Kitaeleweka tu
Member
- Dec 16, 2013
- 23
- 25
Wana JF,
Leo naomba tumjadili kidogo mtu anayeitwa JosephineMshumbuzi a.k.a Mchumba wa Dr. Slaaaliyeshindwa kufunga ndoa na hicho kibabu chake baada ya mke mwenzie (RoseKamili) kuwakamata mahakamani. Huyu mwanamke ni tatizo na Slaa ameshindwakabisa kumdhibiti na sijui anatakaje urais ikiwa hawezi hata kumdhibiti mkewake. Naweza kudondoa machache hapa kuhusu huyu mwanamke na athari zake kwachama:
Kama nilivyomnukuu Dr. Slaa kwenye thread nyingine.
Leo naomba tumjadili kidogo mtu anayeitwa JosephineMshumbuzi a.k.a Mchumba wa Dr. Slaaaliyeshindwa kufunga ndoa na hicho kibabu chake baada ya mke mwenzie (RoseKamili) kuwakamata mahakamani. Huyu mwanamke ni tatizo na Slaa ameshindwakabisa kumdhibiti na sijui anatakaje urais ikiwa hawezi hata kumdhibiti mkewake. Naweza kudondoa machache hapa kuhusu huyu mwanamke na athari zake kwachama:
- Tunaweza kusema wazi kwamba kama CDMitazama leo kwa wimbi la ACT-Tanzania linaloonekana kuja kuipiga CDM, chanzo niJosephine. Ndiye aliyeanzisha mgogoro na Mwigamba na kushinikiza Slaa kumfukuzaMwigamba kinyume cha taratibu za chama kwa sababu alikuwa anazuia dili zakekama ile ya kutengeneza database ya computer kwa milioni 10 bila kupitia tendercommittee, kwa kutumia Microsoft access wakati program hiyo inatengenezwa kwalaki 5. Akadanganya kwamba hiyo ni accounting package wakati siyo. HatimayeMwigamba alikuja kujiunga na akina Zitto na leo tunashuhudia akiwa ni nguzomuhimu kwenye ACT-Tanzania kama katibu mkuu na CDM hawajui uwezo wa Mwigambawala hawajawahi kujiuliza Mwigamba aliijengaje Arusha ikawa ngome ya CDM katikamuda wa miezi 4 tu tangu achaguliwe kuwa Mwenyekiti wa Mkoa. Subirini kivumbicha ACT – Tanzania kitakavyoisambaratisha CDM ndo mtamwelewa huyo jamaa.
- Ni Josephine huyo huyo ambaye amekuwaakiendesha mapambano dhidi ya Zitto kwa kuhofia kwamba Zitto atakuja kuwatishio kwa mume wake kwenye kugombea urais kupitia CDM. Matokeo yake kukawa nauhasama mkubwa kati ya Zitto, Slaa na Mbowe. Naomba niwahakikishie kwamba ulewaraka wa siri unaomsema Zitto kwamba alikuwa akipokea mabilioni ya CCM naUsalama wa Taifa kuimaliza CDM ni kitu kilichoandaliwa na Mshumbuzi na vijanawake kwa makusudi ya kummaliza Zitto. Lakini leo Zitto anasemekana kuwa nyumaya akina Mwigamba katika kuanzisha ACT-Tanzania na Mbowe na Slaa wanajidaiwamesahau uwezo wa huyu kijana. Subirini ACT-Tanzania ipate usajili wa kudumuhalafu Zitto ahamie huko ndo tutaona kimbunga chake.
- Ni Josephine Mshumbuzi aliyeliweka jimbo laKawe sokoni kwa sasa. Alitumia muda mwingi kuwalobby madiwani wa CHADEMA waKawe ili hatimaye Halima Mdee aonekane hafai na yeye Mshumbuzi aje kugombeahapo 2015. Mdee akajikuta kwenye wakati mgumu sana. Wakati fulani wabunge waCDM wakiwa retreat pale Morogoro na Katibu mkuu Slaa akiwepo, Halima hakuwepo.Alipigiwa simu aeleze jinsi Josephine Mshumbuzi anavyovuruga jimbo lake,alikuwa anaongea akilia kwenye simu. Wachambuzi wa mambo wanasema Mdee kurudiKawe ni ndoto na Mshumbuzi ana mchango wake mkubwa kwa hilo.
- Ni Josephine Mshumbuzi aliyesababishakudumaa kwa BAWACHA. Anatumia ki-NGO chake cha wanawake kuhakikisha anawafikiawanawake wa CDM na kuunda mtandao wake na kumwambia mchumba wake kwamba katibumkuu wa BAWACHA Taifa (Naomi Kaihula) hafanyi kazi. Mara kadhaa Slaaamemshambulia Kaihula kwenye vikao akimwambia kwamba "Huna watu wewe, sijuiunafanya kazi gani. Mama (Josephine Mshumbuzi) amezunguka nchi nzima na tayariameshatengeneza mtandao mkubwa wa wanawake. Wewe unafanya nini". Hayo manenoyamekuwa yakimuumiza sana na kumkatisha tamaa Kaihula na hatimae barazalimedolola. CDM haina toucha kabisa na wanawake. Inang'ang'ana na vijana tenawale wa vijiweni wanywa viroba na kutafuna mirungi ambao hawana shahada zakupigia kura. Tukiendelea hivi tutaendelea kupigwa na 2015 tutapigwa tukiwatumesimama.
- Josephine Mshumbuzi ndiye aliyetuma messageile ambayo inadaiwa ilitumwa kwa IGP Mwema na Slaa siku moja kabla ya mauaji yaMwangosi. Hata Mbowe anajua kwamba ile msg aliiandika Josephine kwenye simu yaSlaa kisha akamwambia Slaa, "shika umtumie hii IGP", Slaa akachukua simu nakutuma. Ndo huyo aje kuwa rais wetu!!!??? Haikuwa msg ya busara hata kidogo na haifai kutumwa na kiongozi mkuu wachama tena anayedai kujiandaa kuingia madarakani. Lakini yote ni udhaifu kwamke mpaka kushindwa kumkatalia kufanya vitu vya kijinga.
- Kwa wale wanaojua, kuna ID humu JF inaitwa"Dr. W P Slaa". ID hiyo ipo pia facebook. Kiukweli hii ID haitumiwi na Slaabali Josephine. Anaitumia wakati mwingine kupost vitu vya kijinga, manenoyasiyo ya busara, spelling zimekosewa kosewa, lugha imekaa kama ya mtu wadarasa la saba, halafu eti maneno hayo yanaonekana yameandikwa na msomi kamaDr. Slaa. Soma mfano maneno hayo ya hapo chini alipokuwa anamjibu Msuki. Hiisiyo lugha ya Slaa. Huku ni kumdhalilisha Slaa mwenyewe na kumshushia hadhi yakuwa rais mtarajiwa na Slaa anajua yote anayoyaandika mkewe kwa kutumia jinalake na ameridhika! Nawaambia watanzania tushtuke. Tukichagua Slaa kuwa Raisnawahakikishia tutakuwa tumeingiza balaa kuliko Lucy Kibaki ndani ya ikulu yaTanzania. Mpaka mawaziri watachapwa makofi na mke wa rais. Tafakari!!!
Kama nilivyomnukuu Dr. Slaa kwenye thread nyingine.
Msuki,
Taarifa yako inaweza kuwa ni nzuri. Ili tusikuite mzushi na mpotoshaji, ebu wawekee watanzania tamko lolote au ushahidi wowote ambapo viongozi wa Chadema wametamka kuchangisha Watanzania kununua ndege, magari na kadhalika.
Mwaga nyaraka mkuu watu wakuamini. Vinginivyo ni chuki tu. Nadhani tukiamua kuweka mafanikio ya operation mbalimbali za Chadema utakimbia, kwa kuanzia na " madai ya Katiba, ambayo ccm haiku nayo kwenye ilani yake 2010, hakuna asiyekumbuka matamko ya mawaziri wa JK kuwa Taifa hili halihitaji Katiba Mpya, kususiwa JK na Wabunge wa Chadema kushinikiza Katiba Mpya, Maandamano mikoa mbalimbali....
Ningeweza kutoa malengo mbalimbali na mafanikio yake kwa kila operation. Kamanda, Kama hujui kufanya tathmini ya jambo omba wenye ujuzi wa jambo hili badala ya kukurupuka na kupotosha.
Bahati nzuri umma wa Watanzania wanaelewa malengo ya operations za Chadema. Jipime kwanini wewe uko upande wa wachache wasioelewa, huenda wewe ndio tatizo.