Jidu La Mabambasi
JF-Expert Member
- Oct 20, 2014
- 16,101
- 25,971
Michezo ni uhamasishaji, na michezo yaweza kuwa siasa.
Kati ya watu ambao wameonyesha commitment kwa nchi ya Tanzania, hadi duniani, watu wamepata Phd katika Management ni Mtanzania John Peter Aquari.
Mfano wa John Peter Aquari ni somo tosha la the highest level of commitment kutokana na mtu kuipenda nchinyake.
Wengi hawamfahamu lakini kitu alichofanya mtanzania huyu mwaka 1968 kinajulikana dunia nzima kupitia misimamo ya kuhamasika kwa binadamu kuitumikia nchi yake.
Mwaka 1968, John Peter Aquari alikuwa kijana mdogo kutoka JWTZ , na alishiriki marathon ya Olympics huko Mexico.
Hakushinda na wala hakuwa mmoja wa washindi kumi wa kwanza katika marathon hiyo.!
Anachokumbukwa John Peter ni kwamba, licha ya kuumia na kutenguka goti, aliendelea kujikongoja hadi mwisho wa utepe, na muda huo ulikuwa saa moja nzima baada ya mashindano kuisha.
1 hr baada ya mashindano kuisha, na watazamaji wengi kuanza kuondoka, ndo mwanariadha wa mwisho aliingia uwanjani akiongozwa na pikipiki ya polisi na king'ora!
Watazamaji waliokuwa wakiondoka walirudi kumshangilia mwanariadha huyu mtanzania na alikuwa anajikongija !
Kilichowashangaza wengi ni hii spirit na level ya commitment na kujitolea kwa ajili ya taifa lake kwa huyu kijana, John Steven Aquari.
Alipoulizwa nini msukumo wake kumaliza Marathon akiwa peku na ameumia, John Peter alijibu ;
"Nimetumwa na nchi yangu kushiriki, na kumaliza mashindano ya marathon"
Leo taarifa ya habari ITV saa mbili nimemsikia huyu John Peter Aquari akilalamika kuwa hata zawadi aliyoipewa ya cheki, imeliwa na wajanja, toka mwaka 1968.
Machozi yamenitoka.