Jorginho for Ballon D`or 2021

Kwa kuongoza kiungo cha Klabu yake ya Chelsea kushinda kombe ya ligi ya Mabingwa ya Ulaya na kwa kujenga kiungo Imara cha timu ya Taifa ya Italia na kuiwezesha kushinda kombe la Fainali za Euro 2020, Jorge Luiz Frello Filho almaarufu Jorginho ambaye huko Italia anajulikana kama "Regista"(DIRECTOR kwa kiingereza) anastahili kushinda hii tuzo na kuwa Mcheza bora wa dunia kwa mwaka huu wa 2021.



Nini maoni yako mwanabodi.


Messi anachukua ya 7 asubuhi mapemaa, idadi ya ballon na namba 7 ya Jersey inayovaliwa na jamaa yako CR7 🤣🤣🤣🤣🤣
 
Kwa kipi labda! Tuanzie hapo

Hii ni Messi ama lewa fullstop,

Kante angefika final ama kubeba angalau, hata mi ningekusapoti.

Ukitaka top player wa tano walionesha kiwango cha juu kwenye hii tournament hawezi kuwepo, uefa nako hawezi kuwepo sasa anapewa kwa kigezo kipi!

Ballon d or lazma individual statistics ziwe vizuri kulingana na position yako
 
Hajaonesha kiwango cha maana cha kumuwezesha kushinda hiyo tuzo. Ana bahati tu ya kushinda mataji hayo mawili makubwa, basi.

Hapo Italia kwa mfano, kuna aliyeongoza kujenga kiungo imara kumshinda Verratti wa PSG?

Kulingana na ripoti mbalimbali, Messi ndiye anayeongoza kinyang'anyiro, akifuatiwa na Harry Kane, Kante na wengineo. Isitoshe, hii ni kabla ya Messi kuchukuwa Copa America na Argentina saa kadhaa zilizopita.
Mm nilimewaambia tangu kwenye ile Thread ya Euro kua wajipe moyo tu lkn when time comes Messi anabeba ya 7 na there is nothn they can do abt it.
 
Angeanza kwanza kuchukua tuzo ya mchezaji bora wa Euro (Golden Ball). Hajachukua sababu hajastahili. Huko unakotaka apafikie bado ni parefu sana!

Kiungo mwenzake [Modric] alichukuwa UEFA CL, pia alichukuwa tuzo ya mchezaji bora wa Kombe la Dunia mwaka 2018 ndipo akashinda Ballon d'Or iliyofuata.
Bora ww umeanza wapa na mifano hai.
 
Iniesta na xavi walipokuwa kwenye peak walikosa tuzo..!
Sembuse hiyo dagaa haina assist hata moja wala goli..!
Pale italia verrati, kina Federico chiessa wameupiga mwingi.

Hatuna cha kukusaidia una Safari ndefu ya kujifunza
 
Back
Top Bottom