Joseph Mbilinyi 'Sugu' ataja pengo aliloacha diwani

Joseph Mbilinyi 'Sugu' ataja pengo aliloacha diwani

Replica

JF-Expert Member
Joined
Aug 28, 2017
Posts
1,716
Reaction score
9,051
pic+sugu.jpg

Wakati Mwenyekiti wa Baraza la Wanawake la Chadema (Bawacha), Halima Mdee akitarajiwa kuongoza mazishi ya aliyekuwa diwani wa viti maalumu Mbeya Mjini, Ester Mpwiniza leo, Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi ‘Sugu’ ametaja pengo aliloliacha diwani huyo.

Sugu alisema Mpwiniza aliyewahi kuwa mwenyekiti wa Bawacha Wilaya ya Mbeya Mjini, alikuwa kiunganishi muhimu ndani na nje ya chama hicho.

“Mama Mpwiniza alikuwa kiongozi mkubwa ndani na nje ya chama, hivyo hatuwezi kuharakisha maziko yake. Tunasubiri viongozi wa kitaifa akiwamo Mwenyekiti wa Bawacha Taifa, Halima Mdee na viongozi wengine. Sijajua makaburi atakakopumzishwa lakini itakuwa ni hapahapa Mbeya Mjini,” alisema Sugu.

Mwenyekiti wa CHADEMA Wilaya ya Mbeya Mjini, Obadia Mwaipalu alisema diwani huyo alianguka nyumbani kwake Ijumaa na alipelekewa Hospitali ya Rufaa Mbeya alikofariki dunia kutokana na shinikizo la damu.
 
Back
Top Bottom