Joshua Nassari Kumwoa Halima Mdee?

Huyu anadai alikuwepo na hukusikia hayo



Me nilikuwa pale na nilikuwako katika kila mkutano wa Kampeni. Asemayo Liverpool ni kweli. Mkusanyiko uling'ang'ania Halima azungumze. Aliposhika MIC alisema, "tuachieni sisi tuyazungumze kiutu uzima, tukikuballiana Chama kina wachungaji" na lengo hasa ni kuwafurahisha tulokuwa pale tukinyeshewa mvua huku tuki-shout shemeji shemeji.


NIWAZaVYO: ni jambo jema likitendeka. Ila mahazeti acheni kukuza mambo.
 
Me nilikuwa pale na nilikuwako katika kila mkutano wa Kampeni. Asemayo Liverpool ni kweli. Mkusanyiko uling'ang'ania Halima azungumze. Aliposhika MIC alisema, "tuachieni sisi tuyazungumze kiutu uzima, tukikuballiana Chama kina wachungaji" na lengo hasa ni kuwafurahisha tulokuwa pale tukinyeshewa mvua huku tuki-shout shemeji shemeji.


NIWAZaVYO: ni jambo jema likitendeka. Ila mahazeti acheni kukuza mambo.

na kweli baadhi ya magazeti yamezidi,hata kama mhusika alikua anatania kwenye gazeti hawatasema kama ilikua utani,by the way mi sioni ubaya hata wakioana lol!
 
Well hata mimi nilikuwepo Halima aliongea alipokaribishwa kuwasalimu wananchi but i guess alikuwa anajoke watu wacheke wasisikie baridi baada ya kunyeshewa mvua. Lakini hata kama ni kweli kwani kuna tatizo gani wote si wamekamilika katika uumbaji wa Mungu??
 
kwani halima mdee hayupo hapa jf? Atuweke wazi basi kwani akiendelea kunyamaza ndio ccm wanapata mwanya wa kumchafua

mara nyingi we post zako ni za kukurupuka na kutotumia akili, cha kumchafua hapo ni kipi? Kuolewa ama nini basi? Mbona ni jambo zuri na heshima kubwa kwa wenye busara? Cha msingi ni kutafuta ukweli wa hili suala na sioni kama kuna kumchafua mtu hapo! Umetaja pia magamba yamekujaje hapa, sidhani kama watanzania tumefikia kuchukiana kwa tofauti za kisiasa..!!
 
MBUNGE wa Kawe, Halima Mdee (Chadema) amesema sasa yuko tayari kufunga ndoa na Mbunge mteule wa chama hicho wa Jimbo la Arumeru Mashariki, Joshua Nassari.

“Nafurahi kwamba Nassari hatimaye ameshinda ubunge katika uchaguzi mdogo,” alisema Mdee wakati akihutubia maelfu ya wakazi wa Arusha na Meru juzi katika viwanja vya Leganga kusherehekea ushindi wa chama chake katika uchaguzi huo.

Mdee alifafanua, kwamba yeye na chama chake walikuwa wamebanwa na kampeni za kuhakikisha Chadema inatwaa jimbo la Arumeru Mashariki na ndiyo sababu hakujibu mara moja maombi ya Nassari ya kumwoa aliyoyatoa katika moja ya mikutano yake ya kampeni.

“Naondoka kwenda Dar es Salaam kujiandaa kwa Mkutano ujao wa Bunge, kisha nitakwenda Dodoma ambako nitamsubiri Nassari na kwa pamoja tutafanya maandalizi,” alisema Mdee huku akishangiliwa na hadhira hiyo huku wakiimba na kucheza katikati ya mvua iliyokuwa ikinyesha.

Mdee alisema ndoa kati ya wabunge hao wawili wa Chadema ni wazo zuri na itatangazwa sana na kuandika historia.

Alipoona anashambuliwa sana na wapinzani wake juu ya useja wake katika kampeni hizo, Nassari hatimaye alitangaza kumwoa Mdee ambaye pia hajaolewa.

Na katika moja ya mikutano ya hadhara, alisimama naye jukwaani kukampeni.

“Kuna viongozi wengi wa kidini Dodoma, ikiwa ni pamoja na ndani ya Bunge ambao watatushauri jinsi ya kulitimiza hili,” alisema Mdee na kuongeza kwamba baba yake Joshua, Mchungaji Samuel Nassari alipata kusema, ‘mwanamke mzuri ni zawadi kutoka kwa Mungu’.

Source; Habari Leo
 
Ni wanafiki na wambea wakubwa sana hawa, hata hivyo mboan hayawahusu? waache mambo ya watu waandike jinsi walivyoumbuka
siliamini hili gazeti..........................ni la kimagamba
 
Hili nalo gazeti la udaku!!! dhu. Walishindwa kuandika mambo ya kampeni leo waja na ndoa. Kwa kodi zetu!!
 
Silisomi ingawa habari nimeipata huku; wanatafuta uchawi kwa watu binafsi baada ya sera zao kushindwa wanadeal na petty issue
 
Teh Teh Teh kwahiyo tuanze kudai kodi zetu au? Maana mi nimekuwa naona siku zote habari yao kubwa ni kesi ya Lema
 
Itakuwa safi ila Nassri bado mdogo sana na Mdee sasa anakaribia 35, sijui itakuwaje gap la age km 7 years hv, licha ya mapenzi si umri but kwa kiafrika mume akiwa mdogo sana kuliko mke aaah haipendezi, ila km wameamua kuoana let it be sisi tunawaombea kheri tu.Lakini kwa nn waandike gazeti la serikali wakati walikuwepo hawaku sikia? Kitendawili hiki.
 
Hatutaki Nassari ahamie Kawe. Wananchi wa Arumeru walimchagua ili awatumikie kwa ukaribu zaidi
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom