Joseph Mbilinyi(Sugu) afichua madudu ya TAZARA Mbeya

Joseph Mbilinyi(Sugu) afichua madudu ya TAZARA Mbeya

ALFA OMEGA

Member
Joined
Feb 9, 2014
Posts
20
Reaction score
51
· WAFANYAKAZI WAFUKUZWA KAZI OVYO · AITAKA SERIKALI KUWARUDISHA KAZINI MARA MOJA Mbunge wa Mbeya Mjini Joseph Mbilinyi "Sugu" amefichua madudu ambayo wanafanyiwa Wafanyakazi wa TAZARA Mbeya ikiwemo kufukuzwa kazi ovyo. Akiongea bungeni Mbunge huyo alisema ni aibu kwa serikali kufukuza wafanyakazi wake bila sababu za msingi eti kisa tu Mbunge alienda kusikiliza kero zao na kupigia kelele ili zitatuliwe.

Sugu anasema Wafanyakazi hao walimumualika katika kikao cha kuzungumzia matatizo yao ikiwemo kutokulipwa mshahara kwa takribani kipindi cha miezi mitano na huku viongozi kadhaa wa serikali hadi wa Chama tawala walikuwa wakienda kuwasikiliza na kuwaahidi ahadi kemukemu ambazo walikuwa awazitekelezi. Alisema baada ya kufika yeye akasikiliza kero zao na kisha kutoa tamko kwa serikali na wahusika wote kuhakikisha wawe wamewalipa wafanyakazi hao haraka iwezekanavyo, ndipo Wafanyakazi hao wakalipwa mishahara yao ya miezi minne.

Cha ajabu baada ya kulipwa tu Wafanyakazi 86 wakapewa barua za onyo na kujieleza kwa nini wasichukuliwe hatua za kinidhamu huku wafanyakazi 26 wakipewa barua za kufukuzwa kazi, na moja ya sababu iliyoandikwa kwenye barua zao ni kumkaribisha unauthorized person (mtu asiyeruhusiwa). "yaani inafika kipindi Mbunge anaitwa mtu asiyeruhusiwa kuongea na watu wa jimbo lake na mnafukuza watu kwa ajili ya sababu hiyo? " alihoji Mbunge huku akisisitiza anao ushahidi wa kuthibitisha hili. Akaendelea, "Mheshimiwa Mwandosya…wewe ni Waziri unayeingia wizara yoyote, serikali yenu mnatuumizia watu wetu Mbeya, nukuomba mzee wangu hakikisha suala hili linamalizika na wafanyakazi hawa wanarejeshwa kazini maana walikuwa wakidai haki zao,".

Pia Mbilinyi aliongea kuwa ajabu yake Wafanyakazi wa TAZARA upande wa Zambia waliokuwa wakidai mishahara serikali yao iliwalipa na kuwapa mapumziko ya siku tatu ili wakapumzike na familia zao, na akaahidi kupigania haki za wafanyakazi hao, kwani walichofanyiwa ni uonevu usiokubalika.

Mwandishi wa habari hii alipofuatilia kujua kwa kina suala hili kwa upande wa TAZARA Zambia akataarifiwa kuwa wafanyakazi wa upande huo walifanya vurugu kubwa iliyopelekea uharibifu wa mali ikiwemo majengo na magari ndipo serikali yao ikawalipa na kuwapa hizo siku za mapumziko. Chanzo kingine cha habari kinaelezea kwa upande wa Wafanyakazi wa TAZARA Mbeya kuna ushahidi wa baadhi ya Wafanyakazi ambao walipewa barua ya kufukuzwa kazi tarehe 12 mwezi septemba na huku kikao cha kusikilizwa (hearing court) kikipangwa tarehe 15 septemba hiyo ikimaanisha kuwa walifukuzwa kabla hata ya kuhojiwa.
 
shirika la utangazaji bbc limemumbua waziri wa uchukuzi harrison mwakyembe kwa kuwahoji wafanyakazi wa tazara waliofukuzwa kazi kwa kudai mshahara ile hali jana alikanusha na kumkanusa rais wa mbeya sugu
 
atasema wanatumiwa
 
Baadhi ya watendaji wa serikali kama vile wana kichaa fulani hivi!
 
Hii nchi bana.....ukiwa mzembe unasimangwa...ukichapa kazi maadui wanakuandama kama Nyuki.....

No wonder wengine huishia tu kuwa mafisadi kwani mwisho wa siku wanaonekana mashujaa wanaporudi kwenye jamii zao, tofauti ya kujitoa muhanga kwa jamii yenye majungu na upofu wa macho na akili.
 
Ukitaka ufaidi na ule vizuri kwenye Serikali hii ya MaCCM we kuwa mnafiki, mmbeya, jipendekeze kwa wakubwa na ikiwezekana kuwa hata kuwadi wao... hapo hata kama kazi yako ni muangalizi wa ofisi fedha utakazokuwa unapata ni zaidi ya Afisa au Mkurugenzi wa Idara..
 
nimesikia bbc mfanyakazi mmoja akisema amefukuzwa kazi kisa aliongea na bbc
 
Mwakyembe anatia aibu sana ! Mbona yeye tulimsaidia sana kwenye mgogoro wa kiwira coal mine ?
 
nimesikia bbc mfanyakazi mmoja akisema amefukuzwa kazi kisa aliongea na bbc

Tazara wanaiua hivihivi bila makosa ! Natoa agizo maalum kwa serikali mpya ya UKAWA kuhakikisha tazara inafufuliwa ndani ya miezi 6 na kukamata wote waliohusika kuliua , hii ni pamoja na kupaka rangi majengo yote hasa makao makuu , na kuhakikisha zile taa zinawaka kama zamani .
 
Ha! ha! haaa! Mbeya nchi Rais SUGU.Mwandosya na Mwakyembe wanatakiwa kutekeleza maagizo ya RAIS SUGU!
 
· WAFANYAKAZI WAFUKUZWA KAZI OVYO · AITAKA SERIKALI KUWARUDISHA KAZINI MARA MOJA Mbunge wa Mbeya Mjini Joseph Mbilinyi “Sugu” amefichua madudu ambayo wanafanyiwa Wafanyakazi wa TAZARA Mbeya ikiwemo kufukuzwa kazi ovyo. Akiongea bungeni Mbunge huyo alisema ni aibu kwa serikali kufukuza wafanyakazi wake bila sababu za msingi eti kisa tu Mbunge alienda kusikiliza kero zao na kupigia kelele ili zitatuliwe.

Sugu anasema Wafanyakazi hao walimumualika katika kikao cha kuzungumzia matatizo yao ikiwemo kutokulipwa mshahara kwa takribani kipindi cha miezi mitano na huku viongozi kadhaa wa serikali hadi wa Chama tawala walikuwa wakienda kuwasikiliza na kuwaahidi ahadi kemukemu ambazo walikuwa awazitekelezi. Alisema baada ya kufika yeye akasikiliza kero zao na kisha kutoa tamko kwa serikali na wahusika wote kuhakikisha wawe wamewalipa wafanyakazi hao haraka iwezekanavyo, ndipo Wafanyakazi hao wakalipwa mishahara yao ya miezi minne.

Cha ajabu baada ya kulipwa tu Wafanyakazi 86 wakapewa barua za onyo na kujieleza kwa nini wasichukuliwe hatua za kinidhamu huku wafanyakazi 26 wakipewa barua za kufukuzwa kazi, na moja ya sababu iliyoandikwa kwenye barua zao ni kumkaribisha unauthorized person (mtu asiyeruhusiwa). “yaani inafika kipindi Mbunge anaitwa mtu asiyeruhusiwa kuongea na watu wa jimbo lake na mnafukuza watu kwa ajili ya sababu hiyo? “ alihoji Mbunge huku akisisitiza anao ushahidi wa kuthibitisha hili. Akaendelea, “Mheshimiwa Mwandosya…wewe ni Waziri unayeingia wizara yoyote, serikali yenu mnatuumizia watu wetu Mbeya, nukuomba mzee wangu hakikisha suala hili linamalizika na wafanyakazi hawa wanarejeshwa kazini maana walikuwa wakidai haki zao,”.

Pia Mbilinyi aliongea kuwa ajabu yake Wafanyakazi wa TAZARA upande wa Zambia waliokuwa wakidai mishahara serikali yao iliwalipa na kuwapa mapumziko ya siku tatu ili wakapumzike na familia zao, na akaahidi kupigania haki za wafanyakazi hao, kwani walichofanyiwa ni uonevu usiokubalika.

Mwandishi wa habari hii alipofuatilia kujua kwa kina suala hili kwa upande wa TAZARA Zambia akataarifiwa kuwa wafanyakazi wa upande huo walifanya vurugu kubwa iliyopelekea uharibifu wa mali ikiwemo majengo na magari ndipo serikali yao ikawalipa na kuwapa hizo siku za mapumziko. Chanzo kingine cha habari kinaelezea kwa upande wa Wafanyakazi wa TAZARA Mbeya kuna ushahidi wa baadhi ya Wafanyakazi ambao walipewa barua ya kufukuzwa kazi tarehe 12 mwezi septemba na huku kikao cha kusikilizwa (hearing court) kikipangwa tarehe 15 septemba hiyo ikimaanisha kuwa walifukuzwa kabla hata ya kuhojiwa.

Sugu yuko njema sana,haigopi kusema ukweli
 
So hill tuu hata wakati alipopukutika ngozi tulimsupport na kumuonyesha upendo iweje yeye awe name chuki

Siyo kumuonyesha upendo tu , bali sisi ndio tuliomtonya kwamba kapewa kitu , basi tu binadamu hawana wema .
 
Siyo kumuonyesha upendo tu , bali sisi ndio tuliomtonya kwamba kapewa kitu , basi tu binadamu hawana wema .

Eti alipopewa cheo akakana kuwa hakupewa sumu na kumtosa swahiba wake Six aliyekuwa anazunguka makanisani kumuombea sumu iishe mwilini.
Na bado hajarudi kusema kama sio sumu ilikuwa nini? Ukoma au maradhi ya kurithi?
 
Tazara wanaiua hivihivi bila makosa ! Natoa agizo maalum kwa serikali mpya ya UKAWA kuhakikisha tazara inafufuliwa ndani ya miezi 6 na kukamata wote waliohusika kuliua , hii ni pamoja na kupaka rangi majengo yote hasa makao makuu , na kuhakikisha zile taa zinawaka kama zamani .

Kirahisi rahisi hivyo?
 
Eti alipopewa cheo akakana kuwa hakupewa sumu na kumtosa swahiba wake Six aliyekuwa anazunguka makanisani kumuombea sumu iishe mwilini.
Na bado hajarudi kusema kama sio sumu ilikuwa nini? Ukoma au maradhi ya kurithi?

hawa watu ni wanafiki sana .
 
Back
Top Bottom