Kwa muda mrefu haijawahi tokea katika Afrika kupatikana rais mwenye kuguswa na matatizo ya wananchi masikini kama rais wetu, John Pombe Magufuli.
Katika enzi za kupigania Uhuru Afrika palikuwa na wazalendo kama Mwl.Julius Nyerere , Patrick Lumumba, Kwame Nkuruma na wengine wengi.Wapigania Uhuru hawa walikuwa na moyo wa kizalendo wa hali ya juu katika nchi zao.
Wazalendo hawa walijitoa muhanga wa maisha yao kwa faida ya nchi zao na vizazi kwa vizazi.
Miaka ya sasa wazalendo kama hawa wako wachache sana.Libya alikuwepo Gaddafi, na Tanzania yupo rais John Pombe Magufuli.
Rais JPM amejitoa katika kuwatumikia wananchi maskini Tanzania.Hapati usingizi akiwafikiria kuwakomboa wananchi maskini.
Juhudi zake za kupinga rushwa, ufisadi na uwajibikaji wa viongozi ni kielelezo tosha rais huyu ana uzalendo uliotukuka.
Wananchi wa Tanzania wanabahati kubwa ya kumpata kiongozi huyu mwenye UCHUNGU na nchi.
Kila ninaposikiliza hotuba zake( Mhe.rais, Dr. John Joseph Pombe Magufuli) na matendo yake hakika unalolisema naliona. Ni uchungu wa kweli kutoka moyoni. Tatizo lake ni dogo tu lakini linamadhara makubwa kwa nchi. Nalo ni hili hapa. Kuamini kuwa hakuna mtu mwingine mzalendo kama yeye na hakika kila anayesema kinyume na anachokiamini yeye sio mzalendo.
Madhara ya dhana hiyo ni yale yanayotokea Libya na Tanzania leo hii, nchi za Gadaffi na Mwl. Nyerere . Ushahidi wa hili ninalolisema ni hali ya sasa ya nchi zao hawa watawala wawili ambao wote wameisha tangulia mbele ya haki. Mwl. Julius Kamabrage Nyerere na Tanzania aliyoijenga na Kanali Muhamed Gadaffi na Libya aliyoijenga. Wote walitokwa na jasho jingi lakini wamepata matokeo tofauti.
Mwl. alifundisha, akaelekeza na akasimamia ujenzi wa mifumo. Alijenga mfumo wa mahakama uliokuwa unaelekea kuifanya ijitegemee, akajenga bunge lenye mwelekeo thabiti wa kutunga sheria na kusimamia serikali na akajenga serikali iliyokuwa inasimamiwa na mihimili hiyo miwili niliyoitaja hapo juu.
Kawafundisha watu umihimu wa kujitegemea. Akatawala kwa miaka 23, akaondoka, akakabidhi nchi kwa mtu ambaye hakuwa chaguo lake bali chaguo la mfumo alioujenga. Akaacha katiba bora kwa wakati huo na jamabo moja bora kabisa aliloliweka kwenye katiba ni ukomo wa uongozi; miaka isiozidi 10 kwa kila rais na uchanguzi kila baada ya miaka mitano. Hatima ya maisha ya kila mtazania imekuwa mikononi mwake miaka yote. Hakuwapa watu vyakula wala hakuwajengea nyumba. Alijenga miundo mbinu kulingana na uwezo wa serikali yake. Akatangulia mbele ya haki taifa la bado linamtukuza nadhani litaendelea kumtukuza hadi mwisho wa dahari.
Kanali Muhamad Gadaffi, alijua umasikini wa watu wake aliowapenda mno. Akakomboa uchumi wa taifa lake kutoka kwenye makucha ya mabeberu. Akawapa kila kitu wananchi wake , elimu, afya, miundo mbinu, kila kitu isipokuwa uhuru wa kujieleza. Kila kitu isipokuwa hakujenga mifumo ya kutawala nchi. Aliwajengea mazingira mazuri ya kiuchumi isipokuwa domokrasia. Akatawala miaka arobaini. Watu wakamchoka na mabeberu wakapata mwanya, wakawatumia watu hao hao na kulivuruga taifa. Leo hii Libya ni shamba la bibi lisilokuwa na kesho. Hiki ndicho ninachokiogopa.