni tete sana.

Katibu mkuu wa chama hiki kongwe amejitenga nacho na sasa yupo kimya.
Aliyekuwa katibu wa itikadi na uenezi, ambaye sote tunajua alikitoa chama hicho shimoni hana raha tena ndani ya chama hicho.

Wanachama wengi wakubwa kwenye ushawishi mkubwa mfano, Mwandoaya, Membe, Mkapa, n.k sasa wamekitelekeza kabisa chama.

Kweli Mwinyi, Warioba, Butiku, Kinana, Makinda na Kikwete. Badala ya kuwasikiliza na kufanyia kazi waliyoyasema ni wa kutupiwa kijembe kwamba eti wanawashwa washwa!?

Kitendo cha Lazaro Nyalandu kujiondoa ccm leo na sababu alizozitoa ni mwanzo tu wa wengi waliokichoka chama na kuchoshwa na mwenendo mbaya wa serikali ya awamu ya tano.

Kuna kila sababu kwa mwenyekiti wa chama hiki ngazi ya kitaifa kukaa chini na wanaccm wenzake ili kutathimini ni wapi wameteleza.
Mafisadi lazima yajikaange kwa mafuta yao, yanajitoa chamani yenyewe, joto ni kubwa!!
 
Ivi unaota au uko macho? Kweli kuondoka kwa Nyarandu CCM inakwenda kufa? Napata shaka kama kweli Jamiiforum ina tofauti na Facebook.
Acha kuifananisha jf na vitu vyaajabu mkuu.
 
Mkuu unataka kunambia unajaribu kumshuri mkulu.!!

My friend acha tu yule sizonje hashauriki kabisa.
 
Ivi unaota au uko macho? Kweli kuondoka kwa Nyarandu CCM inakwenda kufa? Napata shaka kama kweli Jamiiforum ina tofauti na Facebook.
Acha ukilaza na elewa kilichoandikwa... wapi kasema kuondoka kwa Nyarandu CCM inakufa?
Tulia soma mambo uelewe kwa ujumla wake sio vipande vipande.
 
Aliondoka mwenye kadi namba mbili na hadi leo hii CCM ipo juu.

Aende zake.
Si idadi ya wanao ondoka wala kisalia ,ni pale itakapo ccm itapo anza kuondoka mioyoni mwa wananch jata bila kuhama chama wala kubadilisha jezi
Hio ndo itakua hatari
So usiangalie nani amehama angalia sababu alizotoa kama hazina msingi then its ok chama kiko imara kabisa hakima kasoro hata moja tena mwenyekiti wake anaruhusu demokrasia ya mitandao kuliko kipindi chochote na yyee anafuatilia na kukoment so ni uroho wake wa madaraka ndo umemkimbiza walà kwenda pipoz
 
Najiuliza tu hivi ile kauli ya "....wanataka kuja CCM na wanaotaka kujiunga na chama kingine waje hapa.... " ndio angetumia nafasi hiyo katika Jukwaa la JPM, Mh. Nyalandu kuhama ingekuwaje?
 
Imemdodee mara ngapi? Si unaona mashambulizi kutoka kwa Mwinyi, Warioba, Butiku, Kinana, Makinda na Kikwete. Badala ya kuwasikiliza na kufanyia kazi waliyoyasema yeye akaamua kuwatusi eti wanawashwa washwa!
Hivi hawa nao wakitangaza kusema wanahamia upinzani nao wataanza kuchafuliwa kama huyu waziri wa zamani au?
 
Ivi unaota au uko macho? Kweli kuondoka kwa Nyarandu CCM inakwenda kufa? Napata shaka kama kweli Jamiiforum ina tofauti na Facebook.
...JF haina tofauti na Facebook but yet umekomaa humu humu si uhamie badoo?
 
Imdodee mara ngapi? Si unaona mashambulizi kutoka kwa Mwinyi, Warioba, Butiku, Kinana, Makinda na Kikwete. Badala ya kuwasikiliza na kufanyia kazi waliyoyasema yeye akaamua kuwatusi eti wanawashwa washwa!
Mzee mwinyi usimtaje
 
Kiukweli kuanzia mashimani kuna viongozi wapya wengi wasiokuwa na uzoefu wa siasa
 
Kwani lile bango lenu lililokuwa hapa Jf" Ccm kumfia Kikwete" liko wapi? Mambo iko poa tu
 
Binafsi sioni faida ya maghufuli zaidi ya kutuletea taharuki inchini. Kama ni miundo mbinu kikwete alijenga zaidi pamoja na kuto kusanya kodi
 
Back
Top Bottom