CHADEMA na UKAWA kupitia Prof.Lipumba walikuwa wanashinikiza uandikishaji usitishwe kwa sababu una kasoro nyingi sana(kwa mujibu wao) pia wakasema uchaguzi mwaka huu hautakuwepo kwa sababu muda wa kuandikishwa watu wote hautoshi.
Dr.Slaa akiongea siku alipotua uwanja wa ndege wa Mwl.Nyerere akitokea Marekani alisema BVR ni ufisadi mtupu. Huku akisisitiza kuwa mfumo huo haujawahi kufaulu sehemu yeyote ile duniani.
Sasa huu mpango wa CHADEMA na washirika wake kujidai wao ndio vinara wa kushawishi watu wajiandikishe umetoka wapi? Ina maana wameshasahau mapingamizi yao ya awali serikali ilipoanza mchakato huu?
Ni Lini BVR imekuwa sio mpango wa kifisadi kama alivyotuambia Mzee Slaa? Ni lini Lipumba na Mbowe wamegeuka na kuiunga Mkono serikali kuhusu uandikishaji huu?
CHADEMA na UKAWA acheni kuwa vigeugeu!