Kuna njia mbili za kufanikisha hilo kutegemeana na aina ya version na nini unachotaka kufanya.
1. Kutumia static landing page:
Hii inafanana na mtindo waliotumia
RipotiRushwa Campaign Tanzania yaani mtembeleaji atachagua lugha kwenye kurasa ya mwanzo na baada ya hapo, utakuwa na folders mbili, moja ni kiswahili na nyingine ya kingereza.
Faida Mtembeleaji anachagua nini anataka kwenye hatua ya kwanza.
Utata: Kama haupo fiti kwa sana kwenye joomla, inabidi uwe na website mbili tofauti kitu ambacho kitaongeza kazi kwa administrator kwani tovuti ya kiswahili na ile ya kingereza zipo kwenye folders tofauti. Ingawa unaweza kusynchronize users kwa kutumia baadhi ya plugin, ila zinahitaji ufundi kimtindo na ni ngumu kwa mafaili, so kwa mtu ambaye hana ujuzi wa kutosha anaweza kuishia njiani.
2. Kutumia Joomla multiple languages:
Uzuri wa Joomla 2.5 imekuja na hii kitu, yaani siku hizi hatuhitaji tena Joomfish ili kutengeneza tovuti ya lugha nyingi, nimetengeneza tovuti yenye lugha hadi nne, tena zikijumuisha hadi zile za RTL (kama kiarabu na kihebrew). Ukishamaliza unaweza tumia Module (Vijibendera) kumfanya mtembeleaji kuchagua lugha anayotaka, pia kwenye backend unaweza kuset kuwa ama watembeleaji watapelekwa kwenye site ya lugha moja then wabadili wenyewe (default language) ama lugha iangalie lungha inayotumika kwenye browser.
Faida: Ni rahisi kuimplement, kumanage na kiutendani.
Utata: Kwakuwa hadi sasa hakuna language pack ya kiswahili, kama unaijua Joomla vyema, inakubidi kutengeneza language pack yako mwenyewe
(Wengi wamekuwa wakitumia option ya 1 juu ambapo , wanachukua ile ya kingereza halafu wanabadilisha mafaile kwenye .ini) tatizo lingine ni kuwa ni wachache mno wanatumia browser zenye lugha ya kiswahili, hivyo ni ngumu kuifanya hii process automatic.
NOTE: Kutengeneza language pack sio kazi, ila inahitaji patient, bado tunamalizia maneno fulani kwenye pack ya kiswahili, then nitashare hapa ili wadau wafaidike.
Kama ningekuwa wewe: Kama ningekuwa wewe, ningetumia option ya pili kwakuwa ni scalable na stable, pia inaonesha ukomavu.
Picha inaonesha tovuti moja ya E Commerce ambayo tumetengeneza ina lugha nne, hii kuonesha uwuzekano wa hili.
Msaada zaidi: Kama bado una utata au unahitaji professional help, ni PM kuona ninakusaidiaje. Pia unaweza kuangalia tutorials jinsi ya kufanya hivyo kwa kiswahili.
12. Kusetup tovuti yenye lugha nyingi kwenye Joomla - Part 1
13. Kusetup tovuti yenye lugha nyingi kwenye Joomla - Part 2
Hope nimesaidia.