Nyaka-One
JF-Expert Member
- Oct 27, 2013
- 4,627
- 6,561
Wadau pengine mimi ndiye siko sahihi. Lakini kwa mtazamo wangu huyu mkurugenzi wa Radio One na ITV angepaswa kuendesha kipindi kingine badala ya hiki kiitwacho "Aibu Yako, Hata Wewe?". Nasema hivi kwa sababu kwa mtazamo wangu hiki kipindi ambacho uonyesha kasoro kadhaa zinazohusiana na magari ya abiria hasa daladala, hakihitaji weledi sana na hasa kwa hadhi yake kama mkurugenzi ambaye alitakiwa awe na kipindi kinachohitaji umakini mkubwa na weledi wa hali ya juu na hivyo kuwa mfano hata kwa watangazaji wengine walio chini yake na watazamaji/wasikilizaji wa kipindi kwa ujumla. Naona kipindi kiko simple sana kwa hadhi yake.