Amesema jambo ambalo kwa haraka linaonekana lina mantiki lakini linapuuzia uzito wa alichokisema. Kama ni mtu mdogo hivyo aligombea ubunge wa nini? Kama anakosa hekima ya kupima madhara ya maneno yake - watu wanaweza kuumia kwa kauli moja tu ya mtu mwenye ushawishi - kwa sababu yeye ni 'mtu mdogo' ananitisha. Yeye anaweza kuwa na umri mdogo lakini nguvu ya ushawishi wake inashinda baruti na siyo watu wote wanaomsikiiliza wanamchukulia kuwa ni mtu 'mdogo'. grrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrr
Leo baada ya mahojiano na polisi Arusha mjini zaidi ya masaa sita,Nassari akiongea na waandishi wa habari alisema "Mimi ni mdogo,kama ninauwezo wa kuigawa nchi hii basi nchi hii haikupaswa kuwepo"
Source;ITV News 2000hrs*
Tusiwe na mapenzi kwa chama kiasi kwamba tunatafuta udhuru wa tabia mbovu. Kuna mambo ambayo sasa CDM inapaswa ikemewe na wale wanaoipenda pasi ya kusita. Mambo mengine yakiachwa yaendelee yana matokeo mabovu huko mbeleni.
.
Sasa mbunge anaposimama na kutoa kauli ambayo vyombo vya usalama vinaiona ni ya vitisho dhidi ya Rais ni kutokuwa makini kudhania tu ni jambo dogo. Alichotakiwa kusema Nassari ni hiyo kauli yake ya kwanza tu kuwa hakumaanisha ubaya wowote na kama mtu yeyote amekwazwa anaomba radhi. Lakini siyo kusema kuwa ati yeye ni mtu mdogo na asingeweza kugawa nchi; well hilil ni zaidi ya kugawa nchi. Hivi akisema kuwa Rais asikanyage na Kikwete akaamua kukanyaga na mwehu mmoja akaamua kufanya kitu kibaya kwa msafara wa rais watu watamlaumu mwehu kwa vile ni mwehu siyo? Lakini, yule mwehu ukimuuliza atasema "rais wetu" alitoa amri Kikwete asikanyage Arusha na akakanyaga!
Hii ni sababu moja ambayo inanifanya miye nisiwe shabiki sana ya hoja ya 'uongozi bora ni ujana' kwani tayari tumeshaona mengi yasiyo ya lazima ambayo vijana wameyafanya na kuthibitisha ukosefu mkubwa wa hekima na utulivu unaotokana na busara. Siyo lazima useme kila kinachoingia kichwani hata kama unaamini ni sahiihi. Kuna vingine unaweza kuvisema ila kwa namna tofauti. Hili huwezi kufundishwa shuleni au chuoni!
Ni matumaini yangu Polisi hawatoliendeleza hili na Nassari atakuwa amegundua (sidhani kwa sababu arrogance ya madaraka nayo nimbaya sana!) makosa yake. Sitaki ajisikie ameonewa bali ajue genuinely hakupaswa kutoa kauli hiyo na ni unfortunate. Kwa mfano Lema angekuwa makini na kauli zake wala asingevuliwa Ubunge! HEKIMA, HEKIMA, HEKIMA!!
Udogo kwa mtazamo wangu mimi ni wa kimamlaka sio wa kiumri. Inawezekanaje kauli yake ionekane tishio kwa kiwongo cha kuifanya jamii iamini kuwa ni ya hatari sana? Ni kweli kwamba hakuna wanasiasa ambao wameshawahi kutoa kauli kali kama au kuliko hiyo? Wamefanywa nini? Nahisi jeshi la polisi haliko makini! Nashwaishika kuamini kuwa wanapokea maagizo katika kushughulikia baadhi ya mambo, hususani yanayowahusu wanasiasa wa upinzani!Hapa mimi sikubaliani na wewe kabisa. Udogo anaomaanisha Nassari ni wa yeye kuigawa nchi. Najua hata wewe unajua Nassari hana uwezo wa kuigawa nchi kwa sasa. Na hana maana kwamba kila siku atakuwa mdogo. Haya maneno kayatamka leo lakini haina maana kwamba atakuwa mdogo na kesho pia
Leo baada ya mahojiano na polisi Arusha mjini zaidi ya masaa sita,Nassari akiongea na waandishi wa habari alisema "Mimi ni mdogo,kama ninauwezo wa kuigawa nchi hii basi nchi hii haikupaswa kuwepo"
Source;ITV News 2000hrs*
Hakuna chembe ya mantiki hapo hata kidogo ndugu yangu! Amefanya kosa then analeta mzaha. CHE GUEVARA alikufa akiwa na miaka 38, ndani ya muda huo mfupi akawaadabisha mabepari wakubwa kama Marekani.
Kwanza ni kujidharirisha mwenyewe, anajifananisha na mtoto asiyejua jema na baya, hali lukuki ya wana-arumeru wana tumaini naye? Anataka waamini wamekosea kumchagua?
1. Akiri kuteleza ulimi, na kuomba radhi, ni jambo la kawaida sana, sisi kama watz tuko tayari kumsamehe, na ajipange upya, tuko nyuma yake.
2. Chadema itoe tamko la kulaani, na kutoa karipio kwa maneno hayo. Na sio kuishia kusema "hayo sio maneno ya chadema", kwani ametoa nani na wapi?
3. Asipokubaliana na yote hayo, basi chdma kama chama makini, kisisite kumuwajibisha. Lakini sitegemei kufikia huko!
Mungu wetu anaita?
Acha kujikomba kwa Mzee Mwanakiji amechemka sana. Sidhani kama ni yeye ama kaibiwa password.
Siungi na sikubaliani na kauli ya Dogo Janja, lakini pia sikubaliani na pumba alizoongea MMK. Suala la msingi ni kwamba ile kauli haikuwa kauli ya chama, ndiyo maana ilikanushwa pale pale uwanjani na Mbowe, na hili Mzee Mwanakijiji alijua mapema siku hiyo. Jambo alilotakiwa kulijadili Mzee Mwanakijiji kama nguli humu Jf ilitakiwa iwe ni nini kilisababisha Dogo Janja afikie hatua ya kutamka yale manen, nini kiliwaudhi au kilimuudhi. Hii ndiyo ilitakiwa iwe pakuanzia.
Tusiwe kama wapumbavu wanaopiga vita uvutaji wa sigara wakati huo huo wanasimamia uzalishaji wa sigara.
Hii kauli ya Kaskazini kujitenga mnaona kama kauli mbaya ya kibaguzi kuliko kauli ya uvccm mkoa wa pwani ambayo hadi leo hakuna kiongozi wa ccm aliyethubutu kanusha kwa kumwogopa Riz1! Shame on you guys!
Ni afadhali ya CHADEMA waliothubutu kukanusha kauli ya Dogo Janja pale pale.
Mwanakijiji ameongea vema kuhusu kauli za baadhi ya viongozi wa Chadema akitolea mfano wa Lema kupoteza ubunge ni sababu ya kauli si vitendo. Hali kadhalika Slaa baadhi ya kesi ni lugha si vitendo. Kinachomsumbua leo Nasari ni lugha si vitendo. Nimeongea hili jana hapa jf lakini mdau mmoja alivyoniporomoshea matusi namsamehe kwa kuwa hajui kuwa najua hajui alitetealo.
Elimu ya usemaji ni muhimu sana katika majukwaa, si kupanda na kuropoka kikutokacho kichwani, licha ya kujiandaa namna gani uwepo jukwaani kama alivyotokea mbunge wa Tabora wakati wa Kampeni Igunga kupanda jukwaani na trigger. Profesa moja alituambia chuoni, kama huweze kuwa msetirivu katika mada yako na kushtukia unayumba kutoka nje ya mada jitahidi kuandika na uyasome uliyoyaandaa hadi utakakuwa mzoefu wa kudadafula dhamira inayokusudia bila kutoka nje ya dhamira.
Ni nadharia ya kawaida upandapo jukwaani utakuwa umejiandaa vya kutosha nini utaenda kuongea hadharani. Ni bora uandike na uanze kusoma tangu mwanzo mpaka mwishi kama unaona unashindwa kuzuia ulimi wako kuropoka kila kikutokacho kwani uliyojiandaa huwa umeshayachuja yapi yanafaa kwa watu utakaokutana nao badala ya kuongea tu kukujiacho uwapo jukwaani ndio matokeo yake mbunge anafikia hatua ya kumwekea mipaka Rais wa nchi asigusi ndani ya mipaka ya jimbo au ukanda wake, ni kitu kisichoingia akilini mwa wengi wenye upeo wa kuelewa nini dhamana ya viogozi wetu watarajiwa.
Uongozi bora haupimwi kwa usemaji mwingi jukwaani, bali busara hekima na maoni ya umoja kitaifa ndiyo kigezo cha kujenga nchi kwa amani na utulivu. Siasa inaweza kukugeukia upande mbaya mara moja kutokana na kosa moja tu hata kama umefanya mengi mazuri.
Kesi karibu zote zilizopo mahamakani ni za maneno ya uchochezi, hilo ni jambo ambalo Viongozi wa Chadema wanapaswa kuwa waangalifu sana. Viongozi wa Chadema wasidanganywe na uwingi wa watu kuona kwamba ndio kigezo cha kuongea watakavyo bila kupima nini kinatakiwa kuongelewa katika nafasi walizo nazo mikutanoni na kuonyesha umahiri wao wa kisiasa. Mvuto wa kisiasa ni uwezo wa kujenga hoja nzuri na kuzitetea na wala si kutukana au kusema kauli za kuashiria uchochezi.
Hakuna chembe ya mantiki hapo hata kidogo ndugu yangu! Amefanya kosa then analeta mzaha. CHE GUEVARA alikufa akiwa na miaka 38, ndani ya muda huo mfupi akawaadabisha mabepari wakubwa kama Marekani.
Kwanza ni kujidharirisha mwenyewe, anajifananisha na mtoto asiyejua jema na baya, hali lukuki ya wana-arumeru wana tumaini naye? Anataka waamini wamekosea kumchagua?
1. Akiri kuteleza ulimi, na kuomba radhi, ni jambo la kawaida sana, sisi kama watz tuko tayari kumsamehe, na ajipange upya, tuko nyuma yake.
2. Chadema itoe tamko la kulaani, na kutoa karipio kwa maneno hayo. Na sio kuishia kusema "hayo sio maneno ya chadema", kwani ametoa nani na wapi?
3. Asipokubaliana na yote hayo, basi chdma kama chama makini, kisisite kumuwajibisha. Lakini sitegemei kufikia huko!
Mungu wetu anaita?