majebsmafuru
JF-Expert Member
- May 1, 2017
- 453
- 635
Wanabodi, karibuni jukwaani, JPM na Waziri Mkuu Majaliwa wanataka kutueleza nini kuhusu kufuata sheria bila shuruti? Tumeshuhudia yule mke wa Mh. aliyembabaisha trafiki? JPM akampandisha cheo. Hii ya Mh. A Malima? Kamanda Sirro akawa bega kwa bega na askari Abdul. Madawa ya Kulevya? JPM katoa support ya kila aina, sukari? Kulipa kodi? Madini? Mimba utotoni na shuleni? Manji? Vyeti feki. Mishahara/Posho lumbesa serikalini? Kurudisha hela BOT? Watu kuheshimu kazi, tena nasikia na nimeona saa moja asubuhi wako ofisi?! Hii haijawahi tokea kabisa, na kuondoka wanaondoka muda sahihi, hakuna cha kwenda kunywa kifungua kunywa masaa au lunch masaa (kumbukeni wengine walikuwa hawarudi wakienda lunch). Ukijenga mabondeni yala kwako, ukijenga bila kibali wala nawe, ukipata tenda serikalini fanya ama sivyo wanakufilisi, ukichukuwa mikopo ya benki zao issue kama hulipi, usipolipa umeme issue wako nawe, barabarani ndio usiseme, ukitanuwa issue, uki over speed unayo ticket, gari haina road licence ibaki home, ila utailipia tu au utoe taarifa imekufa, ukila hela za umma wako nawe. Nakadhalika nakadhalika.
Yote haya JPM na Waziri Mkuu Majaliwa wameonesha kuyakubali yanavyoshughulikiwa na walio chini yao, sasa sisi raia labda tukune vichwa na kusema, utawala huu LABDA uko tofauti kabisa na tawala zilizopita. TUANZE KUFUATA SHERIA BILA SHURUTI. Ukiona waonewa mahakama zipo, kafunguwe kesi, ila sheria, taratibu na ilani za serikali imefika muda ziheshimiwe bila kujali wewe maskini, tajiri, mheshimiwa, wa kawaida nakadhalika.
KARIBUNI..