Tukumbuke kuna vyama vya siasa na kuna wanasiasa, haimaanishi kuwa kwa sababu chama cha CCM kimeshikwa na wanasiasa MAFISADI basi miongoni mwa wanasiasa/wanachama wa CCM hakuna wachapakazi au watu safi. Ni MAGUFULI huyuhuyu alisimama kidete kuhusu kuuzwa kwa jumba za serikali na baadhi ya nyumba anatuhumiwa kuchakachua uuzaji wake watu wote walimshambulia hata wasio safi mfano. ROSTAM kupitia gazeti lake la RAI walibeba Bango sana kuhusu kashfa hiyo sababu si mwanamtandao wenzao. Leo karudi tena kwenye CHAT, CDM mnaanza kudai ni member wenu mmempandikiza CCM je alipochakachua kuhusu mijengo ya UMMA mbona hatukuwasikia kusema ni Pandikizi lenu ndani ya CCM?
Tabia hii ya CDM kukimbilia majina makubwa (wanasiasa) inaanza kuwatafuna bila wao kuelewa oneni mlivyo mkumbatia MABERE MARANDO bingwa wa kutetea MAFISADI mahakamani ktk kesi wanazo shtakiwa kwa UFISADI wa Rasilimali za UMMA. Pia mmembeba SHIBUDA ambaye kwenye nyeupe anasema nyeupe na nyeusi anasema nyeusi mnaanza kumuona MZIGO. Sasa MAGUFULI anarudi kwenye kiwango chake mnadai PANDIKIZI lenu. Kweli siasa ni mchezo wa karata tatu.
Tukumbuke CCM,CUF,CDM,NCCR,TLP,NLD,NRA,UMD,UPDP,JAHAZI ASILIA vyote ni vyama vya siasa ambavyo ndani yake kuna wanasiasa, wanasiasa hao wamo wasafi na wachafu, wazalendo na Mafisadi. Hivyo Tusizame katika kushabikia vyama kama vile vinaongozwa na MALAIKA tukummbuke vyama vyote vinaongozwa na wanasiasa hivyo ni jukumu letu kuwapima na kuamua nani anatufaa kuwa kiongozi wetu