Joyce Ndalichako Atakiwa kujiuzulu, ni maafa kwa taifa

Juzi juzi kuna mtoto huko huko Bagamoyo amefikishwa mahakamani kwa kumchapa makonde na kumtoa Jino mwalimu wake kisa eti alimuhamisha shule ya Kata bila ridhaa yake.

Huyu naye akifutiwa matokeo kwasababu ya kuandika mashairi ya Bongo flava na kuchora akina Lione Messi kwenye karatasi ya mitihani napo tutamsingizia Dr. Ndalichako na Wakatoliki. Hivi shule iliyoongoza kitaifa Feza boys ni ya wakatoliki?

Tuache majibu rahisi kwa maswali magumu.
 
Hii ni 'kero' mpya ya Muungano. Inaashiria kwamba siku za mbele jambo lolote ambalo linafanywa kimuungano litakuwa linaleta utata tu, suluhisho ni kila upande u mind their own business, every business, tunakataa ukweli tu Watanzania, tunakataa ukweli, watu wamechoka na Muungano. Mimi naamini kwamba hata baada ya Katiba mpya, muundo wowote ambao utakuja baada ya Katiba mpya haitakuwa mwisho wa 'kero' za Muungano. Kila siku itakuwa kuongelea kero za Muungano, kero, kero, kero...

Lakini Zanzibar ni sehemu ndogo sana ya Tanzania (Zanzibar haijazi hata robo ya Mtwara!) lakini ina distract national agenda ya nchi nzima, inakula national attention ya nchi, ya nini?

Wanadai Zanzibar haina wajumbe wa kutosha kwenye bodi ya NECTA, na Wamakonde nao tudai equal representation kwenye bodi ya Wakurugenzi wa NECTA?

Na Wasukuma nao wakidai? I mean, kuna Wasukumu milioni 5 unusu, Wazanzibari milioni moja, nani ana haki ya kudai equitable representation kwenye bodi ya Wakurugenzi wa NECTA, Wasukuma au Wazanzibar? Wazanzibari kwani wao nani?

Wee! Usiwaamshe Wasukuma. Wako zaidi ya milioni kumi na tatu. Wao ni taifa (kwa kanuni za umoja wa mataifa) kadri ya moja ya tatu ya pua zote za binadamu zilizoko Tanzania ni Wasukuma. Wangekuwa kabila lingine mbona "tungeshakomaga na kukomaga".
Wasukuma, Mungu awabariki. Ukiona upole wa kikondoo wa Watanzania hiyo ni roho ya Kisukuma.
 
ndalichako huyachakachua matokeo ya wanafunzi kwa Kikanda. Huyu mama ni janga la kitaifa

kwani Ndalichako ndio anaesaiisha ayo makaratasi ya wazenj??
Mi naona kama kweli mnauchungu na watoto wenu,mkakate rufaa pepa zisaiishwe upya ili mmuumbue uyo mama.
 
Inaelekea kwenye hili watu wameamua kudili na majina ya watu na kuwazushia tuhuma kwa sababu zao binafsi.Matokeo ni mabaya in general!Elimu inashuka siku hadi siku.Hatuoni tatizo!Tunaangalia matokeo(effects) badala ya kiini cha tatizo.Waliopata div I-III ni asilimia 9(9%)ya waliofanya mtihani.Tunalaumu chombo chenye authority na mitihan tunaviacha vyombo vinavyohusika kumuandaa mwanafunzi kabla ya mtihani.Tunamlaumu Joyce.Anaachwa Shukuru.Anaachwa Jumanne.Anaachwa Mizengo.Anaachwa Jakaya.Tunamlaumu Joyce.Sijui ndo mfumo dume?Tuache kukwepa tatizo jamani.Tusiendekeze siasa kwenye elimu wakati ndizo zimetufikisha hapa.Watoto hawajaandaliwa vizuri ndo sababu ya hata udanganyifu kutokea.Kuna mambo ya msingi ya kuadress kwenye hili kuliko hili la kutupiana lawama za "wao" na "sisi".Kuna mwanafunzi,wazazi,walimu,serikali na jamii kwa ujumla.Wote hawa wana mkono wao katika hili.Tuache udini hata pasipohusika.
 
Tena imekuwa vizuri wao z'bar wanao kina Shukuru na Jumanne wao, ikiwa pamoja na kina Seif, Balozi Idd na Rais wao. Wawabane waimarishe elimu ili watoto wasiendelee kufanya vibaya badala ya kulalamikia wasahihishaji.
 
wazanzibar wamefutiwa matokeo,sio kufeli. lkn wabara hamna chochote, tukiwa pamoja vyuo vikuu uwezo wenu unaonekana, mnaongoza kwa disco.mnafeli sana. mnaringiwa mbeleko ya ndalichako tu

Mie nimesomea udsm class ya 2006-2009. nilikuwa so, nimesoma na dada zako kibao na simu zao za kuslide, hawakuwahi kufanya discussion pasipo mimi. aliyekuwa anajiweza ni mkaka mmoja naye siyo kiviiileee, kuna aliowazidi na kuna waliomzidi tena wengi. Mwisho wa siku, waliofanya vizuri wamebakishwa chuo kwani ni resource ya chuo
 
Kabla ya kuandamana inabidi kufikiri kwa makini kwanza, msijekuwa kama hao waliofanya udanganyifu mkawa kituko.
  1. jiulize na kupitia kama sheria iliyotumika kufuta matokeo haipo katika kanuni za mitihani, msiwe wavivu kusoma
  2. Kuna uthibisho gani wa zaidi ya kuoneshwa wazi miandiko tofauti katika skrpti za watahiniwa au mfanano wa majibu husio wa kawaida, kama unafikiri mitihani umevuja ulivuja vipi na wapi, ulivuja mikononi mwa Ndalichako, kama sio wapi, yeye mtu mmoja, kama mlifungua mkawapa wacopy majibu wakati mmeshaletewa Ndalichako kavujisha vipi mitihani? Mtihani kuvuja kwa ndalichako unavuja kabla hajauleta huko kwa mikoani na mashuleni, mlitaka afanyeje?
  3. Ukitaka kujua idadi ya waliofutiwa Zanzibar na bara jambo ambalo haliwezi kukusaidia kwani udanganyifu mwishoni unamwathiri mtu mmoja mmoja, nenda kaangalie website ya matokeo kwa vituo vyote Z,bar na kisha hesabu waliofutiwa then toa na 3,303 utapata jibu wazenji wangapi. Majina pia utayapata hapo na si kazi ya ndalichako
  4. kero za Muungano kivipi, nadhani uchungu ungeupeleka zaidi katika kufuatilia nyenendo za wanafunzi mashuleni na uwepo wa vitabu na walimu wa kutosha mashuleni. Bila kuimarisha elimuya dunia haitasaidia kitu. kama bado watoto wanachora picha, wanaandika mistari ya nyimbo, wanaandika matusi, badala ya kujibu maswali ya mtihani, hata mkirudishiwa ukweli upo pale pale kwani ufaulu si maksi za bure, ila unafahamu nini
  5. Nashauri tuangalie tatizo kwa mapana zaidi na si jazba, wamevuna walichopanda, wangepita hao keshokutwa wakafanya madudu serkalini angelaumiwa nani. siku za mwizi ni arobaini
  6. hakuna huku ya jumla hapo waheshimiwa, ila kila aliyefanya udanganyifu amefungiwa kufanya mitihani miaka mitatu, ujumla uko wapi hapo
  7. hakuna mtu binafsi anaweza kukandamiza mwingine kwa suala la matokeo ya mtihani even Dr Ndalichako, kama mwanae hana uwezo angeipokea Div O ingawa ana head Baraza hilo la Mitihani
  8. Dr Ndalichako Keep UP, kwa hili inabidi watu waanze kusoma kwa bidii na kuacha ujanja ujanja
 
Back
Top Bottom