Joseph Mbilinyi ataka bandari ya nchikavu Mbeya | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Joseph Mbilinyi ataka bandari ya nchikavu Mbeya

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Bujibuji, Sep 17, 2010.

 1. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #1
  Sep 17, 2010
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,322
  Likes Received: 22,149
  Trophy Points: 280
  MGOMBEA ubunge wa jimbo la Mbeya Mjini kwa tiketi ya Chadema, Joseph Mbilinyi amewaahidi wananchi wa Mbeya kuwa endapo atachaguliwa kuwa mbunge atahakikisha serikali inaweka bandari ya nchi kavu mkoani hapa ili kuwarahisishia kazi wafanyabiashara wa nje na kukuza maisha ya wakazi wa mjini hapa.

  Mbilinyi, mmoja wa wasanii waliotangaza muziki wa kizazi kipya akitumia jina la Mr ll 'Sugu' alitoa kauli hiyo wakati wa kampeni zake akisema wakati umefika wakati kwa mkoa wa Mbeya kuwa na bandari ya Nchi kavu ili kuwezesha wafanyabiashara wanaotoka nchi jirani za Zambia na Malawi kupata bidhaa kirahisi mkoani hapa badala ya kusafiri hadi Dar es salaam.

  Mbilinyi alisema Mbeya imekosa mkakati wa kusaidia wafanyabiashara kutoka nje kupata bidhaa zao mkoani hapa na ndio maana hupitiliza kwenda Dar es salaam kufuata bidhaa, wakati mji huu ni kiungo kikubwa cha kibiashara na nchi za Malawi na Zambia.

  Alisema mfumo wa biashara mkoani hapa umekua kikwazo kwa wafanyabiashara wengi ndio maana hata wafanya biashara wa Mbeya wamekimbilia Dar es salaam kuendeleza biashara na kuutelekeza mkoa wao.

  “Tukiwa na ushirikianao mzuri baina ya serikali na wafanyabiashara na kuwa na bandari ya nchikavu itasaidia wafanyabiashara kutoka Malawi, Congo, Zambia na Zimbabwe kununua bidhaa zao hapa na kuongeza mapato kwa serikali ya Mbeya,” alisema Mbilinyi.

  Alisema watoto wa mkoani hapa wamekuwa wakichangishwa michango mingi kwenye shule zao kutokana na serikali ya mkoa kutokuwa na vyanzo vingi vya mapato.

  Mbilinyi pia alisisitizia ahadi yake ya kuhakikisha kila shule ya Mbeya Mjini inakuwa na kompyuta 30 ambazo alisema zitapatikana kutoka kwa wafadhili ili kusaidia wanafunzi kielimu.

  "Sijaja kuihubiri Chadema, bali nimekuja kukomboa Mkoa wa Mbeya na hasa jimbo la Mbeya Mjini ili kuweka heshima ya jiji kwa wakazi wake kuwa na maisha yenye kupendeza... ni aibu kuona mkoa wa mbeya unapendeza pembezoni huku katikati kukiwa na maisha mabovu kwa wananchi," alisema.

  "Maendeleo hayahitaji wageni toka nje ya nchi bali kushirikiana kwa pamoja kutasaidia jamii yetu."
   
 2. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #2
  Sep 17, 2010
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,322
  Likes Received: 22,149
  Trophy Points: 280
  Safi sana SUGU,
  Mbeya wanahitaji mawazo mapya kama ya kwako,
  Mpesya na sisiem wake hakika hawana jipya, na wanarusisha nyuma nmaendeleo ya mkoa wa MBEYA
   
 3. Devils Advocate

  Devils Advocate Member

  #3
  Sep 17, 2010
  Joined: Dec 16, 2009
  Messages: 78
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mr II anatoa ahadi chache lakini ni za muhimu. its about time mbeya kuwa Inland Port kwa Malawi na Zambia. Its so logical. Hili la computer 30 nalo zio gumu sana kwa mtu aliyeishi marekani. Refurbished computers zinapatikana kwa bei chee sana. Hata kwa mshahara wa ubunge ti anaweza leta zote.

   
 4. F

  Froida JF-Expert Member

  #4
  Sep 17, 2010
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 7,900
  Likes Received: 1,328
  Trophy Points: 280
  Mr II kweli kabisa klazima Mbeya iwe kitovu cha biashara na kiungo muhimu kwa nchi zote zilizo kusini mwa Afrika kumbuka Mbeya ilivyo tajiri katka nyanja zote Mazao,Madini,rasilimari misitu,maji,watu wenye bidii na kujituma,kazana tu baba inawezekana na usisahau kurudisha hadhi ya Mkoa wa mbeya katika nyanja zote za kiuchumi,michezo kumbuka akina nzaeli mwinga,zambi,walitokea mbeya imarisha michezo na kujenga viwanja vipya bustani na usisahau kuboresha mazingira ya mji wa mbeya kwa ongeza kasi ya upandaji miti na bustani,kurudisha ari ya vijana kukamata soko la nchi jirani,kila la heri bwana mdogo
   
 5. M

  Mkulima JF-Expert Member

  #5
  Sep 17, 2010
  Joined: Feb 4, 2007
  Messages: 698
  Likes Received: 113
  Trophy Points: 60
  Hili la Mbeya kuwa na bandari ya nchi kavu mbona liko hatua za mwisho za utekelezaji?

  Kuna watu ninawafahamu wanashughulikia huo mradi ingawaje sijui lini utaisha. Mr II akienda chama cha wafanyabiashara pale Mbeya nafikiri ataelezwa ukweli wote.
   
 6. N

  Nsaji Mpoki JF-Expert Member

  #6
  Sep 17, 2010
  Joined: Nov 5, 2007
  Messages: 396
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Hawa ndiyo vijana wanaotakiwa,anahubiri kuongeza fursa za ajira na uwekezaji mkubwa mkoani mbeya.Fursa za aina hii zitasababisha kuongezeka kwa uzalishaji wa bidhaa mbalimbali na kuongeza kipato kwa Mkoa na Taifa nzima.Upande wa CCM wao wahubiri kugawa watu kwa kufuata ukabila kitu ambacho hakina manufaa yeyote zaidi ni machafuko na mtafaruku kwenye jamii.
  Nakupa tano Mr II
   
 7. Mtu wa Pwani

  Mtu wa Pwani JF-Expert Member

  #7
  Sep 17, 2010
  Joined: Dec 26, 2006
  Messages: 4,095
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 135
  na huyu hayuko mbali kurudi CCM, na akirudi hawi tena Shujaa.

  maana Shujaa kwa sera ya watu hawa uwe CHADEMA
   
 8. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #8
  Sep 17, 2010
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,322
  Likes Received: 22,149
  Trophy Points: 280
  Suguuuu....ahhhh
  kweli umekua,
  akili imepanuka sana. Tofauti sana na hawa waimba ubongo wa flava
   
 9. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #9
  Sep 17, 2010
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  hivi huwa anahutubia kwa kunesanesa au kitulivu??
   
 10. Naloli

  Naloli JF-Expert Member

  #10
  Sep 17, 2010
  Joined: Aug 26, 2010
  Messages: 416
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  shutuma anazozipata NAKAYA kazi tafuta mwenyewe hiv lazima ukirudi CCM uuze sura jukwaani? Ndio maana watu wanahisi anamtega baba Ridhiwan baada ya kuona mwenzake VICKY KAMATA katoka kimaisha. uhuru wa kujiunga na chama chochote ni wa kikatiba na hata kutokuwa na chama pia katiba inaruhusu. Lakini unajiunga na chama leo kwa mbwembwe tena wewe ni mtu maarufu kesho unajitoa tena kwa kusubiri JK aje mkoani kwako upande jukwaani uuze sura kwa kujinadi umerudi chamani, lazima wenye akili wakutilie shaka. Hiv kwanini usiwarudishie kadi wenye nayo (CHADEMA) au kwanini usiende kwenye Tawi la CCM na kuchukua kadi ya kujiunga nao au Kwanini usijiunge na chama hicho wakati wa kampeni za mgombea uDiwani wao? badala yake unasubiri aje rais? Je sera na umakini wa CCM KAUONA SIKU YA MKUTANO HUO? Pia maneno aliyokuwa anayatoa akiwa mwana CHADEMA ndio yanayo muhukumu.Hivyo ukiwa mtu mashuhuri ni lazima upstairs kuwekunafanya kazi vizuri umemuona Nyimbo,Shibuda,Mwera walivyofanya? Busara inahitajika kila unapofanya maamuzi mazito maana Uzito wa mtu ni Akili na si Kg
   
 11. Albedo

  Albedo JF-Expert Member

  #11
  Sep 17, 2010
  Joined: Feb 24, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Ha ha ha Mkuu nitakutumia video clip? Ukiimagine unaweza muona Sugu akighani Jukwaani!
   
 12. M

  Mwafrika JF-Expert Member

  #12
  Sep 17, 2010
  Joined: Nov 20, 2006
  Messages: 5,490
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0
  crap
   
 13. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #13
  Sep 17, 2010
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,322
  Likes Received: 22,149
  Trophy Points: 280
  Duh...
  Sisi tunataka sera sio style ya uhutubiaji
   
Loading...