Joyce Mhavile na kipindi ''Aibu yako hata wewe''

Joyce Mhavile na kipindi ''Aibu yako hata wewe''

Kile kipindi kiliitwa KULIKONI?
Yes!!!! nilikuwa nakipenda sana maana kilikuwa kinatuonyesha adha wanazopata watanzania wenzetu abao ni masikini kwelikweli na kutukumbusha sisi how fortunate we are!!!!
 
Joyce alikuwa anaendesha kipindi kizuri sana zamani nadhani kabla hajawa mkurugenzi. Kipindi kilikuwa kinaibua watu masikini na wenye matatizo katika nchi hii. Nimesahau jina ila kilikuwa kizuri sana. Sielewei kwa nini ITV waliacha hicho kipindi.
Kiliitwa KULIKONI.
 
Sio Joyce Mhavile.

Kinaonekana ni rahisi, ni kwa sababu kuna akili kubwa ilitumika mwanzoni nyuma ya pazia.
Hiki kipindi ni copy and paste ya kipindi kama hicho kutoka TV station moja ya nchini Kenya kama sikosei ni KTN au K24.
 
b
Wadau pengine mimi ndiye siko sahihi. Lakini kwa mtazamo wangu huyu mkurugenzi wa Radio One na ITV angepaswa kuendesha kipindi kingine badala ya hiki kiitwacho "Aibu Yako, Hata Wewe?". Nasema hivi kwa sababu kwa mtazamo wangu hiki kipindi ambacho uonyesha kasoro kadhaa zinazohusiana na magari ya abiria hasa daladala, hakihitaji weledi sana na hasa kwa hadhi yake kama mkurugenzi ambaye alitakiwa awe na kipindi kinachohitaji umakini mkubwa na weledi wa hali ya juu na hivyo kuwa mfano hata kwa watangazaji wengine walio chini yake na watazamaji/wasikilizaji wa kipindi kwa ujumla. Naona kipindi kiko simple sana kwa hadhi yake.
huwezi kutambua kama gari limefanya kosa kwa still pictures, hata ukiweza haya mambo yamekaa kisheria zaidi huwezi kulitoa gari lenye namba zangu za usajili kwenye chombo chq habati ukilituhumu ni mpaka lithibitishwe na mamlaka husika na sio waandishi wa habari binafsi nikiliona gari langu namshitaki anatuletea mambo ya OFM hapa wa TZ tuamke...yaani ni sawa sawa wanasheria watusaidie hapa hiyo inaiywa deformation yaani ni sawa kumtoa mtu kwenye tv na kusema mtu huyu ni mwizi, bila kuhusisha mamlaka husika plisi na mahakama.....elimu ndogo tu inahitajika...SASA UNAINGIA MKOA WA MARA KAA KIKAKAMAVU.
 
Wadau pengine mimi ndiye siko sahihi. Lakini kwa mtazamo wangu huyu mkurugenzi wa Radio One na ITV angepaswa kuendesha kipindi kingine badala ya hiki kiitwacho "Aibu Yako, Hata Wewe?". Nasema hivi kwa sababu kwa mtazamo wangu hiki kipindi ambacho uonyesha kasoro kadhaa zinazohusiana na magari ya abiria hasa daladala, hakihitaji weledi sana na hasa kwa hadhi yake kama mkurugenzi ambaye alitakiwa awe na kipindi kinachohitaji umakini mkubwa na weledi wa hali ya juu na hivyo kuwa mfano hata kwa watangazaji wengine walio chini yake na watazamaji/wasikilizaji wa kipindi kwa ujumla. Naona kipindi kiko simple sana kwa hadhi yake.
Ni halali hicho kipindi kitangazwe na mtu mkubwa kama Joyce. Ni kipindi nyeti kuliko vyote kwani uhai wa wengi unapotea. Ingewezekana hata Mengi angeingia usukani ili wahusika waguzwe.
 
Nani Aliyekuambia Kuwa Kusoma Sana au Kuwa Na Elimu Kubwa Ndiyo Huwezi Kuendesha KIPINDI? Kwanza Katika Media Kila Mwandishi Wa Habari Awe Wa Runinga, Redio au Magazeti Anatakiwa Awe Very Flexible KUNAKOTUKUKA. Isitoshe Katika Media Huwa Hatuna Huo UBAGUZI Waka KIKABURU Na Watu Wote Wanatakiwa Kuwa Treated Equally. Ukimshangaa Leo Mama Joyce Mhavile Mbona Humshangai Mtangazaji Charles Nkwanga Hillary Ambaye Hapo Nyuma Alipokuwa Redio One Alikuwa Ni Bosi Tena Mkubwa Tu Lakini Alipoenda MAMTONI BBC Akawa Mtangazaji Tu Wa Michezo? Mkuu Kazi Ni Kazi Tu Kikubwa TAALUMA Yako INATUMIKA Ipasavyo Na Unailetea MAPATO Kampuni. Halafu Tabia Hizi Hizi Za KUJIKWEZA Kwa Watanzania Ndiyo Maana Wenzetu WAKENYA Wanatupiga Gap Kwani Licha Ya Wao KUTUZIDI Hata KIELIMU Na KIMAENDELEO Lakini HAWACHAGUI KAZI. Huwa Nacheka Mno Ninapowaona Baadhi Ya Watanzania Tena Wenye ELIMU Kubwa Tu Wakisafisha VYOO, KUZIBUA MITARO Na KUWACHAMBISHA VIKONGWE Ulaya Lakini Huku Bongo MNAJIKWEZA Na Kujifanya WAKUBWA au Mna HADHI. Hakuna RAHA Kama Kuwa MSOMI ULIYETUKUKA, MWEREVU KISAWASAWA Halafu UKAJISHUSHA Kwa WATU ULIOPO NAO KARIBU Kwani Hali Hii HUKUFANYA KUJIJENGEA HESHIMA, KUPENDWA Na Hata Kama UKITIMULIWA KAZI NA Rais Magufuli Watu WATAKUKUMBUKA KIMTINDO Kama Si KUKULIA Lakini Jifanye Hivyo Na Hayo MARINGO au SHOBO Hizo Zako Kwa WAFANYAKAZI Wako Unaowaongoza Halafu Magufuli AKINUKISHE Kama Hutaona Wafanyakazi Wako WANAPIGA TU MISAMBA SAKAFUNI Kwa KUFURAHI Kutimuliwa Kwako, Wengine Wakicheza Break Dance Tena Mbele Yako Na Baadhi WAKIKUZOMEA!

Huu ni mtazamo wako. Na uzi ni mtazamo wangu. Kuna vipindi vinavyohitaji weledi mkubwa na vipo visivyohitaji weledi mkubwa. Kuna ma MC wa birthday parties na ma MC wa harusi na hafla za kitaifa au kimataifa n.k. MC wa hafla za kitaifa anapokuwa MC wa birthday parties tena za uchochoroni anaweza kuwa kaishiwa. Hakuna weledi mkubwa unaotumika kwenye kipindi tajwa na kwa ujumla hakina msisimko wowote.
 
Sababu ya kutompenda ni nini? Kama mwanadamu naye ana mapungufu yake kama ulivyo wewe, hivyo tujitahidi kuvumiliana
 
Wabongo mshakariri vipindi yaani mmecategorize vipindi vyenye uweledi na visivyo mpaka inafikia hatua ya kuwa na chuki

Mkuu katika uzi unaweza uka cite mahali popote nilipoonyesha kwamba nina chuki na Joyce zaidi ya kuzungumzia kipindi kilivyo na ambavyo angestahili kwa weledi alionao kufanya kipindi ambacho pengine kina impact kubwa katika jamii kuliko hicho?
 
Wabongo mshakariri vipindi yaani mmecategorize vipindi vyenye uweledi na visivyo mpaka inafikia hatua ya kuwa na chuki

Kama ambavyo baadhi ya wabongo walivyokariri kwamba hakuna haja ya categorization ya vipindi kwa kuzingatia weledi unaohitajika! Na kwamba anaekosoa kwa nia njema ana chuki binafsi!
 
Wadau pengine mimi ndiye siko sahihi. Lakini kwa mtazamo wangu huyu mkurugenzi wa Radio One na ITV angepaswa kuendesha kipindi kingine badala ya hiki kiitwacho "Aibu Yako, Hata Wewe?". Nasema hivi kwa sababu kwa mtazamo wangu hiki kipindi ambacho uonyesha kasoro kadhaa zinazohusiana na magari ya abiria hasa daladala, hakihitaji weledi sana na hasa kwa hadhi yake kama mkurugenzi ambaye alitakiwa awe na kipindi kinachohitaji umakini mkubwa na weledi wa hali ya juu na hivyo kuwa mfano hata kwa watangazaji wengine walio chini yake na watazamaji/wasikilizaji wa kipindi kwa ujumla. Naona kipindi kiko simple sana kwa hadhi yake.
Lakini mbona katumia ubunifu mkubwa kwa hicho kipindi. Kwanza kinaelimisha jamii. Pia watu watakuwa makini waonapo hicho kipindi. Ni kizuri ucmuonee mama wa watu.
 
Na hicho kipindi ni copy and paste kutoka Citizen Tv ya Kenya (Shame on You),lack of creativity.
 
Huu ni mtazamo wako. Na uzi ni mtazamo wangu. Kuna vipindi vinavyohitaji weledi mkubwa na vipo visivyohitaji weledi mkubwa. Kuna ma MC wa birthday parties na ma MC wa harusi na hafla za kitaifa au kimataifa n.k. MC wa hafla za kitaifa anapokuwa MC wa birthday parties tena za uchochoroni anaweza kuwa kaishiwa. Hakuna weledi mkubwa unaotumika kwenye kipindi tajwa na kwa ujumla hakina msisimko wowote.
Rafiki, hakuna jambo ambalo utahisi ni la watu wa kama fulani, tunachotaka kukuelewesha ni kwamba Kuwa na weledi /elimu au upeo mkubwa kunaleta ufanisi na sio kukutenganisha kufanya jambo fulani, nina mtu ambaye ni graduate wa chuo mwenye shahada ya kwanza na ni Mc, na anafanya stand up Comedy, angekuwa na mawazo hasi ya elimu yake asingekuwa amejenga, ameoa na Kuwa na gari nzuri. Sijajua kigezo ulichotumia kusema Joyce asitangaze kile kipindi, by the way ni moja kati ya vipindi vizuri sana. Weledi unaotumika pale sio mdogo as unavyodhani. Na usifikirie kila anayeuza chips ni darasa la 4 au 7, ngoja nikuambie niliwahi uza chips nikiwa mwaka wa 3 chuo shahada ya benki na fedha. Tusipende kujikweza rafiki, ila tusijidharirishe pia. Fanya kazi, jitume Mungu atabariki. Ndio maana mhandisi havai suti akiwa field!
 
Mkuu ahsante kwa kunielewesha. Ubarikiwe. Ila bado sijaamini kama hicho kipindi na NAMNA KINAVYOENDESHWA hadi sasa kama ndiyo kipindi chake huyu mama cha kutolea mfano kwa walio chini yake. Sidhani kama kina audience kubwa kutokana na kukosa msisimko. Kimsingi sina maana ya kudharau kipindi. Ila ninachoona ni kipindi kutoonekana kuwa na mvuto mkubwa kutoka kwa mtu kama yeye wakati kuna vipindi vingine vinavyoendeshwa na walio chini yake na vina mvuto zaidi kwa watazamaji. Ni hayo tu.
 
Back
Top Bottom