Jokate Mwegelo: Mpaka Wananchi wanalalamika tupo wapi?

JUMA JUMA

JF-Expert Member
Jan 5, 2013
666
835
DC TEMEKE JOKATE MWEGELO:"HILI NI SUALA LINALOGUSA TAIFA"

Mkuu wa wilaya ya Temeke Mhe. Jokate Urban Mwegelo ameungana na wakuu wa idara pamoja na wataalamu kutoka mamlaka ya mapato Tanzania (TRA) na uhamiaji katika ziara ambayo amegundua changamoto mbalimbali.

Mhe. Mwegelo ametembelea kiwanda cha KTM kilichopo eneo la Mission kata ya Mbagala ambapo amebaini changamoto wanazopitia wafanyakazi wa kiwanda hicho ikiwemo kucheleweshwa kwa mishahara, mazingira mabaya ya kazi, na maswala mbalimbali ya kodi pamoja na mapato.

"Mpaka wananchi wanalalamika tupo wapi? Tunafanya nini kuwasaidia? Fikiria watu wanafanya hizi shughuli kwenye maeneo yetu halafu hamna hatua ambazo wanachukuliwa....naomba tuwe watendaji tunaowajibika"

Mhe. Mwegelo amesema kuwa kwa kuunganisha nguvu na kufanya kazi kwa ushirikiano na idara zote pamoja na wataalamu mbalimbali Temeke itaweza kujikusanyia mapato zaidi ambayo walikua wakiyakosa.

"Kufanya kazi kwa pamoja ni utaratibu mzuri....nategemea sasa nitapata taarifa za kutosha katika ofisi yangu ili kama kuna mapato serikali iliyapoteza tuweze kuyarejesha na kama faini tujue ni shilingi ngapi na hawa vijana hapa wapate stahiki zao..ili mradi kila kitu kikae kwenye mstari tukumbuke hili ni suala linalogusa taifa si Temeke tu"

Aidha Mhe. Mwegelo ameziagiza idara zote zilizogundua changamoto katika kiwanda hicho ( ikiwemo idara ya kazi, biashara,uhamiaji,na mazingira) kuzifanyia kazi haraka changamoto hizo na amewahakikishia wafanyakazi wa kiwanda hicho kuwa serikali itahakikisha wanapata stahiki zao mapema iwezekanavyo.

IMG-20210720-WA0083.jpg

IMG-20210720-WA0082.jpg
 
Yaani hii nchi ni ngumu sana!!akiwepo kiongozi sehemu fulani anavyo jimwambafai, kuwa ametatua kero zote kubwa kubwa!!kumbe kuna vikero vidogo vidogo vingi vimemshinda!!siku moja GONDWE, aliwafokea hasa wachina wanaojenga barabara ya kilwa, na kuwapa muda wa kumaliza hiyo kazi, wakamwambia tatizo ni fedha hawapewi on time, akasema sitaki kusikia hiyo sababu!!kumbe vitu vidogo tu hivyo hakuviweza!!
 
"Mpaka wananchi wanalalamika tupo wapi? Tunafanya nini kuwasaidia? Fikiria watu wanafanya hizi shughuli kwenye maeneo yetu halafu hamna hatua ambazo wanachukuliwa....naomba tuwe watendaji tunaowajibika"

Mhe. Mwegelo amesema kuwa kwa kuunganisha nguvu na kufanya kazi kwa ushirikiano na idara zote pamoja na wataalamu mbalimbali Temeke itaweza kujikusanyia mapato zaidi ambayo walikua wakiyakosa.

"Kufanya kazi kwa pamoja ni utaratibu mzuri....nategemea sasa nitapata taarifa za kutosha katika ofisi yangu ili kama kuna mapato serikali iliyapoteza tuweze kuyarejesha na kama faini tujue ni shilingi ngapi na hawa vijana hapa wapate stahiki zao..ili mradi kila kitu kikae kwenye mstari tukumbuke hili ni suala linalogusa taifa si Temeke tu"

Huyu DC ndiye alifaa kuwa RC wa Dar, she is brilliant she conciders citizens' challenges first, wakati RC wake anafanya kinyume chake

Tunakuomba Jokate umfikishie Makala ujumbe huohuo ajitafakari, you are younger than him but clever than he is

Yaani hii nchi ni ngumu sana!!akiwepo kiongozi sehemu fulani anavyo jimwambafai, kuwa ametatua kero zote kubwa kubwa!!kumbe kuna vikero vidogo vidogo vingi vimemshinda!!siku moja GONDWE, aliwafokea hasa wachina wanaojenga barabara ya kilwa, na kuwapa muda wa kumaliza hiyo kazi, wakamwambia tatizo ni fedha hawapewi on time, akasema sitaki kusikia hiyo sababu!!kumbe vitu vidogo tu hivyo hakuviweza!!
Ni Walokole wachache sana wenye Akili.
 
Back
Top Bottom