Jokate Mwegelo ni kati ya wajasiriamali 30 wanaofanya vizuri- Forbes Africa

kirerenya

JF-Expert Member
Aug 27, 2013
1,696
2,253
Mjasiriamali jokate Mwegelo almaarufu kama Kidoti ametajwa katika orodha ya jarida la Forbes ya wajasiriamali 30 wa Afrika wanaofanya vizuri wenye umri chini ya miaka 30.

My take: Hii ni hatua nzuri kwa juhudi alizoonesha kwenye ujasiriamali wake. Vijana wengine tuige mfano wake tupambane bila kuchoka.

Hongera kwake, ila kama umri wake ni under 30 basi wangu ni under 10, mana akiwa chuo mwaka wa kwanza mimi nilikua darasa la 7 zamani sana
 
Hahahaaa...Napata mashaka na hili jarida la Forbes..
Jokate Miss Tanzania No2 mwaka 2006, sasa kama ni under30 ina maana kamati ya Lundenga mwaka huo waliruhusu mtoto kushiriki Umiss...
 
hahaha hii habari za Forbes kuhusu watanzania mara nyingi huwa siziamini maana kuna habari ililetwa ya mtu mashuhuri watu wakaitetea kumbe ilikuwa ni cooked
 
Mjasiriamali jokate Mwegelo almaarufu kama Kidoti ametajwa katika orodha ya jarida la Forbes ya wajasiriamali 30 wa Afrika wanaofanya vizuri wenye umri chini ya miaka 30.

My take: Hii ni hatua nzuri kwa juhudi alizoonesha kwenye ujasiriamali wake. Vijana wengine tuige mfano wake tupambane bila kuchoka.

Yale yale ya kina Jackline Mengi, kibiashara kinaanzishwa jana - leo kinatambuliwa na Forbes africa.

- Anafanya biashara gani serious ?

- Kampuni yake inaitwaje ?

- Kaajiri watu wangapi na ulipaji kodi wake ukoje ?

UJINGA MTUPU na vikampuni vya mfukoni kama WEUSI hata ofisi hakuna

- Kama Forbes wataendelea kumwamini MFONOBONG NSHEHE ( Forbes Africa Under 30 ) wanaweza kupoteza wasomaji makini, maana amekuwa MTUNZI tu wa STORI na mpenda RUSHWA i think
 
Mzee biashara zipo nyingi. Usishangae sana. Anaweza kuwa ni mjasiriamali wa mwili wake.
 
Umri wake n 32 anazeeka sasa.... napata mashaka na hili jarida..
Pia wamekuwa wakimg'ang'ania Mo/Gulam kama tajiri namba moja Tz lkn ukijaribu kuangalia kwa haraka haraka Bakhresa yuko mbali sana ukiangalia raslimali alizonazo ni nyingi kuliko Mo......hawa jamaa hata sijui wana malengo gani......eti Jokate hajafikisha miaka 30? Khaaaah!!!
 
Kwa Mo ni mwenye umri mdogo
 
Back
Top Bottom