Joyce Ndalichako Atakiwa kujiuzulu, ni maafa kwa taifa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Joyce Ndalichako Atakiwa kujiuzulu, ni maafa kwa taifa

Discussion in 'Jukwaa la Elimu (Education Forum)' started by thatha, Feb 20, 2012.

 1. t

  thatha JF-Expert Member

  #1
  Feb 20, 2012
  Joined: Apr 29, 2011
  Messages: 15,228
  Likes Received: 143
  Trophy Points: 160
  Salma Said


  BAADHI ya wazazi ambao watoto wao wamefutiwa matokeo ya mitihani ya kidato cha nne visiwani Zanzibar wanakusudia kulifikisha mahakamni Baraza la Mitihani la Tanzania (NECTA) kwa kutoa adhabu hiyo kinyume cha sheria.

  Wazazi hao walitoa kusudia hilo mjini hapa jana katika wakati wa mjadala uliowashirikisha wadau mbali mbali wa sekta ya elimu na wanaharakati kujadili uamuzi wa Necta wa kuwafutia matokeo wanafunzi 3,303 kutoka Tanzania bara na Zanzibar na kuwazuia kufanya mitihani kwa muda wa miaka mitatu.
  Ameir Hassan Ameir alisema pamoja na kuchukua hatua za kisheria dhidi ya baraza hilo , kuna haja kwa wananchi visiwani humo kuitisha maandamano makubwa kupinga kufutwa kwa matokeo hayo na kushinikiza kuondolewa kwa dhabu dhidi ya wanafunzi.
  Akipinga taarifa ya Necta kwamba mitihani hiyo imefutwa kwa sababu ya udanganyifu uliofanywa na wanafunzi, Ameir alisema baraza limeshindwa kuthibitisha udanganyifu huo na hivyo haliwezi kujiondoa katika kashfa ya kuvuja mtihani.
  Alisema kushindwa kwa Katibu Mtendaji wa Necta, Joyce Ndalichako kutoa maelezo juu ya idadi na majina ya wananfunzi waliofutiwa mitihani kutoka kila upande wa Muungano, kumeibua hisia kwamba Tanzania bara imeandaa njama za kuua elimu elimu Zanzibar .

  "Necta wanayo majina ya shule na namba za shule zote za Zanzibar , hivyo si kweli kwamba hawajui majina ya wanafunzi waliofutiwa mitihani," alisema Ameir huku akihoji uwepo finyu wa ushiriki wa Zanzibar katika muundo wa Bodi ya Wakurugenzi wa Necta.
  Kwa mujibu wa taarifa zilizopatikana wakati wa mjadala huo, bodi ya Necta ina wajumbe 14 na kati ya hao sita wanatoka upande wa Zanzibar .
  "Sisi tuna uchungu na Zanzibar yetu, kuvuja kwa mitihani na watoto kufutiwa mitihani ni matokeo ya kero za Muungano. Adhabu ya miaka mitatu itawapotezea watoto wetu muda wa kusoma, Wazanzibari tuungane tulishtaki Necta," alisema.
  Ali Hassan, Mkuu wa zamani wa Wilaya ya Kati, Mkoa wa Kusini Unguja alisema ingawa Necta imeshindwa kutoa idadi ya wanafunzi waliathirika na uamuzi wa kufutwa matokeo, anaamini asilimia kubwa wanatoka upande wa visiwani wa Muungano.
  Alisema maelezo ya Mkurugenzi Mtendaji wa Necta mbele ya mkutano na waandishi wa habari Februari 14 mjini hapa yanapaswa kusikilizwa tu na mtu asiyejua chochote na kuongeza kuwa kwa hatua hiyo: " Mama Ndalinacho amefeli astep down." Akiwa na maana aachie ngazi.

  Faisal Mohamed, ambaye pamoja na Ali walisema ni miongoni mwa waathirika wa watoto wao kufutiwa mtihani alisema alivishambulia vyombo vya habari na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) kwa alichoeleza kuwa kushindwa kuandika kwa kina habari za kashfa ya mitihani na kupokea kutoka Necta na kusaini taarifa bila kudadisi maelezo ya baraza hilo juu ya utata wa matokeo na hatua zilizochukuliwa dhidi ya wanafunzi.

  Hata hivyo walalamikaji wote hawakueleza kusudio la kulishtaki baraza litatekelzwa kwa sheria, lakini walisema chini ya makosa ya jinai ni kinyume cha sheria kutoa hukumu ya jumla kwa kosa ambalo ni la mtu mmoja mmoja.
   
 2. C

  CHUAKACHARA JF-Expert Member

  #2
  Feb 20, 2012
  Joined: Jun 3, 2011
  Messages: 12,018
  Likes Received: 3,612
  Trophy Points: 280
  Nyie wazenji, acha jaziba. Nawapa ushauri wa bure:
  1. Thibitisha kama watoto wenu walifanya udanganyifu
  2. Kama walifanya udanganyifu, Sheria inasemaje
  3. Adhabu yake ni nini
  4. Adhabu waliyopata inastahili kisheria-ndiyo iliyoainishwa kisheria
  Then from there utafikia conclusion kama haki imetendeka. vinginevyo mtatumia jaziba na mtashindwa huko mahakamani.
   
 3. BADILI TABIA

  BADILI TABIA JF-Expert Member

  #3
  Feb 20, 2012
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 30,025
  Likes Received: 5,193
  Trophy Points: 280
  ijumaa niliona kipindi cha kipima joto huyu mama alikuwa anahojiwa
  tena alionyesha baadhi ya mtihani watoto walivyojibu ni aibu tupu, wamechora picha
  mtoto wa form four mwandiko kama mtoto wa nursery school
  wengine wameandika mistari
  wapo waliojaza majibu ambayo hayapo, mfano chagua kati ya a,b,c,d wanafunzi, tena shule nzima wamechagua herufi O ambayo haipo.
  kuna mwanafunzi ameandika kwenye answersheet kuwa baba yake ndo anamlazimisha kusoma

  hao wazazi wengefuatilia maendeleo ya watoto wao toka shule ya msingi, wangekuwa bega kwa bega na walimu wo watoto wasingefeli.
  na linapokuja swala la feki, pesa za kununua feki watoto wanatoa wapi?

  unaposema ufinyu wa memba toka znz, hata wakiwa memba wa znz 10 ndo wawape alama za ufaulu wanafunzi hata kama wamefeli? hebu wagrow up na kutia msisitizo kwenye alimu na si kulilia upendeleo usio na mantiki
   
 4. C

  CHUAKACHARA JF-Expert Member

  #4
  Feb 20, 2012
  Joined: Jun 3, 2011
  Messages: 12,018
  Likes Received: 3,612
  Trophy Points: 280
  wazenji,
  Nawashauri vitu vyote mvipe uzito sawa, elimi ya dini na elimu ya dunia. Naamini hao waliofeli/waliofutiwa masomo ya madrasa wanayaweza sana. Ni kuweka juhudi pote pote!!! Msiwe na jaziba, tafuteni ukweli wa mambo, na mtapata amani.
   
 5. t

  thatha JF-Expert Member

  #5
  Feb 20, 2012
  Joined: Apr 29, 2011
  Messages: 15,228
  Likes Received: 143
  Trophy Points: 160
  hiii 2011? au unasema kabala ya mapinduzi?
   
 6. Opaque

  Opaque JF-Expert Member

  #6
  Feb 20, 2012
  Joined: Oct 24, 2008
  Messages: 1,138
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  :bounce:
   
 7. t

  thatha JF-Expert Member

  #7
  Feb 20, 2012
  Joined: Apr 29, 2011
  Messages: 15,228
  Likes Received: 143
  Trophy Points: 160
  hizo propagnda za wakiristo wa tanganyika. mbona hakuna waziri mzanzibar mkiristo lkn nchi ipo juuu kuliko kwenu kwenye wakiristo rushwa imejaa?
   
 8. T

  Taso JF-Expert Member

  #8
  Feb 20, 2012
  Joined: Jun 12, 2010
  Messages: 1,532
  Likes Received: 252
  Trophy Points: 180
  Hii ni 'kero' mpya ya Muungano. Inaashiria kwamba siku za mbele jambo lolote ambalo linafanywa kimuungano litakuwa linaleta utata tu, suluhisho ni kila upande u mind their own business, every business, tunakataa ukweli tu Watanzania, tunakataa ukweli, watu wamechoka na Muungano. Mimi naamini kwamba hata baada ya Katiba mpya, muundo wowote ambao utakuja baada ya Katiba mpya haitakuwa mwisho wa 'kero' za Muungano. Kila siku itakuwa kuongelea kero za Muungano, kero, kero, kero...

  Lakini Zanzibar ni sehemu ndogo sana ya Tanzania (Zanzibar haijazi hata robo ya Mtwara!) lakini ina distract national agenda ya nchi nzima, inakula national attention ya nchi, ya nini?

  Wanadai Zanzibar haina wajumbe wa kutosha kwenye bodi ya NECTA, na Wamakonde nao tudai equal representation kwenye bodi ya Wakurugenzi wa NECTA?

  Na Wasukuma nao wakidai? I mean, kuna Wasukumu milioni 5 unusu, Wazanzibari milioni moja, nani ana haki ya kudai equitable representation kwenye bodi ya Wakurugenzi wa NECTA, Wasukuma au Wazanzibar? Wazanzibari kwani wao nani?
   
 9. Shedafa

  Shedafa JF-Expert Member

  #9
  Feb 20, 2012
  Joined: May 21, 2008
  Messages: 798
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35
  Kwani elimu nayo imo kwenye mambo ya muungano, imekuwaje Z'bar ikatafuta kusahihishiwa mitihani yao na Necta si wangesahihisha wenyewe?
   
 10. C

  CHUAKACHARA JF-Expert Member

  #10
  Feb 20, 2012
  Joined: Jun 3, 2011
  Messages: 12,018
  Likes Received: 3,612
  Trophy Points: 280
  Kweli inawezekana, lakini jitahidi kwa nyanja zote
   
 11. Emmani

  Emmani JF-Expert Member

  #11
  Feb 20, 2012
  Joined: Jan 27, 2012
  Messages: 525
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Huyu mama naona mnaonea tu!
   
 12. Shedafa

  Shedafa JF-Expert Member

  #12
  Feb 20, 2012
  Joined: May 21, 2008
  Messages: 798
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35
  Si ajabu wanasiasa wakataka watafute umaarufu wa siasa hapa kwa kutaka kuwa na mambo ya uwakilishi kama hao wasio na kazi za kufanya wanavyotaka, wakumbuke hili ni eneo la taaluma liachwe lijiendeshe kitaaluma.
  Chonde chonde wanasiasa p'se stay out of this!
   
 13. Shine

  Shine JF-Expert Member

  #13
  Feb 20, 2012
  Joined: Feb 5, 2011
  Messages: 11,514
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Du kama kuna majibu kama hayo basi wazazi wa leo wanaotaka maendeleo ya wanao wana kazi ya ziada
   
 14. ntamaholo

  ntamaholo JF-Expert Member

  #14
  Feb 20, 2012
  Joined: Aug 30, 2011
  Messages: 9,583
  Likes Received: 1,647
  Trophy Points: 280
  chika kuitwa mzanzibar kuanzia leo ingawa mimi si mzenji na zenji sijawahi fika. Mtu ametekeleza majukumu yake ajiuzulu? kwa nini kama mnawaamini wanafunzi wenu msidai mtihani mwingine kwa eitha ku appeal baraza au kuandika barua kwa waziri wa elimu mkiomba watoto wenu wapewe mtihani mpya ili mmshike vizuri NDALICHAKO?

  Akijiuzulu unadhani watoto wenu ndo watafaulu?
   
 15. BADILI TABIA

  BADILI TABIA JF-Expert Member

  #15
  Feb 20, 2012
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 30,025
  Likes Received: 5,193
  Trophy Points: 280
  alaaaaaaaaahhhh!!! kwani unadhani ni matokeo gani ninayoyaongelea?
   
 16. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #16
  Feb 20, 2012
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,082
  Likes Received: 38
  Trophy Points: 0
  Kwanza hakuna sheria ya kuhukumu watu wote kwa kosa la mmoja. Pili anaehukumu ndio aonyehe hiyo adhabu kaitoa wapi na kwanini, sio anehukumiwa. Kuwa makini kidogo.
   
 17. BADILI TABIA

  BADILI TABIA JF-Expert Member

  #17
  Feb 20, 2012
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 30,025
  Likes Received: 5,193
  Trophy Points: 280
  tena wana kazi kubwa sana, inabidi kufuatilia kwa ukaribu wa hali ya juu maendeleao ya wanafunzi. Imahine mwanafunzi anachora vikatuni kwenye karatasi ya majibu. na kwenye malezi yetu wazazi tuweke msisitizo wa elimu, watoto washike elimu. sio kutaka favours na kuzalisha mabomu ya baadae
   
 18. zimmerman

  zimmerman JF-Expert Member

  #18
  Feb 20, 2012
  Joined: Feb 17, 2011
  Messages: 531
  Likes Received: 150
  Trophy Points: 60
  Kwani Ndalichako ndiye aliyefanya mitihani? Mfeli nyie mumsingizie Ndalichako?
   
 19. ntamaholo

  ntamaholo JF-Expert Member

  #19
  Feb 20, 2012
  Joined: Aug 30, 2011
  Messages: 9,583
  Likes Received: 1,647
  Trophy Points: 280
  kuna wakristo na wanaojiita wakristo. wakristo ni wafuasi wa KRISTO kwa kila jambo, lakini wanaojiita wakristo, ni wale wanaotumia jina hilo, kwa mazoea tu, lakini ukiwaweka kwenye mizani hawana sifa.

  Tanganyika kuna rushwa tena sana, nakubali lakini watanganyika sio watu wa kupenda upendeleo kama wazanzibar mlivyo shame on you.

  mambo mengine mnatakiwa kuangalia,
  1.je mna walimu wa kutosha kuanzia shule za msingi hadi sekondari?
  2.walimu wanatekeleza majukumu yao inavyotakiwa?
  3. wazazi mnakaa na watoto kuwasisitiza kujisomea au mnatilia mkazo kwenda baharrini kuvua saladini, kibua, chnagu, mkisi na wengine? (kipaumbele kinaamua nature ya matokea ya mwanao)
  4. wanafunz wako serious na kitabu?

  maswali haya yanaweza kuwajenga na sio kuwa walalamishi na kutaka upendeleo tu hapa
   
 20. t

  thatha JF-Expert Member

  #20
  Feb 20, 2012
  Joined: Apr 29, 2011
  Messages: 15,228
  Likes Received: 143
  Trophy Points: 160
  ndalichako huyachakachua matokeo ya wanafunzi kwa Kikanda. Huyu mama ni janga la kitaifa
   
Loading...