Jeshi la polisi na Propaganda za "kutii sheria bila shuruti" maudhui ya kitabu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Jeshi la polisi na Propaganda za "kutii sheria bila shuruti" maudhui ya kitabu

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Kiranja, Aug 15, 2011.

 1. K

  Kiranja JF-Expert Member

  #1
  Aug 15, 2011
  Joined: May 19, 2007
  Messages: 754
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Jeshi la polisi Tanzania wamechapisha kijitabu walichokiita "UZALENDO"Haki na Utii bila Shuruti.............

  kitabu hiki kimekuwa kikisambazwa nchi nzima na jeshi la polisi tangu CHADEMA walipoanzisha maandamano ya kuzunguka nchi nzima kuhamasisha wananchi juu ya haki zao na wajibu wao pamoja na haki ambazo wanapaswa kupewa kutoka serikalini .

  kwa kifupi maudhui ya kitabu hiki ukurasa kwa ukurasa ili muweze kujua kwanini kichwa changu cha habari nimeandika ni propaganda za jeshi la polisi Tanzania.

  utangulizi
  .

  Kijitabu hiki kimeandikwa na mtu anayeitwa Justine Bufure na kimechapishwa na Toto's Group .

  Dibaji ya kitabu hiki imeandikwa na IGP Said Mwema na kwenye dibaji kaandika yafuatayo; "kitabu hiki kimebeba ujumbe mzito unaolenga kutuamsha,kutufikirisha na kutupa hamasa ,ili turejee misingi ya uwajibikaji katika harakati za kujiletea maendeleo yanayozingatia wajibu wa kudumisha amani,usalama,na utulivu kama mtaji namba moja wa ustawi wa jamii"...........kila raia mwema ana wajibu wa kutambua na kuepuka viashiria vya vurugu na uvunjaji wa amani na kuhakikisha anatii sheria bila kungoja kushurutishwa .Kwa sababu ushurutishaji unaweza kusababisha madhara,lakini pia ni hatua yenye gharama kubwa". Ni matuamaini yangu kwamba ,kitabu hiki kitatuandaa kutumia haki na uhuru wetu tukizingatia wajibu wa kutii bila shuruti"

  utangulizi huu ukiona ni kama vile IGP analiandaa taifa kuingia kwenye matumizi ya nguvu ambayo yatafanywa soon na vyombo vya dola na haswa polisi ndio maana anatoa vitisho kuwa wasisubiri shuruti... nitaeleza kwanini hapo baadae kwenye uchambuzi wangu.

  ukurasa wa pili na tatu umeonyesha kuwa ni mamlaka ya kuongoza dola.

  Kwenye eneo hilo wameweka picha ya wananchi wakiwa wanapiga kura kwenye vituo na ukitazama picha hiyo inaonyesha wananchi wakiwa na huzuni kubwa na hii ni ishara kuwa wanaenda kupiga kura lakini hawana imani na kura wanazopiga.......... hii ni picha ambayo haikupaswa kuwekwa kwani inaonyesha jinsi ambavyo wananchi hawana imani na kura zaoa na wamekaa kwa huzuni kubwa na hawajui kama wao ndio wanapaswa kutoa ridhaa ya kuongoza ama ni wakina nani.

  ukurasa wa nne na tano ....umeandikwa usimamiaji wa utii wa sheria za nchi.

  katika eneo hilo wameweka picha ya rais Kikwete akiwa anakagua kikosi cha polisi wa FFU na picha hiyo inaonyesha akiwa na uso wenye kufura na sio tabasamu kama ambavyo amezoeleka . Kuna maandishi kuwa mamlaka ya rais ni kuhakikisha kuwa kila mmoja anatii mamlaka na yeyote ambaye hatatii basi lazima atashurutishwa na hakuna neno kuwa vyombo vya sheria vitachukua mkondo wake ila ni kushurutisha ... hapo inaonyesha jinsi ambavyo polisi hawapo tayari tena kufuata sheria bali ni kushurutisha wananchi bila kujali sheria nyingine.

  ukurasa wa sita na saba ... wajibu wa vyama na watu walioshindwa ..

  hapa hakuna picha yoyote ila ni kurasa pekee ambayo hakuna picha kati ya kurasa zote 29 za kitabu hiki. na wameandika maandishi makubwa kwa rangi nyekundu na pia ndio ukurasa pekee uliowekwa rangi nyekundu maandishi yanasema ifuatavyo naomba kunukuu "wajibu wa vyama vya siasa na watu walioshindwa kupitia sanduku la kura ,ni kuyakubali matokeo au kuyapinga matokeo kwa mujibu wa sheria za nchi" ......"utaratibu wa kuwashawishi wananchi au kuwachochea wafuasi kufanya fujo au kufanya harakati za kuhamasisha umma kuigomea mamlaka halali ni kosa,lakini pia ni ukiukwaji wa misingi ya ukuaji na ustawi wa demokrasia . Harakati za vyama vya siasa na wanasiasa baada ya uchaguzi ,unapaswa kuzingatia ukweli kwamba mchakato wa uchaguzi tayari umekemilika.Tabia ya kutumia shida au kero za jamii kuchochea hasira ,munkari na jazba dhidi ya viongozi halali ni kosa na ni matendo hatari kwa ustawi na usalama wa jamii"

  kurasa hizo mbili ndio zimeishia hapo, hii ukisoma kwa makini utaona kuwa ni kutaka kufanya propaganda kwa wananchi kuwa vyama vikishindwa chaguzi basi vinapaswa kukaa kimya mpaka uchaguzi mwingine na hivyo havipaswi kuendesha harakati za aina yeyote mpaka wakati wa kampeni .

  Pili, hakuna mahali ambapo kitabu hiki kimeonyesha wajibu wa vyama na watu walioshinda sasa hii inaonyesha dhahiri kuwa lengo sio kwa ajili ya elimu bali ni kufanya propaganda kwa sababu ambazo wanazijua wao wenyewe polisi na ndio maana hawataki kusema kjuwa ni wajibu wa walioshinda kuhakikisha kuwa shida za wananchi zinamalizika na hivyo paiwepo na mtu wa kuchochea kama walivyosema kwa vyama vilivyoshindwa .

  tatu, jeshi la polisi linataka kuaminisha wananchi kuwa mgombea urais akishindwa kimazinngira basi anawezaq kwenda kupinga matokeo mahakamani , kitu ambacho sio kweli kwani sheria zetu zimetukataza na katiba haitoi fuirsa hiyo mahakama pekee kwa wagombea urais ni wananchi ndiko ambako anaweza kwenda kuwaeleza .

  ukurasa wa 8 na 9....hakuna uhuru usiokuwa na mipaka.

  hapa wameweka picha ya mizani ya mahakama inayomaanisha haki ila wameandika maneno yafuatayo nanukuu "kuipenda nchi si kigezo cha kufanya harakati ambazo jamii ya waliostaarabika huziita za kihuni ,kwa kudai haki bila kuzingatia wajibu wa kisheria katika kudai haki.........ni wajibu wa wananchi kuepuka kushiriki katika mikutano ,maandamano au harakati za kuichokoza mamlaka ya dola ,kwa uwasilishaji wa malalamiko au kero kwa njia ambazo zinasababisha bughudha au karaha kwa wengine".........

  hapa utaona tena kuwa lengo nio kuwatisha wananchi wasiende kwenye mikutano na hata kushiriki maandamano kwa kisingizio kuwa ni kuchokoza mamlaka za dola na hivyo ni kuvunja sheria za nchi.

  Hapa utawaona polisi wakiozungumzia jamii za watyu waliostaarabika na kuhusisha na uhuni kuwa maandamano na mikutano ni mambo ya kihuni , hii ni kusema kuwa polisi wanataka kupoka haki za kikatiba ambazo wananchi wanazo kwa kisingizio kuwa ni uhuni eti kuandamana na kudai haki .... hao waliostaarabaika kwa wizi wa pesa za umma anataka wasiulizwe wala kuhojiwa .................

  ukurasa wa 10 na 11 ....uwajibikaji katika kuwasilisha mawazo mbadala.

  hapa wameweka picha ya watu ambao wanaonyesha kutoridhishwa na jambo fulani na mmoja mwenye koti jeusi kakunja ngumi ya mkono wa kushoto na watu wamesimama kama kuna taharuki fulani. wameandika ifuatavyo "Ni imani potofu kuamini kwamba tabia mithili ya wehu,ugagwe na ubedui inawezesha kuaminiwa na kukubalika katika jamii .Ni vema kufahamu kwamba uwasilishaji wa hoja kwa njia ya hekima na busara ,husababisha upatikanaji wa ufumbuzi wa kero au tatizo bila kuathiri misingi ya ustawi wa jamii"

  Hapa utaona kuwa polisi wanataka kusema kuwa watu ambao wamekuwa wakionyesha kutokuridhishwa na mwenendop wa serikali ni wehu, mabedui na magangwe..... sasa hapa unajiuliza busara ya polisi iko wapi wanataka kuwatukana hata wazee wetu ambao wamekuwa mstari wa mbele kusema kuwa viongozi wamekiuka misingi ya uongozi bora iliyowekwa na hayati baba wa Taifa. sasa hapa busara na hekima ambayo wanataka watu wengine wawe nayo iko wapi kwa upande wao waandishi wa kitabu hiki?

  Polisi wanafanya propaganda na wana jaziba hata wakati wanaandika kitabu chao sasa wanataka mabedui na wehu wawatiii? kama kila asiyeridhishwa na utendaji wa serikali wamempa jina hilo?

  ukurasa wa 12 na 13 .wajibu wa viongozi wa kisiasa.
  wameandika ,nanukuu "viongozi wa kisiasa wenye dhamira njema na watu ,hawapendi kupanda mbegu ya chuki, ubaguzi au vurugu miongoni mwa jamii.Bali watajenga na kusimamia hoja wakiipa nafasi jamii kupima ,kuchanganua na kujenga msimamo"

  hapa utaona kuwa polisi wanawataka viongozi wa kisiasa wasitoe suluhisho kuhusiana na matatizo mbalimbali bali wawaache wananchi sasa hapo jukumu la kuongoza linafanywa na viongozi waliopewa dhamana au wananchi .Ni kwanini wasiseme wazi kuwa hakuna haja ya kuwa na Bunge kwani wabunge mara zote wamekuwa wakisema na kuelekeza ili wananchi wachukue wajibu wao wa kupima na kujenga msimamo? Polisi hapa wanajua maana ya viongozi wa kisiasa ? au wanafikiri ni vyama vya upinzani? Nawaona polisi kama wasiojua sheria na IGP ameamua kuwanyanganya viongozi wote wa kisiasa akiwemo rais,mawaziri,wabunge,madiwani ,wenyeviti wa mitaa, vijiji na vitongoji kuongoza na badala yake anawataka waseme halafu waishie hapo na wananchi ndio waamue nini cha kufanya.

  uk.14 na 15 uhuru wa kuabudu na wajibu wa viongozi wa dini ...

  hapa kuna picha ya waumini wa kiislamu wakiabudu na wakristo pia wananabudu.......mimi sio mjuvi wa eneo hili hivyo sina comment kwa sasa.

  ila polisi wanasema kuwa nanukuu "kwa mujibu wa sheria ,madhehebu yote yana wajibu ufuatao kwa masilahi ya jamii:
  • dini zipo kwa ajili ya usalama wa jamii
  • dini zipo kwa ajili ya amani katika jamii
  • dini zipo kwa ajili ya kulinda maadili ya jamii
  • dini zipo kwa ajili ya kujenga umoja na ustawi wa taifa
  wameenda mbali zaidi na kuandika "kwa lugha nyingine ,viongozi wa dini ni askari wanaofanya doria za roho.Ili kupima kufanikiwa au kushindwa kwa asikari wa doria ya roho,ni kuongezeka au kupungua kwa waumini wanaotenda uhalifu"

  Kama nilivyosema awali hapa sina comment ila najua wapo wajuvi watachambua.

  ukur.wa 16 na 17 migogoro ya kijamii na utatuzi .

  hapa wameweka picha ya wananchi waliovalia mavazi maarufu ambayo huvaliwa na wamasai wameandika mstari wa kwanza ifuatavyo, nanukuu "Jamii ya watu si kama maji yaliyotulia katika mtungi .Harakati za maendeleo ya kijamii,kiuchumi na kiutamaduni huchochea uwezekano wa kutokea mifarakano.Je,jamii na viongozi wa jamii wamewezeshwa kutambua mifumo ya kuzuia na kutatua migogoro?"

  Hapa utawashangaa polisi hao hao waliosema kuwa kwenye uk.10&11 kuwa kama kutatokea watu wanaonyesha kudai haki kwa nguvu ni mabedui na matusi kibao sasa wanataka kusema nini hapa? Naona wanajichanganya kwani lengo halikuwa ni kuelimisha bali ni kufanya propaganda ........

  uk.18 na 19 ...madhara ya kujichukulia sheria mikononi.

  Hapa wameweka picha ya wanachi wa Kenya mara baada ya uchaguzi mkuu wao ulioleta vurugu na kama mnakumbuka ile picha maarufu ya vijana waliokuwa wamebeba mapanga,marungu ,sime na rungu waliokuwa kwenye lile eneo maarufu la Nairobi Kibera . sasa sijui mantiki ya kuweka picha hiyo kwenye eneo la kujichukulia sheria mikononi ilikuwa nini , hivi walikuwa wanajichukulia sheria mikononi ama uchaguzi ulivurugwa?

  wameandika nanukuu "uchochezi wa tabia ya hasira kali katika siku za karibuni ,unaonekana kushabikiwa na kutiwa chumvi na wanasiasa ,je?,wanaitakia mema jamii yetu?katika hali kama hiyo hakuna aliye salama mbele ya watu wenye hasira kali na unaweza kujikuta mbele ya watu hao wakati wowote. Tafakari ,watu wenye hasira kali wanaweza kutumia muda gani kugeuza hali na mwenekano wako?......"

  hapa naona ni propaganda zile zile kwani wananchi wanaonekana sasa wanaweza kuyavamia mafisadi na kuchukua hatua sasa polisi wanajaribu kuwatishwa wananchi kuwa kufanya hivyo kunachochewa na wanasiasa . Kma wananchi wanajichukulia sheria mkononi basi polisi wajue kuwa wameshindwa kuchukua hatua na ndio maana wananchi hawana imani nao tena kutokana na w2ao kutokutenda haki pindi wanapofikishiwa malalamiko na wananchi .

  Hapa polisi wasitafute mchawi kwani mchawi ni wao wenyewe , kwani mara zote wananchi wamekuwa wakijichukulia maamuzi kutokana na vyombo vya dola kutokutenda hjaki kutokana na rushwa na ufisadi uliomo miongoni mwa vyombo hivyo .

  uk 20. Ulinzi wa makundi maalum.

  hapa wameweka picha ya binti mmoja mwenye ulemavu wa ngozi akiwa amebeba mtoto .

  Hapa wanaihamasisha jamii kulinda jamii hiyo na sioni tatizo ila tuu , wanaokamatwa na polisi huwa wanafikishwa mahakamani? au kw2a kuwa wanaoshiriki ni wakubwa kama BBC ilivyowahi kutoa taarifa yake iliyopelekea Vicky Ntetema kuondoka kabisa nchini kuitokana na kutoa ripoti maalum kuwa wapo vigogho wa polisi ambao wanahusika na biashara haramu ya viungo vya binadamu pamoja na viongozi walioko serikalini.

  uk.21 Mikusanyiko na Maandamano.

  kwenye ukurasa huu kuna kivuli cha picha za wananchi wakiwa wananyoosha mikono juu .
  hapa wanaandika nanukuu "sheria inampa mamlaka Ofisa wa Polisi wa himaya inayohusika kusitisha maandamano ,mkutano au mkusanyiko wakati wowote endapo atabaini kwamba kuna habari au taarifa kwamba kufanyika au kuendelea kufanyika mkusanyiko huop kunaweza kusababisha uvunjaji wa amani au kuhatarisha hali ya usalama" .............Endapo amri hiyo itaonekana kupuuzwa kwa namna yoyote ile hata kama maandamano ,mkutano au mkusanyiko ulikuwa halali utatambuliwa kisheria kwamba ni haramu hivyo hatua za kuwatawanya kwa njia ya shuruti itafuata ikiwamo kuwakamata waandaaji na washiriki kwa lengo la kuwafikisha mahakamani kujibu mashitaka"

  Hapa utaona jinsi ambavyo Polisi wa Tanzania hawataki kutimiza wajibu wao wa kulinda raia , kwani kusema kuwa kuna uvunjifu wa amani badala ya kukabiliana na wanaotaka kufanya hivyo dhidi ya watu waliokaa na kutulia kwa amani wao suluhisho ni kuwatyawanya waliokaa kwa amani na sio wanaotaka kufanya fujo.

  uk.22 na 23 mikusanyiko na maandamano yanayoweza kufanyika bila kibali.

  hapa wameonyesha mikutano ifuatayo kama ambayo haipaswi kutafutiwa kibali. Hapa kuna picha ya mwanamke akiwa na mabango kwenye maandamano.
  1. mikutano ambayo wazungumzaji/mzungumzaji atakuwa ni waziri.
  2. mikusanyiko yoyote inayoandaliwa na mamlaka za serikali za mitaa kwenye himaya yake ya utawala.
  3. mikusanyiko ya kijamii yenye lengo la kutoa elimu,burudani ,michezo n.k
  Hapa najiuliza hivi polisi hawajui kuwa hata wabunge wapo kwenye kundi hili?
  mbona hawajui sheria na hata kuzitafsiri? hivi kweli IGP alisoma kabla ya kuandika dibaji ya kitabu hiki?

  uk.24 na 25 jukumu la polisi katika mikusanyiko .
  Hapa kuna picha ya mbwa wa polisi akiwa ameachama kinywa chote nje akiwa amesikiliwa na askari nafikiri ni wale wa kikosi cha mbwa.

  Hapa wameandika kuwa nanukuu "Jukumu la polisi ni kuzuia vurugu na ghasia zisitokee au zikitokea ni kuzithibiti ili zisisambae na kuvuruga usalama ,amani na utulivu wa watu wengine wasiohusika .Pia ni wajibu wa Polisi kuhakikisha usalama wa waandamanaji au watu waliokusanyika ,ili watimize haki yao ya kikatiba ya kukusanyika na kutoa mawazo yao bila kuvunja sheria kwa kutoa luhga chafu,vitisho au uchochezi"

  hapa nimenukuu uk mzima jinsi ulivyo kwani nawaona polisi wameshasahau kule kwenye mikusanyiko uk.21 walisema kuwa jukumu lao ni kutawanya na sio kulinda vurugu zisitokee huku wanasema lingine .IGP umesoma kabla ya kuandika dibaji ya kitabu hiki ?mbona unajichanganya sana ?ama mahali popote penye neno maandamano basi uandishi wake ni tofauti?

  uk 26 na 27 umuhimu wa kubaini na kuzuia vyanzo vya migogoro katika jamii.
  Hapa kuna picha ya mtoto mdogo ambaye amembeba mtoto mwenzake na nguo zake zimechakaa , biila shaka ni wale watoto wa mitaani .

  Ujumbe mkuu hapa ni umuhimu wa familia kutovurugana na kufarakana ili kuepusha tatizo la watoto wasiokuwa na wazazi ama makazi.

  uk.28 na 29. Matumizi ya nguvu katika kushurutisha Utii wa Sheria.

  hapa imewekwa picha ya askari polisi wawili wakiwa wamevalia mavazi yao ya kivita yaani FFU wakiwa fulu na makofia , rungu, bullet proof na wamemshikilia kijana mmoja ambaye amekaa chini akionyesha kujitetea lakini asikari wanampiga na fimbo /rungu na amenyanyuliwa akiwa anajishikilia na vidole vya mikono ardhini.

  wameandika nanukuu "Askari polisi wetu wamefundishwa jinsi ya kuthibiti vurugu na kushurutisha utii wa sheria ,lakini mbinu na mafunzo hayo yanatumika endapo mhusika au wahusika wataweka mazingira ya kisheria yanayoruhusu vurugu kutumika dhidi yao............Hivy jamii inapaswa kuepuka kuwachukia polisi ,kwa sababu ni watekelezaji wa matakwa ya sheria ya nchi inayotaka anayekaidi ashurutishwe kutii sheria"

  Hizi ndio akili za polisi wetu .

  Nawasilisha .
   
 2. H

  Haki sawa JF-Expert Member

  #2
  Aug 15, 2011
  Joined: Oct 3, 2007
  Messages: 4,701
  Likes Received: 559
  Trophy Points: 280
  Na nyie CDM muache kuchochea vurugu kwani ndio mliosababisha hadi polisi kutunga kitabu ili kuwathibiti. Hizi pesa zingeweza kujenga nyumba ila kwa kuwa nyie mnaleta ukaidi mnasababisha upotevu wa hela za polisi bila sababu zozote zile .

  N a polisi mnawaogopa hawa jamaa mpaka muamue kutunga kitabu? Mbona Pemba hamkufanya hivyo? mbona Mwembechai hamkufanya hivyo? Mbona ni kwa CDM tuu ndio mnatunga kitabu? mnaogopa nini ?
   
 3. m

  mndeme JF-Expert Member

  #3
  Aug 15, 2011
  Joined: Sep 2, 2008
  Messages: 322
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  naambiwa wamekisambaza kama njugu huko mikoani mpaka vijijini kabisa! ndo utajua kuwa ishu ikishawagusa viongoz wa juu wanatumia nguvu kubwa sana kuikabili, utakuta shule hazina vitabu vya kiada na ziada lakini kwa kuwa kakijitabu hako kanalinda maslahi ya magamba
   
 4. DSN

  DSN JF-Expert Member

  #4
  Aug 15, 2011
  Joined: Feb 2, 2011
  Messages: 2,745
  Likes Received: 76
  Trophy Points: 145
  Kama kitabu chenyewe ndiyo maelezo yake,Polisi wangefanya utafiti [Researach] kujua ktaibua fikra gani kwa umma,na si kuibuka na kitabu kilicho na mwonekano hasi kwa umma.Ukizingatia vuguvugu kubwa la kisiasa linagulupu kubwa sana la vijana hasa wa kiume ambao kwa mujibu wa maisha yalivyo wengi wao hawana kazi na maisha yao wengi ni ya kubahatisha [Bangaiza] kwa hivyoo kimapokeo kitabu hicho kinawahusu sana kwa kuwa wengi wao ndio wenye mwamko mkubwa katika kuleta msisimko mkubwa wa kudai haki.

  Ni matarajio yangu kuwa watafute njia sahihi hasa kwa kutumia aina nyingine ya kufikisha ujumbe kwa umma kwa kutumia nija shirikishi na si ujumbe wenye propaganda ya kuwatisha.

  Kazi ndo kwanza imeanza.
   
 5. DSN

  DSN JF-Expert Member

  #5
  Aug 15, 2011
  Joined: Feb 2, 2011
  Messages: 2,745
  Likes Received: 76
  Trophy Points: 145
  Kwa kusambaza mikoni na vijijini ni kuweka elimu ya woga na bomu lijalo.Lakini wasitegemee fujo kuanzia au vulugu za maandamano kuanzia mikoani zinaanzia mijini na majiji na hao wa mikoani ni kitendo cha petroli kukamata mwanga wa kiberiti cha gesi,ambao unaanzia kwenye miji mikuu na majiji yetu.
   
 6. F

  FJM JF-Expert Member

  #6
  Aug 15, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Nimekiona hiko kijarida (sio kitabu). Hivi Mwema anaweza kusema nini chanzo cha watu kutotii sheria? Ni sheria ipi hasa anaongelea hapa? Na hizi sheria ni one way traffic au?
   
 7. SOKON 1

  SOKON 1 JF-Expert Member

  #7
  Aug 15, 2011
  Joined: Dec 28, 2010
  Messages: 1,115
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 145
  Sisi uku Arusha 2mekikataa na hatutaki kukiona kwani ni ukandamizaji wa demokrasia.
   
 8. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #8
  Aug 15, 2011
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Hivi polisi nao wanafuata sheria? waonyeshe kipengele kinachosema polisi anaruhusiwa kuuwa raia asiyekuwa na silalha. Pambaff!!!
   
 9. AirTanzania

  AirTanzania JF-Expert Member

  #9
  Aug 15, 2011
  Joined: Mar 17, 2011
  Messages: 1,127
  Likes Received: 678
  Trophy Points: 280
  Magamba wanajiandaaa na Uchaguzi wa 2015 kwa kuvigawa kwa vingi huko vijijini iliwawaogepeshe watanzania waishio vijijini. Mwema na wahuni wenzake wanafanya Propaganda ya Chama cha Magamba. Na sisi Tunasema hivi kama umo humu JF Mwema au mpambe wa magamba na jeshi la polisi au TISS Tuna kuambia kuwa Watanzania hawataacha kudai haki zao kwa Vitisho vyenu.

  Mapambano Bado yanaendelea Mpaka tunalikomboa Taifa letu na nyie Wahuni mnakwenda jela au kuwanyonga kwa kutumia Rasilimani zetu vibaya
   
 10. kapotolo

  kapotolo JF-Expert Member

  #10
  Aug 15, 2011
  Joined: Sep 19, 2010
  Messages: 3,727
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 145
  Nilikuwa na shwali kama hili, kwamba mwananchi anatakiwa atii sheria bila shuruti lakini mbona polishi wanashurutisha watu kutii sheria? Kama Yaliyotokea Arusha ile ilikuwa ni kushurutisha watu kutii sheria ingawa kiukweli hakuna sheria iliyokuwa imevunjwa

  Hii nayo ni kati ya ngonjera nyingi za mwema, polisi jamii sijui nini na sasa utii wa sheria bila shuruti, sijui inafuata ngonjera gani tena
   
 11. Mumwi

  Mumwi JF-Expert Member

  #11
  Aug 16, 2011
  Joined: Jan 9, 2011
  Messages: 592
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Dr. Slaa alisema Arusha juzi kuwa hicho kitabu kimetungwa kwa ajili ya chadema watu wakipuuze na kama hata Polisi wakimkamata ataendelea kusema hivo.
   
 12. N

  Nyadunga Member

  #12
  Aug 16, 2011
  Joined: Aug 12, 2011
  Messages: 98
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 25
  Hizo sheria anazosema zimetungwa na nani? Hata Adolf Hitler katili namba one duniani alikuwa anafanya hivyo kwa kufuata sheria zilizowekwa. Uzoefu unaonyesha kuwa sheria zinatungwa ili kuwalinda watawala.Tanzania inahitaji kurudi kwenye drawing table iangalie tulijikwaaa wapi na si kuleta vijitabu visivyofanyiwa research kma ya kwao hiyo.Watanzania wanatii sheria sana na ndo maani kuna UTULIVU la sivyo tusingekuwa hapa. Kwanza haw watu wanaotuambia watu wapelekwe JKT wakapate uzalendo ndo hao walienda lakini ndo wanatafuna nchio kam hawana akili nzuri. Vijana tubadiilike na tuanze safari mpya........Second REICH
   
 13. S

  SEAL Team 6 JF-Expert Member

  #13
  Aug 16, 2011
  Joined: Jun 10, 2011
  Messages: 655
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kwa wale ambao wamekwisha kisoma hicho kijarida, ninaomba kuuliza na pia IGP atoe ufafanuzi wa UCHAKACHUAJI WA KURA je kuna maelezo yoyote yaliyotolewa katika hicho kijarida?? Pia rais Kikwete alichakachua kura za Dr. Slaa je IGP ameelezea madhara yake kwa taifa??? Jambo lingine ni kwa vipi hakuainisha kuhusu Polisi, Usalama wa Taifa na JWTZ kumsaidia Kikwete kuiba kura?? Ni kwa vipi hakuzungumzia polisi kupiga wagombe hadi kuwavunja mikono na miguu- MTWARA- KATANI A. KATANI polisi hawakuchukuliwa hatua zozote!!! Swali tena kwa IGP katika mazingira haya nani wa kulaumiwa?? Hapo kuna HAKI kweli????
   
 14. Dingswayo

  Dingswayo JF-Expert Member

  #14
  Aug 16, 2011
  Joined: May 26, 2009
  Messages: 4,011
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 145
  Ningependa kujua idadi ya Watanzania wanaoujua kusoma na kuandika ni wangapi. Hapo zamani kulikuwa na msisitizo wa kutoa elimu ya watu wazima hasa katika fani ya kusoma na kuandika. Kuna kipindi fulani, nchi ya Tanzania ilikuwa inaongoza kwa kuwa na idadi kubwa ya wanaojua kusoma na kuandika. Kwa sasa, idadi hiyo imeshuka kwa kiwango kikubwa sana (kwa bahati mbaya sina takwimu sahihi).

  Sababu kubwa ya kushuka kwa viwango vya kusoma na kuandika ni serikali kupuuzia elimu hiyo, hasa baada ya kuingia mfumo wa vyama vingi. Hapo awali, kabla ya mfumo wa vyama vingi, elimu ya watu wazima ilikuwa inatolewa, pamoja na mambo mengine, kueneza itikadi ya chama tawala, CCM. na vilevile kutoa elimu ya kumuwezesha mwananchi aweze kushirikikatika kuinua uchumi wa nchi.

  Juhudi za kusambaza elimu ya watu wazima, hasa kusoma na kuandika, zingetiliwa mkazo kama ambavyo uandishi na uasamabazaji wa kitabu hicho cha IGP Mwema. Usambazaji wa kitabu hicho umewezekana tu kwa vile kusudi lake ni kuzima moto wa mapinduzi halisi ya wananchiwa Tanzania ambao umeshaanza na kamwe hauwezi kuzimika. Moto huo unaweza usiwe na kasi kama moto wa petroli, lakini naufananisha na moto wa pumba ambao huungua taratibu, lakini matokeo yake ni sawa na ule wa petroli au zaidi kwa vile huwaka taratibu zidi na huchoma kwa uhakika.

  Kitabu hicho kingeandika, sambamba na wananchi kutakiwa kutiii amri bila kushurutishwa, vile vile haki na sheria zipi ambazo zinawalianda wananchi pindi amabapo kuna dalili za uonevu kwa wananchi, uonevu ambao matokeo yake yatakuwa uvunjaji wa amani.

  Sipendi kusema haya, lakini nalazimika kusema kuwa, pamoja na kusambaza vitabu hivyo kwa wingi, havitasomwa na wengi! Ni kwanini inakuwa hivyo? Nilianza kwa kusema kuwa elimu ya watu wazima, kusoma na kuandika vimepuuzwa. Wananchi wengi wamekuwa, kwa muda mrefu sasa, hawana desturi ya kujisomea vitabu. Vitabu hivyo, ninaamini kabisa vitaishia kuwashia moto, au kugeuzwa karatazi za kusokotea sigara.

  Wakati wa kampeni za uchaguzi mkuu uliopita, kuna kiongozi wa CCM aldiriki kuwaambia waandishi wa habari kuwa hata wakiandika habari dhidi ya ufisadi unaotendeka na viongozi wa CCM, habari hizo hazitafika vijijini kwa vile magazeti hayafiki vijijini, na huko hawaoni TV kwa vile hakuna umememe. Sasa basi, kutokana na kukosa utamaduni wa Watanzania kutopenda kujisomea, azma ya vitabu hivyo itakuwa kama nilivyoeleza hapo juu. Kuna msemo katika lugha ya Kiingereza unaosema, 'What goes around, comes around'!
   
 15. d

  dotto JF-Expert Member

  #15
  Aug 16, 2011
  Joined: Sep 29, 2010
  Messages: 1,720
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Naona waliompa jina la Mwema walikosea! au yeye ameshawakosea!
   
 16. Mpaka Kieleweke

  Mpaka Kieleweke JF-Expert Member

  #16
  Aug 17, 2011
  Joined: Feb 27, 2007
  Messages: 4,137
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
  Hili ndio jeshi letu la weledi ,badala ya kupambana na uhalifu wao wanajipanga kuandika propaganda na kuwatisha wananchi, badala ya kuelimisha wananchi juu ya sheria wao wanawatisha, badala ya kukamata mafisadi wao wanawatisha wananchi ili waendelee kutii mafisadi, badala ya kufanya kazi za kujenga jamii inayohoji wao wanataka jamii isiyohoji na hivyo kuifanya jamii kuwa goigoi.
   
 17. Mkolon

  Mkolon Member

  #17
  Aug 17, 2011
  Joined: Jul 15, 2011
  Messages: 20
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  ole wao wanaotunga sheria zisizo za haki watu wanaopitisha sheria za kukandamiza.
  Huwanyima maskini haki zao,na kuwaibia maskini wa watu wangu maslahi yao.
  Wajane wamekuwa nyara kwao;Yatima wamekuwa mawindo yao.
  Je mtafanya nini siku adhabu,siku dhoruba itakapowajieni kutoka mbali?
  Mtamkimbilia nani kuomba msaada?
  Mtakwenda wapi kuweka mali yenu?
  Litakalowabakia ni kujikunyata kati ya wafungwa na kuangamia pamoja na wanaouawa vitani.
  ISAYA 10:1-4
   
 18. mmbangifingi

  mmbangifingi JF-Expert Member

  #18
  Aug 17, 2011
  Joined: Mar 9, 2011
  Messages: 2,855
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  Alipoingia/kuteuliwa Igp Said Ally Mwema alionekana mtu independent and Firm hadi kufifisha dhana kwamba "kateuliwa sababu ya ushemeji" Lkn sasa kabadilika sana karibu kila anachofanya ni kulinda/kutetea CCM na obvious aliyemteua. Njoo katiba mpya!!! ondoa kabisa mandate ya Rais kuteua kila kiongozi wa idara/taasisi kwa vigezo known to the president himself!!!
   
Loading...