Joseph Selasin, Mbunge wa Rombo, anaandika

Kwani kuna sehemu alisema zimeibiwa ?

Yeye anataka Maelezo zipo wapi
Akisema zimeibiwa akienda mahakamani uthibitisho atatoa ?
Ye aliposimamishwa na Rais aliikana report yake mwenyewe wakati report inasema hazionekani matumizi yake, ameonyesha uoga mbana wakati anahojiwa na azam tv alisema hazionekani na kuwataka wabunge waibane serikali itoe majibu
 
Hamna jipya hapa.

Tungekuwa tunajadili,kushauri na kutoa maelekezo kwenye maeneo yote yaliyotajwa yana HATI CHAFU kwenye report ya CAG bila ya kuangalia huyu wa chama changu au huyu rafiki yangu tungefika mbali sana.

Lakini tunafanya na tunaendelea kukumbatiana kwa style yetu ya siku zote kwamba kwa vile huyu ni wangu nikimwambia ukweli nitamuudhi. Tuwe wa kweli kwenye report ya CAG HATI CHAFU imetajwa kwa CCM na Serikali yake tu? Navyojua kula ni kula tu haijalishi umekula kidogo au kikubwa.
 
Nilikuwa sijajua hiyo trillion 1.5 inayosemwa, sasa Mh. Selasini enielewesha vizuri na nimeelewa! Kweli watoe majibu bwana kama wamekosea magazijuto warudie tena! Mwaka huu jiwe lazima afe kwa pressure, siku 2 tu Zitto kambana mpaka Jana anatoka hadharani akiwa afya mgogoro!!
Hahaah hii nilidhani nimeiona peke yangu....mkuu ushawahi muona mtu aliyefumaniwa???
 
yani ukiskia mtu kutoa hoja zilizokwenda shule ndo huku.....mtu unamhoji maneno yamgusa lakn hayamkwazi ila yanamuingia mpka kwenye figo
 
Nimependa comment yako. Isije ikawa hata hao wanaowatisha wenzao hawajaelewa kama wewe ulivyokuwa hujaelewa au hata hawajasoma kabisa hiyo ripoti , learning is a process lakini hii principle inakuwa ngumu kwa wanaokariri.
Ni kweli mkuu,, hata jiwe halijaelewa kabisa lenyewe linategemea lione hela imeibwa kabisa! Kumbe kuna hela imepotelea juu kwa juu!! Basi si wangedanganya hata kama imebaki balance!!
 
Ebu funua ukurasa unaohusu mapungufu ya CHADEMA umpe ushauri MBOWE!
CDM wamepewa hati ya mashaka, na sababu aluzozitoa CAG ni kuwa wameweka ununuzi wa ardhi na majengo pamoja, jambo ambalo ni kosa kihasibu. Hayo ni makosa ya kihasibu lakini siyo upotevu wa fedha. Wala hajasema kuna hela haionekani. Ameqapa pia ushauri namna ya kufanya ili makosa kama hayo yasirudiwe tena.

Mapungufu ya CDM kwenye report ya CAG yanaeleweka na yanaelezeka lakini siyo 1.5 trillion ambayo haijulikani iko wapi!
 
Ye aliposimamishwa na Rais aliikana report yake mwenyewe wakati report inasema hazionekani matumizi yake, ameonyesha uoga mbana wakati anahojiwa na azam tv alisema hazionekani na kuwataka wabunge waibane serikali itoe majibu
Hajaikana ripoti yake amejibu kile kilichopo kwenye ripoti yake acheni kumlisha maneno CAG.
 
Ebu funua ukurasa unaohusu mapungufu ya CHADEMA umpe ushauri MBOWE!
Mada ni Trilion 1.5 ziko wapi hilo la Mbowe kwa mujibu wa taarifa ni makosa na yeye ni kikaango kimoja tu

Mtu akipoteza tutasema tu awe CHADEMA au chama kingine, hatupo kusifia ujinga
 
Back
Top Bottom