John Pombe Magufuli unatuchefua


Kama usemayo yana ukweli ndugu yangu jaribu kumwambia mkuu wa kaya wamkate huyu fisadi wetu sielewi ni nini kinachomshinda mkuu wa kaya kumkamata na kumfunga na kurudisha hela zetu au kutaifisha mali za huyu fisadi mkuu
Yaani kama leo mi ndo nimechefuka kabisa kwenye taarifa ya habari ya saa mbili eti Magufuli anasema " umeme huu unao katika katika ni matokeo ya ufisadi wa huyu huyu mamvi" ina maana mr.mamvi ana nguvu kuliko mkuu wa kaya???? huyu mtu ana jeshi la kukodi marekani au???? kwanini kutuaminisha ni fisadi halafu serikali haiwezi kumkamata???? nachefuka kusikia uongo wa KIWANGO cha juu namna hii, Mungu ibariki Tanzania.
 
Mlete baba yako kama ataweza kazi za Magufuli kila MTU NA KIPAJI CHAKE

Acha upuuzi wewe baradhuli , hapa wanaume tunazungumzia mustaqbali wa nchi .
Ukosapo cha kuandika kafanye shughuli nyingine . Wawezatumia mda wako hata kupunguza mchicha mwilini mwako , badala ya kuufuga !
 

Hoja yako nzuri mno. Ni hivi: kila jambo lina wakati wake. Wakati wa haya mafisadi kushughulikiwa umefika. Ni lazima ujue kwamba hatuchezi na fisadi mmoja tu bali tunacheza na taasisi ya kifisadi yenye mbinu za hali ya juu ya kusimika dola ya kifisadi kupitia mikataba tena ya kisheria na ukienda vibaya inakula kwako na ndiyo maana nchi iko makini na kwa tahadhari ya juu katika kuwakamata na kuwafunga na kurejesha vyetu. Hatua ya kwanza ilikuwa ni kuwakata na wakakatwa. Hatua ya pili ni kuweka rais ambaye hawafanani kabisa kimtazamo na hatokani na msaada wa taasisi ya kifisadi na tena mwenye pumzi ya kuwatazama mafisadi machoni mchana kweupe na kuwambia hapa hapana. Hatua ya tatu ni kwamba taasisi ya kifisadi itakapokuwa hana tena influence na dola ndipo sasa access ya data zao zote zitakapokuwa huru na ndipo swala la kisheria litakapokuwa na nguvu maana ushahidi sasa utakuwepo tena huru Ndiyo maana nchi inahangaika kulibana kundi hili la taasisi ya kifisadi maana likiingia ikulu this time litashindilia mikataba ya kufa mtu na haitakaa ifutwe labda kwa vita. Hebu uwe unaangalia basi na movies za kifisadi na kimafia ili ujue jinsi ambavyo makundi haya hujijenga na kuwa taasisi na kupenya vilivyo hadi kwenye system na dola ya nchi. Huu siyo udhaifu wa siku moja bali ni likitu lilianza tangu zamani sana na walioasisi wengine ni hayo makapi yaliyohamia huko kwenu na lengo lao ni kupenya tena wakatetee walichokianzisha kwa kutumia uvivu na ushamba wa watanzania katika kufahamu operesheni za kifisadi. Funguka!
 
Mletamada , afadhali yako wewe anakuchefua tu, mimi ananitapisha!
 
Umeandika nini?
 
Ufisadi ni taasisi, ni zao la udhaifu wa miaka mingi, tena ni taasisi makini ambayo ina mvuto wa pekee kwa wasio na maono, tena ina sifa za kupenya hadi ngazi zote, hutumia watu kuibeba na kuitetea hasa watu wasiojitambua na wavivu wa kufikiri. Taasisi ya kifisadi huwa haipotezi dira tena ina specific objectives na targets. Ipo katika matabaka yooote ya jamii. Kuliangusha hili dude wanahitajika watu dizaini ya Magufuli ambaye kwake hapendwi mtu ila kazi tu. Kuanzia kupatikana kwa Magufuli ni mkono wa Mungu ule ambao umeletwa kwa ajili ya kulidondosha hili dubwana janja ambalo bila akili, ujasiri na ushujaa huliwezi. Mungu mbariki Magufuli atudondoshee hili kitu mbaya kwani anaweza
 
Acha upuuzi wewe baradhuli , hapa wanaume tunazungumzia mustaqbali wa nchi .
Ukosapo cha kuandika kafanye shughuli nyingine . Wawezatumia mda wako hata kupunguza mchicha mwilini mwako , badala ya kuufuga !

Katika wanaume wanaozungumzia mustakabali wa nchi na wewe unajihesabu umo? Kashifa ndiyo umeona inajenga acha upumbavu Magufuli huwezi ukamtukana halafu wewe usitukanwe kama una hoja ya msingi sema na siyo kukashifu watu hivi wapinzani wangemwacha kama angakuwa mchafu kama ulivodai? Wapinzani wake wote akiwemo huyo unayemshabikia ambaye ana nyenzo za kupata habari sahihi bado hajamsema vibaya Magufuli wewe mganga njaa unapata wapi data za kumsema Magufuli ? Hivi wewe unaweza kupata data kwa usahihi za waziri kuliko boss wake ambaye alikuwa waziri mkuu? Mkitumwa muwe mnawauliza usahihi wa yale mliyotumwa na siyo kukurupuka kama ulivyofanya wewe na ujinga wako.
 
Tazameni Uzi ni wa mwaka gani. Naona watu wanajiachia tuuuu. Poleni!!!!
 

umemaliza, mimi siongezi kitu..
 

Mkuu safi sana,umeongea inavyotakiwa,I'm speechless,kudos
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…